Saturday, December 10, 2016

TAKUKURU BAGAMOYO, WAADHIMISHA SIKU YA MAADILI.

Wa kwanza kushoto ni mkuu wa TAKUKURU wilaya ya  Bagamoyo, Raymond  Kitima, wa pili  kushoto ni Makamo mkuu  wa Chuo  kikuu cha  Marian, (MARUCO)  Dkt.  Zakayo  Kimaro. kutoka kulia wa kwanza ni Mkuu  wa  Polisi  wilaya ya Bagamoyo, Mrakibu  Mwandamizi  wa  Polisi, SSP- Adam  Maro, na wapili kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bagamoyo, Fatma Omari Latu.
..........................................................
Taasisi ya Kuzuia na  Kupambana na Rushwa Nchini TAKUKURU wilaya ya  Bagamoyo imeadhimisha siku ya maadili duniani, ambapo wilaya ya Bagamoyo imefanyika katika Chuo  Kikuu cha  Marian University College  (MARUCO).

Katika Maadhimisho hayo  uliendeshwa Mdahalo wa kujadili mmomonyoko  wa maadili katika Jamii  hali inayopelekea kichocheo cha rushwa kwa vijana.

Watoa mada mbalimbali walieleza  namna jamii  ilivyotoka kwenye maadili mema kuanzia ngazi ya familia na hatimae taifa  kwa ujumla hali inayosababisha kuwepo kwa Rushwa katika kila sekta  bilaya  kuwa na hofu yoyote.

Aidha, imeelezwa kuwa, tamaa ya kupata mafanikio kwa haraka ni  miongoni  mwa vichocheo vinavyopelekea rushwa kwakuwa kila  mwenye nafasi fulani katika kazihuona njiapekee yakupatya  mafanikio ni   kupokea rushwa.

Mdahalo huo uliowajumuisha wanafunzi kutoka vyuo vya  TaSuBa, ADEM, MARUCO NA SLADS Washiriki walitaka baadhi ya sheria katika maeneo mbalimbali zifanyiwe marekebisho  ili kupunguza  urasimu  katika mambo maeneo mbalimbali ya kupata huduma ambayo kwa kiasi  kikubwa huchangia  vitendo vya Rushwa.

Kwa upande wao viongozi wa  dini  wameitaka jamii  kurudi kwenye mafundisho ya dini  zao ili waweze kuwa n a Hofu juu ya  Mungu ambapo wataweza mkusimamia haki na kupinga Rushwa kwakuwa  vitendo vya Rushwa vinapingana na upatikanaji wa haki  kwa mwenye haki.

Mkuu  wa Taasisi ya  Kuzuia na Kupambana na Rushwa Wialaya ya Bagamoyo, Raymond Katima,  aliwataka wananchi wilayani  Bagamoyo kutoa ushirikiano na Taasisi ya  kuzuia na  kupambana na Rushwa ili kufichua vitendo  vya hivyo.

Alisema Rushwa ina miziz mingi katika jamii tatizo na  kwa kiasi gani vitendo hivyo vinaripotiwa ili viweze kushughulikiwa kisheria.

Aidha,  aliwataka wanafunzi  kuweka bayana namna  Rushwa ya  ngono   ilivyotawala  katika vyuo  mbalimbali  wilayani Bagamoyo na  kwamba  iki bainika hatua zichukuliwe dhidi ya muhusika.

Aliongeza kuwa jamii  imeathirika na vitendovya Rushwa na  kupelekea hata   paleunapomuhudumia kwa moyo mmoja akili yake haimini kama umemuhudumia na kuanza kuteneza  mazingira ya kukupa Rushwa yeye  mwenyewe  bila ya  kuomb wa hali ambayo inarudisha nyuma mapambano dhidi ya Rushwa.

Siku ya  maadili duniani huadhimishwa Desemba 10  ambapo kaulimbiuya  mwaka huu ni  Kujenga na kukuza maadili,  Haki za Binadamu, Uwajibikaji,  Utawala bora na Mapambano dhidi ya Rushwa.
Dkt. Eligius Mkulima Mhadhiri wa chuo Kikuu cha  Marian (MARUCO) akiwasilisha mada katika Mdahalo huo.
Washiriki wa Mdahalo huo katika siku ya  maadili  wakifuatilia mada zilizowasilishwa.
 Wa kwanza kushoto ni mkuu wa TAKUKURU wilaya ya  Bagamoyo, Raymond  Kitima, wa pili  kushoto ni Makamo mkuu  wa Chuo  kikuu cha  Marian, (MARUCO)  Dkt.  Zakayo  Kimaro. kutoka kulia wa kwanza ni Mkuu  wa  Polisi  wilaya ya Bagamoyo, Mrakibu  Mwandamizi  wa  Polisi, SSP- Adam  Maro, na wapili kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bagamoyo, Fatma Omari Latu.
 Washiriki wa Mdahalo huo katika siku ya  maadili  wakifuatilia mada zilizowasilishwa.
Mhadhiri wa Chuo kikuu cha  Marian, (MARUCO) Dkt. Samuel Nguni, akiwasilisha mada katika mdahalo huo.
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya, wakifuatilia Mdahalohuo.
Mtoa mada  katika Mdahalohuo, Endrew Maselele, akiwasilisha mada.
Mkuu wa TAKUKURU Bagamoyo, Raymond Kitima.
 Mkuu wa TAKUKURU Bagamoyo, Raymond Kitima.
 Makamu mkuu wa  Chuo cha Marian Bagamoyo, (MARUCO) Dkt. Zakayo  Kimaro akifunga mdahalo huo.

MZEE WA BARAZA KIBAHA, AHUKUMIWA JELA MIAKA 3 KWA RUSHWA.

Mahakama ya hakimu mkazi kibaha, imemuhukumu mzee wa baraza Francis Issaya (64) kwenda jela miaka 3 au kulipa faini laki 5 baada ya kukutwa na hatia ya kupokea Rushwa.

Akisoma hukumu hiyo Hakimu Mkazi Harieth Mwailolo amesema mahakama hiyo imeridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa jamuhuri na hivyo anatoa adhabu ya kwenda jela kwa mzee huyo ili iwe fundisho kwa wengine. 

Awali mwendesha mashitaka wa Takukuru Sabina Weston aliieleza mahakama hiyo kuwa mzee huyo wa baraza alitenda kosa hilo mwezi uliopita kwa kumshawishi Omari Hiza ampe kiasi cha Tshs. 100,000/= ili aweze kumsaidia mkewe Mariam Hussein aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya Jinai 329/2016 kosa Shambulio la kudhuru mwili.

Wakati huohuo Mahakama ya hakimu mkazi kibaha ya mhukumu Abduly Omar (27) mkazi wa kwa mathias kibaha kwenda jela miaka 30 baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kujaribu kubaka. 

Akisoma hukumu hiyo hakimu mkazi wa mahakama ya hakimu mkazi kibaha Aziza Mbadyo alieleza kuwa mahakama imeridhika na ushahidi uliowasilishwa kwenye mahakama hiyo usio acha shaka yoyote hivyo mtuhumiwa ataenda jela miaka hiyo ili iwe fundisho kwa wengine. 

Awali mwendesha mashitaka wa serikali Lulu Ukwaju aliileza mahakama hiyo kuwa mnamo tarehe 07 July 2016 huko kwa Mathias Kibaha Abduly Omary alijaribu kumbaka binti ambaye jina linahifadhiwa kwa sasa na kabla ya kutekeleza azima yake hiyo alikurupushwa na wanachi

09 DESEMA, DC. BAGAMOYO AZINDUA KILIMO CHAMA CHA USHIRIKA RUVU (CHAURU)


Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Alhaji, Majid Hemed Mwanga, leo Tarehe 09 Desemba 2016 amezindua rasmi kilimo katika shamba  la Chama cha Ushirika Ruvu, (CHAURU) kwa msimu wakilimo kwa mwaka 2016/17.

Akizungumza wakati wa uzinduzi  huo, mkuu huyo wa wilaya aliwataka CHAURU kuanzisha utaratibu wa kuuza mchele badala ya mpunga ili kupata soko kwa urahisi na kupunguza mfumuko wa bei ya Mchele katika Halmashauri ya Chalinze.

Alisema kutokana na uchaguzi mzuri wa mbegu inayotum ika katika mashamba hayo, mchele unaolimwa CHAURU umekuwa mzuri na kwamba unao uwezo wa kuingizwa kwenye ushindani  wa  kibiashara.
 Mkuu wa wilaya ya  Bagamoyo, Majid  Mwanga, akizungumza katika Mashamba ya  Chama cha Ushirika Ruvu (CHAURU)
 Baadhi ya Matrekta yaliyokuwa yakizindua kilimo katika Mashamba ya CHAURU.

WAHITIMU WA MAFUNZO YA MGAMBO BAGAMOYO KUPATIWA AJIRA JKT.

Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid HemedMwanga, akizungumza  wakati wakufunga mafunzo ya  Mgambo, kata ya Mapinga.

Vijana 102 waliohitimu mafunzo ya  Mgambo kata ya Mapinga wilayani Bagamoyo, wamepata  Ajira Jeshi  la  Kujenga Taifa, JKT.

Akifunga mafunzo hayo ya mgambo, Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Alhaji, Majid Hemed Mwanga, alisema mgambo hao tayari wamefa nyiwautaratibu wa kupata Ajira kupitia jeshi  la Kujenga Taifa JKT, ili kuondoa changamoto ya ajira ambayo inawakabili vijana wengi hapa nchini.

Alisema Serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais, Dkt. John Magufuli, imeweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha inaondoa tatizo la Ajira  kwa vijana ikiwa ni pamoja na kuwatengenezea mazingira rafiki ya kuajiriwa na kujiajiri.

Majid, Alisema katika  kukabiliana na changamoto ya ajira,  wilayani Bagamoyo Bagamoyo tayari kuna viwanda vitatu vinavyotarajiwa kufunguliwa wakati wowote ili kutoa fursa kwa vijana  kupata ajira.

Alifafan ua  kuwa, Kata ya Mapinga kuna  Kiwanda c ha kusindika Matunda cha Elvin ambacho kitatoa fursa kwa watu watakaolima matunda mbalimbali ikiwemo manasi, maembe, Nyanya nk. kwenda kuyauza na kujiongezea kipato ambapo matunda hayo yatakaushwa na kwenda kuuzwa nje ya nchi.

Aidha, alisema Kiwanda cha pili ni kiwanda cha Sayona  kilichopo  kata ya Msoga Halmashauri ya Chalinze ambacho kitanunua matunda ya Manansi Maembe kwaajili ya kutengeneza juisi na kuongeza kuwa kiwanda cha tatu ni kiwanda cha kusndika Pilipili kilichopo kata ya Kisutu Bagamoyo mjini na kwamba pilipili aina zote zitapata soko katika Kiwanda hicho.

Majid aliwataka wahitimu wa mafunzo ya mgambo kuheshimu sheria za nchi na kulinda kiapo chao ili wasitumike  vibaya  na kusababisha uhalifu.

Alisema kila mgambo anapaswa kuchunga misingi ya sheria za nchi na atakaekiuka na kufanya uhalifu kwa namna yoyote ile atakuwa amevnja  katiba na  kukiuka kiapo chake na kwamba atastahiki kuchukuliwa hatua.

Wakati huohuo amewaonya wawekezaji katika wilaya ya Bagamoyo kuacha kuwanyanyasa mgambo na badala yake kila mgambo anapaswa kuwa na mkataba utakaomlinda  kimaslahi  katika  kufanya kazi yake.

Aidha, aliwataka wawekezaji katika wilaya ya Bagamoyo kuajiri mgambo waliopata mafunzo ili kujiwekea ulinzi wenye uhakika wao na mali zao.

 Baadhi ya wahitimu wa mafunzoya mgambo kata ya Mapinga wilayani  Bagamoyo
 Mshauri wa mgambo wilaya ya Bagamoyo, Meja Iddi Musira katikati akifurahia jambo   mara baada ya kumaliza sherehe za  kufunga mafunzoya  mgambo kata ya  Mapinga.
 MG. Hilda Msaki akizun gumza na vyombo vya habari mara baada ya kumaliza mafunzo hayo ya mgambo.