Thursday, June 15, 2017

DC BAGAMOYO AZINDUA VISIMA 3 KATA YA KIROMO

Mkuu wa wilaya ya  Bagamoyo Alhaji, Majid Mwanga aliyevaa Kanzu, akizindua kisima kitongoji cha Mto wa Nyanza, kata ya Kiromo, katikati ni Mwenyekiti wa kitongoji cha Mto wa Nyanza, Omari Said Salum  na wa kwanza kulia ni Diwani wa kata ya Kiromo Hassan Usinga.
 
 Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Alhaj, Majid Mwanga ameishukuru Taasisi ya Dhi Nureyn Islamic Foundation yenye makao yake makuu mjini Iringa kwa kuchimba visima katika wilaya ya Bagamoyo. 

Akizungumza na wananchi wakati wa uzinduzi wa visima vitatu kata ya Kiromo, Mkuu huyo wa wilaya amesema Taasisi za dini zinamchango mkubwa katika kuleta maendeleo katika jamii. 

Alisema  licha ya kufanya kazi za kiroho lakini pia zimekuwa mstari wa mbele kusaidia huduma za kijamii kama vile ujenzi wa  visima, ujenzi wa Hospitali na shule, na kuongeza kuwa, hilo ndio lengo la serikali kusajili  taasisi  za  dini pamoja  na kutoa huduma za kiroho lakini pia zisaidie kuleta maendeleo.

Aliongeza kuwa uwepo wa Taasisi za dini ni muhimu katika jamii, kwani husaidia kuwajenga wananchi katika misingi ya imani, kumtambua Mungu na kuwajengea  hofu juu ya kutenda maovu mbalimbali ikiwemo uhalifu na   badala yake jamii inahimizwa kudumisha amani kutokana na imani zilizopo miongoni mwa wana dini.

Akii zungumzia Taasisi ya Dhi Nureyn Islamic Foun dation, Mkuu huyo wa wilaya ya B aga mo yo ,   alisema Taasisi hiyo kwa muda mfupi toka i an ze kusaidia B agamoyo imeweza kufanya mamb o makubwa kiasi ambacho inastahili kupongezwa. 

Alisema Taasisi hiyo kwa sasa imeshac himba  visima  10 wilayani Bagamoyo  vyenye thamani zaidi ya shilingi milioni mia moja  na kujenga wodi ya kina ma ma katika Hospitali ya wilaya ya Bagamoyo ye nye uwezo wa kukaa  vitanda 40 pamoja na jengo la mapokezi ya wagonjwa mahututi. 

Mratibu wa miradi ya Dhi Nureyn Islamic Foundation, Iddi Musa aliwataka wananchi wa waliopata visima katika maeneo yao  kuvitunza  visima hivyo ili waendelee  kufaidika na huduma hiyo ya maji huku thawabu zikiwafikia  wale waliotoa. 

Nao wananchi wa kata ya Kiromo wamemshuku mkuu wa wilaya ya Bagamoyo kwa kuwatafutia  wafadhili  wa  kuwachimbia visima ili waondokane na adha ya kutafuta maji umbali mrefu. 

Walisema awali walikuwa wanapata tabu kutafuta maji na kulazimika kuchota maji kwenye mabwawa hali iliyokuwa ikihatarisha afya zao pamoja na usalama wao.                             
                                                                                                                                                                                                                                       
     
Diwani wa kata ya Kiromo Hassan Usinga, akijaribu kufungua maji wakati wa uzinduzi huo wa visima katika kata yake.
 

Mratibu wa miradi ya Dhi Nureyn Islamic Foundation, Iddi Musaakizungumza katika uzinduzi huo.

 

wananchi wa kata ya Kiromo waliojitokeza katika uzinduzi huo.

Wednesday, June 14, 2017

KUWAIT YAKABIDHI VIFAA VYA UZAZI KWA SERIKALI YA TANZANIA

unnamed
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea beseni lenye vifaa vya uzazi kutoka kwa Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem.
Kuwait imetoa mabeseni 200 ya vifaa vya uzazi kwa hatua ya awali ambapo watatoa zaidi ya mabeseni 1000 yenye vifaa vya uzazi
1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia beseni lenye vifaa vya uzazi kutoka kwa Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem.
Kuwait imetoa mabeseni 200 ya vifaa vya uzazi kwa hatua ya awali ambapo watatoa zaidi ya mabeseni 1000 yenye vifaa vya uzazi. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
......................


Balozi wa Kuwait hapa nchini Jasem Al- Najem amemkabidhi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan vifaa tiba vya uzazi zaidi ya 200 ambavyo vitasambazwa katika hospitali mbalimbali kwa Tanzania Bara na Zanzibar.

Makabidhiano ya vifaa hivyo vya uzazi yamefanyika leo Ikulu ya Dar es Salaam ambapo Balozi wa Kuwait hapa Nchini Jasem Al- Najem amesema Serikali ya nchi hiyo imetoa vifaa hivyo kama hatua ya kuendelea kudumisha na kuendeleza mahusiano mazuri kati ya nchi hiyo na Tanzania.

Amesema kuwa Serikali ya Kuwait imetoa vifaa hivyo ikiwa ni awamu ya kwanza na lengo ni kutoa vifaa hivyo zaidi ya 1000 vyenye thamani ya shilingi milioni 40 kwa wanawake wajawazito na waliojifungua katika hospitali mbalimbali nchini.

Mara baada ya kupokea msaada huo, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ameishukuru Serikali ya Kuwait kwa msaada huo ambao utasambazwa katika hospitali mbalimbali kwa Tanzania Bara na Zanzibar.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema msaada huo utasaidia sana wanawake wajawazito na waliojifungua kupata vifaa za uzazi ambavyo vinahitajika wakati wanamke mjamzito anapojifungua na baada ya kujifungua.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa vifaa hivyo vitaanza kusambazwa kuanzia mwezi huu na mchakato wa kuainishwa hospitali zitakazopata msaada huo unaendelea.

Makamu wa Rais pia amesisitiza kudumishwa kwa mahusiano mazuri yaliyopo kati ya nchi ya Kuwait na Tanzania kwa ajili ya manufaa ya wananchi wa pande zote Mbili.

Aidha Balozi huyo wa Kuwait hapa nchini Jasem Al- Najem amemhakikishia Makamu wa Rais kuwa Serakali ya Kuwait itaendelea kusaidia Serikali ya Tanzania katika uimarishaji wa sekta ya afya na elimu nchini ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na za msingi.

Tuesday, June 13, 2017

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA WAKUU WA MIKOA WOTE

2WAKUU1WAKUU2

POLISI WATOA TAHADHAR YAI MATAPELI

Katika siku za hivi karibuni, kumeibuka  kikundi kidogo cha matapeli wanaozunguka katika maeneo mbalimbali hususani vijijini na kuwalaghai vijana kwamba wao ni watumishi ama waajiriwa wa Jeshi la Polisi na kujipatia fedha kutoka kwa wananchi/vijana hao kwa udanganyifu kwamba watawapatia ajira ndani ya Jeshi la Polisi jambo ambalo siyo la kweli.

Jeshi la Polisi nchini, linatoa tahadhari kwa  wananchi kwamba ndani ya Jeshi la Polisi hakuna ajira zilizotangazwa, na hivyo tunawataka wananchi wote kuwa makini na mtandao huo wa matapeli. Mfumo wa ajira ndani ya Jeshi la Polisi ni wa wazi na una utaratibu maalum ambao hutangazwa kwa wananchi kwa mujibu wa taratibu za Jeshi la Polisi.

Kufuatia hali hiyo,  Jeshi la Polisi linatoa onyo kali kwa wote wenye tabia hiyo ya utapeli kuacha mara moja na endapo mtu yeyote atabainika hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Jeshi la Polisi linatoa rai kwa wananchi wote wenye taarifa za matapeli hao kuzifikisha haraka katika kituo chochote cha Polisi kilicho karibu ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.

Imetolewa na:
Advera John  Bulimba – ACP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Makao Makuu ya Polisi.