Sunday, October 30, 2016

DC. MUHEZA,HAJAT, MHANDISI, MWANAASHA TUMBO, ATEMBELEA ZAHANATI MPYA YA KIJIJI CHA ZENETI

 Mkuu wa wilaya ya Muheza,Haja Mhandisi,Mwanasha Tumbo katika akiongozwa na Diwani wa Kata ya Potwe,Rashid Mdachi na Mwenyekiti wa Serikali ya  Kijiji cha Zeneti wakitembelea Jengo jipya la Zanahati ya Zeneti iliyojengwa kwa ushirikiana baina ya Halmashauri,Wananchi na Shirika la World Vision na Mbunge wa Jimbo hilo ambalo limegharimu kiasi cha milioni 35.2.
 

Kulia ni Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Muheza,Mathew Mganga akimuongozwa Mkuu wa wilaya ya Muheza, Hajat, Mhandisi Mwanasha Tumbo aliyetembelea zahanati ya Zeneti kuona jinsi inayoendelea na ujenzi wake kushoto ni Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Zeneti
 

Kaimu Mganga Mkuu wa wilaya ya Muheza,Mathew Mganga kulia akisisistiza jambo kwa Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo wa pili kutoka kushoto kuhusu ujenzi wa zahanati hiyo katikati ni Diwani wa Kata ya Potwe,Rashid Mdachi.
 

Diwani wa Kata ya Potwe,Rashid Mdachi akimuonyesha kitu Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat, Mhandisi Mwanasha Tumbo wa pili kulia
 

Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo katikati akisisitiza jambo kwa Diwani wa Kata ya Potwe,Rashid Mdachi.
 

Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo katikati akiangalia baadhi ya vyoo vya Zahanati hiyo wakati alipoitembelea kuikagua na kuona namna ujenzi wake unavyoendelea.
 

Diwaniwa Kata ya Potwe,Rashid Mdachi akizungumza na wananchi  katika ziara hiyo ya Mkuu wa wilaya katika Zahanati ya Kijiji cha Zeneti

RAIS DKT. MAGUFULI KUFANYA ZIARA YA SIKU MBILI NCHINI KENYA

11rais-magufuli-awasihi-watanzania-kuungana-na-waislamu-kuliombea-taifa
Top of Form
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, kesho tarehe 31 Oktoba, 2016 ataanza ziara ya Kiserikali ya siku mbili nchini Kenya kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta.

Rais Magufuli anatarajiwa kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta Jijini Nairobi majira ya saa nne asubuhi na baadaye kupokelewa rasmi na mwenyeji wake Rais Kenyatta katika Ikulu ya Nairobi ambako viongozi hao watafanya mazungumzo rasmi.

Pamoja na kufanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake, Rais Magufuli atakwenda kutoa heshima katika Kaburi la Rais wa Kwanza wa Kenya Hayati Mzee Jomo Kenyatta na pia anatarajiwa kuhudhuria dhifa ya kitaifa aliyoandaliwa na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta
Ikulu Jijini Nairobi.

Katika ziara hii Rais Magufuli anatarajiwa kutembelea kiwanda cha maziwa cha  Eldoville kilichopo Karen Jijini Nairobi, na pia anatarajiwa kuzindua barabara mchepuko ya Southern By-pass iliyopo Jijini Nairobi.

Barabara hiyo mchepuko ya Southern By-pass ni moja kati ya miradi mikubwa ya barabara nchini Kenya, inaunganisha maeneo mbalimbali ya Jiji la Nairobi kwa barabara za juu na chini na imejengwa kwa lengo la kupunguza msongamano wa magari katika Jiji hilo.

Rais Magufuli anatarajiwa kumaliza ziara yake tarehe 01 Novemba, 2016 na kurejea Jijini Dar es Salaam.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Nairobi 30 Oktoba,
2016. 
Bottom of Form

MJADALA MUSWADA WA HUDUMA ZA HABARI WAHITIMISHWA, SERUKAMBA ASEMA MFUKO WA WA MAFUNZO YA HABARI UTAWANUFAISHA WAANDISHI

mbunge-wa-kigoma-mjini-peter-serukamba
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Peter Serukamba amesema kuwa uanzishwaji wa  Mfuko wa Mafunzo ya Habari utaweka utaratibu wa maslahi ya waandishi wa habari utakaowasaidia kuwa na bima za afya, mikataba inayoeleweka pamoja na kuwaendeleza kimasomo.

Serukamba aliyasema hayo leo Mjini Dodoma alipokuwa akihitimisha kikao cha Kamati hiyo kilichokuwa kikijadili juu ya muswada wa habari ambao kwa mara ya kwanza uliwasilishwa Bungeni mnamo mwezi Septemba mwaka huu.

Serukamba amesema kuwa Kamati hiyo imesikiliza maoni ya kila mmoja na imejitahidi kupitia kifungu hadi kifungu cha muswada huo na Serikali imekubali kuyafanyia mabadiliko baadhi ya maeneo ya muswada huo kulingana na maoni yaliyowasilishwa na wadau mbalimbali.

“Muswada huu utakapokuwa sheria tunategemea kuunda Mfuko wa Mafunzo wa Habari ambao utawaendeleza waandishi wa habari kwa kuwawekea utaratibu wa maslahi yao, utakuwa ni kwa ajili ya waandishi wa habari wote watakaothibitishwa na Bodi ya Ithibati”, alisema Serukamba.

Amefafanua kuwa mfuko huo utawezesha mafunzo kwa wanataaluma ya habari, utakuza programu za uendelezaji maudhui ya ndani ya nchi pamoja na kuchangia utafiti wa maendeleo katika nyanja za habari na mawasiliano ya umma, hivyo, utasaidia kurudisha taaluma ya habari kwenye hali nzuri nchini.

Aidha, ameongeza kuwa sheria hiyo itahakikisha inalinda haki za waandishi wa habari, vyombo vya habari pamoja na wananchi wa kawaida  kwa sababu itaweka  utaratibu juu ya utatuaji wa kesi zinazohusiana na  vyombo vya habari kwa muda mfupi hivyo kusaidia watu  kupata haki zao haraka.

Muswada huo pia umetoa kipindi cha mpito cha miaka mitano kwa wanahabari kujiendeleza kielimu katika taaluma ya habari ili wawe na vigezo vitakavyowawezesha kuwa wanahabari kamili waliobobea kwenye taaluma hiyo.

RAIS DK. MAGUFULI AMTEUA JENERALI MSTAAFU GEORGE WAITARA KUWA MWENYEKITI WA BODI YA TANAPA

waitara-anatembea
 

Rais wa Jamhuri ya Muunganowa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 30 Oktoba, 2016 amemteua Jenerali Mstaafu George Marwa Waitara kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania  (TANAPA).

Taarifa iliyotolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi huo umeanza tarehe 29 Oktoba, 2016.

Jenerali Mstaafu George Marwa Waitara ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu.

WAKATI HUO HUO,Rais Dkt. Magufuli amemteua Dkt. Eligy Mussa Shirima kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI)
Uteuzi wa Dkt.Shirima umeanza tarehe 29 Oktoba 2016.

Kabla ya uteuzi huu Dkt. Eligy Mussa Shirima alikuwa Mtafiti Mkuu na Msimamizi wa Utafiti wa Nyama ya Ng’ombe Makao Makuu ya TALIRI.
 
Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
30 Oktoba, 2016

DC BAGAMOYO AAHIDI KUZISIMAMIA ASILIMIA 10 YA FEDHA KUTOKA HALMASHAURI ZIWAFIKIE VIJANA NA KINAMAMA.

MKUU wa Wilaya ya Bagamoyo Majidi Mwanga amesema kuwa atahakikisha anazisimamia ipasavyo fedha  amabazo zinazotolewa na Halmashauri kwa ajili ya  kuwasadia vijana na kinamama lengo ikiwa ni kuona zinatumika katika vikundi mbalimbali lli kukuza uchumi na kuleta chachu ya kimaendeleo.

Mwanga ameyasema hayo jana wakati alipokuwa akihojiwa na kituo kimoja cha redio cha Jijini Dar es Salaam kuhusiana na changamoto  mbali mbali zilizopo katika utendaji wa kazi pamoja na mikakati aliyoiweka katika kuwahudumia wananchi wake wa Bagamoyo.

Alisema kwamba halmashauri zinanapaswa kutenga kiasi cha asilimia kumi cha makusanyo ya mapato yake ambapo vijana wanatakiwa kupatiwa asilimia tano na kwa upande wa kinamama wanatakiwa wapatiwe asilimia tano kwa ajili ya kuendeshea shughuli zao za ujasiriamali.

“Mimi kama mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo mikakati yangu ni kuhakikisha kwamba fedha hizo ambazo ni asilimia kumi zinawafikia walengwa wote bila ya kuwa na ubaguzi, hivyo nitazisimamia na kuona ni jinsi gani zinaweza kuleta mabadiliko chanya kwa vijana pamoja na kinamama ambao watapatiwa fedha hizo,”alisema Mwanga.

Aidha mkuu huyo wa wilaya alisema kwamba ana imani kwamba endapo Halmashauri ikitilia mkazo suala hilo la kuhakikisha  asilimia kumi inatolewa katika kila bajeti kutaweza kuwa mkombozi mkubwa kwa kuviwezesha vikundi vya aina mbali mbali ili viweze kuendesha biashara zao na kukuza mitaji waliyonayo.

Pia alifafanua kuwa fedha hizo zinatolewa kwa utaratibu maalumu ambapo inatakiwa vijana au kinamama kuunda vikundi vyao na kuvisajili ili pindi fedha hizo zinapotolewa ziweze kuwafikia walengwa kwa wakati na  kuwanufaisha kwa kiasi kikubwa katika kuendeleza biashara zao ambazo  wanazifanya ili kukua zaidi.

 “Katika Wilaya yangu ya Bagamoyo kwa sasa nina halmashauri mbili, ambapo kuna halshauri ya Bagamoyo, pamoja na halmashauri ya mji mdogo Chalinze, kwa hivyo zote hizi zinatakiwa kutenga asilimi hiyo kumi kwa ajili ya  vikundi hivyo ” aliongeza Mwanga.

Alisema kwamba kwa sasa kuna fedha ambazo tayari zimeshatolewa na halmashauri  kwa ajili ya kuvisaidia vikundi hivyo vya kinamama na vijana, ambapo katika halmashauri ya bagamoyo kumeshatolewa kiasi cha shilingi milioni 120 na kuongeza kuwa fedha hizo zitakuwa zinatolewa kwa mzunguko ili ziweze kuwafikia walengwa wote.

Katika hatua nyingine Mwanga alitoa wito kwa vijana na wakinamama ambao watapata fursa ya kupatiwa fedha hizo kuhakikisha   wanazitumia vizuri katika kuendeshea biashara zao ili kukuza waweze kuirejesha kwa wakati na vikundi vingine vipatiwe pia.