Tuesday, October 3, 2017

CGP. AWEKA JIWE LA MSINGI GEREZA LA KIGONGONI BAGAMOYO.


Kulia ni Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP, Dkt. Juma Aliy Malewa, akiweka jiwe la msingi nyumba mbili za askari magereza katika gereza la Kigongoni wilayani Bagamoyo, kushoto ni Mkuu wa Gereza la Kigongoni, Mrakibu wa Magereza, SP. Muyengi Bulilo.

Mkuu wa Gereza la Kigongoni, Mrakibu wa Magereza, SP. Muyengi Bulilo. (aliyeshika karatasi mkononi) akimunesha nyumba za askari zinazojengwa katika Gereza hilo.
........................

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP, Dkt. Juma Aliy Malewa, ameweka jiwe la msingi ujenzi wa nyumba mbili za Askari magereza na kuzindua jengo la wageni katika Gereza la Kigongoni wilayani Bagamoyo.

Akizungumza mara baada ya kuweka jiwe la msingi na kuzndua jengo la wageni,CGP. Dkt. Juma Malewa alisema magereza zote hapa nchini zinakabiliwa na changamoto za kukosa nyumba za kuishi Askari na kwamba mkakati uliopo ni kujenga nyumba hizo kwa kutumia nguvu kazi iliyopo ndani ya magereza.

Aidha, alisema Serikali imejipanga kuhakikisha inaondoa tatizo la nyumba za Askari magereza kwenye magereza yote hapa nchini na kuongeza kuwa katika kuhakikisha lengo hilo linatimia, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hivi karibu alitoa pesa kiasi cha shilingi Bilioni 10 ambazo zitatumika kujenga 380 za askari magereza katika gereza la Ukonga jijini Dar es Salaam.

Awali akitoa taarifa mbele ya Kamishna Jenerali wa Magereza, Mrakibu wa Magereza SP. Muyengi Bulilo alisema nyumba hizo zinajengwa kwa kutumia nguvukazi waliyonayo gerezani na hivyo kuokoa kiasi cha pesa ukilinganisha na ujenzi wa kutumia nguvu kazi za nje ya gereza.

Alisema nyumba hizo mbili kila moja itakuwa na familia tatu hivyo nyumba hizo zitakapokamilika zitachukua familia sita za askari magereza na hivyo kupunguza tatizo la uhaba wa nyumba za askari katika gereza hilo.
 
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP, Dkt. Juma Aliy Malewa,(kushoto) akizindua jengo la wageni katika gereza la Kigongoni Bagamoyo 


 
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP, Dkt. Juma Aliy Malewa, katikati akifurahi pamoja na maafisa wa jeshi la magereza mara baada ya kukata utepe kuashiria ufunguzi wa jengo la wageni pamoja duka katika Gereza la Kigongoni Bagamoyo, kulia ni mkuu wa Gereza hilo la Kigongoni, Mrakibu wa Magereza SP. Muyengi Bulilo. 

 
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP, Dkt. Juma Aliy Malewa, akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Bagamoyo, pamoja na maafisa wa jeshi la magereza katika Gereza la Kigongoni Bagamoyo.

RATIBA YA FAINALI YA MAZINGIRA CUP 2017 BAGAMOYO.



MAZINGIRA KABUMBU CUP 2017 BAGAMOYO
Fainali kati ya Magomeni Vs Nianjema itakua tarehe 6.10.2017.

Mshindi wa tatu atakua kati ya Dunda Vs Zinga tarehe 4.10.2017 michezo yote Itafanyika Mwanakalenge.

Aidha Fainali kati ya Bwilingu Vs Pera Itafanyika tarehe 14.10.2017 ktk uwanja wa Msata sekondari. 

Pia mshindi wa tatu kati ya Miono na Mbwewe itachezwa tarehe 9.10.2017 ktk uwanja wa msata  sekondari. 

Nawatakia maandalizi mema
IMETOLEWA NA MWENYEKITI WA MASHINDANO YA MAZINGIRA KABUMBU CUP.

NDG. KAPIRIMBA

MAGAZETI YA LEO TAREHE 03 SEPTEMBA 2017.

NAIBU WAZIRI AWATOA HOFU WAKAZI WA KIJIJI CHA MKENGE BAGAMOYO.



Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Tate Wilimu Ole nasha amewatoa hofu wakazi wa kijiji cha Mkenge kata ya Fukayosi wilayani Bagamoyo ambao wamepakana na Ranchi ya Ruvu na kuwataka waendelee na shughuli zao za kilimo kama kawaida wakati wakisubiri maamuzi ya kupitia upya mipaka ya Ranchi ya Ruvu.

Naibu waziri huyo alitoa kauli hiyo alipotembelea katika kijiji cha Mkenge na kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusu Ranchi ya Ruvu kuingilia mashamba ya asili ya wanakijiji hao jambo ambalo linasababisha usumbufu na kukosa sehemu ya kulima.

Aidha, naibu waziri huyo wa kilimo, Mifugo na uvuvi, aliwataka wenyeji wa kijiji hicho kuacha kuwakaribisha wageni kuja kuweka makazi katika maeneo hayo kwani kwa kufanya hivyo kutavuruga mpango wa serikali wakuandaa mipango ya kurekebisha mipaka.

Alisema kwa sasa wananchi wa kijiji hicho wanaweza kuendelea na shughuli zao za kilimo na kwamba maamuzi ya serikali yatakapotolewa hayawaathiri wananchi hao na kuwataka kuwa na subira na kufanya shughuli zao kilimo kwa amani na utulivu. 

Wakati huo huo, Nibu Waziri wa Kilimo, mifugo na uvuvi aliwataka wafugaji kuheshimu mashamba ya wakulima na kuacha kupeleka mifugo kwenye mashamba.

Alisema vijiji vimeandaa mpango wa matumizi bora ya Ardhi ikiwa ni pamoja na kutenga maeneo ya wafugaji na wakuli hivyo kila mmoja afanye shughuli zake kwenye maeneo ambayo ameruhusiwa kisheria bila ya kuingiliana.

Naibu waziri, Ole nasha, aliwataka makabila mawili jamii ya wafugaji, wamasai na wabarberi kuacha tofauti zao na badala yake wakae pamoja kwa maelewano.

Alisema kitendo cha kutokuelewana baina ya wamasai na wabar beri kunapelekea kundi moja kuhama sehemu waliypangiwa na hatimae kusababisha wavamizi wa maeneo ambayo sio rasmi kwa ufugaji.

Nae Mbunge wa jimbo la Bagamoyo, Dkt. Shukuru Kawambwa alimshukuru naibu Waziri huyo kwa kufika katika kijiji cha Mkenge ili kusikiliza kero za wananchi ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakimsumbua kuhusu mgogoro wa mipaka kati yao na Ranchi ya Ruvu.

Awali wananchi, wakazi wa kijiji cha Mkenge walimueleza Naibu waziri wa Kilimo, Mifugo na uvuvi kuwa wanapata usumbufu kwenye mashamba yao baada ya Ranchi Ruvu kuwataka kuondoka kwenye mashamba hayo ili kupisha hifadhi ya Ranchi jambo ambalo linapelekea kushindwa kuendelea na shughuli zao za kilimo.

Diwani wa Kata hiyo ya Fukayosi, ambae pia ni mwenyekiti wa Halmashauri ya Bagamoyo, Aliy Aliy Issah, alimuomba Naibu waziri huyo kuangalia uwezekano wa kuwaachia wananchi wakazi wa kijiji cha Mkenge maeneo yao ya kulima ambayo wamekuwa wakilima hapo kwa miaka mingi iliyopita.

wananchi wakazi wa kijiji cha Mkenge wakimsikiliza Naibu waziri wa kilimo, Mifugo na uvuvi, Wiliamu Ole nasha alipotembelea kijini hapo.

Mbunge wa jimbo la Bagamoyo, Dkt. Shukuru Kawambwa akizungumza katika mkutano huo.

Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, akimkaribisha Naibu waziri wa kilimo, Mifugo na uvuvi kuzungumza na wananchi katika kijiji cha Mkenge.

Monday, October 2, 2017

MAKAMU WA RAIS ATEMBELEA BONDE LA NGORONGORO

2
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiangalia bonde kuu la Ngorongoro mara baada ya kuwasili tayari kwa Uzinduzi wa Makumbusho Mpya ya Olduvai utakaofanyika kesho tarehe 3, oktoba 2017.
 4

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na Naibu Mhifadhi Dkt. Maurus Msuha mara baada ya kutembelea bonde kuu la Ngorongoro mara baada ya kuwasili tayari kwa Uzinduzi wa Makumbusho Mpya ya Olduvai utakaofanyika kesho tarehe 3, oktoba 2017.
Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais