Sehemu
ya washiriki wa UMITASHUMTA wa Halmashauri ya Chalinze.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid Mwangaakizungumza wakati wa uzinduzi wa UMITASHUMTA wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze Said Omari Zikatimu, wa tatu ni Afisa Elimu msingi Zainabu Makwinya na wa mwisho ni Afisa Elimu Taaluma Miriam Kihiyo.
................................................
Majid
aliyasema hayo wakatai wa uzinduzi wa mashindano ya Uendeshai wa Michezo ya Taaluma Shule za
Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) uliofanyika katika viwanja vya shule ya Lugoba
Halmashauri ya Chalinze.
Alisema
michezo inaibua vipaji kwa watoto lakini ni vyema vipaji hivyo vikatumika
sambamba na elimu kwani mwenye elimu hutumia vizuri kipai chake.
Aidha
aliwataka walimu kuwasimamia watoto mashuleni katika kuhakikisha wanapata elimu
bora sambamba na kudumisha michezo ambayo itawajenga ki afya na ukakamavu wa
miili yao.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chalinze Edes Lukoa amewataka
vijana wa shule za msingi kuwa na bidii katika michezo ili kukuza vipaji vyao
kwaaili ya maendeleo ya baadae.
Alisema
wachezaji wakubwa wa michezo mbalimbali duniani wameanza wakiwa wadogo hivyo na
wao wasikate tamaa na badala yake waongeze juhudi.
Aidha,
aliwataka kuwa na nidhamu kwa walimu wao ili waweze kuelewa kile
wananchofundishwa na hatimae kufaulu vizuri katika masomo yao pamoja na michezo.
Awali
akisoma Taarifa mbele ya mgeni rasmi Afisa Elimu Taaluma Halmashauri ya
Chalinze Miriam Kihiyo alisema Halmashauri ya Chalinze itatoa timu moja
itakayoshiriki katika mashindano ya kumtafuta mshindi wa Mkoa.
Alisema
michezo itakayoshindaniwa ni Mpira wa miguu, Mpira wa pete, Mpira wa Mikono na
Mpira wa wavu.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze Saidi Omari Zikatimu akizungumza katika uzinduzi wa UMITASHUMTA.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chalinze Edes Lukoa akizungumza katika uzinduzi wa UMITASHUMTA.
Afisa Elimu Taaluma wa Halmashauri ya Chalinze Miriam Kihiyo akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Risala.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chalinze Edes Lukoa akiwa gorini kwaajili ya kudaka mpira kuashiria uzinduzi wa UMITASHUMTA katika Halmashauri ya hiyo.
Vijana
kutoka timu ya Msata na Chalinze wakichuana katika mechi ya ufunguzi
iliyofanyika katika viwanja vya shule ya Lugoba.
No comments:
Post a Comment