Friday, June 8, 2018

WAFICHUENI WANAOWAPA MIMBA WANAFUNZI.

Wanafunzi wa shule za Bagamoyo wakiwa kwenye maandamano kuadhimisha wiki ya Elimu.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) Alphonce Amuli, akiongea kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo.
.....................................
Wazazi na walezi wilayani Bagamoyo wametakiwa kutoa ushirikiano ili kuwafichua wale wote wanaowapa mimba wanafunzi.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga katika hutuba iliyosomwa kwa niaba yake na Kaimu Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) Alphonce Amuli wakati wa maadhimisho ya wiki ya Elimu.

Alisema watoto wengi hukatisha masomo kwasababu ya kupewa mimba lakini juhudi za kukomesha vitendo hivyo zinakwama kutokana na wazazi au walezi kutotoa ushirikiano kwa vyombo vya sheria ili hatua kali zichukuliwe dhidi yao.

Aliongeza kwa kusema kuwa serikali imetunga sheria kali katika kuhakikisha vitendo vya kuwapa mimba wananfunzi vinakomeshwa ili watoto wa kike wapate elimu ambayo ni haki yao ya kikatiba.

Akizungumzia swala la elimu Amuli alisema kufuatia viwanda vinavyoendelea kujengwa wilayani Bagamoyo watoto wanapaswa kupewa elimu itakayowanufaisha katika soko la ajira na ile ya kujiajiri.

Aidha, alisema serikali kwa kutambua umuhimu wa elimu inatoa elimu bure kwa wote na kutoa fedha zitakazosadia upatikanaji wa elimu bure ili kila mtoto apate elimu.

Aliongeza kuwa walimu wakuu wanapaswa kusimamia vizuri fedha za elimu bure ikiwa ni pamoja na kuzipeleka kwenye matumizi stahiki ili lengo la serikali liweze kutimia.

Alisema kufuatia hali hiyo wazazi na walezi jukumu lao ni kuwapeleka watoto shule na kuwasimamia ipasavyo.

Awali akisoma Taarifa ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bagamoyo, Afisa Elimu Msingi Peter Fussi alisema kufuatia utoaji wa elimu bure idadi ya wanafunzi  wanaoandikishwa shule za awali na msingi imeongezeka kutoka wanafunzi 25228 mwaka 2017 na kufikia 27508 mwaka 2018.

Hata hivyo fussi alisema Halmashauri ya Bagamoyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa vyumba vya madarasa ambapo mahitaji  katika idara ya elimu ya msingi ni vyumba 621 na kwamba vilivyopo ni 292 na hivyo kufanya upungufu wa vyumba vya madarasa ni 329.

Aliongeza kuwa idara ya elimu sekondari mahitaji ni vyumba vya madarasa 162 yaliyopo ni madarasa 124 ambapo pungufu ni madarasa 38.

Wiki ya elimu huadhimishwa kila mwaka ikiwa na lengo la kutoa fursa kwa shule, serikali na wadau mbalimbali kutathmini changamoto zilizopo na kuzitafutia ufumbuzi.

Kauli mbiu ya mwaka huu ni  Uwajibikaji wa pamoja kwa elimu bora kwa watu wote.
 
 Kaimu Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) Alphonce Amuli akipokea maandamano ya wanafunzi yalipowasili uwanjani.
 Wanafunzi wa Chuo cha Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM)wakiongoza maandamano katika maadhimisho ya wiki ya elimu yaliyofanyika uwanja wa majengo Bagamoyo.
Mgeni rasmi katika maadhimisho ya wiki ya elimu yaliyofanyika Bagamoyo Alphonce Amuli akikagua mabanda yaliyoandaliwa na shule mbalimbali kama anavyoonekana pichani akiwa katika banda la shule ya msingi Nianjema ambapo alijionea Teknolojia ya habari na namna ya masomo mengine yanavyofundishwa.

Alphoncee Amuli ni kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu ( ADEM) ambae alimuwakilisha Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga.
 
Mgeni rasmi katika maadhimisho ya wiki ya elimu yaliyofanyika Bagamoyo Alphonce Amuli akikagua mabanda yaliyoandaliwa na shule mbalimbali kama anavyoonekana pichani ambapo alijionea namna ya masomo yanavyofundishwa.


Alphonce Amuli ni kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu ( ADEM) ambae alimuwakilisha Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga.
Mgeni rasmi katika maadhimisho ya wiki ya elimu yaliyofanyika Bagamoyo Alphonce Amuli akikagua mabanda yaliyoandaliwa na shule mbalimbali kama anavyoonekana pichani ambapo akiwa katika banda la ADEM ambapo alijionea namna ya masomo yanavyofundishwa.

Alphonce Amuli ni kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu ( ADEM) ambae alimuwakilisha Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga
Sehemu ya wananfunzi walioshiriki maadhimisho hayo ya wiki ya elimu.
Wanafunzi wa shule ya Mwanamakuka wakionyesha umahiri wao katika maonyesho ya sarakasi

No comments:

Post a Comment