Wednesday, August 23, 2023

CHALINZE WAPOKEA GARI LA ZIMAMOTO

 

Halmashauri ya Chalinze wamepokea gari la Zimamoto na Uokoaji kwaajili ya kukabiliana na majanga ya moto mara tu yanapotokea  wilayani humo toka kwa Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ( SSF) Jenifa Shirima.

Akiongea kwa niaba ya wananchi wa Chalinze, Mbunge wa jimbo la Chalinze Ndg. Ridhiwani Kikwete amemshukuru Mrakibu mwandamizi kwa niaba ya serikali kwa kuona kuwa katika mipango ya serikali Chalinze nayo iwe moja ya maeneo ya kipaumbele katika uhitaji wa gari hilo.

Mbunge alikumbusha kilio cha muda mrefu cha wananchi wa Chalinze na majanga yaliyo wahi kuwakuta na ujio wa gari hili ni ukombozi mkubwa.

Akizungumza kabla ya kumkabidhi Mbunge wa jimbo hilo, Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la zimamoto na uokoaji (SSF)Jenifa alimpongeza Mbunge kwa kuwasemea wananchi wake na gari hili ni utekelezaji wa maombi ya Mbunge na Naibu Waziri Kikwete.

Mrakibu Mwandamizi huyo alimuahidi Mbunge kuendelea kutatua kero za zimamoto katika halmashauri zote mkoa na kwamba pia kumshukuru Mkurugenzi mtendaji wa Chalinze kwa kuwapatia Kiwanja ambacho watajenga Jengo la zimamoto la wilaya na ofisi zao.

Pia alimuhakikishia Mbunge kuwa serikali inajipanga kwa ajili ya ujio wa gari kubwa wilaya hiyo.

Wananchi wa Chalinze kwa jumla yao wameishukuru Serikali kwa kutatua kero hii ya muda mrefu na kuahidi kulitunza Gari hilo.









DHAHABU YA BILIONI 9 YAKAMATWA SHINYANGA.

 


Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limekamata mawe yenye madini ya dhahabu yenye uzito wa gramu 6753.4 na thamani ya Tsh. Bilioni 9 yakitoroshwa kutoka kwenye mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu wilayani Kahama huku pia likikamata Carbon yenye mchanga wenye madini yadhaniwayo kuwa ni dhahabu yenye uzito wa kg 261 ambayo thamani yake bado haijajulikana katika maeneo ya Manzese Kahama.


Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo Jumatano Agosti 23,2023 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Janeth Magomi amesema mali hizo zimekamatwa kwa kipindi cha kuanzia tarehe 26/07/2023 hadi tarehe 22/08/2023 baada ya kufanya misako na doria katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Shinyanga.


“Pia tumekamata jumla ya lita 603 za mafuta aina ya Diesel katika maeneo tofauti ya mradi wa Reli ya mwendokasi SGR. Mafuta haya yamewekwa kwenye chupa ndogo, wezi wa mafuta sasa hivi wamebuni mbinu ya kutumia vichupa badala ya madumu makubwa”,amesema Kamanda Magomi.

Amesema , katika misako hiyo Jeshi la polisi Shinyanga pia limefanikiwa kukamata Bunduki aina ya Riffle yenye namba 2/49PF78701 ambayo ilikuwa inatumika katika shughuli za ulinzi bila kibali.

Vitu vingine vilivyokamatwa na jeshi la polisi ni madawa ya kulevya aina ya Bangi yenye uzito wa Kg 71, seti moja ya computer, Pikipiki 03, tiles Box 14, mabomba 06 ya chuma na vipande 09, Mabati 17, Plastic 3 za rangi ya majumba, mifuko 02 ya Cement, mifuko 7 ya chokaa, pamoja na Packet 120 za vipodozi vinavyoaminika kuwa na sumu.

Kamanda Magomi amesema, jumla ya watuhumiwa 31 wanashikiliwa katika vituo mbalimbali vya Polisi kuhusiana na makosa hayo na wengine wamepewa dhamana huku wakisubiri kufikishwa mahakamani.


Kwa upande wa mafanikio mahakamani,Kamanda Magomi ameeleza kuwa jumla ya kesi 34 zilipata mafanikio mahakamani ambapo kesi 5 za kubaka zilihukumiwa vifungo kati ya miaka 30 na pia kifungo cha nje miezi 12 kwa kesi za watoto (juvenile), kesi 01 ya kulawiti ilihukumiwa kifungo cha maisha Jela, kesi 02 za uvunjaji zilihukumiwa vifungo vya miezi 6, kesi 03 za ukatili kwa watoto zilihukumiwa vifungo vya miaka 05 jela, kesi 01 ya kusafirisha madawa ilihukumiwa kutumikia jamii kwa miaka 03, kesi 05 za wizi zilihukumiwa vifungo vya miezi 06 hadi mwaka 01 jela, kesi 01 ya kumtorosha mwanafunzi ilihukumiwa kifungo cha miaka 03 jela, kesi moja ya kuharibu mali ilihukumiwa kifungo cha mwaka 01 jela na kesi 01 ya kukiuka masharti ya leseni ya biashara ilihukumiwa faini ya Tsh. 500,000/=.

Kwa upande wa usalama barabarani, amesema jumla ya makosa 4017 yalikamatwa ambapo magari 3084 yalikamatwa kwa makosa mbalimbali ikiwemo kutokuwa na leseni 07, kutokuwa na Bima 179, Mwendokasi 637, kuzidisha abiria 422 na makosa mengine madogomadogo ni 588.


“Makosa ya pikipiki yalikuwa 933 ambapo kutokuwa na leseni 228, kutokuwa na Bima 164, kuzidisha abiria 121, kuendesha pikipiki bila kofia ngumu 229, kuendesha pikipiki mbovu 64, na makosa mengine ya pikipiki ni 127”,amesema Kamanda Magomi.


“Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga linapenda kuwaasa wananchi wote kwa ujumla kufuata sheria za nchi na pia kutoa ushirikiano kwa Jeshi ili kudumisha amani na utulivu uliopo”,ameongeza Kamanda Magomi.














MCHENGERWA, WABUNGE WAONGOZA MAMIA MAMIA YA WAGENI TUKIO LA SERENGETI GRAND MIGRATION.

 

Waziri wa Maliasili na Utalii, *Mhe. Mohamed Mchengerwa,* wageni kutoka sehemu mbalimbali duniani kushuhudia tukio la kihistoria la kuhama kwa Wanyama (Nyumbu) kwenye eneo la Kogatende katika mbuga ya Serengeti.


Katika tukio hilo lililodumu kwa zaidi ya masaa mawili Nyumbu zaidi ya elfu kumi wakisindikizwa na mamia ya pundamilia na baadhi ya Tembo wamevuka mto Masai Mara kutoka upande wa Kenya kuja Tanzania. 


Pamoja na Waziri wa Utalii Mhe. Mohammed Mchengerwa, pia walikuwepo viongozi wengine ambazo ni Naibu wake, Mary Masanja, Katibu Mkuu, Dkt. Hassan Abbasi na Naibu Katibu Mkuu Benedict Wakulyamba, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mhe Timotheo Mnzava ambae aliongoza baadhi ya wajumbe wa Kamati hiyo kushuhudia tukio hilo la kihistoria na kubaki wakishangazwa na maajabu hayo. 


“Ndio tumeanza kutekeleza mikakati kabambe ya kuutangaza utalii wetu. Tukio hili ni la kihistoria na huwezi kulikuta popote duniani; ujio wetu hapa ni kulipia tukio hili heshima na kulitangaza zaidi duniani,” alisema Waziri Mchengerwa. 


Akitoa hotuba mara baada ya kushuhudia makundi makubwa ya nyumbu kuvuka mto Mara Waziri Mchengera amesema sekta ya utalii ni miongoni mwa nguzo muhimu katika uchumi na maendeleo ya nchi ya kutokana na mchango wake katika pato la Taifa,


Amesema sekta hiyo huchangia zaidi ya asilimia 17 ya pato la Taifa (GDP) na takriban ajira milioni 1.5 za moja kwa moja na ambazo si za moja kwa moja na amefafanua kwamba Sekta ya Utalii nchini imevunja rekodi mwaka wa fedha 2022/2023 kwa ongezeko ambalo halijawai kutokea. 


Amesema takwimu zinaonesha kipindi cha mwaka wa fedha 2022/2023 Tanzania ilipata jumla ya watalii 1,638,850 walioingizia taifa jumla ya shilingi bilioni 522.7 ikilinganishwa na watalii 1,123,130 walioingizia taifa shilingi bilioni 290.4 mwaka wa fedha 2021/2022. 


Hii ni sawa na ongezeko la asilimia 45.9 ya watalii na mapato asilimia 80, amesema na kuongeza kuwa lipo ongezeko kubwa la watalii na mapato kwa kipindi cha Januari hadi Juni, 2022/2023 ukilinganisha na kipindi kama hicho 2020/2021. Kutoka 575,397 na mapato ya shilingi bilioni 130,592,796,544 Januari hadi June, 2022 hadi kufikia watalii 759,327 na mapato shilingi bilioni 202,375,961,009 Januari hadi Juni, 2023.


Ameongeza kuwa Watalii wote waliokuja nchini Mwaka wa fedha 2022/2023 asilimia 37.6 walitoka nchi kumi za bara la Ulaya, Amerika na Asia ukilinganisha na asilimia 31 ya watalii waliofika nchini kutoka nchi hizo kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2021/2022. Watalii kutoka Marekani (118,108) waliongoza mwaka wa fedha 2022/2023 wakati watalii kutoka Ufaransa (76,084) waliongoza kwa mwaka wa fedha 2021/2022. 


Amefafanua kuwa ukuaji huu unatokana na juhudi za kutangaza Utalii kupitia Filamu ya Tanzania the Royal Tour iliyoasisiwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na mikakati mbalimbali iliyowekwa na Wizara ya Maliasili na Utalii ambapo amesisitiza kuwa pamoja na mambo mengine, Mikakati hiyo imewezesha Tanzania kuchaguliwa na Shirika la Utalii Duniani (UNWTO) kuwa Makamu wa Rais Baraza Kuu UNWTO Kimataifa, kuwa Mjumbe Kamati ya Utendaji UNWTO Kimataifa na kuwa Mjumbe wa Kikundikazi cha Wataalam (Brand Africa).


Tukio la kuhama kwa nyumbu katika Mfumo Ikolojia wa Serengeti hutokea kwa mwaka mzima ikijumuisha nyumbu wanaokadiriwa kuwa zaidi ya milioni 1.5 wakiambatana na wanyamapori wengine wakiwemo Pundamilia takriban 400,000, Swala 200,000 na Wanyamapori wengine kutafuta malisho, maji na hali nzuri ya hewa. Wakati wa kuhama wanyamapori hawa hupitia maeneo mbalimali yenye vikwazo na fursa katika kukamilisha mzunguko wao. 


Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mhe. Timetheo Mnzava amesema; “Tumejionea maajabu leo na tunaipongeza Serikali na wahifadhi wetu kwa kuwalinda wanyama hawa mpaka leo tumejionea tukio hili la aina yake,”.

Amepongeza kazi nzuri inayofanywa na Wizara katika kipindi hiki huku akisisitiza kuwa kamati yake itashirikiana kikamilifu na Wizara katika kukuza na kuboresha sekta ya utalii nchini. 








WATUMISHI WA UMMA VYOMBO VYOMBO VYA ULINZI MSIWAPIGE RAIA DKT SAMIA HATAKI HIYO TABIA-QS KIPANGA


 Na Mwandishi Wetu


Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknologia Mhe Qs Omar Kipanga ametoa ufafanuzi kuhusu tabia ya badhii ya watumishi wa umma mafia kupiga raia kwa kisingizio Cha Wao wapo Kikazi Zaidi,


Akiziungumza 22.08.2023 wakati wa ziara ya Kikazi ya kukagua Utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya Mafia katika Tarafa ya kusini kata ya jibondo vijiji vya Chole na juani kwa wakati tofauti amepokea Malalamiko ya badhi ya watumishi kupiga raia,


*Mhe Qs Kipanga Naibu waziri Wetu kuna watu walikuja hapa visiwani chole na juani wakatupiga na kuondoka bila ya sababu yoyote na pia wanatuita majina sio Mazuri kisa tu Wao ni watumishi tunaomba utusaidie kwanza Ujue hii shida kwetu pia uwambie Kabisa sisi wananchi wa kata ya jibondo na vijiji hivi sio Magaidi alisisitiza Omar Mkaazi wa Chole


*"Akitolea ufafanuzi Hoja hiyo ya hao watumishi Mhe Qs Kipanga alisema jukumu moja wapo kuu ni kulinda raia na mali zao sio kuwapiga naagiza kuacha mara moja hii tabia na pia nitaomba baadhi ya wakazi kwa Siri kubwa mnitajie majina Yao kama mnawatambua ili sheria ichukue mkondo wake mie nikawasilishe kwa mkuu wa Wilaya Mafia na ikidhibitika wamefanya makosa Washitakiwe rais Dkt Samia Suluhu Hassan hataki kuona uonevu unafanyika kwa Watanzania wasio na makosa alimalizia Mhe Qs Kipanga*" 

MAGAZETI YA LEO JUMATANO TAREHE 23 AGOSTI 2023.

 


























MASHEIKH SASA WALIPWE MISHAHARA MINONO.

 


Akiongea kwenye mkutano mkuu wa Bakwata mkoa wa Arusha hibi karibuni, Katibu Mkuu wa Bakwata, Alhaj Nuhu Jabir Mruma, amesema sasa kuna haja kubwa kuweka utaratibu mzuri na wa wazi kuwawezesha masheikh wanaofanya kazi ya dini kwenye ngazi zote Madrasa, Misikitini NK. walipwe mishahara minono ili wawe na pato halali kwa kazi wanazofanya badala ya kuwaacha na kuwawekea mazingira ya kuwalaumu au kwadhania kuwa wanajipatia pato kwa njia nyingine.


Amesema kwa kuwa muda wao wote ni kuwahudumia waislamu ni muhimu waislamu wawaandalie mazingira mazuri na ya wazi kuwawezesha kupata pato ili waendelee kuwahudumia waislamu huku wakiendesha maisha yao na familia zao kama wafanyakazi au wanajamii wengine.


Wakati huohuo Katibu Mkuu huyo wa BAKWATA  aliongeza kwa kusema kuwa viongozi wa BAKWATA  wanapaswa kujenga  utamaduni wa kuambizana ukweli pale ambapo mmoja amekosea ili kujenga nidhamu ya maadili na uadilifu katika uongozi.


"Ili tufanikiwe lazima sisi viongozi wa Bakwata tujenge utamaduni wa kuambizana ukweli, mmoja wetu akienda kombo au akijisahau tuna wajibu wa kumwambia, tutamsaidia yeye, Baraza na waislamu kwa ujumla" Alisema.


"Tusinyamazie makosa kwa sababu tutaanguka sisi sote, muhimu ni kutumia lugha nzuri kuambizana na siyo kukashifiana au kutukanana, Alimalizia Sheikh Mruma.


Imenukuliwa na:-
Dr. Harith Nkussa
Mwandishi Maalum wa Mufti
Sanawari. Arusha

POLISI BAGAMOYO WATAKIWA KUBADILIKA KIUTENDAJI.


 Askari Polisi Wilaya ya Bagamoyo wametakiwa Kubadilika kifikra na kufanya kazi kwa weledi na kuachana na utendaji kazi wa mazoea.

Hayo yamesemwa hivi karibuni na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Kamishina Msaidizi wa Polisi, (ACP) Pius Lutumo  wakati wa ziara yake ya Ukaguzi wa kuangalia utendaji wa kazi Wilayani hapo  wakati akizungumza na Maafisa, wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali ambapo amewataka kuzingatia ufanyaji kazi kwa mujibu wa Sheria za nchi na kuacha kufanya kazi kwa mazoea na kupeleka utendaji usioridhisha.


Pia, Kamanda Lutumo amesisitiza umuhimu wa kufanya kazi kwa nidhamu na kuzingatia maadili ya Jeshi la Polisi kwa kujiepusha na vitendo vya mmomonyoko wa maadili vitakavyolichafua Jeshi ambavyo huweza kusababisha kufukuzwa kazi.


Kadhalika, amewataka askari kufanya kazi kwa kusimamia misingi ya utendaji bora kwa kutenda haki kwa tunao wahudumia vituoni " Wananchi hawapendi kuja kwenye vituo vyetu ila wanafika kwa kuwa wanashida zinazohitaji kusaidiwa nasi hivyo ni jukumu letu kuwapa huduma bora wanapofika kwenye vituo vyetu vya Polisi”, Alisema.


Aidha, amewakumbusha askari umuhimu wa kutunza vizuri vielelezo na kutokuwa na tamaa au kushawishika katika kuiba vielelezo hivyo viwapo kituoni. "Ni jukumu letu kulinda vielelezo vilivyopo kituoni na kuhakikisha vinatunzwa vizuri na siyo kuwa sehemu ya upotevu wa vielelezo hivyo ambavyo vitatumika kama ushahidi Mahakamani.


Kutoka Dawati la Habari
Polisi (M) Pwani.



Tuesday, August 22, 2023

BUNGE LATAKA TIJA UWEKEZAJI SOKO JIPYA LA KARIAKOO


 Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Denis Rondo akitoa maelekezo kwa serikali  kuhakikisha Ofisi ya Rais TAMISEMI inaweka mazingira wezeshi kwa wafanyabiashara wadogo wa soko la Kariakoo waweze kufanya kazi zao kwa mpangilio na uratibu mzuri pale soko litakapokamilika kujengwa.

.............................,

Na. Mwandishi wetu KMC

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Denis Rondo amelitaka shirika la Masoko ya Kariakoo (KMC) kuhakikisha uwekezaji  mkubwa uliofanywa na serikali kwa kutoa shilingi Bilioni 28.03 kukarabati na kujenga soko la Kariakoo unakuwa na tija kwa taifa  na kuwezesha wafanyabiashara kuwa na mazingira mazuri kuchangia ukuaji wa uchumi.

Hayo yamebainishwa leo  ( Agosti 22,2023) bungeni jijini Dodoma wakati Kamati hiyo ya Bunge ilipokutana na Menejimenti ya Shirika la Masoko ya Kariakoo kupokea taarifa ya utekelezaji wa shughuli za shirika hilo kwa mwaka 2022/23.

Rondo ameitaka pia Ofisi ya Rais TAMISEMI kupitia idara ya miundombinu kusimamia kwa ukaribu miundombinu ya soko la Kariakoo ili thamani ya fedha iliyowekwa na serikali iweze kuonekana.

" Idara ya miundombinu TAMISEMI isimamie miundombinu ya masoko ili shilingi Bilioni 28 za serikali iwe na tija kwa Nchi" alisema Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Bunge.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Deo Ndejembi alisema katika kuhakikisha uwekezaji mkubwa uliofanywa na serikali ya awamu ya sita kwenye ,Shirika la Masoko ya Kariakoo litaanza kutumia mfumo wa kielektoniki wa TAUSI katika kusajili na kutoa leseni kwa wafanyabiashara tofauti na ilivyokuwa awali.

Ndejembi aliongeza kusema kuwa Ofisi ya Rais TAMISEMI itashirikiana na Wizara ya Viwanda na Biashara kuweka mazingira wezeshi kwa wafanyabiashara wadogo kwenye soko la Kariakoo na masoko mengine nchini ili wafanye kazi zao kwa utulivu na  hivyo kuchangia pato la taifa na kuepukana na migogoro.

Kwa upande wake Kaimu  Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo Sigsibert Valentine alisema mradi wa ukarabati na ujenzi wa soko la Kariakoo ulioanza Mwaka 2022 unatarajia kukamilika mwezi Oktoba 2023 na kuwa shirika liko kwenye maandalizi ya kuwarejesha waliokuwa wafanyabiashara kabla ya soko kuungua na kuweka mfumo utakaotumika kuingiza wafanyabiashara wapya kutokana na nafasi za biashara kuongezeka toka 1'660 hadi takribani 2,300.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Deogratius Ndejembi akitoa maelezo kuhusu utendaji kazi wa Shirika la Masoko ya Kariakoo leo Agosti 22,2023 wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ilipopokea taarifa ya utendaji kazi wa Shirika la Masoko ya Kariakoo jijini  Dodoma.

Kaimu Meneja Mkuu w Shirika la Masoko ya Kariakoo Sigsibert Valentine akitoa ufafanuzi wa hoja za wabunge leo jijini Dodoma ambapo alieleza kuwa mradi wa ujenzi na kukarabati wa soko la Kariakoo uliogharimu shilingi Bilioni 28.03 utakamilika Oktoba 2023 na kuwa taratibu za wafanyabiashara kurejea zinaendelea kukamilishwa .

( Habari na Picha na Shirika la Masoko ya Kariakoo)



BANDARI YETU NA USHAURI KWA RAIS SAMIA

 

Na Albert Kawogo.


SINA kumbukumbu na marais wa awamu ya kwanza Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi kwenye malalamiko kuhusu bandari lakini marais waliobaki hadi huyu wa sasa kwa nyakati tofauti wamelalamika juu ya ufanisi wa Mamlaka yetu ya Bandari na wao kuthibitisha kwa kauli ya ujumla kuwa Mamlaka hii ingekuwa inafanya kazi vizuri ingeweza kuchangia hata nusu ya mapato ya Bajeti yetu. Ni kweli kabisa naungana na Marais hawa kwenye hili.


Mfupa wa Bandari ni mfupa uliowasumbua Marais karibu wote waliowahi kutawala Tanzania! Hii imekuwa kawaida kila Rais mpya akiingia au Waziri Mkuu mpya akiteuliwa sehemu ya kwanza ni kwenda kulalamika na kuonya kuasa na hata kutumbua watendaji wa Mamlaka ya Bandari Tanzania.


Kwa kumbukumbu zangu kuanzia kwa Mkapa, Kikwete, Magufuli hadi sasa Samia, Bandari hapajawai kupoa.


Hoja yangu kuu kwenye hili ni kwamba inawezekana sana bado hatujajua shida ni nini hasa pale Bandarini na kwa uelewa wangu mdogo napenda leo nimshauri Mhe Rais mambo ya kufanya na naamini kama nilivyoshauri kuhusu Ngorongoro na ikafanyika na sasa imefanikiwa basi nashauri juu ya hili la Bandari na naamini ikifanyika itafanikiwa


1. Lazima tukubali kuwa Bandari ya DSM haiwezi kuwa na ufanisi kwa sababu imekuwa finyu kuhimili idadi ya mizigo, Meli na Magari kiushindani


2. Lazima tukubali kuwa Serikali haiwezi kuendesha bandari kwa ufanisi tunaoutaka katika dunia hii ya ushindani. Bandari kubwa zote duniani na zinazofanya vizuri kwenye soko la ushindani kuanzia Dubai, Hong Kong, Singapore, New York na nyinginezo, zinaendeshwa either kwa sehemu kubwa na private sector au kwa ubia baina ya Serikali na sekta binafsi.


Hivyo ili kufanikiwa kupata ufanisi hapa Tanzania kwenye sekta ya Bandari , Lazima tutake tusitake, tufanye yafuatayo


a. Kwa haraka sana, Ijengwe Bandari ya Bagamoyo ambayo iwe na Gati zisizopungua 40. Bandari hii iendeshwe na Private sector with exception kwenye masuala ya Ulinzi, Usalama na Kodi


b. Sekta binafsi wapewe pia fursa ya kujenga Miundombinu ya Reli na barabara kuunganisha Bandari ya Bagamoyo na Jiji la Dar es Salaam ikiwemo reli ya kati SGR na TAZARA


c. Bandari za DSM, Tanga, Mwanza na Kigoma na Mtwara ziendeshwe kwa ubia na sekta binafsi. Serikali isimamie masuala ya kodi , ulinzi na usalama tu!


d. Barabara ya Mandela Road( DSM) itanuliwe kuwekwa njia 8 kutokea Bandarini hadi Ubungo na utanuzi wa njia 6 uendelee kutoka Kimara hadi Ubungo. Hii ni ili kuleta ufanisi wa usafirishaji mizigo katika Jiji la Dsm. Ikiwezekana sekta binafsi washirikishwe kwenye hili.


e. Kulikuwa na Mpango wa Kujenga Barabara ya Malori kutokea Bandarini hadi Chalinze. Mpango huu ufufuliwe na barabara hii ijengwe hata kwa kutumia sekta binafsi. Fedha zitarudi haraka sana hata kwa toll tax!


Nchi kubwa duniani ziliona hili na wakaamua kufanya! Hata kwa Tanzania Serikali iking'ang'ania kuendesha bandari kila siku mtaishia kushikana uchawi na kutumbuana!


Ni suala la kuamua tu na wakati ni sasa.