Kaimu
meneja wa TFS Chalinze Jonathan Mpangala (katikati) akiwaonyesha wajumbe wa kamati siasa wilaya ya Bagamoyo mipaka ya msitu wa Zigua katika kijiji cha kwa Mduma.
..........................................
Serikali
wilayani Bagamoyo imepokea ombi la wnanchi katika kijiji cha Kwa Mduma kata ya
Kibindu la kutaka kuongezewa eneo la makazi kutoka msitu wa Zigua.
Kauli
hiyo imetolew na Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga wakati wa ziara ya
kukagua mipaka ya Msitu wa Zigua.
Mkuu
huyo wa wilaya alisema lengo la ziara hiyo ambayo imewajumuisha kamati ya siasa
wilaya ni kupata uelewa wa pamoja kuhusu hitajio la wananchi wa kwa Mduma na
kuona namna gani wanaweza kuwasilisha maombi ya wananchi hao ngazi za juu.
Alisema
kufuatia ukweli kwamba sehemu wanayodai ni muhimu kwakuwa tayari kuna zahanati
ambayo inawahudumia wananchi hao, serikali ya wilaya inachukua ombi hilo na kuwasilisha kw
Mkuu wa Mkoa ili kuona namna ya kurekebisha mipaka ya TFS katika kijiji hicho.
Kaimu
meneja wa TFS Chalinze Jonathan Mpangala lisema
katika harakati za kuondoa wavamizi ndani ya msitu wa zigua zipo baadhi
nyumba kijiji cha kwa Mduma hazikubomolewa kutokana na kusikiliza maoni ya
wananchi wa kijiji hicho.
Alisema
nyumba hizo ni pamoja Zahanati, nyumba ya Mganga na nyumb 8 za watu binafsi
ambapo vikao vimefanyika ngazi ya wilaya ili kuona namna kurekebisha mipaka
upande huo wa kijiji cha kwa mduma.
Aliongeza
mchakato unaendelea kuanzia ngazi ya kijiji, wilaya nakanda ambapo ofisi ya
kanda itawasilisha mapendekezo hayo ngazi Taifa.
Nae
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Bagamoyo Abdu Rashid Zahoro amesema Chama cha
Mapinduzi wilaya kitashirikiana na serikali kuona namna bora ya kurekebisha
mipaka ya msitu huo.
Alisema
CCM wilaya imejionea hali halisi ya malalamiko ya wananchi hao na kwamba
wameona haja ya kuwashughulikia malalamiko yao
ili eneo hilo libaki kwa makazi ya watu na
shughuli za kibinadamu kama watakavyoona
inafaa serikali ya kijiji.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Bagamoyo Abdu Rashid Zahoro akizungumza na wananchi wa kijiji cha kwa Mduma.
Kaimu meneja wa TFS Chalinze Jonathan Mpangala (katikati) akiwaonyesha wajumbe wa kamati siasa wilaya ya Bagamoyo ramani ya msitu wa Zigua katika kijiji cha kwa Mduma.
Wajumbe
wa kamati siasa wilaya ya Bagamoyo wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM wilaya, wakati walipotembelea msitu wa Zigua katika
kijiji cha kwa Mduma.
Kaimu
meneja wa TFS Chalinze Jonathan Mpangala (wa pili kushoto) akiwaonyesha wajumbe
wa kamati siasa wilaya ya Bagamoyo mipaka ya msitu wa Zigua katika
kijiji cha kwa Mduma.
No comments:
Post a Comment