Wednesday, January 15, 2020

DC KILWA AKERWA NA UCHELEWESHWAJI NAKALA ZA HUKUMU

NA HADIJA HASSAN, LINDI.

MKUU wa Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi Christopha Ngubiagai amesema ucheleweshwaji wa nakala za hukumu katika Mahakama ya Wilaya ya Kilwa ni Donda ndugu linalohitaji mwarobaini kwa baadhi ya wafungwa ambao wapo katika gereza la Wilaya hiyo Ngubiagai ameyasema hayo leo (jana) wakati akitoa salamu za Wilaya hiyo mbele ya Jaji Mkuu wa Tanzania Profesor Ibrahimu Juma katika khafla fupi ya ufunguzi wa jengo jipya la Mahakama Wilayani hapo lenye thamani ya shilingi milioni 705.

Ngubiagai alisema usimamizi wa sheria na utoaji haki bado unakabiliwa na changamoto nyingi ambapo miongoni mwa changamoto hizo ni kupungua kwa uadilifu kwa watumishi wachache wenye dhamana ya kusimamia sheria na kutoa haki.

Alisema wapo watumishi ambao wanadai rushwa, na wengine ambao wanatoa hukumu za upendeleo pamoja na kuchelewa kuandika hukumu na hata nakala za hukumu.

“Mfano katika gereza la Wilaya ya kilwa kuna jumla ya wafungwa 88 ambao wanatumikia vifungo vyao lakini hawajaweza kupatiwa nakala za hukumu zao” Ngubiagai alisema.

Ucheleweshwaji wa nakala hizo za hukumu zinawafanya wafungwa hao wanaoendelea kutumikia vifungo vyao kushindwa kuendelea na haki zingine ikiwemo ya kukata rufaa.

Kwa upande wake Jaji Mfawidhi wa Mahakama ya kanda Mtwara Paulo Ngwembe alisema kuwa kwa mujibu wa mwongozo na taratibu za Mahakama kuu zinataka nakala za hukumu pamoja na mienendo ya Mashauri zitolewe ndani ya siku 30 ambapo kwa Mtendaji yeyote wa Mahakama anaechelewesha kupatikana kwa vielelezo hivyo anahesabika anaihalifu mahaka.

“lakini sisi kama majaji na mahakimu katika kanda ya Mtwara tulikubaliana kwamba nakala za hukumu na mwenendo wa mashahuri zitolewe ndani ya siku (7), (14) mpaka 28 pale ambapo kutakuwa na hali isiyo ya kawaida hatukutaka kufikia ile iliyowekwa kwa mujibu wa uongozi wa mahakama kuu”

Kufuatia hali hiyo Jaji mkuu wa Tanzania Professor Ibrahimu Juma alitoa wito kwa watumishi watakao tumia jengo hilo kuwa wanapaswa kuliheshimu jengo hilo kama wanavyoyaheshimu majengo ya ibada na kwamba litumike kwa kazi tarajiwa ya kutoa haki pamoja na kutoa elimu ya sheria kwa umma.

Hata hivyo professor Ibrahimu aliongeza kuwa Mahakama inayoongozwa na professor Ibrahimu Juma haitakuwa na uvumilivu kwa mtumishi yeyote ambae anaharufu ya rushwa huku akieleza kuwa yeyote atakaebainika atashughulikiwa kwa mujibu wa Sheria.

MKAZI KIDUGALO AUAWA NA TEMBO

Na Omary Mngindo, Chalinze,

MKAZI wa Kijiji cha Kidugalo, Kata ya Bwilingu Halmashauri ya Chalinze Wilayani Bagamoyo Pwani John Taimu, amepoteza maisha kwa kushambuliwa na Tembo akiwa msituni.

Taimu ambaye inadaiwa alikwenda katika moja ya msitu uliopo Midulu jirani na msitu wa Kambi ya Jeshi, mwili wake umeokotwa ndani ya msitu huo, hatua inayoelezwa imetokana na mkazi huyo kwenda huko kutafuta kuni.

Diwani wa Kata ya Bwilingu Lucas Lufunga alimweleza Mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu kwamba, tukio hilo lililotokea january 13, 2020, mbali ya kuleta hofu kwa jamii, pia kifo hicho kimeacha simanzi kubwa kwa wanafamilia na wananchi wa maeneo hayo.

Amesema kuwa tangu Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli kuingia madarakani miaka minne iliyopita, imeweka mikakati madhubuti ya kudhibiti matukio ya mauaji ya Tembo, kumekuwepo na ongezeko kubwa la wanyama hao, hivyo kuongeza hofu kwa wananchi.

"Kwanza tunaishukuru Serikali kwa udhibiti wa matukio ya mauwaji ya wanyama hususani Tembo, hii imeongeza wingi wa wanyama hao kuzaliana, hivyo kutembea mpaka kwenye makazi ya watu kisha kusababisha uharibifu wa mali na majeruhi wananchi," alisema Lufunga.

Aidha diwani huyo amewaasa wananchi kuwa makini wakiwa katika shughuli zinazowaingizia kipato, kwani hivi sasa wanyama hao ndani ya Halmashauri ya Chalinze wameripotiwa kuongezeka, hivyo kusababisha madhara ikiwemo uharibifu wa vyakula mashambaani.

"Marehemu Taimu alikwenda katika msitu huo kwa lengo la kutafuta kuni, lakini kwa bahati mbaya akakutana na Tembo, waliosababisha kifo chake, ambapo mawili wake ulikutwa kwenye msitu huo, leo muda huu wa saa 7 mchana tunazika (jana)," alisema Lufunga.

Aidha amewataka wananchi kujilinda kwenye maeneo yenye wanyama, huku akiiomba serikali kuendelea na utoaji wa elimu kwa ili kukabiliana na tatizo linaonekana kushamiri maeneo ya Matipwili, Mkange, Kiwangwa na sasa Matulii.

Tuesday, January 14, 2020

MAJALIWA AMPNGEZA JAJI MKUU WA TANZANIA KWA UJENZI WA MAHAKAMA ZA KISASA.




NA HADIJA HASSAN, LINDI.

WAZIRI MKUU Kasimu Mjaliwa amempongeza jaji mkuu wa Tanzania Profesor Ibrahim Juma kwa kutumia teknolojia ya ujenzi wa gharama nafuu (MOLADI) inayoiwezesha Mahakama kujenga mahakama nyingi zenye ubora ,kwa muda mfupi na kwa gharama nafuu.

Majaliwa aliyasema hayo jana wakati akifungua jengo la Mahakama ya Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi, Lenye thamani ya Shilingi milioni 780.

Majaliwa Alisema mahakama ndio chombo cha kwanza kilichoweza kumuunga mkono Rais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania DK, John Pombe Magufuli, kwa kutumia vizuri fedha ya Serikali



“kama ambavyo mmesikia jengo hili na thamani yaeke ni milioni 780, nataka niwajulishe gharama hii ni ya chini ukilinganisha na zabuni zilizokuwa zinatolewa za kujenga mahakama, na hiyo ndio ilikuwa inafanya mahakama nyingi Nchini zikashindwa kujengwakwa sababu ya gharama.


“hata mahakama hii pamoja na mahakama hile ya kibaa na mahakama zilizotangulia, baada ya kuwa zimerushwa zabuni kutafuta wazabuni wa kujenga zilipatikana zabuni mbili ambapo mzabuni wa kwanza alitaka kujenga kwa bilioni moja na milioni mia saba na mzabuni wa pili alitaka kujenga kwa bilioni moja na milioni miatano , mahakama iliacha na wakasema watatafuta utaratibu wa kujenga ambao ni wakutumia (MALODI)” aliongeza Majaliwa.


Majaliwa alisema mahakama ni chombo muhimu katika kudumisha amani na kuleta maelewano ndani ya Nchi au jamii kupitia mahakama migogoro mingi hupata usuluishi na hivyo kuimarisha hali ya amani na utulivu.

Aliongeza kuwa Mahakama inapokuwa imara Taifa letu hubaki salama na kufanya wananchi waliopo katika taifa hilo kuendelea kufanya kazi zao za kujiletea maendeleo hivyo mahakama ni mhimili muhimu katika Nchi.

Awali Jaji Mkuu wa Tanzania Profesor Ibrahim Juma alisema kuwa kwa muda mrefu, Mahakama ya Tanzania imekuwa ikikabiliwa na changamoto kubwa ya uhaba, na uchakavu wa majengo katika ngazi zote za Mahakama, yaani—Mahakama za Mwanzo, Mahakama za Wilaya, Mahakama za Hakimu Mkazi (Mahakamaza Mikoa), Mahakama Kuu na hata Mahakama ya Rufani.


Alisema Ili kukabiliana na ukubwa wa changamoto ya upungufuna na uchakavu wa majengo yake, Mahakama ya Tanzania ilitayarisha Mpango wa Miaka Mitano wa Maendeleo ya Miundombinu (2016-2021). Ambao umetathmini hali ya majengo ya Mahakama katika Mikoa na Wilaya zote za Tanzania Bara, ambao umelenga kupunguza au kuondoa kabisa uhaba na uchakavu. Jengo jipya la Mahakama ya Wilaya ya Ruangwa ni kielelezo cha utekelezaji wa Mpango wa Miaka Mitano wa Maendeleo ya Miundombinu ya Mahakama ya Tanzania.

Hata hivyo aliongeza kuwa pamoja na uzinduzi wa miradi iliyokamilika,inayoendelea na ile iliyopo hatua za kukamilika, hivi karibuni wanatarajia kuanza miradi mipya katika maeneo mbalimbali hapa nchini ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi.

Miradi hii yote inayotekelezwa ni matokeo ya mikakati na mipango madhubuti waliyojiwekea kama taasisi kupitia mpango mkakati wa miaka mitano Nae Bashiru kauchumbe Mkazi wa Wilaya ya Ruangwa aliishukuru serikali ya Awamu ya Tano kwa kuwasogezea karibu huduma hiyo ya kimahakama kwani hapo awali walilazimika kusafiri umbali wa kilomita 180 kufuata huduma hizo za mahakama ya wilaya mjini Lindi.

“Wapo wananchi wengi, ambao kwa umbali huo hadi mjini Lindi, waliamua kuacha kufugua mashauri yaliyostahili kufunguliwa mahakama ya wilaya kwa hatua zaawali.

Wapo pia wale ambao walishindwa kutafuta haki ya rufaa katika Mahakama ya Wilaya. Hata kwa wale walidhubutu kwenda Lindi, umbali huo uliwaathiri kwa kutumia muda wao mwingi kutafuta huduma za Mahakama, badala ya kuendelea na shughuli zao za kiuchumi na kijamii” alieleza mwananchi huyo.

SALMA KIKWETE ATAKA MATUSI YAKOMESHWE

Na Omary Mngindo, Bagamoyo

 MKE wa Rais Mstaafu wa Serikali ya awamu ya nne Mama Salma Kikwete, ambae ni Mbunge wa kuteuliwa,  ameitaka jamii kushirikiana ili kukomesha lugha za matusi zinazotolewa kwenye vituo vya mabasi.

Mama Salma alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki katika Kijiji cha Zinga Kata ya Zinga, kwenye mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Jumuia ya Wanawake ya UWT wilaya ya Bagamoyo, akijibu malalamiko ya Mwalimu Luciana Magige aliyelalamikia lugha chafu vituo vya mabasi.

Alisema kuwa vitendo vya matusi vinazidi kukithiri katika jamii, hivyo amewataka wananchi kuwafichua kwa kuandika majina yao kisha kuyawasilisha kwa viongozi hatimae wahusika kufikishwa vituo vya Polisi ili hatua zichukuliwe.

"Hizi tabia za matusi zinazidi kushika kasi, kama Mwalimu Magige alivyosema kuhusiana na matusi katika vituo vya mabasi vilivyokithiri, tuandike majina yao kisha tuyawasilishe kwa viongozi kwenye maeneo yetu ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa," alisema Mama Salma.

Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo Dkt. Shukuru Kawambwa aliyeambatana na mbunge mwenzake Mama Salma Kikwete, yeye alisema kuwa hali hiyo imekuwa changamoto kubwa katika jamii, hivyo amewaomba wananchi kukomesha vitendo hivyo kwa kuweka mikakati madhubuti.

"Kiukweli hali si shwali katika vituo vya mabasi wakati mwingine hata mitaani, niwaombe niwaombe wananchi wenzangu tuuchukue ushauri wa Mama Salma, kisha tuufanyiekazi ili kukabiliana na changamoto hiyo," alisema Dkt. Kawambwa.

Awali Mwalimu Magige aliiambia hadhara hiyo kwamba vijana wanaojihusisha na shughuli za kuitia abiria katika mabasi wanatoa lugha za matusi hali inayiwadhalulisha watu wazima, pia kuwaambukiza watoto lugha hizo.

Mbali ya changamoto ya matusi katika vituo hivyo pia Mama Salma amepokea kilio cha wasafiri wanaotokea Bagamoyo kuelekea jijini Dar es Salaam ambapo wanalazimila kupanda mabasi matatu badala ta moja kama ilivyokuwa hali awali.