Saturday, February 26, 2022

ULEGA ATAKA VIKUNDI VYA BAGAMOYO VIKOPESHWE FEDHA ZA HALMASHAURI, KWA KUTUMIA VIZURI FURSA YA UCHUMI WA BLUU.

 No description available.

Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega, akizungumza na wana kikundi cha ufugaji wa Majongoo Bahari kilichopo Kaole kata ya Dunda Halmashauri ya Bagamoyo, kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Muharami Mkenge.

................................................ 

Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bagamoyo, kuvipatia fedha vikundi viwili vilivyopo Bagamoyo ambavyo vinajishughulisha na ufugaji wa Majongoo Bahari na kilimo cha Mwani.

Ulega ametoa agizo hilo Tarehe 25 Februari 2022 alipotembelea vikundi hivyo ili kujionea shughuli zinazofanywa na vikundi hivyo.

Naibu waziri huyo alifika Bagamoyo kufungua  kikao kazi cha mkakati na kampeni ya kuhamasisha shughuli za ukuzaji viumbe Bahari ambacho kilijumuisha wataalamu kutoka mikoa ya Dar es salaam na Pwani lengo likiwa ni kutoa elimu juu ya fursa zilizopo kwenye uchumi wa bluu ambao unjumuisha mazao ya Bahari ikiwemo ufugaji wa Majongoo Bahari, Ufugaji wa Kaa, ukuzaji wa Kamba kochi na kilimo cha mwani.

Kikao kazi hicho kilijumuisha kutembelea vikundi vilivyopo Kaole na Mlingotini ambavyo tayari vinatumia fursa ya uchumi wa bluu kwa kutekeleza ufugaji wa majongoo Bahari na kilimo cha mwani.

Kufuatia kazi nzuri alizoziona Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bagamoyo, kuwapatia fedha za Halmashauri zilizotengwa kwaajili ya vikundi ili waweze kuzitumia kuendesha miradi yao.

Alisema serikali inapotoa fedha inapenda kujiridhisha juu ya utendaji kazi wa hicho kikundi ambapo kwa kikundi cha ufugaji Majongoo Bahari cha Kaole tayari kimeonyesha juhudi kwa kufanya kazi inyoonekana pamoja na kikundi cha Msichoke cha Mlingotini kinachojishughulisha na kilimo cha mwani pamoja na utengezaji wa bidhaa mbalimbali.

Wakati huo huo amemuomba mbunge wa Jimbo la Bagamoyo Muharami Mkenge kuwasaidia kufuatilia upatikanaji wa nembo ya tbs kwaajili ya bidhaa wanazozalisha ili waweze kutafuta masoko nchi nzima na nje ya nchi.

Pia amemuagiza Mkurugenzi wa Benki ya Kilimo kurudi Bagamoyo baada ya wiki moja ili kuwasikiliza wana vikundi hao na kuwapa ushauri wa kitaalamu na baadae kuwakopesha fedha ambazo zitatua changamoto zao.

Awali kikundi cha ufugaji majongoo bahari cha kaole kimesema kinabiliwa na changamoto ya wizi wa majongoo hivyo wanaomba kupatiwa Boti itakayowasaidia kufanya doria eneo la mradi, huku kikundi cha Msichoke cha Mlingotini nacho kimesema wanahitaji fedha zitakazowaongezea kupata mashine ya kukaushia Mwani na kusindika, pamoja na boti itakayowasidia katika shughuli za ulimaji wa mwani hasa pale maji yanapojaa.

Vikundi vyote hivyo vimeishukuru serikali ya wilaya kwa kuwapa ushirikiano wa karibu ili kufanikisha kazi zao.

No description available.

Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega, akiwa ameshika jongoo bahari wanaofugwa na kikundi cha ufugaji wa majongoo bahari kilichopo Kaole kata ya Dunda Halmashauri ya Bagamoyo.

No description available.

Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega, akisikilza taarifa ya kikundi cha ufugaji wa majongoo bahari kilichopo Kaole kata ya Dunda Halmashauri ya Bagamoyo.

No description available.

Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega, akiwa anakunywa juisi ya Mwani iliyotengenezwa na kikundi cha Msichoke kilichopo kijiji cha Mlingotini kata ya Zinga Halmashauri ya Bagamoyo, Kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, na kulia ni Katibu mwenezi wa CCM wilaya ya Bagamoyo, John Francis (Bolizozo)

No description available.

Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega, akizungumza na wana kikundi cha Msichoke ambacho kinaajishughulisha na kilimo cha Mwani na utengenezaji wa bidhaa zinazotokana na zao la Mwani.

No description available.No description available.

Hizi ni baadhi ya bidhaa zinazotokana na zao Mwani, ambazo zinatenezwa na kikundi cha Msichoke kilichopo kijiji cha Mlingotini kata ya Zinga Halmashauri ya Bagamoyo.

 

No comments:

Post a Comment