Friday, November 9, 2018

JESHI LA POLISI PWANI LAKAMTA LUNINGA KUMI ZA WIZI

Kamanda wa polisi mkoani Pwani Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP)  Wankyo Nyigesa akielezea msako endelevu unaendelea mkoani humo huku akieleza kauli mbiu yake ya Tindua Tindua hadi kieleweke. (picha na Mwamvua Mwinyi)

Kamanda wa polisi mkoani Pwani Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP)  Wankyo Nyigesa akionyesha baadhi ya luninga flat screen zilizoibiwa katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo (picha na Mwamvua Mwinyi)

Mmoja wa watu walioibiwa luninga zao, mzee Lebul Mfinanga (wa kulia aliyebeba luninga) akiwa ametoka kutambua luninga yake makao makuu ya polisi Pwani .
Picha na Mwamvua Mwinyi
...................................................

Na Mwamvua Mwinyi, Pwani 

JESHI la polisi mkoani Pwani, limekamata luninga kumi flat screen zenye thamani ya sh. mil.18, ambazo ziliibiwa katika matukio mbalimbali ya uvunjaji, mkoani humo. 

Aidha linamshikilia mtu mmoja jina limehifadhiwa baada ya kukumatwa akiwa na madumu kumi yenye ujazo wa lita 20 ya mafuta aina ya dizeli  ,aliyoiba katika mradi wa ujenzi wa reli ya standard gauge , Soga wilaya ya kipolisi Mlandizi. 

Akithibitisha kutokea kwa matukio hayo, kamanda wa polisi mkoani Pwani (ACP)  Wankyo Nyigesa alisema, wanashikilia watu nane kwa tuhuma za kuhusika kwenye matukio hayo. 

Nyigesa alieleza katika msako huo wamekamata jenereta mbili kubwa zenye thamani ya milioni 6.5 ambazo ni aina ya Euro power EP. 6500E na boss BG -2500 .

Alifafanua, vitu vingine vilivyokamatwa ni deki mbili, vingamuzi viwili, speaker mbili, music system mbili, home fieta moja, rimoti sita, speaker twiter mbili, flash moja kapeti za chini ya sakafu mbili, stendi ya vyombo moja na extention moja. 

Hata hivyo kamanda huyo alisema , mtuhumiwa aliyekamatwa kijiji cha Mperamumbi akiwa amepakia mafuta kwenye pikipiki aina ya sanlg namba MC. 197 BJD kutoka mradi wa standard gauge wanamhoji na atafikishwa mahakamani. 

Katika tukio jingine wamekamata pikipiki saba na bangi kiroba kimoja kilichokuwa kinasafirishwa kwenda kuuzwa. 

Nyigesa alibainisha, katika tukio hilo mmiliki wa pikipiki yenye namba za usajili MC 951 BSA  anaombwa kujisalimisha mwenyewe kituo chochote cha polisi ndani ya siku tatu vinginevyo watamsaka popote ili kueleza kuhusu bangi hiyo.  

“Sisi wakati tukiwa kwenye hapa kazi tuu, wao wapo kwenye wizi tuu, tunawapa salamu wakati wengine wakifyekelea mbali, kwa sisi mkoa wa Pwani tunaendelea na operesheni na msako wa TINDUA TINDUA, tutatindua mpaka kieleweke “alisisitiza Nyigesa. 

Alitoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kununua vitu mikononi bila ya kupewa risiti kwani atakaekutwa na mali ya wizi nae atachukuliwa hatua za kisheria. 

Nyigesa aliwaasa pia kuwa ,wabia katika suala la ulinzi shirikishi kwenye maeneo yao ili kukabiliana na ujambazi, uvunjaji na uhalifu mbalimbali.

 


DC MURO AMALIZA MGOGORO WA ARDHI WA MASHAMBA YA MALULA ARUMERU*

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru *Mhe Jerry Muro* ametatua Mgogoro uliodumu kwa zaidi ya *Miaka Saba*  kati ya wakulima na wafugaji wa kata ya *Malula wilayani Arumeru* na  kuwataka wakulima waendelee kulima katika mashamba ya Malula ambayo ni ardhi ya serikali iliotengwa kwaajili ya uwekezaji wa *viwanda na bandari kavu*

Aidha *Dc Murro* amewataka wanasheria wanaowapotosha wakulima na *wafugaji wa vijiji vya kata ya Malula* kwa kutumia uwepo wa migoogoro ya ardhi kwa njia ya kujinufaisha  kuacha mara moja tabia hiyo na kufuta kesi hizo mahakamani kwani ardhi ni ya serikali na mwenye dhamana na ardhi hiyo ni  *Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli*

*Dc Muro* Amezungumza wakati wa ziara yake ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi wa kata ya *MALULA*  ambapo mgogoro huo umetokana na wakulima na wafugaji kufanya maeneo ya mashamba hayo kuwa ya kwao na wengine kupeleka mashtaka mahakamani dhidi ya wananchi walioazimwa maeneo hayo na serikali kwaajili ya kilimo.

*Imetolewa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya  Arumeru.*

MAKAMU WA RAIS ASEMA HALMASHAURI HAZITEKELEZI AGIZO LA UPANDAJI MITI IPASAVYO.


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia baadhi ya kazi za wanafunzi wakati wa hafla ya ufunguzi wa Ukumbi wa Mihadhara na Bweni la Wanafunzi katika chuo cha Misitu, Olmotonyi, Arusha. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
  .................................................................
Na Amiri Mvungi-Arusha
Makamu wa rais mheshimiwa Samia Uuluhu Hassan  ameeleza kutokuridhishwa na utekelezaji wa agizo la ofisi yake kwa halmashauri za wilaya kote nchini kupanda miti akibainisha kuwepo kwa udanganyifu wa takwimu zinazotolewa za idadi ya miti inayopandwa.

Akizungumza mara baada ya kuzindua rasmi majengo ya mabweni na ukumbi wa mihadhara yaliyojengwa katika chuo cha mafunzo ya misitu olmotonyi,mama Samia Suluhu amesema bado hali ya mazingira nchini sio ya kuridhisha na hapa anaagiza kuwa ni vyema  miti inayopamdwa ijumuishwe na miti ya mazao…mh samia suluhu-makamu wa rais.

Ujenzi wa majengo hayo  yaliyogharimu zaidi ya  shilingi bilioni moja nukta nane ni moja ya utekelezaji wa mradi wa uendelezaji  shirikishi wa misitu unaofadhiliwa na serikali ya norway majengo ambayo naibu waziri wa maliasilina utalii Japhet Hasunga anasema licha ya kuwapunguzia adha wanafunzi wa kike waliokuwa wakiishi nje ya chuo pia yataongeza kasi ya udahili…japhet hasunga ..naibu waziri maliasili na utalii.

Elisabeth Jacobsen ndiye balozi wa norway hapa nchini ,anasema ufadhili huo  unalenga  kudumisha ushirikiano na tanzania katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi yanayoonekana kuathiri mataifa yote ulimwenguni..elisabeth jacobsen-balozi wa norway nchini.

MAGUFULI AMTUMBUA BALOZI WA TANZANIA NCHINI CANADA