Sunday, July 31, 2016

MOTO WATEKETEZA GODAONI LA KUHIFADHIA MATAIRI DAR.

 
Godaoni la kuhifadhia mataili pamoja na vifaa vinginevyo vya magari lililopo Sinza Lego ambalo mmiliki wake hakufahamika mara moja, limeteketea kwa moto ambapo kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wamedai kuwa chanzo cha moto huo ni mataili, mpaka jioni hii kikosi cha kuzima moto kilikuwa eneo la tukio kuendelea kusaidiana na wananchi katika  kuzima  moto huo, Taarifa kamili itatolewa na Jeshi la Polisi.
 
Godaoni linalosadikiwa kuhifadhi vipuri vya magari likiwa linateketea kwa moto jioni hii Sinza Lego jijini Dar es salaam ambapo juhudi za kuzima moto zinaendelea japokuwa kazi ya kuzima imekuwa ngumu kutokana na aina ya vipuri vinavyohifadhiwa katika ghala hilo kuwa aina ya mipira na mafuta ya vilainishi vya vipuri.
 

Moto ukiwa umeshika kasihuku juhudi za kuuzima zikiendelea

ENJOY ENVIRONMENT TO VISIT DAR ES SALAAM NATURE STUDY .

Citizens from Canada enjoying beautiful landscape and wind in Dar es Salaam Nature study. Do not wait to be told come today and see for yourself.

DAR ES SALAAM NATURE STUDY, KITUO CHA MAARIFA.

Suleiman kuliwa, akitoa somo kwa wanafunzi wa shule ya wasichana ya Lukman ya jijini Dar es Salaam, mara walipotembelea kituoni hapo kujifunza ma mbo  mbalimbali.
Mwalimu Yasini Mkwizu akitoa ufafanuzi kuhusu aina mbalimbali za miti na faida zake mbele ya wanafunzi wa shule ya Lukmani walipotembelea eneo hilo ambapo waliweza  kujifunza  mambo mbalimbli ikiwemo umuhimu wa kuhifadhi misitu.
Ukiwa Dar es Salaam Nature  study  unaweza  kufahamu majina ya miti mbalimbali na faida  zake.
Wanafunzi wa shule ya Lukmani ya Sinza jijini Dar es Salaam wakionekana  kwa mbali katikati ya msitu  wakijifunza mambo mbalimbali  walipokuwa katika  ziara ya kimasomo katika msitu huo unaohifadhiwa na kituo cha Dar es Salaam Nature Study.

Mwalimu, Sadiki Kizuki, ambae ni mwalimu wa Jografia  na Historia akiwapa somo wanafunzi wa shule ya sekondari Chamanzi mife walipotembelea katika hifadhi ya msitu wa Dar Nature Study ili kujifunza  mambo mbalimbali.
Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Chamanzi mife wakimfuatilia mwalimu Sadiki Kizuki hayupo pichani, walipokuwa katika kituo cha Mpopoma, baadae  walielekea mto Nyebulu kisha kupanda Mlima wa Togwa lengo likiwa kujifunza  mambo mbalimbali.
Mwalimu Sadiki, mwenye  miwani akiwapa  somo  wanafunzi wa Chamanzi Mife.
Ukifika  Dar es Salaam Nature Study,  utakutana  na  mwalimu  huyu, mwalimuSadiki Kizuki mtaalam wa Jografia, Historia na elimu ya viumbe.

Saturday, July 30, 2016

LOLENS VIBES WAZINDUA CHOMBO MPYA, DAR BAGAMOYO

 Wazee wa kazi, kutoka kulia ni Dereva wa Kampuni ya Lolens Vibes, Issa Mondoma, wa pili kulia ni Kondakta wa kampuni hiyo, Muhsin Haji, wa kwanza  kushoto ni Mratibu wa safari za kampuni hiyo, Aly Mbond, na wa  pili  kushoto ni Konakta, Shabani Suleiman.

KAMATI ZA ULINZI NA USALAMA ZA WILAYA NNE ZATOKA NA MAAZIMO 10 BAGAMOYO, KUHUSU MSITU WA ZIGUA.

Mwenyekiti  wa Mkutano huo, ambae  ni Mkuu wa  wilaya ya Bagamoyo, Majid Hemed Mwanga.


Mkutano wa kamati za ulinzi na usalama za wilaya nne uliofanyika mjini Bagamoyo kuhusu wavamizi wa msitu wa Zigua, umetoka na maazimio 10, ambayo yanatakiwa kutekelezwa.

Mkutano huo uliozijumuisha kamati za ulinzi na usalama za wilaya nne ambazo ni Bagamoyo, Mvomero, Kilindi na Handeni, umefanyika mjini Bagamoyo ili kujadili namna ya kuwaondoa wavamizi waliovamia msitu wa Zigua.

Awali akiwasilisha mada mbele ya mkutano huo meneja wa Wakala  wa Misitu Tanzania TFS wilaya ya Bagamoyo, Charles Mwafute, alisema wameamua kushirikisha kamati za ulinzinausalama za wilaya hizo zinazopakana na hifadhi ya msitu wa Zigua ili kupata ushirikiano wakutosha katika kukabiliana na wavamizi.

Nae Mwenyekiti wa Mkutano huo Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Hemed Mwanga aliwataka viongozi wote katika wilaya hizo kuelimisha jamii juu ya utunzaji wa misitu ikiwa ni pamoja na kupanda miti mipya ili jamii iendelee kuwa na misitu.

Baada ya majadiliano mkutano huo umetoka na maazimio 10 ambayo yanatakiwa kutekelezwa kwa manufaa ya Taifa ili kuunusuru msitu wa Zigua nayo ni:

1.   Kuwaondoa wavamizi wote ndani ya  hifadhi  ya  msitu ifikapo Tarehe 30 Septemba 2016.

2.   Kila wilaya  itambue maeneo yaliyovamiwa.
3.   Mtu yeyote aliyeshiriki, au atakaeshiriki kugawa maeneo ndani ya Hifadhik achukuliwe hatua za  kisheria.

4.   Kuunda kikosi kazicha kufuatilia maeneo yaliyovamiwa na kutoa taarifa kamati.

5.   Kuanzisha Doria  za mara kwa mara  ndani ya hifadhi kwa wilaya zote nne  mara baada ya kuwatoa wavamizi.

6.   TFS, izingatie utoaji wa motisha kwa watakaoshiriki katika doria na watakaotoa taarifa  za wavamizi.

7.   Mipaka iendelee kuimarishwa kwa kushirikisha jamii inayozunguuka hifadhi.

8.   Kutoa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa hifadhi ya msitu kabla na baada ya kuwaondoa wavamizi.

9.   Katika  kuwaondoa  wavamizi sheria izingatiwe.
10.                Kuweka walinzi wa misitu baada  ya kuwaondoa wavamizi.
Mkuu wa wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe.
Mkuu wa wilaya  ya Mvomero, Mohamed  Utaly.
 
Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, Mwl. Sauda Mtondoo.


Friday, July 29, 2016

WILAYA NNE ZAKUTANA BAGAMOYO KUJADILI MSITU WA ZIGUA.

Wenyeviti wa kamati za ulinzi na usalama  za wilaya nne, kutoka kushoto ni Mkuu wa  wilaya ya  Handeni, Godwin Gondwe, wapili kushoto ni mkuu wa wilaya ya Kilindi, Mwl. Sauda Mtondoo, wa tatu ni Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, ambae ndiye Mwenyekiti  wa mkutanohuo, na  wa kwanza kulia  ni mkuu wa wilaya ya Mvomero.
Wajumbe wamkutano wa kamati za ulinzi na usalama za  wilaya nne ambazoni Bagamoyo, Mvomero, Kilindi,na Handeni,wakiwa  katika ukumbi wa Halmashauri ya Bagamoyo  
Wajumbe  wa mkutano wa kamati za ulinzi na usalama za wilaya nne wakifuatilia mkutano huo leo Tarehe 29 Julai 2016
Wajumbe wa mkutano huo wakiwa katika ukumbi wa Halmashauri ya Bagamoyo wakifuatilia mkutano
Meneja Wakala  wa Hifadhi za Misitu Tanzania TFS wilaya ya Bagamoyo, Charles  Mwafute, akiwasilisha mada katika mkutano  huo  wa  kujadili namna ya kuwaondoa  wavamizi wa msitu wa Zigua.
Katikati, ni Mwenyekiti wa mkutano huo mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Hemed Mwanga, kutoka  kushoto ni Mwenyekiti wa  Halmashauri ya Chalinze, Saidi Zikatimu, wa pili kushoto ni Mkuu wa wilaya  ya Handeni, Godwin Gondwe, wa  tatu ni Mkuu wa wilaya ya Kilindi, Sauda Mtondoo, Kutoka  kulia wakwanza ni Meneja waTFS kanda ya Mashariki, Dr. Masota  Abel, wa  pili kutoka kulia  ni Mwenyekiti  wa Halmashauri ya Bagamoyo, Aliy Aliy na wa watatu ni ni mkuu wa wilaya ya Mvomero, Mwl. Mohamed Utaly