Saturday, July 27, 2019

NAIBU WAZIRI MAVUNDE AWATAKA VIJANA KUENZI MCHANGO WA BABA WA TAIFA

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde akizungumza na Viongozi, Watumishi wa Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro na wakazi wa Marangu wakati wa hafla fupi ya kuwaaga vijana watakaopanda Mlima Kilimanjaro ikiwa ni ishara ya kumbukizi ya miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere.

....................................

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde (Mb) amewataka vijana kuenzi mchango wa Baba wa Taifa, Mwl. Julius Kambarage Nyerere kwa kuwa wazalendo na wenye mshikamano katika kujenga Taifa.


Mhe. Mavunde amesema hayo wakati wa hafla fupi ya kuwaaga vijana kutoka Mkoa wa Songwe, Arusha, Tanga, Kaskazini Unguja na Kusini Unguja kabla ya kupanda Mlima Kilimanjaro ikiwa ni ishara ya kumbukizi ya miaka 20 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Nyerere iliyofanyika Mkoani Kilimanjaro katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA).


Alisema kuwa vijana wanapaswa kuwa wazalendo kwa kuiga kivitendo yale yote yaliyotendwa na waasisi wa taifa hili, Mwl. Julius K. Nyerere na Hayati Mzee Abeid Karume kwa kuendelea kudumisha upendo, amani na mshikamo kwa mustakabali wa Taifa.


“Vijana waliowengi kipindi hiki wameweka pembeni uzalendo wa kulipenda taifa lao hali ambayo inatubidi tujitahmini na kuenzi falsafa walizokuwa nazo waasisi wetu ambao waliweka maslahi ya Taifa mbele wakati wote,” alisema Mavunde.


Akitolea mfano wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, namna ambavyo amekuwa mstari wa mbele katika kuwatumikia wananchi kwa kutekeleza masuala mbalimbali ya kitaifa wakati wote ili nchi isonge mbele kimaendeleo.


Pia alitumia nafasi hiyo kuwapongeza vijana waliopanda mlima huo awamu ya kwanza na awamu hii ya pili kwa kuonesha ushujaa na uzalendo kwa Taifa lao ikiwemo kuwa mabalozi wazuri katika kutangaza sekta ya utalii.


Aidha, Naibu Waziri Mavunde alitoa wito kwa vijana kuacha kukaa kwenye vijiwe na kujihusisha kwenye mambo yasio na tija, bali wajishughulishe kwenye miradi mbalimbali itakayo wawezesha kiuchumi na kusaidia kukua kimaendeleo, kwa kuwa waasisi wa taifa walikuwa wachapakazi, waadilifu na wabunifu ambao ni mfano mzuri wa kuigwa.


“Hakuna nchi yoyote dunia ambayo inaweza kuendelea pasipo kuhusisha nguvu kubwa ya vijana katika maendeleo ya taifa,” alieleza Mavunde
Aliongeza kuwa ili kufikia malengo kwenye uchumi wa viwanda ni lazima vijana wazingatie uzalendo, utaifa na bidii katika kazi.


Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Mhe. Kippi Warioba alisema kuwa kitendo cha vijana hao kushiriki katika kupanda Mlima huo ni jambo muhimu kwa taifa na inaashiria namna gani vijana wameanza kutambua historia ya waasisi wa taifa lao.


Naye, Kiongozi wa Vijana hao waliopanda Mlima Kilimanjaro Bw. Augustine Gusha aliunga mkono maelezo yaliyotolewa na Naibu Waziri na alitumia nafasi hiyo kuwasihi vijana kudumisha amani ya nchi wakati wote.


Katika Mbio za Mwenge wa Uhuru Mwaka 2019, Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Idara ya Maendeleo ya Vijana inaratibu shughuli ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa Vijana 100 kwa ajili ya kumbukizi ya Miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.


Awamu ya kwanza vijana walipanda mlima huo tarehe 26 Machi, 2019 na awamu ya pili 26 Julai, 2019. Awamu ya Tatu itakuwa mwezi Oktoba.

Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Mhe. Kippi Warioba akielezea jambo kwa vijana 8 walioshiriki katika shughuli hiyo ya kupanda Mlima Kilimanjaro ikiwa ni kuadhimisha kumbukizi ya miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere. Kushoto ni Mkurugenzi wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Bi. Mwanaidi Ali.

Baadhi ya Watumishi wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde (hayupo pichani) wakati wa hafla ya kuwaaga vijana hao.

Sehemu ya Vijana wanaotarajiwa kupanda Mlima Kilimanjaro kwa awamu ya pili wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde (hayupo pichani) kabla ya kuanza safari ya kupanda Mlima huo, Julai 26, 2019.

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde akiwaaga Vijana hao nane (8) kutoka Mkoa wa Songwe, Arusha, Tanga, Kaskazini Unguja na Kusini Unguja alipowasindikiza vijana hao waliokuwa wakipanda Mlima huo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mhe. Kippi Warioba.

Kilo 300 za mirungi zakamatwa Dar









Kabuta akionesha dawa za kulevya aina ya zilizokamatwa jijini Dar es Salaam.
Na Christina Gauluhunga, Dae es Salaam
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini, imefanikiwa kukamata kilo 300 za Dawa za Kulevya aina ya mirungi ambayo ilikuwa ikisafirishwa kwenda nchi za Ulaya hasa Uingereza ikidaiwa kuwa ni majani ya mronge.
Nyingine zimeandikwa kwa majina bandia ili zitambulike kama majani ya ‘morning tea’, ‘morning tea’, ‘tea leaves’, dawa za asili na majani ya mboga.
Hyao yamesemwa na Kamishna wa Intelijensia wa mamlaka hiyo, Fredrick Kibuta, wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 26, jijini Dar es Salaam, ambapo amesema katika tukio hilo watuhumiwa wawili ambao majina yao yamefichwa kwa uchunguzi zaidi wapo mbaroni.
Amesema kwa kushirikiana na Shirika la Posta, Wizara ya Kilimo na Mifugo, Wizara ya Maliasili na Utalii wamefanikiwa kukamata kilo hizo kwenye vifurushi vilivyokuwa vikiingizwa nchini kwa njia ya Posta kwenda nchi za Ulaya.
Amesema vifurushi hivyo vilikuwa vikitumia majina bandia ambapo uchunguzi wa kimaabara wa Mkemia Mkuu wa Serikali umethibitisha majani hayo yana kemikali Aina ya Cathinone ambayo inapatikana kwenye mmea was mrungi.
“Kuna taarifa ya uwepo wa usafirishaji wa kiasi kikubwa wa dawa za kulevya kutoka nchini kwenda nchi za Ulaya kwa njia ya Posta ambapo ilibainika dawa hizo zikiingizwa nchini kutoka nchini Ethiopia kama majani ya mronge kisha kufungwa tena na kwenda nchi za Ulaya, “amesema Kibuta.

Brela yajipanga kutumia maonyesho ya nanenane Simiyu kurasimisha shughuli zisizo rasmi.




Na Selemani Magali; Dar es Salaam.


Wakala wa usajili wa biashara na leseni (Brela) imesema itashiriki kwa nguvu zote katika maonyesho ya nanenane ya mwaka 2019, msisitizo ukiwa ni kuwahamasisha wananchi kurasimisha shughuli zao za uzalishaji ikiwamo mifugo, kilimo na uvuvvi.

Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu afisa Mtendaji Mkuu wa Brela Emmanuel Kakwezi amesema Brela imejipanga vizuri kutoa elimu kuhusu shughuli zinazofanywa na wakala, na kwamba watawashashiwi washiriki na raia watakaotembelea maonyesho hayo juu ya umuhimu wa kurasimisha shughuli zao

Mbali ni dhima ya kuwashauri wananchi kuhusu kurasimisha shughuli zao ambazo mara nyingi zimkuwa zikitumika kwa matumizi ya nyumbani, wanaamini baada ya elimu hiyo watabadilika na kusajili shughuli zao ili ziwaletee manufaa Zaidi.



“Kipindi hiki brela itakuwa inatoa huduma zake palepale viwanja vya simiyu, Brela itakuwa inatoa huduma zake zote ikiwamo kusajili makampuni, kusajili majina ya biashara, kutoa leseni, kusajili alama za biashara kutoa hati na leseni za viwanda,” alisema Kakwezi

Amesema wanataka kuona shughuli uvuvi, kilimo na ufugaji haziishi kukidhi haja ya matumizi ya nyumbani tu, zinatakiwa ziwe shughuli za kibiashara, Brela itawawaeleza utaratibu namna wanavyoweza kusajili makampuni na kuwasaidia namna ya kupata masoko.

 Amesema Brela imejipanga vizuri, tayari wana business portal (mfumo wa kuuza bidhaa nje ya nchi), watatoa elimu hiyo ili kuwafanya jamii ijue namna gani wanavyoweza kuuza bidhaa zao nje ya mipaka ya Tanzania.

Mkurugenzi ametoa wito kwa Wananchi kutembelea banda la Brela kwa sababu limesheheni wataalamu ambao watawasaidia kupata maelezo yote yanayohusu huduma zinazotolewa na  Brela pamoja na kupata elimu ya kurasimisha shughuli zao.

“Wananchi wote watakaofanikiwa kufika katika maonyesho ya mwka  huu wahakikishe wanapita katika banda la Brela ili kujipatia elimu.

Tutawaeleza utaratibu wa kuweza kusajili makampuni, tuwaonyeshe namna gani wanaweza kupata leseni, lakini pia kuwaeleza namna watakavyoweza kupata soko zuri kwa kuuza bidhaa zao,” alisema



MAKAMU WA RAIS KUFUNGUA NANENANE 2019

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019, yatakayofanyika Viwanja vya Nyakabindi Mjini Bariadi kuanzia tarehe 29/07/2019 hadi 08/08/2019.





Akizungumza Jijini Dar es salaam Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema maonyesho hayo yatakuwa ya tofauti sana ukilinganisha nay a mwaka jana, kwa sababu wamefanikiwa kuboresha baadhi ya mambo ikiwamo utoaji wa semina, warsha kwa washiriki wote wa maonyesho hayo.



Mtaka amesema Mhe Makamu wa Rais atafungua rasmi maonesho hayo Agosti Mosi, 2019 na kwamba jumla ya waonyeshaji 300 tayari wameshajiandikisha kushiriki maonyesho hayo.

“Taasisi, Mashirika mbalimbali na wajasiriamali wataanza kuonesha teknolojia, huduma na bidhaa zao Julai 29, 2019, nataka nitumie nafasi hii kawashauri wajasiliamali, wafanyabiashara, wakulima, wavuvi, wafugaji kujitokeza kwa wingi katika maonyeshoya mwaka huu, tumeyaboresha sana na kuna vitu vingi vyenye tija” Alisema Mtaka



Amesema maonyesho hayo yatakaribisha viongozi wa Kitaifa, Agosti 03, 2019 tutakuwa na Mhe. Waziri Mkuu, Agosti 06, 2019 tutakuwa na Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda na kilele chake yanatarajiwa kutembelewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ambaye atayafunga maonyesho hayo..



Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Omary Mgumba amesema ameridhishwa na maandalizi ya Maonesho ya nanenane yanayoendelea mkoani Simiyu na kutoa wito kwa wakulima na wananchi wote kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kushiriki katika maonesho haya ili kuja kujionea teknolojia mbalimbali zitakazojibu changamoto za wakulima, wafugaji na wavuvi.



Aidha, Mhe. Mgumba ametoa wito kwa waoneshaji kuwa wabunifu katika teknolojia, huduma na bidhaa watakazoonesha ili maonesho haya yawe  chachu ya kuwasaidia wakulima, wavuvi na wafugaji  kuongeza tija katika uzalishaji



Naye Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe. Adam Malima amesema matarajio ya mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga inayounda Kanda ya Ziwa Mashariki ni kuwa na maonesho ya tofauti na mwaka jana, lengo likiwa ni kuifanya kanda hiyo kuwa ni mahali pa kudumu pa wakulima, wafugaji na wavuvi kuwa na maonesho ya kilimo biashara.



Maonesho ya Nanenane Kitaifa yanafanyika kwa mara ya pili sasa mkoani Simiyu tangu Kanda ya Ziwa ilipogawanywa katika kanda mbili yaani, Kanda ya Ziwa Mashariki(Simiyu, Mara na Shinyanga) na Kanda ya Ziwa Magharibi(Mwanza, Geita na Kagera) ambapo mwaka huu yanaadhimishwa chini ya kauli Mbiu:-“KILIMO, MIFUGO NA UVUVI KATIKA UKUAJI WA UCHUMI WA NCHI”


WALIOSAMBAZA PICHA ZA WANAWAKE MTANDAONI KUSHTAKIWA


Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu LHRC Anna Henga

Mtandao wa kupinga Ukatili wa Kijinsia (MKUKI) umesikitishwa na vitendo vya kusambazwa kwa picha zinazoonesha wanawake wanne, katika mitandao ya kijamii waliokuwa wakituhumiwa na kushikiliwa katika kituo cha polisi cha Mburahati Jijini Dar es Salaama kwa makosa ya jinai.

Akitoa tamko kwa niaba ya mtandao huo, Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu LHRC Anna Henga, amesema vitendo hivyo ni vya udhalilishaji wa utu wa mwanamke, ukiukwaji wa haki za binadamu pamoja na kuingilia uhuru wa faragha.

"Katika hali isiyokuwa ya kawaida picha za wanawake hao zilisambaa mitandaoni na imethibitika kwamba zilipigwa na maofisa wa polisi wa kituo cha Mburahati na tuliongea na Mkuu wa kituo hicho na akathibitisha kwa kusema zilipigwa kwa manufaa ya kikazi lakini tukaziona kwenye mitandao'' Amesema Anna Henga.

Aidha mtandao huo umetoa wito kwa Jeshi la polisi, kuwachukulia hatua za kinidhamu wahusika wa kitendo hicho ili kulinda utu wa mwanamke na watuhumiwa wa makosa ya jinai.

Ameongeza kwamba mtandao huo hautosita kuchukua sheria, ikiwemo kufungua mashtaka kwa wahusika wa tukio hilo.

Rais Magufuli Aagiza Uchunguzi wa HARAKA wa Matumizi yz Bilioni 15 za TAZARA