Sunday, July 7, 2019

JAHAZI ZAKAMATWA BAGAMOYO KWA KUBEBAA MKAA WA MAGENDO.






Meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) wilaya ya Bagamoyo, Ally Khalfan, akimuonesha Katibu Tawala wilaya ya Bagamoyo, Bi kasilda Mgeni, Majahazi yaliyokamatwa kwa kubeba mkaa wa magendo, majahazi hayo yalikamatwa Bandari bubu ya mto shanga kitongoji cha RAZABA kata ya Makulunge wilayani humo.

....................................


Wakala wa Huduma za Misitu nchini (TFS) wilaya ya Bagamoyo, wamekamata majahazi mawili yaliyobeba mkaa gunia zaidi ya mia mbili katika Bandari bubu ya mto shanga, kitongoji cha RAZABA kata ya makulunge.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo, Bi Kasilda Mgeni, amewataka wananchi wilayani humo kufuata sheria za uvunaji na usafirishaji wa mazao ya misitu ili kuepuka usumbufu ambao wanaweza kuupata.

Akizungumza mara baada ya kufika eneo la tukio katibu tawala huyo alisema watakaokiuka sheria za uvunaji na usafirishaji wa mazao ya misitu serikali itawachukulia hatua za kisheria.

Alisema kutofuata sheria katika uvunaji wa misitu kunapelekea uvunaji holela jambo ambalo ni hatari kwa ustawi wa mazingira.

Alisema misitu inahifadhiwa kwaajili ya utunzaji wa mazingira hivyo shughli zote za uvunaji wa mazao ya misitu ni lazima zifuate sheria na kupata maelekezo kutoka kwa wataalamu wa misitu.

Aliongeza kwa kusema kuwa, uharibifu wa mazingira unaosababishwa na uvunaji holela utapelekea kuwa na maeneo yenye majangwa na kukosa mvua kwa wakati jambo ambalo pia litasababisha ukame wa mazao ya binadamu na wanyama.

Aidha, alibainisha kuwa, utoroshaji wa mazao ya misitu unapelekea pia kuikosesha serikali mapato ambayo kimsingi ndiyo yanategemewa kuleta maendeleo katika jamii.

Alisema serikali haikatazi wananchi kufanya shughuli zao lakini kinachotakiwa ni kufuata sheria na taratibu zilizowekwa ili mwananchi ajiongezee kipato, mazingira yatunzwe huku serikali ikiwa inainaingiza mapato kwaajili utekelezaji wa huduma za jamii.

Kwa upande wake Meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) wilaya ya Bagamoyo, Ally Khalfani amesema kitendo hicho ni kinyume cha sheria ya misitu namba 14 ya mwaka 2002 na muongozo wa uvunaji wa mazao ya misitu wa mwaka 2017.

Alisema kukamatwa kwa majahazi hayo ni muendelezo wa doria zinazofanywa na kikosi cha TFS kwa kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ili kubaini watoroshaji wa mazao ya misitu.

Hivi karibuni Wakala wa Huduma za Misitu wilaya ya Bagamoyo walifanya semina elekezi kwa watumiaji wa majahazi na bodaboda zinazobeba mkaa ili kuwafahamisha sheria za usafirishaji wa mazao ya misitu na kuwasisitiza kufuata sheria.

 

Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo, Bi Kasilda Mgeni, akizungumza na waaandishi wa habari eneo la tukio.

 

Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo, Bi Kasilda Mgeni, akitoa maelekezo kwa Meneja wa TFS wilaya, Ally Khalfani (kushoto) mara baada ya kufika kwenye bandari bubu ya mto shanga iliyopo kitongoji cha RAZABA kata ya makulunge, eneo hilo hutumika kwa uturoshaji wa mazao ya misitu na bidhaa nyingine za magendo.

  Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo, Bi Kasilda Mgeni, picha ya juu kulia na picha ya chini kushoto, akiwa anavuka mito na mikondo ya bahari ya hindi ili kuelekea kwenye bandari bubu ya mto shanga kujionea utoroshaji wa mazao ya misitu katika eneo hilo.

 

Utoroshaji wa mazao ya misitu licha ya kuharibu mazingiraa pia unaoikosesha serikaali mapato.

  Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo, Bi Kasilda Mgeni, akiongoza Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya wakielekea kwenye Bandari bubu ya mto shanga iliyopo kitongoji cha RAZABA kata ya Makulunge, kushoto ni 

  Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo, Bi Kasilda Mgeni, akiangalia tanuri la mkaa ambalo wahusika wa tanuri hilo hawakufuata sheria za uvunaji wa misitu na hivyo kusababisha uharibifu wa mazingira, Meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) wilaya ya Bagamoyo, Ally Khalfani


Watendaji wa TFS WILAYA YA Bagamoyo wakiwa katika eneo la tukioa baada ya kukamata majahazi mawili yaliyobeba mkaa kinyume cha sheria.

Mtafiti abuni kitasa kinachofunguliwa na simu






CHRISTINA GAULUHANGA – DA ES SALAAM
Mtafiti kutoka Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Filbert James, amebuni kitasa cha mlango wa nyumba kinachofunguliwa kwa simu ya mkononi ili kukomesha utumiaji funguo bandia.
Akizungumza na BAGAMOYO KWANZA BLOG  katika Maonyesho ya Sabasaba leo Jumamosi Julain 6, Filbert amesema kukamilika kwa mfumo huo kutasaidia pia kuepukana na suala la uvunjaji kufuli.
Amesema mfumo huo unasaidia kufungua geti la mlango unaotembea ambapo mtumiaji akishaingia geti hujifunga lenyewe.
“Ili kupata mfumo huu ni la lazima uwe na mlango wa kutembea na mota halafu unaingiza simu kadi ambayo ndio itakuwa inakuruhusu kama unafahamu namba yake ya simu na ukichukua namba nyingine kiholela inagoma hadi ile uliyoitambulisha kwenye mfumo,” amesema.

Saturday, July 6, 2019

Makamba Atoa Neno Mradi wa Magari ya Umeme Tanzania


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba amesema ni lazima athari za usafiri wa magari ya umeme kwenye mazingira ziangaliwe kabla ya huduma hiyo kuanzishwa.

Makamba ametoa mwongozo huo kupitia ukurasa wake wa Twitter kufuatia taarifa ya TANAPA jana Julai 5, 2019 kwamba inajipanga kuleta usafiri wa magari ya umeme ili kurahisisha utalii.

Taarifa ya TANAPA ilieleza hivi, ''Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA), inatarajia kuanzisha usafiri mpya wa kutumia magari ya umeme yanayopita kwenye nyaya (Cable Cars), kupeleka watalii Mlima Kilimanjaro''.

Leo Julai 6, 2019 Waziri Makamba amesema ''Inabidi watu wa Mazingira tupitishe na kutoa cheti kwanza kabla hawajaanza. Na tutafanya studies ili kujua impact kwa mazingira na uthabiti wa mitigation measures''.

Wakala wa misitu waandaa safari ya msitu wa magamba,




Na Selemani Magali; Daresalaam

WAKALA wa misitu Tanzania (TFS) imewataka watanzania kutembelea vivutio halisi ili kujionea utajili uliopo hapa nchini.

Imesema idadi ya watanzania waotembelea vivutuo vya asili ni mdogo licha ya kuwa wanalipia Sh2,000 pekee kama kiingilio katika maeneo hayo huku wageni wakilipa Dola 10 za kimarekani.

Kutokana na hilo Mamlaka ya misitu Tanzania (TFS) imeandaa safari ya siku tatu kwa ajili Wananchi watakaopenda kutembelea msitu wa Magamba uliopo katika eneo la Lushoto Mkoani Tanga.

Akizungumza katika maonyesho ya sabasaba wakati Naibu waziri wa Maliasili na utalii alipotembelea maonyesho ya 43 ya biashara ya kimataifa,  ofisa utalii na Mafunzo, Samiji Mlemba amesema safari hiyo ipo na wangependa kuona wananchi wanajitokeza kwa wingi kwenda kuona msitu wao uliopo hapo Tanga.

Mlemba alisema watanzania wengi wamekuwa wakishindwa kujua umuhimu wa kutembelea vitu vya asili na kujifunza ili kuweza kuongeza kitu kipya.

“Katika mwaka wa fedha ulioisha tulipokea watalii zaidi ya 3,000 na kati yake 594 pekee ndiyo walikuwa kutoka nchini na mara nyingi huonekana katika msimu wa sikukuu ya pasaka na Mwisho wa mwaka.” Alisema Mlemba

Alisema katika safari ya siku tatu waliyo iandaa wamejipanga kuhakikisha kuwa idadi ya watanzania wanaokwenda inakuwa kubwa ili waweze kujifunza na kutambua vivutio vilivyopo nchini.

“Katika eneo hilo kuna mahandaki ya vita ya kwanza ya dunia, maporomomo ya maji, nyumba za asili, shughuli mbalimbali zinazoendelea na ili kushiriki safari hii mtu mzima atalipia Sh171,000 na mtoto Sh148,000 ikijumuisha malazi, chakula na usafiri.” Alisema





Wadau PS3, GHSC TA – TZ, Waunga Mkono Juhudi za Serikali ya Awamu ya tano





Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dkt. Zainab Chaula akiongoza kikao cha pamoja baina ya Wizara ya TAMISEMI na Wizara ya Afya kilicho wakutanisha Wadau wa Maendeleo kujadili uboreshaji wa Mfumo wa GoTHOMIS ili uweze kutumika katika ngazi zote za kutolea huduma za Afya nchini (Picha na Maktaba ya TAMISEMI) 
…………………… 


Mkurugenzi wa Idara ya TEHAMA,Ofisi ya Rais TAMISEMI, Erick Kitali, akitoa mada wakati wa kikao hicho cha wadau juu ya uboreshaji wa Mfumo wa GoTHOMIS Ofisi za Wizara za Afya eneo la Mtumba mjini Dodoma. (Picha na Maktaba ya OR-TAMISEMI).

Na Atley Kuni- TAMISEMI. 

Wadau wa Maendeleo nchini kupitia mradi wa Uimarishaji Mifumo katika Sekta za Umma (Public Sector Strengthening System-PS3) na (Global Supply Chain Technical Assistance Tanzania-GHSC TA – TZ), wameitikia wito wa serikali na kujitokeza katika kufanikisha zoezi la kuimarisha mfumo wa Uendeshaji wa Shughuli za Afya katika maeneo yote yakutolea huduma za Afya serikalini, ujulikanao (Government of Tanzania Health Operations Management Information System -GoTHOMIS). Wadau hao wameitika wito kufutia maelekezo ya Serikali kutaka mfumo huo uimarishwe kwa kuongezewa maeneo ya kiutendaji. 

Akizungumza na Wadau wa Maendeleo mwanzoni mwa Mwezi Mei, 2019 Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula, wakati wa kikao cha pamoja baina ya Wizara hiyo na ile ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) alisema, umefika muda kwa wadau kuungana na kujenga mfumo wa GoTHOMIS kwani mfumo huo umeonesha kuwa na tija na ufanisi kwenye nyanja ya Afya. 

“Kwa Muda mrefu tumeshuhudia mifumo mbali mbali lakini yote hii ikiwa kwenye maeneo machache ya nchi ikifanywa kwa majaribio ambayo hata hivyo tija yake imekuwa sio yakuridhisha, alisema Chaula na kuongeza kuwa, suala lakutuambia unafanya shughuli ya Jamii halafu hatuoni tija ya unacho kifanya sio wakati wake kwa sasa, lazima wote tuungane na tukubali kutembea kwa pamoja na mfumo huu ambao umeonesha tija na ufanisi” alisema Dkt. Chaula. 

Wito wa Katibu Mkuu huyo, ulikuja wakati ambapo tayari mfumo ulikuwa umesimikwa kwenye maeneo yakutolea huduma za afya yapatayo 383 ikiwepo Zahanati 91, Vituo vya Afya 180, Hospitali Teule za Wilaya 12, Hospitali za Wilaya 77 na Hospitali za Rufaa za Mikoa 23 na kufanya asilimia 6 ya maeneo yote yakutolea huduma za afya nchini. 

Akiwasilisha mada katika kikao hicho juu ya uboreshaji wa mfumo wa GoTHOMIS, Mkurugenzi wa TEHAMA Ofisi ya Rais TAMISEMI, Erick Kitali, alisema shabaha iliyo mbele yao nikuimarisha mfumo kwa kutumia wataalam wazawa na wanaamini katika nguvu ya pamoja ikiwepo kushirikiana na wadau wa maendeleo wote. 


Akizungumza kando ya wataalam wanao endelea na kazi ya uimarishaji wa mfumo huo mkoani Morogoro, Mtaalam kutoka Global Supply Chain Tanzania, Alfredy Mchau, alisema wamewiwa kuunga mkono juhudi za serikali katika kuimarisha mfumo huo wa GoTHOMIS kwani ni moja ya vipaumbele vyao katika kushirikiana na serikali kuboresha huduma za Afya kwaajili ya upatikanaji wa taarifa sahihi na kwa wakati. 

“Alipotoa wito Katibu Mkuu, kwa wadau juu ya kuunga mkono suala hili, sisi kama Global Supply Chain Technical Assistance Tanzania (GHSC TA – TZ), tulielewa nini dhamira ya Serikali hii ya awamu ya tano inayo ongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, katika sekta ya Afya, ambayo kimsingi ndio msingi wa maendeleo ya nchi yoyote. 

Mchau aliongeza kuwa, GHSC TA – TZ ilikwisha anza harakati za uboreshai wa mfumo wa GoTHOMIS ili uweze kubadilishana taarifa na mfumo wa eLMIS ili kuboresha upatikanaji wa taarifa za dawa, vifaa tiba na vitendanishi nchi nzima hivyo tunaamini kwa nguvu hii ya pamoja tutapiga hatua kubwa katika kuihudumia jamii, kwani Umoja ni Nguvu na Utengano ni Udhaifu” alisisitiza Mchau. 

Kwa upande wake mmoja wa wafanyakazi kutoka mradi wa kuimarisha Mifumo ya Sekta za Umma nchini PS3 Mhandisi, Revocutus Mtesigwa, alisema huo ni muendelezo wa juhudi ambazo wamekuwa nazo hususan katika uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma nchini. 

“PS.3 Hii kwetu ni muendelezo wa shughuli ambayo tayari tulisha anza hapo awali, kwani tayari kuna maeneo yakutolea huduma za Afya yasiyo pungua 400 ikiwepo Hospitali, Vituo vya Afya na Zahanati tumewezesha kufungwa kwa mfumo na unafanyakazi, maeneo ambayo kama mradi tuliokwisha fanyia kazi ni eneo la Mafunzo kwa watumiaji, ufungaji Miundombinu ya Mtandao Kiambo (Local Area Network-LAN), hivyo Kauli ya Katibu Mkuu kwetu ilituongezea chachu na ari yakuendelea kushirikiana zaidi na Serikali lakini pia Wadau wengine wa Maendeleo katika kujenga nchi. 

Serikali bado inaendelea kuwakaribisha wadau wa maendeleo kujitokeza kwaajili yakufanikisha uboreshaji wa Mfumo wa GoTHOMIS, ambao utakuwa Madhubuti na wenye tija katika ngazi zote za kutolea huduma za Afya nchini.