Sunday, December 16, 2018

BARAZA LA WAFANYAKAZI OR- TAMISEMI LAKUTANA DODOMA.

 Baadhi ya wajumbe wa Kikao cha Baraza la Wafanya Kazi Ofis ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) wakimsikilioza mwenye kiti wa kikao (hayupo pichani) leo katika Kikao cha Baraza la Wafanyakazi jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu (Afya) Ofis ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Dk. Zainabu Chaula akiendesha kikao cha Baraza la Wafanyakazi OR-TAMISEMI leo katika ukumbi wa mikutano Reform jijini Dodoma.
...........................................


Naibu Katibu Mkuu (Afya) Ofis ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Dk. Zainabu Chaula amewataka Wakuu wa Idara kushirikiana kwa karibu na watu wanaowaongoza ili kuleta chachu katika utekelezaji wa majukumu yao.

Hayo yamesemwa leo katika Kikao cha Baraza la Wafanyakazi OR-TAMISEMI kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Reform Jijini Dodoma.

Dk.Chaula amesema ili kupata matokeo bora katika utendaji kazi wowote lazima kuwa na ushirikiano wa karibu na watu unaowaongoza katika kufanya hivyo ndipo unaweza kupata matokeo bora katika utendaji kazi wako.

“Hivyo basi kila Mkuu wa Idara atambue kuwa yeye ni mlezi wa watu anaowaongoza na kuhakikisha kunakuwa na mawasiliano mazuri baina yao ili kutimiza dhamana tulopea ya kuwatumikia watanzania” Alisema Dk.Chaula.

Pia ameongeza kuwa kiongozi mzuri ni yule anayeshirikiana na anaowaongoza na kuweka wazi nini kinafanyika katika idara ili kuleta utendaji bora katika kutekeleza majukum  ya kila siku na kwamba kila mtu afanye kazi kwa moyo mmoja, Alisema Dk.Chaula.

Aidha baada ya kikao hicho Dk.Chaula na wajumbe wa kikao hicho kwa pamoja walifika ulipo Mji wa Kiserkali ambapo ndo Ofisi Mpya za OR –TAMISEMI zinatarajiwa kujengwa.

Dk. Chaula alimalizia kwa kusema kuwa,  katika ujenzi huo OR-TAMISEMI inatumia mfumo wa “Force Account” ambapo kila mfanyakazi wa OR-TAMISEMI anakuwa msimamizi katika ujenzi  na  kunakuwa na kamati mbali mbali ili kuhakikisha ujenzi unakamilika kwa muda uliopangwa.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na afya OR-TAMISEMI (TUGHE), Andrew Mramba amesema chama hicho kimeandaa tuzo maalum ya kumpongeza Katibu Mkuu Mhandisi Mussa Iyombe kwa utendaji kazi bora uliyotukuka.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Ofis ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), wakiwa kitika eneo linapojengwa jengo jipya la ofisi za OR –TAMISEMI leo jijini Dodoma baada ya Kikao cha Baraza la Wafanyakazi.
Baadhi ya wafanyakazi wa Ofis ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), wakiwa kitika eneo linapojengwa jengo jipya la ofisi za OR –TAMISEMI leo jijini Dodoma baada ya Kikao cha Baraza la Wafanyakazi.

Saturday, December 15, 2018

WANA CCM MSOGA WAPIGWA MSASA

Na Omary Mngindo, Msoga

WANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Msoga, Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani, wamepatiwa semina elekezi iliyoandaliwa na uongozi wao, ikiendeshwa na chama hicho ngazi ya Wilaya

Semina hiyo iliyofanyika Kijiji cha Mboga, inaendeshwa na Katibu wa chama hicho Wilaya Kamote Kombo, Katibu Mwenezi Fransis Bolizozo, Kufulu Rashidi Katibu Kata ya Kiwangwa wakiongozwa na viongozi wa Kata chini ya Diwani wao Jamdani Mwinyikondo na viongozi mbalimbali.

Akitoa mada katika semina hiyo, Bolizozo alisema kuwa lengo la semina ni kuwakumbusha wanachama hao kutambua majukumu yao, huku wakitambua kwamba wanaelekea kwenye chaguzi ngazi za Vijiji, Vitongoji na Mitaa zinazotaraji kufanyika mapema mwakani. 

"Chama ngazi ya wilaya kimeamua kuandaa semina elekeza inayolenga kukumbushana majukumu yetu katika utendaji wa kazi zetu, tukumbuke tunaelekea katika chaguzi kuanzia mwakani tutambue majukumu yetu," alisema Bolizozo.

Kamote aliwaasa Wana-CCM hao kuendelea kuwatumikia wananchi, huku aliwajibu Wenyeviti kama wanakutana na wananchi wenye matatizo katika maeneo yao,  huku aliwahimiza kuwa na ratiba za kukutana na kutatua kero zinazowakabili wananchi. 

"Ni jambo jema kwa Wenyeviti kuwa na utaratibu wa kuwa na vikao katika maeneo yenu kwa lengo la kusikiliza kero zinazowakabili watu mnaowaongoza katika ngazi zenu, " alisema Kamote.

Diwani Mwinyikondo alisema kuwa viongozi ngazi hiyo wameweka mikakati maalumu inayolenga kuunda mkono juhudi za Rais Dkt. Joho Magufuli kuhakikisha wanyonge wanapewa kipaumbele katika kutatuliwa changamoto zinazowakabili. 

Mwenyekiti wa chama hicho ngazi ya Kata Idd Tungo aliwashukuru watendaji wa ngazi mbalimbali kwa kuwa karibu na chama hicho katika kuhakikisha wanasaidiana katika kupambana na changamoto zinazowakabili wananchi. 

NAIBU WAZIRI WA NISHATI SUBIRA MGALU AHAHIDI KUIMARISHA MIUNDOMBINU YA NISHATI YA UMEME KTK VITUO VYA AFYA NCHINI

Naibu Waziri wa nishati Subira Mgalu kulia akiangalia mwenendo wa upanuzi wa ujenzi wa kituo cha afya mkoani kushoto kwake ni Mganga mkuu wa halmasshauri ya mji Kibaha. (PICHA NA VICTOR MASANGU).
........................................

VICTOR  MASANGU, KIBAHA   

NAIBU waziri wa nishati Subira Mgalu katika kuumga mkono Juhudi za Rais Dk . John Pombe Magufuli ya kuboresha sekta ya afya hapa nchini  ameliagiza Shirika la umeme Tanzania (TANESCO)   kuhakikisha wanapeleka miundombinu ya nishati ya umeme haraka iwezekanavyo  katika maeneo ya  vituo vipya vya afya 300 pamoja na  hospitali 69 ambazo zinajengwa  na serikali kwa lengo la kuboresha huduma ya  matibabu kwa wananchi wake.

Mgalu  ambaye pia ni Mbunge wa viti maalumu kupitia  Mkoa wa Pwani alitoa  kauli hiyo  wakati wa ziara yake ya kikazi kwa ajili ya  kutembelea miradi mbali mbali ya maendeleo iliyopo katika halmashauri ya mji Kibaha pamoja na kukagua mwenendo wa ujenzi wa upanuzi  katika  kituo cha afya mkoani kilichopo Wilayani Kibaha.

“Kwa kweli nia ya serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha inafikisha kwa haraka miundombinu ya umeme katika vituo vipya vya afya ambavyo vinajengwa pamoja na hospitali hivyo nachukua nafasi hii kuwaagiza Tanesco pamoja na REA kufikisha umeme haraka iwezekanavyo katika maeneo hayo ili wananchi waweze kupata huduma ya afya katika mazingira ambayo ni rafiki kwao na katika hili tunamshukuru sana Rais wetu Dk. John Pombe Magufuli,”alisema Mgalu.

 Aidha alibainisha  kwamba kwa sasa lengo la serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha inaboresha miundombinu ya umeme katika maeneo mbali mbali ili zahanati, vituo vya afya pamoja na hospitali ziweze kupata nishati ya umeme wa uhakika ambao utasaidia kuboresha zaidi katika utoaji wa huduma ya afya kwa wananchi wa Tanzania ambao hapo awali walikuwa wanateseka.

Kwa upande wake Mganga mkuu wa halmashauri ya mji Kibaha Tulitweni Mwinuka alisema  kwamba wamepokea kiasi cha shilingi milioni 500 kutoka serikali kuu kwa ajili ya upanuzi wa kituo hicho  cha afya mkoani katika maeneo ya  wodi ya wazazi,jengo la mionzi  jengo maalumu kwa ajili ya kufulia pamoja na jengo la upasuaji ambapo kukamilika kwake kutaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa changamoto ya  mlundikano kwa wagonjwa.

Nao baadhi ya wanawake Wilayani Kibaha  Elina Mngonja na Selina Wilsoni  wamemshukuru Rais wa awamu ya tano Dk. John Pombe Magufuli kwa kuboresha sekta ya afya hapa nchni ambapo  wamesema kukamilika kwa upanuzi wa kituo hicho hasa katika wodi za kinamama wajawazito  utakuwa ni mkombozi mkubwa katika suala zima la utoaji wa huduma hasa  wakati wanapokwenda  kujifungua.
 
Naibu waziri wa Nishati Subira Mgalu kulia akipokea taarifa ya ujenzi wa upanuzi wa kituo cha afya mkoano kutoka kwa Mganga mkuu wa halmashauri ya mjini Kibaha Tulitweni Mwinuka. (PICHA NA VICTOR MASANGU)
Mganga mkuu wa halmashauri ya mji Kibaha Tulitweni Mwinuka kushoto akimwonyesha ujenzi unavyoendelea  wa mradi wa upanuzi wa kituo cha afya cha Mkoani kilichopo Wilayani Kibaha, Naibu waziri wa nishati Subira Mgalu kulia kwake ambaye alifanya ziara kwa ajili ya kutembelea miradi mbali mbali ya maendeleo. (PICHA NA VICTOR MASANGU)

TFS YAIINGIZIA SERIKALI BILIONI 3.3 MAUZO YA MITI AINA YA MISAJI.

Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) imeiingizia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zaidi ya Tshs Bilioni 3.3 kwa Mauzo ya Miti aina ya Misaji (Teak) kutoka katika Shamba la Miti Longuza yenye jumla ya Mita za ujazo 4,912.616.

TFS kwa niaba ya Serikali inasimamia Mashamba 23 ya kupandwa kati yake 13 ndiyo yamefikia viwango vya kuvunwa na mashamba mawili yanavunwa miti aina ya Misaji wakati yanayobaki huvunwa miti aina ya Misindano,mikaratusi na miti ubani (Cyprus).

Aidha, TFS husimamia pia Misitu ya Asili zaidi ya 500 huku iko hakikisha uzalishaji na usambazaji wa Mbegu bora za Miti unafanya mwa Nchini.

Akizungumza kwa niaba ya Wanunuzi, Bwana Ashok Shanghavi ameuopongeza uongozi wa Shamba la Miti Longuza kwa namna wanavyosimamia Miti yao kitaalam kupelekea ubora wa Miti unaoridhisha wafanyabiashara .

Bwana Ashok ameuomba Uongozi wa TFS Makao Makuu kuhakikisha mashamba yao yote yanajifunza na kusambaza ujuzi huo ili kuwa na ubora unaofanana kwenye Mashamba yote.

Friday, December 14, 2018

VULU AKABIDHI VIFAA VYA MIL. 4.5. WANACCM WAPEWA SEMINA ELEKEZI

Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Pwani, Zainabu Vulu, akikabidhi mifuko 60 ya saruji kwa Diwani wa Utete, Hawa Mchopa 
.....................................

Na Omary Mngindo, Kibiti
 
MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Pwani Zaynab Matiti Vulu, amefanya ziara katika majimbo ya Kibiti na Rufuji mkoani hapa, ambapo amekabidhi vifaa mbalimbali vilivyogharimu sh. Milioni 4.5

Katika ziara hiyo iliyoanza juzi, Vulu akiwa Jimbo la Kibiti alipokelewa na Mbunge wa Jimbo hilo Ally Ungando, aliyeambatana na Diwani mwenyeji Hamidu Ungando na viongozi mbalimbali ambapo baada ya mapokezi alifika shule ya msingi Zimbwini na kukabidhi bati 20 yenye thamani ya sh. Laki 540.

Akizungumza shuleni hapo, Vulu alianza kuwashukuru wananchi hao kwa mwamko wa kujitolea katika kujiletea maendeleo, serikali, wabunge, madiwani pamoja na wadau mbalimbali wanaoendelea kujitoa katika sekta mbalimbali.

"Nami nikiwa mdau wa maendeleo nakabidhi mabati 20 yenye thamani ya shilingi 540,000, pia nitakwenda kukabidhi mapazia maalumu ya kuzunguka kitanda cha mama anayejifungua, pamoja na gharama za mabomba na ufundi zinagharimu sh. milioni mbili hamsini na nane elfu," alisema Vulu. 

Akizungumza baada ya kupokea mabati hayo, Diwani Ungando alimshukuru Vulu kwa msaada huo, huku akisema kuwa umefika wakati mwafaka kwani tayari darasa lililoongezwa limeshakamilika na kwamba kilichobaki na kupauliwa kisha kupigwa bati. 

Viongozi wengine ngazi ya Kata walioongozana na Vulu ni pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Khatibu Chaurembo, Amina Mapande, Moza Kiluya, Zaynab Chitanda diwani Ungando ambao kwa umoja wao wameahidi bati 25.

Vulu akiwa Jimbo la Rufiji amekabidhi mifuko 60 ya saruji isiyogawanyika katika miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa shule ya msingi katika Kitongoji cha Kiwili Kata ya Utete ambapo alishiriki zoezi la ufyatuaji wa tofari. 

Mbali ya mifuko hiyo pia amenunua lori za mchanga ambazo zote gharama yake vimegharimu milioni 2,442,000 ambapo akiwa katika Kitongoji hicho akishirikiana na viongozi wa chama pamoja na wananchi walishirikiana na kusafisha eneo kisha kufyatua tofari.

Hawa Mchopa diwani Kata ya Utete alimshukuru mbunge huyo huku akisema amekuwa bega kwa bega na wananchi wake katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo. 
  
Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Pwani, Zainabu Vulu, akibeba moja ya tofali katika eneo linalotarajiwa kujengwa shule ya msingi.

 
Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Pwani, Zainabu Vulu, akilima eneo la ujenzi kabla ya kuanza kufyatua tofali kwaajili ya ujenzi wa shule ya msingi.

UPEPO WABOMOA NYUMBA 157 NACHINGWEA.

 Na Hadija Hassan- Lindi

Nyumba {157} yakiwemo majengo ya Serikali zimebomolewa kufuatia upepo mkali ulioambatana na mvua  iliyonyesha juzi ,Wilaya ya Nachingwea, Mkoani Lindi.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama Wilaya ya Nachingwea Bi, Rukia Muango ambae pia ndio   mkuu wa wilaya hiyo, 

Alisema kuwa mvua hiyo ilianza majira ya saa 10:30-11:30 jioni iliambatana na Upepo mkali ambao ,licha ya kuharibu Nyumba za kuishi wananchi wa kata za Nachingwea, songa mbele na Stesheni, pia umeharibu  na Zahanati ya  Stesheni.

Pia,alifafanua kwa kutaja maeneo yaliyokumbwa na balaa la  upepo huo ni pamoja na kata za Stesheni Nyumba na Zahanati jumla (83), Kata ya Songa Mbele nyumba  (14) na kata ya Nachingwea Nyumba (60) kufanya idadi kufikia' (157).

Mkuu huyo wa wilaya amesema katika tukio hilo hakuna mtu aliyekuwa amepoteza maisha,bali ni watu wanne {bila kutaja majina},waliangukiwa na kuta za nyumba zao,kisha kukimbizwa Hospitali ya wilaya hiyo,wakatibiwa na kuruhusiwa kurejea majumbani mwao.

Hata hivyo Mwango alieleza Kwamba  bado hasara iliyopatikana haijaweza kufahamika mara moja, na kwamba Ofisi yake imewaagiza wataalamu kufanya upembuzi yakinifu ili kubaini idadi yake.



Mwango ametaja sababu zilizochangia kubomolewa kwa nyumba na Jengo la Zahanati,ni ujenzi usiozingatia ubora,ikiwemo kutokuwepo kwa Linta zilizo na ubora na kutumia mbao zisizokuwa na viwango vinavyohitajika.

“Zahanati nayo mbao zilizotumika kuwekea kenchi ni nyembamba mno,hivyo upepo ulipofika ilikuwa rahisi tu kuezua na kuweka kando”Alisema Mwango.

Hata hivyo Mwango Alisema kuwa kutokana na tukio hilo serikali Wilayani humo imeamua kuifunga zahanati ya stesheni mpaka itakapofanyiwa ukarabati

Pia,Mwango aliongeza kuwa watu wote walioathiriwa na upepo huo,karibu wote wamepatiwa hifadhi na baadhi ya Jamaa na majirani zao,huku Ofisi yake ikiandaa taarifa kupeleka Ofisi ya Maafa kuona namna itakavyoweza kusaidia wale watakaobainika kuathirika zaidi na upepo huo.



Aidha, amewataka wananchi wote wilayani Nachingwea wanaotaka kujenga Nyumba za kuishi kuwatumia wataalamu wa majengo waliopo ili kupata maelekezo ya kitaalamu ili kuepuka hasara kama walivyoipata sasa.

Hii ni mara ya pili kwa Mkoa wa Lindi kupata mkasa wa aina hii,kwani wiki iliyopita upepo aina ya Kimbunga ulioambatana na mvua kiasi umepoteza mkazi mmoja wa Kijiji cha Mbuli na kubomoa Nyumba (38) yakiwemo majengo ya taasisi za Serikali na Ghala la kuhifadhia mazao Kata ya Nangano,wilaya ya Liwale.
 

WANAFUNZI 4,731 WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA KWANZA PWANI KUTOANZA MASOMO KUTOKANA NA UPUNGUFU WA MADARASA 122

 NA MWAMVUA MWINYI, PWANI 

MKUU wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo amewaagiza wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri kuhakikisha wanajenga madarasa 122 na matundu ya vyoo ili wanafunzi 4,731 waliobaki kujiunga kidato cha kwanza waweze kuanza masomo ,ifikapo January 30 mwaka 2019.

Aidha amewaelekeza ,kufuatilia shule za msingi kumi zilizofanya vibaya kimkoa na kuhakikisha wanachukua hatua mahsusi .

Pamoja na hayo, Ndikilo amekemea walimu wavivu na kuwataka wafanye kazi kwa molari ili kuinua ufaulu na taaluma kwa wanafunzi. 

Akitoa maagizo katika kikao cha kamati ya uchaguzi wa wanafunzi waliofaulu kidato cha kwanza mkoani hapo, alieleza wanafunzi 4,731 hawatapata nafasi hivyo watasubiri hadi ujenzi ukamilike awamu ya II. 
Alisema, endapo halmashauri zingekamilisha wajibu wake wa kujenga majengo ya madarasa hali hiyo isingetokea. 

Mkuu huyo wa mkoa alitaja takwimu kihalmashauri ambapo wanafunzi 487 halmashauri ya Bagamoyo hawana nafasi, Chalinze 103, Kibaha Vijijini 285,Kibaha Mjini 711 na Kibiti 537 .

Ndikilo alitaja halmashauri ya Kisarawe wanafunzi 324,Mkuranga 1,071 na Rufiji 213 .

“Halmashauri zote zilizobakiza wanafunzi zijipange, mjiwekee mkakati kuondoa tatizo hili ili watoto waweze kwenda shule “Watumieni wadau wa elimu na wawekezaji kushirikiana kwenye hili “alisisitiza Ndikilo.

Ofisa elimu mkoani Pwani, Abdul Maulid, aliahidi kutekeleza maagizo waliyopewa na mkuu huyo wa mkoa kwani zipo wilaya ambazo zinaendelea na zoezi la kukamilisha ujenzi huo. 

Alisema, kwa mwaka 2018 mkoa wa Pwani umepanda na kushika nafasi ya 11 kitaifa ukilinganisha na 2017 ambapo ilishika nafasi ya 19 kitaifa.