Monday, April 15, 2019

WAZIRI WA AFYA WAMEWATAKA VIONGOZI WA DINI NA WANASIASA KUWAELEZA WANACHI KUWA KIFUA KIKUU KIPO LAKINI KINATIBIKA

 Waziri wa Afya  Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akizungumza katika ufunguzi wa Mkutano wa Wadau uliokuwa na lengo la kupanga mikakati ya kupiga vita ugonjwa wa kifua kikuu. Mkutano huo umefanyika kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam leo Aprili 15, 2019.
....................................


WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu amewataka viongozi wa Dini pamoja na wanasiasa hususani katika kipindi hiki kuelekea kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa kuwaeleza wananchi kuwa kifua kikuu kipo lakini ukigundilika mapema kinatibika.


Amesema kuwa nivema viongozi hao wakawaeleza waumini wao na wapiga kura wao kujenga nidhamu ya kupima afya zao na pindi wanapogunfulika wanakifua kikuu wawahi Hospitali mapema kwani kinatibika.


Waziri Ummy aliyasema hayo jana jijini Dar Es Salaam katika Uzinduzi wa ushirika wa kutokomeza kifua kikuu nchini ambapo alisema kila mwaka watu 154,000 wanagundulika kuwa na ugonjwa wa kifua kikuu.


” Nawaomba viongozi wangu wa Dini kutumia siku za Jumapili na Ijumaa katika mawaidha yao kwa waumini basi wahakikishe wanawahamasisha kupima afya zao na pindi wanapogundulika kuwa wana ugonjwa wa kifua kikuu Mara moja wakapate tiba kwani ugonjwa huo unatibika.” alisema.


Nakuongeza kuwa hata wanasiasa kwa maana waheshimiwa wabunge na wenyeviti wa serikali za mitaa hususani katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi kuhamasisha watu wao kuangalia afya zao.” Alisisitiza Ummy.


Waziri Ummy alisema takwimu za mwaka 2017 zinaonyesha kuwa jumla ya 443 wa kifua kikuu ni sugu waligundiliwa na  kuazishiwa matibanu  na kati ya 1700 wanaokadiliwa kuwa ugonjwa huo  ambao ni sawa na 26 asilimia tu.


Pia alisema  katika mwaka  2018 walikuwa wamewafikia wagonjwa  75,845 sawa na  ongezeko la asilimia  22 kutoka mwaka 2015.


Pia alizipongeza taasisi binafsi  kushirikiana na Serikali katika kupambana na ugonjwa huo wa kifua kikuu nchini  nakwamba katika mapambano hayo waganga wa jadi ni watu muhimu kwani nao wamekuwa wa athirika wakubwa katika vilinge vyao.


Aliongeza kuwa ugonjwa wa kifua kikuu unaathari kubwa kwani katika   mtu mmoja wa kifua kikuu anauwezo wa kuambukiza watu kumi hivyo lazima mapambano dhidi ya kifua kikuu yaongezeke.


Kwaupande wake mtoa mada Kutoka wizara ya Afya ,ambaye pia ni Meneja mpango wa Taifa wa kudhibiti kifua kikuu na ukoma nchini, Dkt Beatrice  Mutayoba   alisema maeneo ya mikusanyiko kwa ujimla wake yanaweza kupatikana maambukizi ya ugonjwa wa kifua kikuu.


Alisema pia mapambano hayo dhidi ya kifua kikuu si  upande mmoja bali ni watu wote wanatakiwa kushirikiana na kwa kufanya hivyo kwa pamoja ugonjwa huo unaweza Kumalizika.


Katika Uzinduzi huo pia ulihudhuliwa na mganga Mkuu wa Serikali   Profesa, Muhamed Kambi Mwakilishi Mkazi wa shirika  Afya Duniani  (who ) Dkt Tigest Ketsela  Mkurugenzi wa Huduma za kinga Dkt. Leonard  Subi ,Mwenyekiti wa  umoja wa wabunge wanaopambana na ugonjwa wa kifua kikuu  Oscar  Mkasi.
 Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Mohamed Bakari, akitoa ufafanuzi  katika katika baadhi ya mambo wakati wa  ufunguzi wa Mkutano wa Wadau uliokuwa na lengo la kupanga mikakati ya kupiga vita ugonjwa wa kifua kikuu. Mkutano huo umefanyika kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam leo 15, 2019.

 Baadhi ya wadau walioshiriki katika mkutano huo uliofanyika kwenye Hoteli ya New Africa leo 15, 2019.


Waziri  wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano huo mara baada ya kuufumgua rasmi.

OMARI MGUMBA ASEMA SERIKALI IMEDHAMIRIA KUKAMILISHA SKIMU ZOTE ZA UMWAGILIAJI AMBAZO UTEKELEZAJI WAKE HAUJAKAMILIKA

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) akijibu swali Bungeni leo tarehe 15 Aprili 2019 wakati wa mkutano wa kumi na tano wa Bunge la Bajeti Jijini Dodoma. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) akifuatilia mkutano wa kumi na tano wa Bunge la Bajeti Jijini Dodoma leo tarehe 15 Aprili 2019. Mwingine pichani ni Naibu Waziri ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe Juliana Shonza (Mb).
......................................


Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma


Serikali inayo dhamira ya kukamilisha skimu zote za umwagiliaji ambazo utekelezaji wake haujakamilika kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ukosefu wa fedha.


Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) ameyasema hayo Bungeni Jijini Dodoma leo tarehe 15 Aprili 2019 wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu Mhe Azza Hillal Hamad aliyetaka kufahamu ni lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Bwawa la Umwagiliaji katika Kijiji cha Ishololo Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.


Mhe Mgumba amesema kuwa Skimu hiyo ipo miongoni mwa skimu za umwagiliaji zitakazopewa kipaumbele katika kutekeleza Mpango Kabambe wa Taifa wa Umwagiliaji (Irrigation Master Plan 2018 – 2025) ambao kwa sasa umeanza kutekelezwa.


Alisema kwa kuzingatia umuhimu wa miradi hiyo ukiwemo mradi wa umwagiliaji Ishololo, tayari
Serikali imekwishaanza mazungumzo na wadau mbalimbali ikiwemo Serikali ya Japan kupitia Shirika lake la Maendeleo la JICA kwa lengo la kuboresha miradi yote ambayo haijakamilika na ile inayofanya kazi chini ya ufanisi uliokusudiwa.


Naibu Waziri huyo wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) alisema kuwa mradi wa ujenzi wa bwawa wa Ishololo uliopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Vijijini ni moja kati ya miradi iliyokuwa ikitekelezwa kupitia Mradi wa Uwekezaji katika
Kilimo katika Wilaya (DASIP) chini ya iliyokuwa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika.


Alisema Utekelezaji wa Mradi huo ulifikia ukomo wake mwezi Desemba 2013 ambapo Benki Maendeleo
ya Afrika ilisitisha kutoa fedha za utekelezaji wa miradi wakati utekelezaji wake ukiwa haujakamilika.

Friday, April 12, 2019

MTU MMOJA AFARIKI KWA KULIPUKIWA NA MTUNGI WA KUCHEMSHIA KOROSHO LINDI.

NA HADIJA HASSAN, LINDI.

MTU mmoja amefaliki Dunia na wengine wawili kujeruiwa baada ya kulipukiwa na Mtungi wa kuchemshia Korosho katika mafunzo ya ubanguaji bora wa korosho yanayotolewa na Shirika la kuhudumia viwanda vidogo vidogo (SIDO) Mkoa wa Lindi.


Akizungumza na Waandishi wa Habari Katibu wa Afya wa Hospitali ya Rufaa Mkoani Lindi Sokoine Bonifas Lymo amekili kupokea majeruhi wawili Amadeo urio lio (27) ambae ni mwanajeshi wa jeshi la kujenga Taifa JKT kambi ya Nachingwe Mkoani Lindi na mwingine ni Asha Ahmedi (30) Mkazi wa Njangao Halmashauri ya wilaya ya Lindi na Maiti moja ya Saada Juma (28) mkazi wa kata ya Msinjahili Manispaa ya Lindi Mkoani humo


Hata hivyo alisema mpaka sasa majeruhi hao wamepatiwa matibabu na wanaendelea vizuri ambapo mmoja wa majeruji hao Asha Ahmedi ambae alipata majeraha ya jicho la kulia baada ya kufanyiwa uchunguzi alionekana hakupata majeraha makubwa ametibiwa na kurudi nyumbani kwao  huku mwingine ambae ni Amadeo Urio lio alionekana amepata majeraha makubwa mapajani na miguu yote miwili pamoja na tumboni  akiendelea kupatiwa matibabu katika hoapitali hiyo 


Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo Ramadhani Zungu Alisema kuwa tukio hilo lilitokea Aprili 11, 2019 majira ya saa tano na nusu Asubuh  wakiwa wanaendelea na mafunzo ya ubanguaji wa korosho


"haya mafunzo tulianza toka jumanne ya Aprili 9 lakini kwa siku ya leo tulikuwa  tumefikia hatua ya kuchemsha , sasa kuna mashine ambayo inatumika kuchemshia korosho hizo ambapo huchemshwa kwa kutumia mvuke Baada ya kuchochea kuni  joto lilipanda wakati ule wenzetu walikuwa wanajiandaa kuruhusu mvuke kuingia kwenye korosho Saada ndie aliekuwa karibu na ule mtungi wa kuchemshia Korosho na Amadeo alikuwa mbali kidogo huku washiriki wengine tukiwa tunaendelea na mambo mengine"


" kabla hata hawajaruhusu ule mvuke kutoka na kuingia kwenye Korosho Mtungi ukawa umelipuka ghafla baada ya kulipuka tukaona yale mabati yake yameenda umbali fulani tukawasogelea wenzetu tukamkuta Amadeo anatembea na kulia kwa sauti na Saada akiwa amelala chini ajiwezi " alisema Zungu


Akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kutembelea eneo la Ajali hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Pudensiana  protas alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema kuwa tukio hilo lilitokea Aprili 11, 2019 majira ya Saa tano asubuhi katika moja ya majengo  ya Shirika hilo la SIDO  huku akieleza kuwa Chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikana.


Mtungi wa kuchemshia Korosho ulioripuka kama unavyoonekana pichani.

 
 Mmoja majeruhi katika ajali hiyo akiwa Hospitali ya Rufaa Mkoani Lindi