Saturday, April 27, 2019

SUBIRA MGALU AKAGUA VIKUNDI CHALINZE.

 Kina mama wa kikundi cha "NAMNYAKI" kilichopo kata ya Lugoba Halmashauri ya Chalinze wakimvisha vizuri mkufu, Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Pwani, Mh. Subira Hamisi Mgalu, alipokuwa kwenye ziara ya kutembelea vikundi vilivyokopeshwa na Halmashauri ya Chalinze, Mkufu huo ambao mara nyingi huvaliwa na jamii ya kimasai alipewa zawadi na vikundi vya kata ya Pera katika Halmashauri hiyo.
 
 Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Pwani, Mh. Subira Hamisi Mgalu, akivishwa Mkufu na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT) kata ya Pera Tatu Bakari Mpogo, Mkufu huo umepewa zawadi kutoka kwa kina mama wa kata ya Pera Halmashauri ya Chalinze alipokuwa katika ziara ya kutembelea vikundi vilivyokopeshwa na Halmashauri hiyo.
........................................ 


Halmashauri ya Chalinze ambayo imeanzishwa mwaka 2015, imeshakopesha milioni 900 kwa vikundi mbalimbali vya wanawake vijana na walemavu kwaajili ya kujiendeleza katika shughuli za kiuchumi.


Hayo yamebainishwa jana Aprili 26, 2019 na Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Pwani, Mh. Subira Hamisi Mgalu alipokuwa kwenye ziara katika Halmashauri hiyo kukagua vikundi vilivyopata mikopo ili kujua maendeleo ya vikundi hivyo.


Subira mgalu ambae ni miongoni mwa wanaopitisha mipango ya Halmashauri hiyo kupitia Baraza la Madiwani alisema ni wajibu wake kupitia vikundi hivyo ili kujiridhisha kama fedha zilizotolewa zimeleta mafanikio au la.


Katika ziara hiyo ameweza kutembelea kata nane za Halmashauri ya Chalinze ambapo amejionea vikundi mbalimbali vilivyokopeshwa na kurejesha kwa wakati.


Baadhi ya kata hizo ambazo vikundi vyake vimepewa miokpo ni pamoja na Bwilingu milioni 88, Msata milioni 70 huku kata ya Msoga ikiwa imepata milioni 49.5 kwaajili ya vikundi vyake.


Mgalu alisema kupitia Halmashauri ya Chalinze vikundi vinaweza kujikwamua kiuchumi kwa kukopeshwa fedha kwaajili kujiendeleza kiuchumi.


Alisema serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wake Rais Dkt. John Magufuli inatambua changamoto wanazopata wananchi kiuchumi ndiomana imeamua kutoa mikopo isiyokuwa na riba ili kuwainua kiuchumi kupitia vikundi vyao.


Wakati huo huo Mgalu ametoa ahadi ya kutafuta walimu wa kufundisha namna ya kutengeneza bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na wajasiliamali ili kuwaongezea ujuzi katika maswala ya kujiongezea kipato.


Aliongeza kwa kusema kuwa, Halmashauri ya Chalinze imekuwa ya kwanza katika ukopeshaji ndani ya mkoa wa Pwani wenye Halmashauri tisa.


Alisema kufuatia hali hiyo, Halmashauri ya Chalinze imeshika nafasi ya kumi kitaifa kati ya Halmshauri 185 zailizopo nchini.


Wakielezea mafanikio waliyopata kupitia mikopo hiyo wanavikundi hao wamesema mikopo hiyo imewainua kiuchumi hali iliyopelekea baadhi ya vikundi kununua magari huku vikundi vikiwa tayari vimemudu kujiendesha bila ya kukopa tena na badala yake wanajikopesha wenyewe ndani ya vikundi kutokana na akiba walizonazo.


Jailani Hafidhi ni katibu wa kikundi cha Walemavu Tunaweza Chalinze (TUCHA) kilichopo kata ya Lugoba amesema kikundi cha wamekopeshwa milioni tatu na kwamba fedha hizo zimewawezesha kuendesha biashara utengenezaji wa maua na kuyauza.


Jailani alisema anaipongeza Serikali ya awamu ya tano ikiongozwa na Rais Magufuli kwa kuwajali walemavu ili nao waweze kufanya shughuliza kujiongezea kipato kupitia mikopo hiyo.


Aidha, alisema katika hali isiyo ya kawaida Rais Dkt. Magufuli ameonyesha kuwajali walemavu kwa kuwapa nafasi mbali mbali wizarani jambo ambalo limewapa faraja walemavu.


Nae katibu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Pwani, Getrude Boniface Sinyiza, amesema wananchi waache kudanganywa na watu wanaodai kuwa watawapa mikopo kwa kulipa gharama kidogo na badala yake waunde vikundi ili wapate mikopo inayotolewa na serikali bila ya kutoa kiasi cha fedha.


Alisema mikopo ya serikali inatolewa kwa kukidhi vigezo kupitia vikundi na sio kwa kutoa fedha kama usajili hivyo wananchi wakaacha mikopo yenye mashaka ili kuepuka usumbufu.

katibu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Pwani, Getrude Boniface Sinyiza, akizungumza na wanavikundi katika Halmashauri ya Chalinze wakati wa ziara ya Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Pwani, Mh. Subira Hamisi Mgalu, (aliyekaa chini katikati) iliyolenga kukagua vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu katika Halmashauri hiyo, wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Bagamoyo, Rukia Masenga.

Kushoto ni katibu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Pwani, Getrude Boniface Sinyiza, katikati ni Katibu msaidizi wa UWT Mkoa wa Pwani, na kulia ni Mjumbe wa Kamati ya utafiti ya UWT Mkoa wa Pwani, Salama Shaibu, ambao waliungana na Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Pwani, Mh. Subira Mgalu katika ziara ya kukagua vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu katika Halmashauriya Chalinze
    Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT) kata ya Pera Halmashauri ya Chalinze, Tatu Bakari Mpogo, (kushoto) akimkabidhi zawadi ya kikapu Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Pwani, Mh. Subira Hamisi Mgalu, wakati alipofanya ziara ya kukagua vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu katika Halmashauri hiyo.

Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Pwani, Mh. Subira Hamisi Mgalu, akizungumza na wana vikundi kata ya Pera Halmashauri ya Chalinze.


 
Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Pwani, Mh. Subira Hamisi Mgalu,akijaribu Gari ambalo limenunuliwa na kikundi cha Amani kilichopo kata ya Bwilingu.


 Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Pwani, Mh. Subira Hamisi Mgalu, akifurahia jambo na wana vikundi Chalinze, wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Bagamoyo, Rukia Masenga.

 Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Pwani, Mh. Subira Hamisi Mgalu, (kulia) akiangalia maua yanayotengenezwa na kikundi cha Walemavu Tunaweza Chalinze (TUCHA) kilichopo kata ya Lugoba, katikati ni Katibu wa kikundi hicho, Mwalimu Jailani Hafidhi, na Kushoto ni Diwani wa kata hiyo Rehema Mwene.
 
Baadhi ya viongozi wa vikundi wa kata ya Lugoba Halmashauri ya Chalinze wakimsikiliza Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Pwani, Mh. Subira Hamisi Mgalu wakati alipofanya ziara ya kukagua vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu katika Halmashauri hiyo.
  Baadhi ya viongozi wa vikundi wa kata ya Msoga Halmashauri ya Chalinze wakimsikiliza Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Pwani, Mh. Subira Hamisi Mgalu wakati alipofanya ziara ya kukagua vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu katika Halmashauri hiyo.

DC MSHAMA AWAASA MADEREVA BODA KULIPIA VITAMBULISHO VYA UJASIRIAMALI

NA MWAMVUA MWINYI, KIBAHA

MKUU wa wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshama, amewaasa madereva wa pikipiki maarufu kama bodaboda, kulipia vitambulisho vya wajasiriamali na endapo watashindwa kufanya hivyo hawataruhusiwa kufanya biashara ya kubeba abiria.


Mkuu huyo wa wilaya aliyasema hayo mjini Kibaha alipokuwa akizungumza na madereva hao na kusema, wao ni moja ya kundi ambalo linapaswa kuwa na vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo ambapo wanatakiwa kulipia shilingi 20,000.


Mshama alisema kuwa agizo la watu wanaofanya biashara ambayo mtaji wake hauzidi kiasi cha sh.milioni nne wanapaswa kuwa na vitambulisho hivyo.


“Mnapaswa kununua vitambulisho hivyo na kwa wale ambao hawatakuwa na vitambulisho hivyo hawataruhusiwa kufanya biashara hiyo hivyo hakuna budi kila mmoja wetu kuhakikisha analipia kiasi hicho ili waweze kufanya kazi bila ya usumbufu,” alisema Mshama.


Aliwataka wafanyabiashara wengine nao kulipa ili wapatiwe vitambulisho ambavyo Rais ametaka wajasiriamali wadogo wawe navyo kwani nao wanachangia uchumi wa taifa.


“Tunaendelea kuwahamasisha wajasiriamali wadogo wachangamkie fursa hiyo kwani ushuru waliokuwa wakilipa kwa sasa utakuwa haupo na kitambulisho hicho ndicho kitakuwa kimefidia na haitaruhusiwa kufanya bishara kama hawana vitambulisho hivyo,” alisema Mshama.


Kwa upande wake Bakari Kapera wa kitengo cha elimu ya mlipa kodi kutoka mamlaka ya mapato (TRA) mkoa wa Pwani alisema kuwa  fedha wanazolipia leseni siyo kodi bali ni ada ili mtu kutambulika kuwa ni dereva.


Kapera alisema Leseni ya udereva ni tofauti na kitambulisho cha Ujasiriamli hivyo aliwataka madereva hao wasikwepe kutekeleza agizo hilo kwa kisingizio kuwa tayari wamelipia leseni za udereva.


 Stanley Ndunguru kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Anga na Majini (SUMATRA) alisema kuwa malipo hayo yanalipwa na mmiliki wa chombo na siyo wao kama madereva kwani hawaruhusiwi kulipa ikiwa ni pamoja na bima. 


Awali Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha Jenifa Omolo alisema kuwa waendesha boda boda nao wametajwa kuwa nao ni mwiongoni mwa wanaotakiwa kulipia vitambulisho hivyo.


Katibu wa Chama cha Wamiliki na Waendesha Pikipiki wilaya ya Kibaha (CHAWAMAPIKI) Shaban Kambi alisema kuwa kilichosababisha wakashindwa kuchukua vitambulisho hivyo ni kutopatiwa elimu juu ya wanaopaswa kulipia.

Thursday, April 25, 2019

MAADHIMISHO YA SIKU YA MALARIA DUNIANI YAAHIRISHWA MKOANI LINDI.

Na Hadija Hassan, Lindi

KUFUATIA  kuwepo kwa taadhari ya uwepo wa kimbunga cha Kenneth Mkuu wa mkoa wa Lindi Godfrey zambi ametangaza kuahailishwa kwa shughuli zote za Serikali ikiwa pamoja na Siku ya Malaria Duniani yaliyokuwa yanatarajiwa kufanyika kitaifa Mkoani Humo April 25, mwaka huu

Mkuu huyo wa mkoa  ameyasema hayo leo April 25, 2019 alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari  Ofisini kwake mkoani humo

Maadhimisho hayo ya Siku ya Malaria Duniani Yalitarajiwa kufanyika Leo katika viwanja vya Shule ya Msingi Mpili pili Halmashauri ya Manispaa ya Lindi Mkoani Humo  ambapo Mgeni Rasmi wa Maadhimisho hayo alitarajiwa kuwa Waziri wa Afya jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu

Zambi amesema kutokana na hali ya taadhari inayoendelea kutolewa na Mamlaka ya  hali ya Hewa hapa Nchini Serikali Mkoani humo kupitia kikao chao cha kamati ya ulinzi na usalama wameamua kufikia maamuzi hayo

“Jana tumepata taarifa ya kuwepo na Kimbunga cha aina ya Kenneth ambacho kwa maelezo ya  taarifa zinazotolewa na mamlaka ya hali ya hewa Nchini , inaonyesha kimbunga hicho kinaelekea katika pwani ya Kusini ya Nchi yetu ambacho kinatarajiwa kuleta madhara makubwa maeneo ya pwani ya kusini , hasa Mikoa ya Ruvuma, Mtwara na Lindi inaweza kuathirika kwa kiasi kikubwa sana Hivyo ni muhimu kwa wakazi wa Maeneo haya tukachukuwa taadhari za kutosha ”

Kwa mujibu wa Zambi alisema kimbunga hicho cha Kenneth kinatarajiwa  kukumba Mkoa huo kuanzia saa sita usiku wa Tarehe 25/04/2019 ambacho kinatarajiwa kuambatana na upepo mkali na Mvua kumbwa

Alisema kimbunga hicho kinatarajiwa kwenda umbali wa kilomita 60  kutoka ufukweni mwa bahari sawa na viwanja 600 vya mpira wa Miguu

Zambi pia aliwataka wananchi wanaoishi katika maeneo ya chini kutoka usawa   wa bahari kuyahama makazi  yao kwa kwende maeneo ambayo ni salama zaidi    mpaka pale hali hiyo itakapotulia

Aidha Zambi  aliwataadharisha watu wote wanaojihusisha na Shughuli za Uvuvi katika pwani hiyo ya Lindi kusitisha shughuli hizo kwa muda pamoja na wale wanaotaraji kusafiri kwa kutumia njia ya Bahari kusitisha safari zao

Hata hivyo zambi alisema kutokana na kasi ya kimbunga hicho kutarajiwa kuwa kikubwa na chenye kasi zaidi pia wameamua pia kusitisha safari zote za Nchi kavu Kwa Taadhari zaidi mpaka pale watakapotangaziwa kupitia vyombo mbali mbali vya Matangazo 

Zambi alisema licha ya kughalisha shughuli za Serikali kwa Siku ya Leo halitawahusu watumishi wa idara za Afya katika zahanati, Hospitari za Rufaha na Wilaya lakini pia taasisi za kijeshi kama jeshi la polisi na zimamoto na uwokoaji pwmoja na kamati za mahafa katika maeneo yao kwamba wataendelea kama kawaida

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Lindi Shahibu Ndemanga alisema kuwa kufuatia taadhari hiyo tayari kama wilaya imeshatenga maeneo maalumu kwa ajili ya kujihifadhi kwa muda wananchi ambao watayahama makazi yao kwa ajili ya kukipisha kimbunga hicho

Ndemanga aliyataja maeneo hayo kuwa ni Shule ya Msingi Wailesi, Mtanda, Tulieni, Shele ya Sekondari ya Angaza pamoja na kambi ya Jeshi iliyopo kata ya Mtanda Manispaa ya Lindi Mkoani humo

Alisema maandalizi mengine ambayo wameafanya ni pamoja na kuweka utayari kwa boti za Halmashauri hiyo pamoja na za watu Binafsi  kwa kushirikiana na jeshi la zima moto na uwokoaji kwa ajili ya uwokoaji endapo kimbunga hicho kitatokea

Nae mkurugenzi wa kinga kutoka Wizara ya Afya jinsia wazee na Watoto Dr Leonard Subi aliwataka wananchi kuendelea kuchukuwa taadhari juu ya kimbunga hicho ikiwa pamoja na kuondoa vitu vinavyoninginia katika nyumba zao , kuepuka kukaa karibu na Madilisha pamoja na kuwashahuri kutofunga milango ya Nyumba zao ili kuruhusu upepo kupita huku akiwataka wananchi hao kukaamaeneo salama hasa ndani ya nyumba wakati wa kimbunga hiko kikitokea

Subi pia Alieleza ili kuepuka vitu vingine kuwadondokea katika miili yao ni vyema kwa wananchi hao wakakaa chini ya meza ama uvunguni mwa kitanda ili waweze kuwa salama kwa wakati huo

“tunajua kimbungi hiki kinaweza kuwa na Mvua nyingi na uwenda kukatokea hata mafuliko ni vizuri pia wananchi mkajiandaa kisaikilojia kwamba jambo hilo linaweza kutokea  tunawashauri wananchi mnaweza pia kutumia madumu kwa ajili ya kujiokoa , na ikitokea hayo mafuliko yakawepo alisema Subi