Posts

WAZIRI WA AFYA AFUNGUA MASHINE YA CT-SCAN HOSPITALI YA RUFAA BUGANDO

Image
waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ameahidi kuwaletea mashine ya uchunguzi ya MRI katika hospitali ya rufaa ya kanda ya ziwa Bugando mwaka huu. Waziri Ummy Mwalimu ameyasema hayo wakati akifungua mashine ya   CT-scan ambayo itakua inapima magonjwa mbalimbali iliyogharimu shilingi za kitanzania bilioni 1.6 ambazo zinetokana na vyanzo mbalimbali vya hospitali hiyo. Aidha,Waziri Ummy ameahidi ndani ya miaka mitatu kuanzisha taasisi ya moyo ili kuweza kupunguza gharama kwa wananchi wa kanda ya ziwa na magharibi wanaopata matatizo ya moyo kwenda kuoata vipimo na matibabu kwenye taasisi ya moyo ya   JKCI ya jijini Dar es Salaam. Waziri Ummy mwalimu akiongea na watumishinwa hospitali ya rufaa ya kanda ya ziwa ya bugando wakati wa uzinduzi wa mashine ya CT-scan Mkurugenzi wa hospitali ya rufaa ya bugando dkt.Abel Makubi akitoa shukrani mara baada ya uzinduzi wa mashine hiyo Askofu wa Jimbo la Geita Ba...