Friday, November 9, 2018

DC DAQARRO ATAKA WADAU WA ELIMU KUHAKIKISHA MPANGO WA LANES UNAENEA ARUSHA NA KULETA MATOKEO CHANYA

Mkuu wa wilaya Arusha mjini Gabriel Daqarro akifungua wiki ya usomaji iliyofanyika kwenye maktaba ya mkoa Arusha pembeni ni mkutubi mkuu wa maktaba hiyo Bi Rafiki Mvamba na kushoto ni Afisa elimu Vielelezo Godfrey Augustino wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi mkuu huyo wa wilaya picha zote na mahmoud ahmad arusha 

 ..........................
Na Ahmed Mahmoud Arusha
Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro amewataka waalimu na Afisa elimu kuhakikisha mpango wa KKK (LANES) unatiliwa mkazo sanjari na kuhakikisha wanafunzi wanajua kusoma kuandika na kuhesabu ili kuleta matokeo chanya na kufikia malengo ya serikali ya wananchi wote kujua kusoma.
Akiongea wakati akifungua wiki ya kusoma na stadi za kukuza kusoma kuandika na kuhesabu (LANES) iliyofanyika katika Maktaba ya mkoa Dc Daqarro amesema kuwa wajibu huo ni wetu sote kuanzia nyumbani hadi mashuleni kuhakikisha kila moja wetu anatimiza wajibu wake.
Amesema kuwa wiki kama hiyo ni ya kujitathmini tumefika wapi na tunaelekea wapi kama taifa kwa ajili ya kukuza uelewa wa vijana wetu kujua kuhesabu kusoma na kuandika ili kuwa na taifa linalopiga hatua kwa wananchi wake kujua kusoma.
“Taifa limejipanga kuondoa  wananchi wasio jua kusoma na kuandika ndio maana ilikaja na mkakati wa kkk hivyo kila mmoja wetu anawajibu kuhakikisha tunafikia malengo ya mkakati huu”alisema Daqarro
Kwa Upande wake Afisa elimu vielelezo Godfrey Augustino amesema kuwa wajibu wa wazazi ni kufuatilia maendeleo ya watoto wao na wao kama waalimu watahakikisha kila kijana anayepata nafasi anajua kusoma kuandika na kuhesabu lengo ni kuondoa vijana wanaomaliza elimu wakiwa hawajui kusoma na kuandika.
Amesema kuwa hatavumilia kuona wilaya hiyo ikiwa ina vijana ambao hawajui kusoma wala kuandika na amejipanga kuhakikisha wanafikia malengo yalioanza kuonekana kwenye ufaulu kwa wilaya kushika nafasi ya kwanza kitaifa katika ufaulu wa Darasa la saba mwaka huu.
Awali mkutubi mkuu wa maktaba ya mkoa Rafiki Mvamba amesema kuwa analishukuru shirika Kwa kufadhili wiki hiyo na kuwataka watanzania kupenda kujisomea na kufuatilia watoto wao ili kujua kusoma na kuandika itakayopelekea taifa kuwa na wananchi wenye elimu ya kuweza kufikia malengo endelevu.
Amesema kuwa mpango huo LANES wa wiki ya kusoma ni kujitathmini na kuwafikia wanafunzi kujua uelewa wao katika kukuza stadi za kusoma kuandika na kuhesabu kuanzia watoto wa awali hadi vyuo vikuu kupenda kujisomea kwani elimu haina mwisho.
“sisi kama maktaba tumejipanga kuhakikisha wanafunzi wote wanaofika hapa wanapata vitabu vyote wanavyohitaji sanjari na kuwapa nafasi na kuwaongoza pale wanapohitaji ili lengo ya kuwa na taifa lenye watu wanaojua kusoma na kuandika linafikiwa”alisema Mvamba.

Afisa elimu Vielelezo Godfrey Augustino akitoa hotuba kwenye ufunguzi wa wiki ya usomaji Lanes kabla ya kumkaribusha mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro (Picha na Mahmoud Ahmad- Arusha)

Pichani juu na chini ni sehemu ya wanafunzi wa shule sita za wilaya ya Arusha walioshiriki mashindano mbali mbali ya kusoma kuandika na kuhesabu wanaoonekana pichani ni wanafunzi wa shule ya msingi Mwangaza na sombetini  wakifuatilia kwa makini matukio mbali mbali yalioendelea kwenye hafla hiyo.

MAGAZETI YA LEO NOVEMBA 09, 2018.

Thursday, November 8, 2018

OKWI ATWAA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA MWEZI OKTOBA TPL

MSHAMBULIAJI wa timu ya Simba ya Dar es Salaam, Emmanuel Okwi amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Oktoba wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) msimu wa 2018/2019.

 Okwi anayecheza nafasi ya ushambuliaji, alitwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda wenzake wawili, Yahya Zayd wa Azam na Eliud Ambokile wa Mbeya City alioingia nao fainali katika uchambuzi uliofanywa Dar es Salaam wiki hii na Kamati ya Tuzo ya TPL inayotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kutokana na mapendekezo kutoka kwa makocha waliopo viwanja mbalimbali ambavyo ligi hiyo inachezwa msimu huu. 

Kwa mwezi huo Oktoba timu 18 zilicheza michezo mitano kila moja,  isipokuwa Simba na Yanga zilizocheza mechi nne. 

Katika michezo hiyo minne ambayo Simba ilicheza, Okwi raia wa Uganda alitoa mchango mkubwa kwa kupata pointi 12  kwa kushinda michezo yote na kumaliza ikiwa nafasi ya pili, huku Okwi akifunga mabao 7 kwa mwezi huo, matatu akifunga katika mchezo dhidi ya Ruvu Shooting ambao Simba iliibuka na ushindi wa mabao 5-0.

Kwa upande wa Ambokile naye alitoa mchango mkubwa kwa Mbeya City kufanikisha kupata pointi 11 baada ya kushinda michezo mitatu na kutoka sare miwili na kushika nafasi ya nane katika msimamo, akifunga mabao manne.

 Kuhusu Zayd alitoa mchango mkubwa kwa Azam akifunga mabao matatu katika michezo mitano ambayo Azam ilicheza ikishinda yote na kupata pointi 15 ikishika nafasi ya kwanza. 

Pia Kamati ya Tuzo, imemchagua Kocha wa Azam FC, Han Pluijm kuwa Kocha Bora wa mwezi Oktoba akiwashinda Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems na Kocha Mkuu wa Mbeya City, Ramadhan Nsazwarimo. 

Pluijm aliiongoza timu yake kupata pointi 15 baada ya kushinda michezo yote mitano iliyocheza na kushika nafasi ya kwanza, huku Aussems akiiongoza Simba kushinda michezo yote minne iliyocheza hivyo kupata pointi 12 na kushika nafasi ya pili, wakati Nsazwarimo alipata pointi 11 akishinda michezo mitatu na kutoka sare mitatu akiiwezesha timu yake kupanda hadi nafasi ya nane.

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara ina utaratibu wa kuwazadiwa wachezaji bora wa kila mwezi, huku pia mwisho wa msimu kukiwa na tuzo mbalimbali zinazohusu ligi hiyo, ambapo msimu wa mwaka 2017/2018 kulikuwa tuzo 16 zilitolewa kwa washindi wa kada mbalimbali, ambapo kwa ushindi huo Okwi atazawadiwa tuzo, king’amuzi kutoka Azam na Sh milioni moja kwa kuibuka Mchezaji Bora wa mwezi. 

Washindi wengine wa tuzo hiyo kwa msimu huu na miezi yao katika mabano ni mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere na mshambuliaji wa Mbeya City Eliud Ambokile. 

Kwa upande wa makocha walioshinda tuzo hizo kwa msimu huu ni Amri Said wa Mbao FC aliyeshinda tuzo ya Kocha Bora wa Agosti na Mwinyi Zahera wa Yanga aliyeshinda tuzo ya Kocha Bora wa Septemba.

MGOGORO WA PINGO, CHAMAKWEZA KWISHA AGOST 2019.

Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete,
 ...................................................

Na Omary Mngindo, Pingo

MGOGORO wa mpaka kati ya Kitongoji cha Pingo kinachokaliwa na jamii ya Wakulima na Kijiji cha Chamakweza cha Wafugaji, Kata ya Pera, halmashauri ya Chalinze, Bagamoyo Pwani, unataraji kunalizika mwezi wa nane mwakani.

Mgogoro huo uliodumu kwa miaka mingi katika eneo hilo linalopakana, umekuwa kikwazo cha kupatikana kwa maendeleo kwa wakazi wapande hizo hali inayokwamisha shughuli mbalimbali.

Hayo yamebainishwa na Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete, alipokuwa anazungumza na wakazi wa Kitongoji cha Pingo, siku moja kabla ya kuelekea mjini Dodoma kwa ajili ya kikao cha Bunge kilichoanza mwanzoni mwa mwezi Novemba.

"Niwaambie kwamba suala la mgogoro wa mpaka kati ya Pingo na Chamakweza suala lake lipo ukingoni kumalizika, kwa sasa lipo kwa wahusika wa ardhi, niwaambie kwamba mpaka ifikapo mwezi wa nane mwakani suala hili litabaki historia," alisema Ridhiwani.

Aliwaambia wakazi wa Kitongoji cha Pingo kwamba, mgogoro wa miaka mingi kati ya Kitongoji hicho na Chamakweza utabaki histotia, huku akiwataka wakazi kuendelea na utulivu, serikali yao inaendelea kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili.

Wakizungumza katika mkutano huo, wakazi Mussa Matungura, na Idd Fuko walisema kuwa mgogoro huo kwa kiasi kilibwa umechelewesha maendeleo kwa upande wa wakulima, kutokana na mifugo kuingia kwa wingi kwenye mashamba yao.

Kwa upande wake mzee Maarufu Rajabu Kiwamba alisema kwamba wakati wa uhai wa Mzee Kikwete (babu yake Rudhiwani) ndie aliyewapokea wafugaji akawatengea eneo la Chamakweza, wakati huo walikuwa wachche, kakini kadri miaka ilivyokuw inakwenda wakawa wanaitana hatimae kuwa wengi na kuingia ndani ya Pingo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kitongoji cha Pingo Miraji Dibwe alisema kuwa, kuna wawekezaji hawatambuliki na serikali wanawekeza, ambapo wanpokwenda kuzungumza nao wanasema wamepata vibali ngazi za juu.

Kauli iliyomkera Ridhiwani ambapo alisema kitu kama hicho hakipo, huku akisema wananchi ndio wenye maamuzi ya kila jambo kwenye eneo lao na si vinginevyo.