Posts

MWENGE WA UHURU, WAZINDUA NA KUTEMBELEA MIRADI YA MILIONI 900. BUKOBA

Image
  MWENGE WA UHURU, WAZINDUA NA KUTEMBELEA MIRADI YA MILIONI 900. BUKOBA Alodia Dominick,  Bukoba Mwenge wa uhuru umezindua, kuweka mawe ya msingi na kutembelea miradi saba yenye thamani ya sh. milioni 900 katika Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera. Mwenge wa Uhuru umewasili Manispaa ya Bukoba Augosti 31, 2026 ukitokea katika wilaya ya Muleba. Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Wazo Mwang'onda akiwa Manispaa ya Bukoba amesisitiza wananchi kuilinda amani, umoja na mshikamano kwani pasipo amani hakuna miradi ya maendeleo inayoweza kutekelezwa. "Ni wajibu wetu wananchi wa Taifa hili kuilinda amani ya nchi yetu chini ya kauli mbiu isemayo Tanzania ni yetu sote tushikamane kuleta maendeleo sambamba na hiyo inatukumbushwa mapambano dhidi ya rushwa, madawa ya kulevya,  mapambano dhidi ya virusi vya ukimwi na mapambano dhidi ya maralia" amesema Mwang'onda  Ameeleza kuwa, ujumbe huo unawataka wananchi kuendelea kulinda amani na utulivu uliohasisiwa na viongozi wa nchi hi...

MAKAMU WA RAIS, ATEMBELEA OFISI YA MAKAMU WA RAIS MUUNGANO NA MAZINGIRA

Image
  MAKAMU WA RAIS, ATEMBELEA OFISI YA MAKAMU WA RAIS MUUNGANO NA MAZINGIRA AWATAKA WATUMISHI KUACHA KUFANYA KAZI KWA MAZOEA     Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, amewataka watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira kuongeza bidii, uwajibikaji na kuachana na utendaji wa kazi kwa mazoea ili kuhakikisha majukumu ya Serikali yanatekelezwa kwa ufanisi na kwa wakati.   Makamu wa Rais ametoa wito huo leo, alipofanya ziara yake ya kwanza katika Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), iliyopo Mtumba, jijini Dodoma, ambako alipokelewa na wafanyakazi pamoja na Menejimenti ya Wizara hiyo.   Amesisitiza umuhimu wa watumishi kubadili mitazamo na namna ya kufanya kazi, akitaka kila mmoja kuwa mbunifu na kuweka mipango inayolenga kuleta matokeo yanayoonekana kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.   Makamu wa Rais amewasihi watumishi kutumia nafasi zao kutoa huduma yenye thamani kwa watanzania na kutambua dhaman...

MAGAZETI YA TANZANIA LEO JUMATATU TAREHE 31 AGOSTI 2026

Image
 

MANISPAA TABORA KULIPA MIL 27 ZA BODI YA MIKOPO

Image
 MANISPAA TABORA KULIPA MIL 27 ZA BODI YA MIKOPO Na Allan Kitwe, Tabora HALMASHAURI ya manispaa Tabora imetenga jumla ya shilingi milioni 27 kwa ajili ya kuwalipia watumishi wake waliosoma vyuo vikuu kwa fedha za mkopo wa Bodi ya Elimu ya Juu (HELB) kabla ya kuajiriwa. Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya manispaa hiyo Dkt John Pima alipokuwa akitoa taarifa ya hesabu za mwisho (final accounts) kwenye kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri hiyo  Amesema kuwa halmashauri imetenga kiasi hicho katika bajeti yake ya mwaka huu ili kuwezesha watumishi wake walionufaika na mkopo wa serikali unaotolewa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HELB) kurejesha mikopo yao kwa wakati. ‘Haya ni maelekezo ya serikali kwa waajiri wote nchini kuhakikisha wanatambua watumishi wao waliosoma kwa fedha za mkopo wa bodi hiyo na kurejesha sehemu ya mikopo yao kila mwaka’, ameeleza.   Dkt Pima amedokeza kuwa wamekuwa wakifanya hivyo kila mwaka ili kuhakikisha kila mtumish...

MAGAZETI YA TANZANIA LEO JUMAPILI TAREHE 30 AGOSTI 2026

Image
 

OFISI YA RAIS, UTUMISHI NA UTAWALA BORA, YAMPONGEZA NDEJEMBI.

Image
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,  Mhe.  Rdhiwani Kikwete na Ofisi yake, wampongeza Mhe. Deogratius John Ndejembi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kuteuliwa kwake kuwa Makamu wa Rais na kuandika ujumbe huu. Salamu nyingi za pongezi na Dua njema toka kwangu Binafsi na Menejiment nzima ya Ofisi ya Rais , Utumishi na Utawala Bora  kuja kwako Mh. Deo Ndejembi, Makamu wa Rais wa JMT katika siku hii muhimu Unapoapa kuanza kazi kubwa ya kuisaidia Nchi yako na kumsaidia Mh. Rais kutimiza ahadi zake za Ilani kwa Watanzania. Ahadi yetu ni ushirikiano mkubwa na kuchapa Kazi kwa kiwango kikubwa sana. Kazi na utu Tunasonga mbele Kazi iendelee

GLOBAL YASAFIRISHA KUNDI LINGINE LA WANAFUNZI KWENDA NJE YA NCHI.

Image
  GLOBAL YASAFIRISHA KUNDI LINGINE LA WANAFUNZI KWENDA NJE YA NCHI. Na  Mwandishi wetu. KUNDI lingine la mamia ya wanafunzi  wa Kitanzania wameondoka nchini Jumamosi kuelekea vyuo vikuu mbalimbali kuanza masomo ya elimu ya juu kupitia Global Education Link (GEL). Wanafunzi hao walioondoka jana kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Terminal 3, jijini Dar es Salaam, wengi wao wamechagua programu zinazohusiana na sayansi, teknolojia na taaluma zinazohitajika katika dunia ya sasa, zikiwemo Computer Engineering, Cyber Security, Artificial Intelligence, Civil Engineering, programu mbalimbali za afya, sheria na biashara. Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education Link, Meneja wa Tawi la Dar es Salaam, Micky Musa, amesema kuondoka kwa wanafunzi hao ni sehemu ya mpango mpana wa kuwaunganisha vijana wa Tanzania na fursa za elimu ya kimataifa. Alisema mbali na India, Global Education Link inaendelea kuwaandaa wanafunzi wengine wanaotarajiwa ku...