Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega, akizungumza katika ufunguzi wa kikao kazi cha mkakati na kampeni ya kuhamasisha shughuli za ukuzaji viumbe vya baharini kwa viongozi na wataalam wa Mikoa ya Pwani na Dar es salaam kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Bagamoyo.
........................................................................
Na Athumani Shomari, Bagamoyo.
Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amewataka viongo mbalimbali wakiwemo wakuu wa Mikoa iliyopo ukanda wa Bahari ya hindi, kuwahamasisha wananchi ili watumie fursa za mazao ya bahari kujiongezea kipato.
Ulega ameyasema hayo mjini Bagamoyo leo February 24, 2022. Alipokuwa akifungua kikao kazi cha mkakati na kampeni ya kuhamasisha shughuli za ukuzaji viumbe vya baharini kwa viongozi na wataalam wa Mikoa ya Pwani na Dar es salaam kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Bagamoyo.
Amesema miongoni mwa vipaumbele vya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ni pamoja na uchumi wa Bluu ambacho ni kipaumbele cha nane, na kwamba utekelezaji wake ni kusaidia kufikia kwa malengo ya Rais kukuza uchumi kwa wananchi.
Alifafanua kuwa uchumi wa bluu ni pamoja na kutumia mazao ya Baharini ikiwemo ufugaji wa Majongoo Bahari, ufugaji wa Kaa na Kilimo cha Mwani, ambvyo vyote hivyo soko lake ni kubwa kimataifa licha ya kuwa watu wengi wa ukanda wa Pwani hawafahamu.
Aliongeza kuwa, lengo la wizara ni kuona wananchi wanazifahamu fursa zinazotokana na Bahari ili wazitumie ipasavyo na kuwataka wataalamu waendelee kutoa elimu ya ufugaji wa viumbe hao wa maji ya bahari kwa wananchi.
Alisema mkakati uliopo wa serikali ni kutoa fedha kwa vikundi vitakavyojishughulisha na mazao hayo ili waweze kutekeleza miradi hiyo kwa ufanisi na kujiongezea kipato huku kukiwa na elimu ya namna ya utunzaji wa mazingira ya Bahari.
Aliendelea kusema kuwa, fursa za uchumi wa bluu katika kipengele cha Bahari ni nyingi sana lakini zinahitaji maandalizi ya namna ya kuzitumia fursa hizo ambapo amewaeleza viongozi hao kuwa, miongoni mwa maandalizi hayo ni pamoja kuwapa elimu wananchi juu ya fursa hizo huku akiwataka kuwa na vikundi vitakavyokuwa na mipango madhubuti ya maendeleo.
Aliongeza kwa kusema kuwa, fedha za miradi hiyo zitakapokuwa tayari hawatapewa watu ambao hawakujiandaa kitaaluma na badala yake watapewa wale ambao wamepata elimu, wameunda kikundi na kuanza utekelezaji wa mfano.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakari Kunenge, akizungumza wakati wa kumkaribisha Naibu waziri, amewataka wataalamu walioajiriwa na serikali kutimiza wajibu wao kwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo huku wakitoa umuhimu kwenye vipaumbele vya Rais Samia Suluhu Hassan katika kufikia malengo ya serikali.
Alisema wataalamu wengi wamekuwa ni wakukaa ofisini wanashindwa kutekeleza majukumu yao kwa vitendo hali inayokatisha tama hata kwa wananchi wa kawaida huku akiwataka kubadilika ili waendane na kasi Rais Samia Suluhu Hassan.
Aliwataka washiriki wa kikao hicho kutoka na mikakati ya utekelezaji wa majukumu ilia waweze kufikia malengo ya kuondoa umasikini kwa wananchi, kuongeza mapato ya serikali ambayo yatapelekea kufikisha huduma bora kwa wananchi.
Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega, akiwasili katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Bagamoyo, akipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakari Kunenge, na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Zainab Abdallaah.
Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega, akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Bagamoyo, wanaofuata kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakari Kunenge, Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Muharami Mkenge, na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bagamoyo, Mohamed Usinga.
Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega, akizungumza katika ufunguzi wa kikao kazi cha mkakati na kampeni ya kuhamasisha shughuli za ukuzaji viumbe vya baharini kwa viongozi na wataalam wa Mikoa ya Pwani na Dar es salaam kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Bagamoyo.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakari Kunenge, akizungumza wakati wa kumkaribisha Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi katika kikao kazi cha mkakati na kampeni ya kuhamasisha shughuli za ukuzaji viumbe vya baharini kwa viongozi na wataalam wa Mikoa ya Pwani na Dar es salaam kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Bagamoyo. kushoto ni Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega, na kulia ni Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Muharami Mkenge, na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bagamoyo, Mohamed Usinga.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Zainab Abdallaah
akizungumza wakati wa kumkaribisha Mkuu wa Mkoa waPwani, kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Bagamoyo, Shauri Selenda.
Washiriki katika kikao kazi hicho ni viongozi kutoka Dar es salaam na Pwani wakiwa katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Bagamoyo mkoani Pwani.
Washiriki katika kikao kazi hicho ni viongozi kutoka Dar es salaam na Pwani wakiwa katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Bagamoyo mkoani Pwani.
Naibu waziri
wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega, (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Madiwani wa Halmashauri ya Bagamoyo na watendaji kata, kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bagamoyo, Mohamed Usinga, Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Zainab Abdallaah, kutoka kulia ni Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Muharami Mkenge, na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Bagamoyo, Shauri Selenda.
Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega, akiwa katika picha ya pamoja na maafisa uvuvi, kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bagamoyo, Mohamed Usinga, Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Zainab Abdallaah, kutoka kulia ni Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Muharami Mkenge, na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Bagamoyo, Shauri Selenda.
No comments:
Post a Comment