MWENGE WA UHURU, WAZINDUA NA KUTEMBELEA MIRADI YA MILIONI 900. BUKOBA
MWENGE WA UHURU, WAZINDUA NA KUTEMBELEA MIRADI YA MILIONI 900. BUKOBA Alodia Dominick, Bukoba Mwenge wa uhuru umezindua, kuweka mawe ya msingi na kutembelea miradi saba yenye thamani ya sh. milioni 900 katika Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera. Mwenge wa Uhuru umewasili Manispaa ya Bukoba Augosti 31, 2026 ukitokea katika wilaya ya Muleba. Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Wazo Mwang'onda akiwa Manispaa ya Bukoba amesisitiza wananchi kuilinda amani, umoja na mshikamano kwani pasipo amani hakuna miradi ya maendeleo inayoweza kutekelezwa. "Ni wajibu wetu wananchi wa Taifa hili kuilinda amani ya nchi yetu chini ya kauli mbiu isemayo Tanzania ni yetu sote tushikamane kuleta maendeleo sambamba na hiyo inatukumbushwa mapambano dhidi ya rushwa, madawa ya kulevya, mapambano dhidi ya virusi vya ukimwi na mapambano dhidi ya maralia" amesema Mwang'onda Ameeleza kuwa, ujumbe huo unawataka wananchi kuendelea kulinda amani na utulivu uliohasisiwa na viongozi wa nchi hi...