Wednesday, August 17, 2016

WAKUU WA WILAYA WASTAAFU WAPEWA ELIMU YA UJASILIAMALI, WAANZISHA SACCOS.

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Global Publishers, Eric Shigongo, (aliyevaa miwani) akiwasikiliza wakuu wa wilaya wastaafu ambapo  Shigongo aliowapa somo la ujasiriamali, aliyepeana nae mkono wa kwanza kulia ni Mkuu wa wilaya mstaafu Bagamoyo, Brother. Ahmedi  Kipozi.
...............................................................................................................................

Wakuu wa wilaya wastaafu waanzisha SACCOS ili kukabiliana na changamoto mbalimbali za kiuchumi.

Akitangaza azimio hilo, mwishoni mwa mafuno hayo yaliyofadhiliwa na Mfuko wa Pensheni wa PSPF, na kufanyika makao makuu ya Mfuko huo jijini Dar es Salaam, Mjumbe wa Sekretariati ya wakuu hao wastaafu, Crispin Meela, alisema, wajumbe 10 wamechaguliwa na wana semina hao ili kushughulikia utaratibu mzima wa kuanzishwa kwa SACCOS hiyo haraka iwezekanavyo.

Wajumbe wa Kamati ya muda ya kusimamia mambo hayo ni pamoja na Ramadhan Maneno (Mwenyekiti), Betty Mkwasa (Katibu), Crispin Meela, Erasto Sima, Geogina Bundala, Farida Mgomi, Said Amanzi, Fatma Ally, Muhingo Rweyemamu na Manzie Mangochie.

Kwenye mafunzo hayo Wakuu hao wa wilaya wastaafu, waliweza kupata elimu kutoka kwa wataalamu mbalimbali wakiwemo Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Beng’ Issa, na wataalamu wa Saikolojia, na Wajasiriamali wenyewe kama vile Eric Shigongo.

Akifunga mafunzo hayo Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu, ametoa changamoto kwa wakuu hao wanaokadiriwa kufikia 100 na ambao wamejiunga uanachama wa Mfuko huo kupitia mpango wa uchangiaji wa Hiari, (PSS), kuwa uamuzi wao utawakwamua kiuchumi na wanachotakiwa ni kuwa na mpango kamambe utakaoweza kutekelezeka kwa ufanisi mkubwa.

kama shirika lingine lolote lile la kutoa huduma za Pensehni na za kifedha, umoja huo ni fursa kubwa kwa Mfuko na ndio maana umeamua kuwaunga mkono  ili mmfikie azma yenu ya kuanzisha SACCOS hiyo”. Alisema.
 5R5A7799
 Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Global Publishers, Eric Shigongo, akiwasilisha mada ya ujasiliamali, kwa wakuu wa wilaya wastaafu katika semina ya mafunzo ya ujasiliamali iliyofadhiliwa na mfuko wa  pensheni wa PSPF na kufanyika makao makuu ya mfuko huo jijini Dar es Salam.
 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, (TAMISEMI), George Simbachawene, (watatu waliokaa), Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashantu Kijaji, (wapili waliokaa), Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PSPF, George Yambesi, (wapili kulia), Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu, (wakwanza kushoto waliokaa) na Mwenyekiti wa Wakuu hao wa Wilaya wastaafu, Ramadhan Maneno, (wakwanza kulia waliokaa) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wastaafu hao
 
Mkuu wa Wilaya mstaafu, Christopher Kangoye
 Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu, akifunga mafunzo hayo Agosti 16, 2016
Meneja wa PSPF, anayeshughulikia Mpango wa Uchangiaji wa Hiari, (PSS), Mwanjaa Sembe, akitoa mada kuhusu faida za kujiunga na mpango huo.
Kaimu Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, (NHIF), Mkoa wa Ilala, Hipoliti Lello, akitoa mada kuhusu huduma zitolewazo na Mfuko huo hususan ushirikiano wa Mfuko huo na PSPF, katoa bima ya afya kwa wanachama wa PSPF
Mkuu wa Wilaya Mstaafu, Betty Mkwasa, akifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa kwenye mafunzo hayo.
Mkuu wa Wilaya Mstaafu, Manzie Manguchie, akifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa kwenye mafunzo hayo.
Mwenyekiti wa Wakuu wa Wilaya Wastaafu, Ramadhan Maneno, (kushoto), akizungumza jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publisher, Eric Shigongo
Mkuu wa Wilaya Mstaafu, Makunga, akitoa maoni yake kuhusu uanzishwaji wa SACCOS hiyo
Meneja wa PSS, Mwanjaa Sembe, akimsikiliza Mkuu wa wilaya mstaafu, Erasto Sima.
 Shigongo akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wakuu wa wilaya wastaafu, baada ya kuwapa elimu juu ya ujasiriamali.
Kaimu Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, (NHIF), Mkoa wa Ilala, Hipoliti Lello, (kushoto), akizungumza jambo na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Abdul Njaidi, (kulia) na Mtafiti wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Mapesi Maagi

WAZIRI PROF. MUHONGO, APIGA MARUFUKU MAFUTA YA TRANSFOMA KUKAANGIA CHIPSI.



Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amepiga marufuku matumizi ya mafuta ya transfoma kwa ajili ya kukaangia chips na kutengeneza mikorogo.

Profesa Muhongo ameyasema hayo alipokuwa akihutubia wakazi wa kijiji cha Kirongo wilayani Muheza mkoani Tanga katika ziara ya kukagua miradi ya umeme  vijijini inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) katika mkoa huo.

Prof. Muhongo  alisema mafuta hayo hayakutengenezwa kwaajili ya kula hivyo kuyatumia kwaajili ya chakula ni  kuhatarisha afya za walaji na kwamba yeyote atakabainika  kutumia  mafuta ya  Transfoma hatua zakisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Aidha, amepiga  marufuku pia utumiaji wa mafuta hayo ya  Transfoma  kuchanganyia na v ipodozi  kaarufu kama Mkorogo, na kusema kuwa matumizi ya  aina hiyo yanatarisha afya za watu.

Kumekuwa na  uvumi  wa muda  mrefu kuwa, baadhi ya wakaanga chipsi wamekuwa  wakitumia mafuta ya Transfoma kuchanganya  na mafuta ya kula kawaida kwa madai  kuwa kwakufanya hivyo hutumia mafuta ya kula kidogo na kuongeza faida  katika biashara zao.

Wakati wakaanga Chipsi wakitumia mafuta hayo  ya Transfoma kukaangia chipsi, watumiaji wa vipodozi nao wamekuwa wakitumia mkorogo (mchanganyiko maalum) unaochanganywa na mafuta ya  Transfoma.

Hali hiyo huwenda ndiyo inayopelekea mara  kadhaa Mafuta ya  Transfoma huripotiwa kuibiwa na kuacha baadhi ya maeneo  kukaa bila ya umeme huku serikali  ikipata hasara ya  kujaza mafuta mengine kwenye Transfoma.

MAGAZETI YA TANZANIA LEO TAREHE 17-08-2016.

nip

Tuesday, August 16, 2016

AJALI YAUA NG'OMBE WATANO BAGAMOYO USIKU HUU TAREHE 16-08-2016 ENEO LA UKUNI.

Ng'ombe watano wamefariki papo hapo baada  ya kugongwa na Gari katika eneo  la Ukuni Bagamoyo mjini usiku huu.

Taarifa za awali kutoka  eneo la tukio  zinasema kuwa  Ng'ombe  hao walitolewa katika kijiji cha Makurunge kata ya Makurunge ambako  kulitokea mapigano kati ya wakulima na wafugaji baada ya wafugaji kuingiza Ng'ombe kwenye shamba la  mkulima na kuharibu mazao.

Akielezea kwa ufupi katika  eneola tukio mkuu wa  polisi wilaya ya  Bagamoyo, Mrakibu  Mwandamizi wa  Polisi, SSP. Adam Maro alisema mara baada ya kupata taarifa za  kuwepo vurugu kati ya wakulima na wafugaji katika kijiji cha Makurunge, polisi walifika eneo la tukio ili kulinda usalama wa raia na mali zao.

SSP Maro alisema wafugaji waliingiza Ng'ombe  katika shamba  la mkulima na kusababisha mazao kuliwa, hali iliyopelekea  wakulima  kuzuia  Ng'ombe.

Aliongeza kuwa mara baada ya wakulima kuzuia  Ng'ombe  hao ndipo kundi  la  wafugaji walipoanzisha fujo kwa kuwapiga wakulima na silaha  m,balimbali za jadi.

Alisema polisi walipofika eneo la tukio na kukuta wafugaji wamekimbia walilazimika  kuondoka  na  Ng'ombe  mpaka kituoni ikiwa ni njia ya kuwapata wahusika wenye mifugo hiyo ambao ndio wahusika wa vurugu hizo.

Hata hivyo, polisi waliwaongoza Ng'ombe hao wakiwa na gari ya polisi iliyokuwa imewasha taa za  kuongozea msafara ambapo walipofika  eneo la Ukuni Bagamoyo mjini maarufu kama barabara  mpya, Gari aina Fuso ambalo namba zake hazikupatika mara moja limegonga msafara huo wa Ng'ombe na kusababisha vifo vya  Ng'ombe watano papo hapo.

ORIGINAL COMEDY KUCHUKULIWA HATUA KWA KUVAA SARE ZA POLISI.

Katika siku za hivi karibuni, kumejitokeza  tabia kwa baadhi ya watu wakiwemo wasanii watu wengine mmoja mmoja kutumia mavazi yanayofanana na sare za Majeshi ya Ulinzi na usalama hapa nchini likiwemo Jeshi la Polisi katika shughuli zao za kisanii au katika kazi mbalimbali, Jambo ambalo ni kinyume cha sheria, kanuni na taratibu za Nchi. 

Kwa mujibu wa Sheria ya kanuni za makosa ya Jinai, sura ya 16 na  marejeo yake ya mwaka 2002,  kifungu cha 178 (1) na  (2) kinachozungumzia makosa dhidi ya sare za majeshi ya ulinzi na usalama,  kinabainisha wazi kuwa ni kosa kisheria kwa mtu yeyote ambaye siyo mtumishi wa majeshi ya ulinzi na usalama kuvaa mavazi yanayotumiwa au kushabihiana na sare za majeshi hayo  bila kibali kutoka kwa  Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kufuatia  kitendo kilichofanywa na kundi la kisanii la “ Original Comedy” kuvaa mavazi yanayoshabihiana na sare za Jeshi la Polisi, Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar Es Salaam linachukua  hatua za kisheria dhidi ya wasanii hao.

Aidha Jeshi la Polisi nchini, linatoa onyo kali kwa mtu ama kikundi chochote kuacha kutumia  mavazi yanayofanana na sare zinazovaliwa na  majeshi ya ulinzi na usalama hapa nchini na atakayebainika hatutasita kuchukua hatua kali za kisheria dhidi yake.

Jeshi la Polisi linatoa rai kwa wale wote wenye mavazi yanayoshabihiana na sare za majeshi ya ulinzi na usalama  kuzisalimisha mara moja katika vituo vya Polisi vilivyokaribu nao.

 Imetolewa na:
Advera John  Bulimba – Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP)
Msemaji wa Jeshi la Polisi.

Makao Makuu ya Polisi.