Sunday, March 17, 2019

MAZOEZI YANALINDA AFYA YA MWILI- MZIBA.

 Afisa Michezo wa Wilaya ya Bagamoyo, Vedastus Mziba akishiriki (kushoto) mazoezi ya kukimbia pamoja na vikundi vya Bagamoyo Joging ya Bagamoyo na HARAKATI joging ya Temeke jijini Dare es Salaam, kwa pamoja walifanya mazoezi ya kukimbi mapema leo asubui tarehe 17, macchi 2019, katika mji wa Bagamoyo.

................................................

Wito umetolewa kufanya mazoezi ya mara kwa mara ili kulinda afya ya mwili kutokana na magonjwa mbalimbali.


Akizungumza mara baada kumaliza mazoezi yaliyoandaliwa na Bagamoyo Joging mjini Bagamoyo, Afisa Michezo wa Wilaya ya Bagamoyo, Vedastus Mziba amesema mazoezi huweka mwili katika hali ya usalama wa kiafya na kuepukana na magonjwa mbali mbali.


Aidha, alisema kuwa michezo ni ajira na ni sehemu ya kufikisha ujumbe kwa vitendo kwakuwa wana michezo wanapaswa kuwa mfano wa kuigwa katika mambo mabli mbali ili jamii ijifunze kutoka kwao.


Aidha, aliwapongeza viongozi wa Bagamoyo Joging kwa kuandaa mazoezi hayo ya kukimbia ambapo wameweza kushirikisha kikundi cha mazoezi ya kukimbia cha Harakati kutoka Temeke jijini Dar es Salaam.


Alisema ilikufanikisha mazoezi vizuri kunahitajika mipango itakayosaidia kupanga ratiba na kufikia malengo ya yaliyokusudiwa kwa kikundi.


Awali akizungumza mara baada ya kuhitimisha mazoezi hayo, Mwenyekiti wa Bagamoyo Joging, Hanga J. Mgumila amesema wameandaa mazoezi hayo ya kukimbia na kuwaalika kikundi rafiki cha harakati kutoka Temeke jijini Dar es Salaam, ili kuwaunganisha vijana katika mtazamo mmoja utakaowafanya waweze kushirikiana katika mambo mbalimbali.


Alisema kikundi cha Bagamoyo Joging kimepata mafanikio katika kuwanganisha vijana kwenye mazoezi ya kukimbia jambo linaloleta faraja kuona sio tu kukimbia bali vijana hao wanaweza kufanya mambo makubwa zaidi kwa pamoja.


Akizungumzia kupiga hatua kwa kikundi cha Bagamoyo Joging, Hanga alisema kikundi kimepiga hatua kwa kufanikiwa kusajili katiba iliyopitishwa na Baraza la Michezo Tanzania (BMT) hali inayowapa uwezo wa kutimiza malengo yao kwa mujibu wa katiba yao.


Aidha, alimpongeza Afisa michezo, wilaya ya Bagamoyo, Vedastus Mziba kwa kushirikiana na Bagamoyo Joging katika kila hatua na hatimae kufanikisha kusajili katika ya kikundi hicho cha michezo.


Kwa upande wake katibu wa kikundi HARAKATI Joging kutoka Temeke jijini Dar es Salaam, Mboke Salim Mboke alisema vijana wakitumia vizuri fursa ya michezo wanaweza kufanya mambo makubwa zaidi ya michezo.


Alisema michezo ni sehemu ya kuwakutanisha watu wenye fikra mbalimbali ambao umoja wao untakiwa uendelee hata nje ya michezo.


Mboke aliendelea kusema kuwa, kikundi cha Harakati licha ya kufanya mazoezi ya kukimbia pia kinajihusisha na shughuli mbalimbali za ujasiliamali ambazo zinawawezesha kuendesha maisha yao ya kila siku.


Alisema vijana wenye fani mbalimbali ndani ya kikundi ndio chachu ya kutoa elimu kwa wengine na hatimae kikundi kinajitegemea kikiwa na bidhaa mbalimbali ambazo zinazalishwa na wana kikundi.


Mboke alimalizia kwa kuwashukuru Bagamoyo Joging kwa suhirikiano walio nao hali iliyowapa moyo wa kuongeza juhudi za ushirikiano baina ya vikundi hivyo ili kufanikisha malengo yao.

 Vikundi vya Bagamoyo Joging ya Bagamoyo na HARAKATI joging ya Temeke jijini Dare es Salaam, kwa pamoja wakiwa kwenye mazoezi ya kukimbi mapema leo asubui tarehe 17 macchi 2019, katika mji wa Bagamoyo.



 Vikundi vya Bagamoyo Joging ya Bagamoyo na HARAKATI joging ya Temeke jijini Dare es Salaam, kwa pamoja wakiwa kwenye mazoezi ya kukimbi mapema leo asubui tarehe 17 macchi 2019, katika mji wa Bagamoyo.

 Vikundi vya Bagamoyo Joging ya Bagamoyo na HARAKATI joging ya Temeke jijini Dare es Salaam, kwa pamoja wakiwa mazoezi ya viungo mara baada ya kukamilisha  mazoezi ya kukimbi mapema leo asubui tarehe 17 macchi 2019, katika mji wa Bagamoyo.
 
 Kushoto ni Mwenyekiti wa Bagamoyo Joging, Hanga J. Mgumila, akieleza machache mara baada kumaliza mazoezi ya kukimbia mapema leo asubui tarehe 17 machi 2019 katika mji wa Bagamoyo.
     Kushoto ni Mwenyekiti wa Bagamoyo Joging, Hanga J. Mgumila, katibu wa kikundi HARAKATI Joging kutoka Temeke jijini Dar es Salaam, Mboke Salim Mboke wakimsikiliza Afisa Michezo wilaya ya Bagamoyo, Vedastus Mziba (hayupo pichani) mara baada kumaliza mazoezi ya kukimbia mapema leo asubui tarehe 17 machi 2019 katika mji wa Bagamoyo.
 
 Picha ya pamoja, Afisa utamaduni wilaya ya Bagamoyo Vedastus Mziba (katikati) akiwa na Vikundi vya Bagamoyo Joging ya Bagamoyo na HARAKATI joging ya Temeke jijini Dare es Salaam, mara baada ya kumaliza mazoezi ya kukimbi mapema leo asubui tarehe 17 macchi 2019, katika mji wa Bagamoyo.

Saturday, March 16, 2019

Mrithi wa Maalim Seif CUF aomba radhi...atema cheche, asema anaanza na hili


 

Mrithi wa nafasi ya Katibu Mkuu wa zamani wa Chama cha wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamadi hatimaye amepatikana mapema hii leo, lakini Katibu huyo ameomba radhi kwa wale wote waliokwazika katika kipindi cha mpito walichopitia na kuwataka kuwa kitu kimoja ili kukijenga Chama Chenye Nguvu ya kushika dola.
Amesema wakati wa kurumbana umekwisha kinachotakiwa ni kufanya kazi kwa bidii ya kukifanya chama kiwe chenye kuaminika na hatimaye kushika dola, jambo ambalo ni dhamira ya Chama chochote cha Siasa.
"Nimepanga kuanza na kuleta umoja ndanii ya chama, nitallisimamia hilo, mimi na wenzangu tutafanya kazi bila kuchoka kukifanya chama hiki kinapata hadhi yake, ndiyo maana nawaomba radhi wale wote tuliowakwaza, ilikuwa ni njia Mungu ametupitisha lakini mwishowe tumefika. Kwa wanachama wa CUF, nataka niiwaambie kama walikuwa wanapenda mtu basi huyo mtu sasa hayupo lakini kama wanapenda Chama basi chama chao kipo imara na kitafanya kazi zaidi ya zamani" Aliongeza Khalifa Suleiman Khalifa
Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba amemtangaza Khalifa Suleiman Khalifa kuwa katibu mkuu wa chama hicho.

Mbali na Khalifa, Profesa Lipumba pia amemtangaza mbunge wa Kaliua, Magdalena Sakaya kuwa naibu katibu mkuu Bara na Fakhi Suleiman Khatibu kuwa naibu katibu mkuu Zanzibar.

Profesa Lipumba amemtangaza Khalifa ambaye ni mbunge wa zamani wa Gando kuchukua nafasi ya Maalim Seif Sharif Hamad leo Jumamosi Machi 16, 2019 makao makuu ya CUF, Buguruni jijini Dar es Salaam.

Katibu mkuu huyo mpya, amepatikana baada ya kuchaguliwa na Baraza Kuu la Uongozi lililokutana jana Ijumaa.

Hata hivyo, hatima ya viongozi hao wapya wa CUF akiwamo Profesa Lipumba aliyechaguliwa na mkutano mkuu Jumatano iliyopita Machi 14, 2019, itajulikana baada ya hukumu itakayotolewa Jumatatu ya Machi 18, 2019 na Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam.

Hukumu hiyo ni ya kesi iliyofunguliwa na baadhi ya wanachana wa chama hicho upande wa Maalim Seif wakipinga uhalali wa Profesa Lipumba kuwa mwenyekiti wa CUF.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya March 16




Friday, March 15, 2019

IGP SIRRO AAHIDI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA KENYA KWENYE MASUALA YA USALAMA

 Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro akisalimiana na balozi wa Kenya nchini Tanzania Dan kazungu leo wakati alipomtembelea ofisini kwake Makao Makuu ya Jeshi hilo kwa lengo la kujitambulisha ambapo kwa pamoja wamekubaliana kuendelea kushirikiana kwenye masuala ya kiusalama baina ya nchi hizo mbili.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akimsikiliza Balozi wa Kenya nchini Tanzania Dan Kazungu leo tarehe 15/03/2019, wakati alipomtembelea ofisini kwake Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujitambulisha ambapo kwa pamoja wamekubaliana kuendelea kushirikiana kwenye masuala ya kiusalama baina ya nchi hizo mbili.Picha na Jeshi la Polisi


ZAIDI YA WATU 40 WAMEUWAWA MISIKITINI NEW-ZEALAND.

Zaidi ya watu 40 wauwawa kwenye mashambulizi ya misikiti New-Zealand.


Misikiti miwili ya ChristChurch nchini New Zealand imeshambuliwa wakati wa sala ya Ijumaa hii leo. Watu wasiopungua 49 wameuwawa.


Polisi wanasema watu wanne, watatu wanaume na mmoja mwanamke wamekamatwa. Haijulikani kama watuhumiwa ni miongoni mwa waliokamatwa.


Kwa mujibu wa mashahidi bwana mmoja aliingia msikitini na kufyatua risasi, Baadae risasi zilifyatuliwa pia katika msikiti wa pili.


Kanda ya video imesambaa mitandaoni ambapo mtuhumiwa anaonyesha jinsi alivyoshambulia msikiti mmoja kati ya hiyo miwili.


Waziri mkuu wa New Zealand Jacinda Ardern amsema watu 49 wameuawa na wengine zaidi ya 20 wamejeruhiwa vibaya baada ya kuzuka mashambulio katika misikiti miwili katika mji wa Christchurch, huko New Zealand.


Waziri mkuu huyo amelitaja shambulio hilo kuwa ni shambulio lililotanda 'kiza kikubwa' siku ya leo nchini humo.


Wanaume watatu na mwanamke mmoja wamekamatwa kwa kuhusika na shumbulio hilo.


Kamishna wa polisi Mike Bush amesema, kwamba huenda washukiwa zaidi wakakamatwa.


Taarifa kutoka nchini New Zealand kwamba washambuliaji hao hawakuwa kwenye orodha ya magaidi wanaosakwa lakini ni wazi kwamba wana itikadi kali.


Waziri mkuu wa Australia Scott Morrison amesema mojawapo ya waliokamatwa ni raia wa Australia.