Friday, March 13, 2020

OCODE YAMUUNGA MKONO RAIS MAGUFULI KWA KUWAJENGEA DARASA JIPYA WANAFUNZI WA KIBWEGERE

Mkurugenzi wa shirika la Ocode Joseph Jackson wa kati kati akiwa na Mkurugenzi mtendaji wa Manispaa ya ubungo Beatrice Dominic  wa kushoto pamona na Afisa elimu wa manispaa hiyo  kulia wakiwa wameshikilia upete kwa ajili ya kuukata ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa darasa moja la wanafunzi wa elimu ya awali Kibwegere ambalo limetolewa na shirika la  Ocode kwa ajili ya kuboresha sekta ya elimu. (PICHA NA VICTOR MASANGU).
..................................................



NA VICTOR MASANGU, UBUNGO.

SEKTA ya elimu hapa nchini licha ya serikali ya awamu ya tano kuweka  sera ya kutoa elimu bure lakini bado katika baadhi ya maeneo ya shule za msingi na Sekondari zilizopo katika Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es Salaam zinakabiliwa na changamoto mbali mbali ya upungufu wa matundu ya vyoo pamoja  na uhaba na uchakavu wa  miundombinu ya madarasa hivyo kusababisha wanafunzi wengine kusoma katika mlundikano mkubwa.


Katika kuliona hilo Shirika lisilokuwa la kiserikali la Organization Community Development (OCODE)  limeamua kumuunga mkono Rais wa awamu ya tano Dk. John Pombe Magufuli katika kuboresha sekta ya elimu kwa kutoa msaada wa madawati 39,ya wanafunzi, viti 13 vya kukalia walimu pamoja na kukabidhi rasmi chumba cha darasa moja jipya  kwa ajili ya wanafunzi wa elimu ya awali katika shule ya msingi Kibwegere.


Akizungumzia kuhusiana na msaada huo Mkurugenzi wa Shirika la Ocode Joseph Jackson amesema kwamba kwa sasa wana tekeleza mradi wa elimu ambao utakuwa wa  kipindi cha miaka mitano ambao umeanza kufanyika tangu 2019- 2023 kwa lengo la kuweza kuwasaidia watoto wa shule za awali na msingi katika kuwawekea mazingira mazuri katika suala zima la upatikanaji wa elimu iliyo bora kwa manufaa yao ya baadae.


Aidha Mkurugenzi huyo alibainisha kwamba katika mradi huo umeweza kugusa ujenzi wa darasa hilo jipya la wanafunzi wa elimu ya awali ambalo mpaka kukamilika kwake limegharimu kiasi cha shilingi milioni 26 na kwamba wana imani kuwa watoto hao kwa sasa waliokuwa wanakabiliwa na changamoto ya kukaa kwa mlundikano watasoma katika mazingira ambayo ni rafiki kwao


“Shirika letu la Ocode kwa sasa linaendelendea kutekeleza program ya mradi wa elimu ambao utakuwa unazigusa baadhi ya shule za msingi ambazo zipo katika maeneo mbali mbali ya Jiji la Dar es salaam, maana nia yetu ni kuwasaidia watoto hawa kuanzia elimu ya awali na kwamba kwa sasa tutajikita zaidi kwa wanafunzi wa darasa la kwanza na darasa la pili pamoja na wale wanafunzi wa ngazi ya awali ili kuweza kuwajengea uwezo wa kupata elimu bora,”alisema Mkurugenzi huyo.


Pia alibainisha kwamba katika kipindi cha utekelezaji wa mradi huo kwa kipindi cha miaka mitano watahakikisha kwamba wanashirikiana bega kwa bega na serikali ya awamu ya tano pamoja na wadau wengine wa maendeleo ili kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo kupitia elimu kuanzia ngazi za chini na kuendelea.


Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Kibwegre  akisoma risala kwa mgeni rasmi katika halfa ya makabidhdiano ya madawati na  uzinduzi wa  darasa hilo amebainisha kwamba kwa sasa wanafanya kazi katika mazingira magumu sana kutokna na ukosefu wa ofisi za walimu na vyumba vya madarasa ambapo wakati mwingine inawalazimu walimu kufanyia kazi zao wakiwa wamekaa chini ya miti hivyo msaada huo ambao umetolewa na Ocode utakuwa ni mkombozi kwa upande wao.


“Shule yetu ya Kibwegere kwa kweli tunapenda kutoa shukrani zetu za kipekee kwa Shirika hili la Ocode kwani wameweza kutuona na kutusaidia katika mambo mbali mbali  ya kutujengea darasa moja, kutupa viti, pamoja na madawati ya wanafunzi hii kwa upande wetu ni moja ya hatua, kwani hapo awali hali ilikuwa ni ngumu kutokana na miundombinu yenyewe ya madarasa pamoja na ofisi za walimu, hivyo napenda kushukuru sana,”alisema Kulemba.


Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic ambaye alikuwa mgeni rasmi katika halfa ya makabidhiano hayo amesema kwamba pamoja na juhudi zinazofanywa na serikali lakini amekiri bado kunachanagmoto kubwa ya miundombinu ya madarasa kwa shule za msingi na sekondari na anatambua walimu wanafanya kazi zao katika mazingira magumu sana hivyo amelipongeza shirika la Ocode kwa kuamua kushirikiana na serikali katika kuboresha sekta ya elimu kuanzia ngazi ya awali.


SHULE ya msingi Kibwegere iliyopo katika Manispaa ya Ubungo nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam  kwa sasa ina jumla ya wanafunzi 1741 ambao wanakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo upungufu wa walimu, uhaba wa miundombinu ya madarasa, ofisi za walimu, pamoja na matundu ya vyoo.

Baadhi ya wanafunzi wanaosoma katika shule ya msingi Kibwegere elimu ya awali wakiwa wameketi katika madawati ambayo yametolewa kwa msaada wa shirika la Ocode katika halfa ya makabidhiano yaliyofanyika katika viwanja vya shule hiyo manispaa ya ubungo Jijini Dar es Salaam, (PICHA NA VICTOR MASANGU).

Mkurugenzi wa Shirika la Ocode Joseph Jackson akizungumza na baadi ya walimu, wanafunzi wa shule ya msingi Kibwegere hawapo pichani wakati wa halfa ya makabidhiano ya uzinduzi wa darasa jipya ambalo limejengwa kwa ajili ya wanafunzi wa elimu ya awali kwa ajili ya kuwasaidia waweze kusoma katika mazingira ambayo ni rafiki. (PICHA NA VICTOR MASANGU)

Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic akifafanua jambo kwa walimu na wanafunzi ambao walihudhulia katika halfa fupi ya makabidhiano ya chumba cha darasa jipya ambacho kimejengwa kwa ajili ya kusomea watoto wa elimu ya awali. (PICHA NA VICTOR MASANGU).

Mkuu wa Shule ya Msingi Kibwegere Charles Kulemba akisoma Risala mbele ya mgeni rasmi wakati wa halfa ya uzinduzi huo wa darasa jipya mablo limejengwa mahusus kwa ajili ya watoto wadogo wanaossoma katika ngazi ya awali. (PICHA NA VICTOR MASANGU)

Mmoja wa walimu ambao wanawafundisha wanafunzi wa elimu ya awali Bi. Eunice Matembo akisoma Risala yake kwa mgeni rasmi amabye ni  Mkurugenzi mteandaji wa Manispaa ya Ubungo hayupo picha wakati wa halfa hiyo ya makabidhiano ya madawati, viti pamoja na uzinduzi rasmi wa darasa hilo la wanafunzi wa awali. (PICHA NA VICTOR MASANGU)

 

Mkurugenzi mtendaji wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic wa katikati akijadiliana  jambo na mwalimu mkuu wa Shule hiyo ya Kibwegere pamoja na watumishi wengine wa Ocode na serikali wakati wa halfa hiyo ya makabidhiano wa misaada mbali mbali ikiwemo meza pamoja na viti kwa ajili ya kukalia walimu. (PICHA NA VICTOR MASANGU)

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Msingi Kibwegere wakiwa wanasikiliza hotuba ambayo ilikuwa inatolewa na Mkurugenzi wa shirika la Ocode Joseph Jackson hayupo pichani wakati wa sherehe ya uzinduzi wa darasa  jipya ambalo limejengwa kwa ajili ajili ya kuwasaidia watoto wa elimu ya awali. (PICHA NA VICTOR MASANGU).

Baadhi ya watendaji wa Shirika la Ocode wakiwa wameketi kwa utulivu wakifuatilia hotuba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic hayupo pichani wakati wa halfa hiyo ya uzinduzi wa darasa moja jipya lililojengwa kwa ajili ya wanafunzi wa elimu ya awali. (PICHA NA VICTOR MASANGU).

Pichani ni kibao ambacho kinaonyesha shule ya msingi Kibwegere iliyopo katika Manispaa ya Ubungo iliyopo Jijini Dar es Salaam.abpo shule hiyo imepatiwa msaada wa madawati, 39 viti 13 vya walimu pamoja na kukabidhiwa darasa jipya kwa ajili ya watoto wa elimu ya awali lililotolewa na shirika la Ocode na kughalimu kiasi cha shilingi milioni 24 (PICHA NA VICTOR MASANGU)

Monday, March 9, 2020

JELA MIAKA 5 KWA KOSA LA WIZI KAZINI.

KIBAHA MARCH 09.2020

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kibaha Mkoa wa Pwani, leo imemuhukumu aliyekuwa meneja wa kituo cha kuuza mafuta cha UKODI INTERNATIONAL COM LIMITED Malima Charles mwenye umri wa miaka 40 mkazi wa Maili moja Kibaha, kwenda jela miaka mitano (5) baada ya kumkuta na hatia katika makosa mawili yaliyokuwa yakimkabili mahakamani hapo ambayo ni KUVUNJA OFISI NA WIZI.

Akisoma hukumu hiyo iliyodumu kwa muda wa saa moja ambayo ilivuta hisia za wakazi wa Kibaha Mkoa wa Pwani, Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Joyce Mushi, ameeleza kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa Jamuhuri na ili kuwa fundisho kwa watumishi wengine wanopewa dhamana ya kusimamia vituo vya mafuta, mahakama imemkuta na hatia na kumhukumu kwenda Jela miaka 5 kwa makosa yote mawili

Mtuhumiwa huyo amekutwa na hatia kufuatia mahakama hiyo kuridhika na ushahidi uliowasilishwa na upande wa Jamuhuri kufutia makosa yote mawili yaliyokuwa yakimkabili na hivyo kumtia hatiani na kutakiwa kutumikia kifungo hicho cha miaka mitano kwa makosa yote.

Mwendesha mashtaka katika kesi hiyo, Wakili wa Serikali Auleilia Mushi alieleza mahakama hiyo kuwa mtuhumiwa akiwa meneja wa kituo cha kuuza mafuta cha UKODI INTERNATIONAL COM LIMITED, alikula njama za kuvunja ofisi na kuiba kiasi cha fedha za Kitanzania zipatazo milioni 45,266,133 za mwajiri wake na kutoweka kusikojulikana huku akijua fika kufanya hivyo ni kosa kisheria.

Mwendesha mashitaka huyo wa Serikali aliongeza kuwa mtuhumiwa huyo alivunja ofisi hizo tarehe 24.12.2018 na kuondoka na mauzo ya siku husika ambayo yalikuwa hayajapelekwa kuhifadhiwa Benki kutokana na siku hiyo kuwa ni siku ya mwisho wa juma na baada ya kutekeleza wizi wake akatoweka hadi pale jitihada zilipofanyika za Jeshi la Polisi kuweza kumsaka na kumtia nguvuni na kuweza kufikishwa mbele ya vyombo vya dola kwa hatua za kisheria.

Akijitetea mbele ya Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo mtuhumiwa huyo Malima Charles maarufu kwa jina la Mukama alikiri kufanya kosa hilo na kuiomba mahakama hiyo impunguzie adhabu kwa kuwa ni kosa lake la kwanza na anafamilia inayomtegemea na yeye akiwa anamatatizo ya kiafya.

WANAWAKE MTWARA WAWAFANYIA UKATILI WAUME ZAO.

HADIJA HASSAN, MTWARA.

WAKATI Dunia ikiadhimisha siku ya wanawake kwa kupinga ukatili dhidi ya kina mama, hali imekuwa tofauti kwa wanawake wa wilaya ya Tandahimba Mkoani Mtwara kwa kugeuka vinara wa kuwafanyia ukatili waume zao.

Hayo yameelezwa na afisa tawala wa wilaya ya Tandahimba Mkoani Mtwara fransisi Mkuti kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo Sebastian Waryoba wakati wa sherehe ya wanawake iliyoadhimishwa kiwilaya katika kijiji cha Chingungwe Wilayani humo.

Mkuti alisema kuwa licha ya mashirika na asasi mbali mbali za kiraia kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake lakini bado kina mama wa wilaya hiyo wamekuwa vinara wa kuwafanyia ukatili waume wao.

“kuna kinamama wanawafanyia ukatili waume zao, kuna kina mama wababe wanawapiga waume zao, wanawapiga biti, wakikaribia kupanda kitandani wanawaambia piga magoti hapo leo hupati mpaka useme ulikuwa wapi? Mnatutaabisha sio vizuri” alifafanua Mkuti.

Hata hivyo Mkuti alieleza kuwa pamoja na mateso na ukatili huo wanaofanyiwa wanaume lakini bado wameonyesha kuwa wavumilivu na kubakia kukaa kimiya kwa kuona aibu kueleza yanayowakuta.

Kwa upande wake Afisa mradi wa kuboresha huduma za kisheria (LIWOPAC) Bi Fatuma Nyama alisema kuwa takwimu zinaonyesha kuwa zaidi ya asilimia 77% ya mashauri mbali mbali yanayopokelewa kwa wasaidizi wa kisheria yanahusiana na wanawake huku asilimia 23% zikiwa ni za wanaume.

Alisema kuwa kati ya mashauri 558 yaliyopokelewa na shirika hilo kwa mwaka 2019 mashauri 430 yaliripotiwa na wanawake na mashauri 128 yaliripotiwa na wanaume.