NAIBU WAZIRI WA NISAHATI AKAGUA MITAMBO YA UMEME ITAKAYOFUNGWA MTWARQ
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amekagua mitambo miwili ya umeme yenye uwezo wa kuzalisha megawati 2 kila mmoja itakayofungwa katika kituo cha kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia cha Mtwara. Amekagua mitambo hiyo tarehe 21 Februari, 2018 katika eneo la Mkandarasi, jijini Dar es Salaam ambapo kampuni ya Mantrac ndiyo iliyopewa kazi ya kufunga mitambo hiyo. Baada ya kukagua mitambo hiyo, Naibu Waziri alisisitiza kuwa, Serikali inafuatilia kwa karibu utekelezaji wa kazi hiyo lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa mitambo hiyo inafikishwa na kusimikwa mkoani Mtwara mapema iwezekanavyo ili kuboresha hali ya upatikanaji wa umeme katika mkoa wa Mtwara pamoja na Lindi. Kabla ya kukagua mitambo hiyo, Naibu Waziri Mgalu alifanya kikao na watendaji wa kampuni hiyo ya Mantrac pamoja na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) lengo likiwa ni kufahamu maendeleo ya kazi hiyo. Akizungumza katika kikao hicho, Mkurugenzi Mtendaji wa Mantrac, Ahmed Saleh alimweleza...