Wednesday, May 17, 2017

SERIKALI KUJENGA MAGEREZA MAEN EO YA KILIMO.

8753-Mhe.Mwigullu nchemba
Serikali inamkakati wa kuhakikisha inajenga Magereza   katika maeneo yenye uzalishaji mkubwa wa kilimo ambayo pia yana ukubwa wa kutosha ili kazi ya kuwarekebisha wafungwa iwe rahisi kufanyika huku shughuli za uzalishaji zikiwa zinaendelea.

Hayo yamesemwa leo Bungeni Mjini Dodoma na Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mhe. Mwigulu Nchemba alipokuwa akijibu swali la Mhe Devotha Minja Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro.

 “Magereza hayo yatajengwa katika maeneo yenye Kilimo  na yatakuwa  ni kwa ajili ya watu waliokwisha hukumiwa huku yale Magereza ya mijini yawe kwa ajili ya mahabusu tu ili wawe karibu na Mahakama,”alisema Mwigulu.                   

 Aliongeza kuwa mkakati huo wa Serikali ni wa muda mrefu na wanahitaji kufanya hivyo ili kurahisisha shughuli za maendeleo zinazofanywa na wafungwa na pia kupunguza msongamano wa wafungwa katika Magereza.

Hili pia linatokana na tamko la Mh.Rais Dkt John Pombe Magufuli alilowahi kulitoa hivi karibuni kuwa wafungwa wako katika kutumikia adhabu hivyo wanatakiwa kufanya kazi hasa za kilimo ili kwanza kujipatia chakula na sio kukaa tu bure na kusubiri kila kitu wafanyiwe na serikali.

Aliongeza kuwa Serikali ina mkakati wa kutumia bajeti inayotengwa na nguvu kazi wanayoipata kutoka kwa wataaalam walionao kwa upande wa askari Magereza na wafungwa ili kukarabati Magereza chakavu na kujenga nyumba za askari.

Aidha alibainisha kuwa suala la kukatwa kwa umeme katika Magereza, nyumba za askari,pamoja na maeneo  na maeneo mengine ya kambi za Jeshi la Polisi na Magereza limeshafanyiwa kazi na serikali kwa kupitia  hazina imekwishatoa fedha kwa ajili ya kutatua tatizo hilo.

Mheshimiwa Waziri aliliambia Bunge kuwa sheria zimeainisha baadhi ya haki za mfungwa zikiwemo huduma za afya kwa wakati,kupewa chakula, uhuru wa kutembelewa na ndugu zake na kupata mawasiliano kwa kusoma magazeti,kusikiliza taarifa za habari na kuandikiwa barua na ndugu zao,haki ya kukata rufaa ikiwa hakuridhika na hukumu yake, malazi safi na yakutosha pamoja na kushiriki michezo mabalimbali.

WATANZANIA WAISHIO UJERUMANI WAFANYA MKUTANO ESSEN

unnamed
Umoja wa watanzania Ujerumani UTU e.V watingisha jiji la Essen nchini Ujerumani baada ya kufanya mkutano mkuu kwa mujibu wa katiba  ulioandamana na sherehe za ushindi wa viongozi wapya. 

jijini Essen katika ukumbi wa Bob’s Cafe, watanzania zaidi ya 75 ambao wanaishi nchini humo walihudhuria mkutano huo ili kutimiza haki yao ya msingi ya kuchagua viongozi wao.  

katika safu ya uongozi mpya Mhe Mfundo Peter Mfundo alichaguliwa tena kuwa Mwenyekiti wa umoja huo baada ya kukosa mpinzani. Makamo mwenyekiti mpya ni Mhe Salim Malumbo Jr. Katibu mkuu ni Julieth Myn, muweka Hazina ni Bi Nashe Mvungi, Mkaguzi wa mahesabu  namba 1 ni Mhe Bi Jovither Mushashu, Mkaguzi wa mahesabu namba 2 ni mhe Bi. Lilian Sorogo. Mjumbe namba Moja ni  Mhe Ebrahim Makunja aka Kamanda Ras Makunja na Mjumbe namba 2 ni Mhe Vanessa Lymo. 

Pamoja na mengi yalioongelewa kwenye mkutano huo azma ya  umoja wa watanzania Ujerumani UTU e.V ni kuwaendeleza watanzaniawanaoishi hapa ujerumani na hata kuwaletea maendeleo watanzania wanaoisho Tanzania, umoja ni Nguvu na utengano ni Udhaifu

MAGAZETI YA LEO TAREHE 17 MAY 2017.

Monday, May 15, 2017

TAARIFA KUTOKA JESHI LA POL ISI MKOA WA MWANZA.

msangii-1
TAREHE  14.05.2017 MAJIRA YA SAA 02:00HRS USIKU KATIKA KISIWA CHA GANA KILICHOPO KIJIJI CHA KAMASI KATA YA ILANGALA WILAYA YA UKEREWE, MTU ANAYEFAHAMIKA KWA JINA LA MKAMA MGENGELE, MIAKA 36, MVUVI NA MKAZI WA GANA KISIWANI, ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA KUMFANYIA UKATILI MTU ANAYEDAIWA KUWA MPENZI WAKE AITWAYE ESTER LAZARO MIAKA 37, MHUDUMU WA NYUMBA YA KULALA WAGENI IITWAYO BACELONA NA MKAZI WA GANA KISIWANI, KWA KUMKATA NA KITU CHENYE NCHA KALI KWENYE KIGANJA CHA MKONO WAKE WA KUSHOTO HADI KIKAANGUKA CHINI KISHA AKAMKATA TENA KWENYE PAJA LA MGUU WA KULIA, KITENDO AMBACHO NI KOSA LA JINAI.

INADAIWA KUWA MTUHUMIWA ALIKUWA NA MAHUSIANO YA KIMAPENZI NA BI ESTER LAZARO KWA MUDA MREFU, LAKINI HIVI KARIBUNI WALIKUWA KWENYE MGOGORO WA KIMAPENZI, INASEMEKANA KWAMBA TAREHE TAJWA HAPO JUU MTUHUMIWA ALIFIKA KWENYE NYUMBA YA KULALA WAGENI IITWAYO BACELONA AMBAPO MPENZI WAKE BI ESTER ANAFANYIA KAZI HUKU AKIWA AMELEWA POMBE NA KUANZA KURUSHIANA MANENO MAKALI.

 INADAIWA ILIPOFIKA MAJIRA TAJWA HAPO JUU MTUHUMIWA ALIMWENDEA BI ESTER LAZARO HUKU AKIWA HAFAHAMU KINACHOENDELEA NA KUMKATA KWA KUTUMIA KITU CHENYE NCHALI KWENYE KIGANJA CHA MKONO WAKE WA KUSHOTO HADI KIKAANGUKA CHINI KISHA AKAMKATA TENA KWENYE PAJA LA MGUU WA KULIA KISHA AKAONDOKA ENEO LA TUKIO.

WANANCHI WALITOA TAARIFA POLISI KUHUSIANA NA TUKIO HILO, ASKARI WALIFANYA UFUATILIAJI WA HARAKA JUU YA TAARIFA HIZO NA KUFANIKIWA KUMKAMATA MTUHUMIWA. MTUHUMIWA YUPO KATIKA MAHOJIANO NA JESHI LA POLISI PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI, MAJERUHI AMELAZWA HOSPITALI YA WILAYA YA UKEREWE AKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU NA HALI YAKE INAENDELEA VIZURI.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA AKIWAOMBA KUACHA TABIA YA KUJICHULIA SHERIA MKONONI KWANI MADHARA YAKE NI MAKUBWA LAKINI PIA NI KOSA LA JINAI. 

AIDHA ANAWAOMBA WANANDOA AU WATU WALIOKUWA KWENYE MAHUSIANO YA KIMAPENZI KWA MUDA MREFU WAKIWA KWENYE MIGOGORO WAENDE POLISI KIPO KITENGO CHA DAWATI  AMBACHO KINAWATAALAMU WANAOSHUGHULIKIA MATATIZO HAYO AU WAENDE KWENYE TAASISI NYINGINE ZA SERIKALI KAMA USTAWI WA JAMII NA SIO KUJICHULIA SHERIA MKONONI.

KATIKA TUKIO LA PILI;

MNAMO TAREHE  14.05.2017 MAJIRA YA SAA 18:30HRS JIONI KATIKA BARABARA YA MWANZA KWENDA SHINYANGA KIJIJI CHA NYANG’HOLONGO TARAFA YA USAGARA WILAYA YA MISUNGWI MKOA WA MWANZA, GARI NAMBA T.571 BHU AINA YA MINBUS FUSO MALI YA MOHAMEDI MAMDALI LIKITOKEA MWANZA KWENDA KAHAMA LIKIENDESHWA NA DEREVA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA FREDY KAWASANGE  MIAKA 39, MKAZI WA KAHAMA, LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU AITWAYE JUMA NKANU, ANAYEKADIRIWA KUWA NA UMRI WA MIAKA KATI YA 40 HADI 50, NA MKAZI WA KIJIJI CHA IBONGOYA “A” NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO.

INADAIWA KUWA MAREHEMU ALIKUWA ANAVUKA BARABARA BILA KUCHUKUA TAHADHARI YEYOTE  HUKU AKIWA AMELEWA NDIPO GHAFLA ALIKUTANA NA GARI TAJWA HAPO JUU LIKIWA KWENYE MWENDO KASI NA KUGONGWA NA KUPELEKEA MAREHEMU KUPOTEZA MAISHA.

DEREVA WA GARI HILO AMEKAMATWA YUPO KATIKA MAHOJIANO NA JESHI LA POLISI, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI, MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHI HOSPITALI YA WILAYA YA MISUNGWI KWA AJILI YA UCHUNGUZI, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA UTAKABIDHIWA KWA NDUGU WA MAREHEMU KWA AJILI YA MAZISHI.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WATEMBEA KWA MIGUU PINDI WAWAPO BARABARANI AKIWATAKA KUWA MAKINI NA KUCHUKUA TAHADHARI WAKATI WOTE  ILI KUJIEPUSHA NA AJALI NA VIFO VINAVYOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA PIA ANAWATAKA WAENDESHAJI WA VYOMBO VYA MOTO KUZINGATIA SHERIA, KANUNI NA TARATIBU ZA USALAMA BARABARANI WAKATI WOTE ILI KUWEZA KUZUIA AJALI ZISIZO ZA LAZIMA.

IMETOLEWA NA:

DCP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA

WAETHIOPIA NANE WAKUTWA WAMEKUFA RUVUMA

unnamed
Raia nane kutoka nchi ya Ethiopia wamekutwa wamefariki katika kijiji cha Amani makolo taarafa ya kingonsera wilayani mbinga mkoani wa ruvuma   huku wengine 25 wakiwa hai wanashikiriwa na jeshi la polisi.

Habari kutoka jeshi la polisi mkoa wa ruvuma kupitia kaimu kamanda wa polisi ACP DISAMASI KISUSI zinasema raia hao wa Ethiopia walikuwa wanasafirishwa kwenda nchi ya AFRIKA KUSINI kupitia Upande wa MALAWI mwa ziwa NYASA.

Vifo vya Waithiopia hao vinatokana na kubebwa kwenye kontena la lori wakitokea NAMANGA, ARUSHWA hivyo kutokana na hali mbaya ya hewa hali zao zilianza kubadilika na kupelekea kufariki.huku miili ya marehemu hao ikiwa imehifadhiwa katika hospitali ya wilaya MBINGA.

Jeshi la polis mkoa wa ruvuma kwa kushirikiana na jeshi la uhamiaji linaendelea na uchunguzi kubaini walioleta miili ya marehemu na wale wasiliokamatwa hatua za kisheria zitafuatwa.