Wednesday, May 13, 2020

KAMATI YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI IMERIDHISHWA NA MAANDALIZI YA ULIPAJI FIDIA LINDI.


NA HADIJA HASSAN, LINDI.

KAMATI ya Bunge ya Nishati na Madini imesema imeridhishwa na kasi ya maandalizi ya ulipwaji wa fidia unaofanywa na Shirika la maendeleo ya Petrol Tanzania (TPDC) kwa wananchi 693 wa Mtaa wa Likong’o , Masasi ya leo na Mto mkavu katika kata ya Mbanja halmashauri ya Manspaa ya Lindi Mkoani humo ili kupisha mradi wa Gesi asilia (LNG).


Kauli hiyo imetolewa na kaimu mwenyekiti wa kamati ya Nishati na Madini ambae pia ni mbunge viti maalumu , Mkoa wa Lindi CCM, Hamida Abdalla mara baada ya kamati hiyo kufanya ziara katika mtaa huo wa likong’o ambako zoezi hilo la maandalizi ya ulipwaji wa fidia linaendelea.


Hamida amesema kulingana na maadalizi yaliyofanywa na shirika hilo yataweza kuondoa malalamiko kwa wananchi walioathirika na mradi huo kwani wamerahisisha kupatikana kwa watu na vitengo vyote muhimu kuwepo katika maeneo hayo.



“Sasa mambo yameiva hayawi hayawi sasa yamekuwa kwa hivyo ndugu zangu wanalikong’o, Masasi ya Leo na Mto mkavu, mambo yote yapo hapa tumerahisishiwa ofisi ya ardhi ipo hapa, watu wa benk wapo hapa wanasheria wapo hapa, wapiga picha pia wapo hapa kwa hivyo tunashukuru sana kwa utaratibu huu ambao Serikali kupitia (TPDC) umeufanya na umewarahisishia wananchi” Alisema Hamida.


Hamida pia alisema kuwa Wananchi wanapaswa kusoma kwa usahii mikataba wanayosaini pamoja na pesa wanazotakiwa kulipwa huku akisisitiza kuwatumia wataalamu waliopo kikamilifu ili kuondoa malalamiko mara baada ya zoezi hilo kukamilika.


Akielezea utaratibu wa zoezi hilo mbele ya kamati ya Bunge ya Nishati na Madini Meneja wa uwendelezaji na uzalishaji wa Mafuta na Gesi (TPDC) Modestus Lumato Alisema kutokana na malipo hayo kuchelewa kulipwa kwa muda uliotarajiwa wananchi hao pamoja na fedha zao za fidia watapaswa kulipwa na fedha za ucheleweshaji wa miaka mitano.


Kwa mujibu wa Lumato wananchi hao walifanyiwa uthamini wa maeneo yao tangu mwaka 2014 ambapo kwa mujibu wa Sheria Mwananchi anatakiwa kulipa fidia ya Eneo lake lililofanyiwa uthamini ndani miezi sita.


Alisema fedha hizo zitalipwa kwa awamu mbili ambapo kwa awamu ya kwanza zitalipwa kwa ucheleweshwaji wa miaka mitatu yaani 2015,16 na 17 huku awamu ya ya pili zikilipwa kwa ucheleweshwaji wa miaka miwili iliyosalia ya 2018 na 2019.


Kwa upande wake Mbunge wa jimbo hilo la Lindi , Hassan Kaunje licha ya kuishukuru Serikali kwa kutoa fedha za ulipaji wa fidia kwa wananchi hao pia aliwapongeza wananchi wa Maeneo hayo kwa kuwa wavumilivu kwa wakati wote ambapo Serikali ikishughulika na Madai yao.


Nae Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga alisema kuwa ili kuhakikisha wananchi hao wanapata maeneo ya makaazi tayari halmashauri hiyo ya lindi imeshapima zaidi ya viwanja 500 kwa ajili ya kuanzisha makazi mapya ya wananchi wanaopisha mradi huo wa gesi asilia wa (LNG).
 

PICHA ZOTE NAHADIJA HASSAN.

Sunday, May 10, 2020

MAENEO YANAYOZUNGUKA VITUO VYA TRENI YA MWENDOKASI KUWEKEWA MPANGO WA MATUMIZI BORA YA ARDHI

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi itaandaa Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi katika maeneo yote yanayozunguka vituo vya treni ya mwendo kasi (SGR) ili kuwezesha ardhi ya maeneo hayo kuendelezwa kwa kuzingatia shughuli zitakazokuwa zikifanyika sambamba na mahitaji muhimu kwa watumiaji wa vituo hivyo.

01.  Mhandisi Yusuph kutoka kampuni ya Yapi Merkezi (wa kwanza kushoto) akiilezea timu ya Maafisa Mipango Miji kutoka Wizara ya Ardhi, ramani ya ujenzi wa kituo kikuu cha Morogoro pamoja shughuli zitakazokuwa zinafanyika katika kituo hicho ili wataalam hao waweze kuandaa mpango wa kuendeleza eneo hilo kulingana na shughuli zitakazokuwa zinatekelezwa katika kituo hicho. Kituo hiki cha Morogoro kimezungukwa na shamba la mkongwe pamoja na makazi ya watu.


Hayo yalibainishwa juzi na Afisa Mipango Miji kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Edward Mpanda wakati timu ya Wataalamu kutoka Idara ya Mipango Miji ilipotembelea mradi huo katika eneo la Kilimanjaro mkoani Morogoro, sehemu kinapojengwa kituo kikuu cha treni ya mwendo kasi.

Alisema, Wizara yake imejipanga kwa kushirikiana na Tume ya Matumizi Bora ya Ardhi pamoja na Shirika la Reli Tanzania (TRC) kuhakikisha inaandaa mpango maalum wa kuendeleza Ardhi inayozunguka vituo vya treni ya SGR ambayo ujenzi wake ulishaanza. 

Kwa mujibu wa Mpanda, Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi pamoja na Tume ya Matumizi bora ya Ardhi itahakikisha pia reli ya kisasa (SGR) inatunzwa kwa kuzingatia mpango uliowekwa ili kuleta ufanisi na maendeleo kwa wananchi wanaoishi maeneo hayo.

‘‘Kama Wizara isiposimamia uendelezaji Ardhi inayozunguka eneo la mradi, basi kila mmoja atakuja na ujenzi wake bila kujali athari itakayotokea kutokana na shughuli zitakazokuwa zikiendelea katika vituo hivyo vya treni’’ alisema Mpanda.

Aidha, Afisa huyo wa Mipango Miji kutoka Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alisema Usimamiaji wa uendelezaji Ardhi katika maeneo yanayozunguka mradi wa ujenzi reli ya kisasa (SGR) utasaidia kuondoa ujenzi holela katika maeneo hayo na kuweka miundo mbinu itakayokuwa na tija kwa watumiaji hasa katika vituo vyote vikubwa na vya kati

Kwa upande wake Mhandisi Hamza Said kutoka Shirika la Reli Tanzania, aliishukuru timu ya Wataalamu wa Mipango Miji kwa kutembelea mradi huo na kubainisha kuwa Wizara ya Ardhi bado haijachelewa kuandaa mipango yake na kusisitiza muda bado upo kwa kuwa ujenzi wa reli ya kisasa unaendelea.

‘‘Kuweka mpango wa kuendeleza maeneo kwenye vituo vya treni ya mwendo kasi itakuwa na faida kwa sababu maeneo hayo yatakuwa na tija kwa watumishi watakaokuwa wakihudumia vituo hivyo lakini pia na kwa wasafiri wa treni ya mwendo ya kasi na ile ya kawaida’’ alisema Mhandisi Hamza

Timu ya Wataalamu wa Mipango Miji kutoka Wizara ya ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ilitembelea mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa kwa lengo la kubaini aina ya Ardhi inayozunguka maeneo inakojengwa ili kuweka mikakati ya jinsi ya kuyaendeleza maeneo hayo.


01.  Mhandisi Hamza Said (mwenye kofia) kutoka Shirika la Reli Tanzania akiwaelezea wataalam wa Mipango Miji Kutoka Wizara ya Ardhi ramani ya ujenzi wa kituo kikuu cha Dar es Salaam na shughuli zitakazokuwa zinafanyika katika kituo hicho. Kituo cha Dar es Salaam ndiyo kituo kikubwa zaidi na kituo namba moja cha treni ya mwendo kasi. Treni ya mwendo kasi na ile ya kawaida zote zitakuwa zinaanzia safari zake katika kituo hiki cha Dar es Salaam ambapo treni ya mwendo kasi itakuwa inapita juu na ile ya kawaida itakuwa inapita chini bila kuathiri shughuli za maendeleo za kila siku.

 

  

Mfumo wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) inayojengwa na Kampuni ya Yapi Merkezi ya nchini Uturuki umegawanywa katika awamu mbili ambapo awamu ya kwanza yenye vituo sita inatoka Dar es Salaam hadi Morogoro huku awamu ya pili ikianzia Morogoro hadi Makutopora Manyoni mkoani Singida ikijumuisha vituo tisa.


01.  Timu ya Maafisa Mipango Miji kutoka Wizara ya Ardhi, wakijadiliana na wahandisi wa ujenzi reli ya kissasa (SGR) jinsi gani wanaweza kushirikiana na Shirika la Reli Tanzania kuendeleza maeneo yanayozunguka vituo kwa kuzingatia shughuli na mahitaji ya vituo hivyo vya treni ili kuepuka ujenzi holela katika maeneo yote yatakayokuwa na vituo vikubwa na vya kati vya treni ya mwendo kasi.

 


Saturday, May 9, 2020

RC PWANI AAGIZA WATENDAJI WALIOKWAMISHA MIRADI 42 BAGAMOYO WAWAJIBISHWE


VICTOR MASANGU, BAGAMOYO
  
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo  amechukizwa na kuona  miradi ya maendeleo ipatayo 42 yenye thamani ya zaidi ya bilioni 1 katika halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo haijakamilika kwa wakati hadi sasa kutokana na kuwepo kwa  baadhi ya watumishi na  watendaji kufanya kazi kwa mazoea na uzembe hali ambayo inasababisha hasara kubwa  na kukwamisha juhudi za serikali ya awamu ya tano  katika kuwaletea wananchi maendeleo hivyo wote watakaobainika kuhusika na ubadhilifu wowote wa fedha wachukuliwe hatua kali za kisheria ili iwe fundisho kwa wengine.


 Kauli hiyo aliitoa  wakati wa mkutano maaalumu wa baraza la madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo  wenye lengo la  kupokea na kujadili majibu ya hoja za mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali (CAG) kwa kipindi cha mwaka wa hesabu kwa mwaka wa 2018/2019.ambapo pia ametoa muda wa siku saba kwa uongozi wa halmashauri hiyo  kufunga hoja zote 38  ambazo bado  hazijakamilika hadi sasa kwani ili kuendana na maagizo yaliyotolewa na serikali ya Mkoa.


 Ndikilo alisema kwamba katika taarifa amabayo imetolewa na mdhibiti na wa hesabu za erikali CAG imeweza kueleza kuwa kuna baadhi ya miradi ambayo bado ijakamilika wakati fedha zake zimeshatolewa hivyo kuna dalili za baadhi ya watendaji kutowajibika kikamilifu katika uetekelezaji wa majukumu yao.


“Fedha zimetolewa kabisa shilingi bilioni 1 na milioni 24 lakini mimi nashangaa miradi 42 bado haijakamilika kwa wakati kabisa hii kwa weli sio sahihi hata kidogo hapa inatakiwa ndugu zangu madiwani wa baraza hili kuangalia kwa makini maana hii miradi ni mingi kwa hiyo mimi ninachokiomba miradi hii iweze kukamilika kabisa kwa wakati na kwa wale watumishi ambao watakuwa wamehusika katika uzembe huu ni lazima wachukuliwa hatua kali z akisheria.


Aidha Mkuu huyo aliongezea kuwa kwa sasa inatakiwa hoja zote ambazo ziliitajika kukamilishwa kwa kipindi hiki ni lazima zifanyiwe kazi haraka iwezekanavyo maana ni agizo ambalo lilishatolewa na serikali ya Mkoa kwa hiyo mimi naagiza ndani ya siku saba kwa maana ya wiki moja hoja hizi 38 na kipindi cha mwak 2018/2019 ni lazima zikamilika pamoja na zile hoja nyingine za miaka iliyopita.


Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Zainabu Kawawa amesema licha ya halmashauri hiyo kupata hati safi kwa mfululizo kuanzia kipindi cha kuanzia mwaka 2015 hadi 1019 lakini watendaji na watumishi wanapaswa kubadilika  kwa kutekeleza majukumu yao kwa weledi hasa katika suala zima  la kudhibiti mianya ya upotefu wa mapato pamoja na kusimamia kikamilifu  fedha zinazotolewa katika miradi ya maendeleo.


Kawawa alibainisha kwamba katika halmashauri ya Wilaya ya Bgamoyo kumekuwepo na changamoto mbali mbali katika suala zima la ukusanyaji wa mapato hivyo kunahitajika juhudi z amakusudi katika kuhakikisha mashine ambazo zinatumika katika ukusanyaji wa mapato hayo zinakuwa zinawashwa kwa lengo la kuweza kuongeza makusanyo tofauti na ilivyokuwa kwa sasa.


“Hii hali ya ukusanyaji wa mapato katika halmashauri ya Wilaya ya Bgamoyo sio mzuri ndio ni kweli tumefnikiwa kupata hati safi kwa awamu nne mfululizo lakini sisi kama viongozi ni lazima tufuatilie kwa umakini kuhusiana na ukusanyaji w amapato haya  mbali mbali maana nasikia kuna mashine nyingine zinakuwa zimeimwa kwa kipindi cha muda mrefu sasa hii ni hatari sana lazima mapato yetu yapotee tuu kutokana na uzembe wa baadhi ya watu,”alisema Kawawa.


Naye mkaguzi wa Ofisi ya Taifa ya ukaguzi na udhibiti wa hesabu za serikali (CAG) wa Mkoa wa Pwani  Mwajuma Kwipunda alibainisha kwamba halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo kwa kipindi cha mwaka 2018/2019 licha ya kuwepo kwa mapungufu ya kutokamilisha mapendekezo kwa wakati imefanikiwa kupata hati safi.


Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa halmashauri hiyo amefarijika kupokea hati safi kwa mara ya nne mfululizo na kuahidi kuyafanyia kaiz kwa vitendo maagizo yote  nane ambayo yametolewa na Mkuu wa Mkoa kuhusina na mambo mbali mbali  katika kusimamia utekelezaji wa miradi ya maeneleo pamoja na utekelezaji wa hoja ambazo bado hazijafanyiwa kazi.


 HALMASHAURI ya Wilaya ya Bagamoyo iliyopo Mkoa wa Pwani licha ya kupatiwa hati safi mfululuzo kuanzia kwa kipindi cha mwaka 2018 hadi 2019 kutoka kwa  mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali (CAG) lakini bado inakabiliwa na changamoto mbali mbali katika masuala ya ukusanyaji wa mapato pamoja na kutokamilisha kwa baadhi ya miradi ya maendeleo kwa wakati.

WAENDESHA BODABODA BAGAMOYO WAMSHUKURU MBUNGE KAWAMBWA.

  Waendesha pikipiki wakiwa katika moja ya vituo vyao kazi mjini Bagamoyo.
.........................................

Na Selestian James.

Waendesha pikipiki Jimbo la Bagamoyo, wamemshukuru mbunge wa jimbo hilo  Dkt. Shukuru Jumanne  Kawambwa kwa msaada wa ndoo na sabuni alioutoa kwao hivi karibuni ili kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa Corona.

Wakizungumza na Bagamoyo kwanza blog katika vijiwe mbalimbali vya  pikipiki wamesema msaada wa mbunge huyo una maana kubwa sana kwao kwani tangu awali walitamani sana kuwa na vifaa hivyo ili kujilinda na ugonjwa huu hatari ambao kwa kiasi kikubwa  unasumbua duniani kote.
      
"Kwa sasa sisi hatuna budi kumshukuru muheshimiwa mbunge kwani hivi vitu ni muhimu sana kwetu sisi binafsi, familia zetu na hata wateja wetu kwani kwa sasa tumejiwekea utaratibu wa kuhakikisha tunanawa kila tunapoingia kijiweni na tumekuwa tunahakikisha hata abiria zetu wanafanya hivyo pia".

Wamesema hata abiria pia wanafurahia utaratibu huu kwani wanaona namna tunavyojali afya zetu na za kwao pia.

"Mwanzoni tulikuwa tunafikiria sana namna ambayo tungeweza kupata ndoo ukizingatia hivi vifaa kuna baadhi ya maduka vimepanda bei unakuta ndoo inauzwa mpaka elfu thelathini, ukizingatia na vipato vyetu vidogo hivyo ilikuwa inatuwia vigumu sana kuweza kumudu gharama hizo".

Aidha waendesha pikipiki hao wamemuomba Dkt kawambwa aendelee na moyo huo huo hasa katika kipindi hiki cha maambukizi ya ugonjwa huo.

"Sisi tumuombe muheshimiwa mbunge akipata chochote ambacho anachoweza kutusaidia hasa katika kipindi hiki cha maradhi haya ya Corona basi atufikishie vijana wake" walisema waendesha boda boda.

 Waendesha pikipiki wkiosha mikono yao, katika moja ya vituo vyao kazi mjini Bagamoyo.

 Picha zote Na Selestian James.