Ofisi
ya Msajili wa Jumuia za Kidini na Vyama vya Kijamii Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, inazikumbusha Taasisi zote za Kidini na Vyama vya Kijamii vilivyosajiliwa
na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kulipa Ada na Madeni waliyonayo kabla ya tarehe
30/6/2018.
Sheria
ya Jumuia, Sura ya 337 iliyofanyiwa mapitio mwaka 2002 (The Societies Act)
inayozisajili Jumuia za Kidini na Vyama vya Kijamii inawataka wote
waliosajiliwa kulipa ada zao za kila mwaka kwani kutokulipa ada ni kukiuka
masharti ya Sheria iliyowasajili.
Jumuia
za Kidini na Vyama vya Kijamii vinatakiwa kufika kwenye Ofisi za Msajili wa
Vyama vya Kijamii na Taasisi za Kidini ili kuhakiki madeni yao hivyo kuwawezesha kulipa madeni stahiki
wanayodaiwa pamoja na ada zao za mwaka huu wa fedha.
Uhakiki
wa madeni hayo utahusisha nyaraka mbalimbali kama
vile risiti ya mwisho ya malipo, nakala ya Cheti cha Usajili na Taarifa ya
Utendaji yenye saini za Viongozi wawili.
Malipo
yote yawasilishwe kupitia benki ya NMB Akaunti namba 20110013811 yenye jina
MOHA REVENUE COLLECTION.
No comments:
Post a Comment