Thursday, May 25, 2017

WAHARIRI HABARI WAPEWA SEMINA.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF), Kees Groenendijk (kushoto) akiwasilisha mada kwa baadhi ya wahariri na wanahabari waandamizi katika semina kwa wanahabari iliyoandaliwa na LSF. Mfuko huo leo umekutana na baadhi ya wahariri na waandishi waandamizi na kutoa semina juu ya mchango wa vyombo vya habari katika kusaidia taasisi zinazotoa msaada wa sheria kwa jamii.
Mwanasheria kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Wakili Harold Sungusia (kulia) akiwasilisha mada kwa baadhi ya wahariri na wanahabari waandamizi katika semina kwa wanahabari iliyoandaliwa na LSF. Wanatasnia hao wa habari wamepata fursa ya kujadiliana kwa pamoja na LSF namna vyombo vya habari vinavyoweza kusaidia upatikanaji wa haki kwa ujumla kwa jamii.
 
Baadhi ya wahariri na waandishi wa habari waandamizi kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiwa katika semina iliyoandaliwa na Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF) kwa na kuzungumzia mchango wa vyombo vya habari katika kusaidia taasisi zinazotoa msaada wa sheria kwa jamii.
Baadhi ya wahariri na waandishi wa habari waandamizi kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiwa katika semina iliyoandaliwa na Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF) kwa na kuzungumzia mchango wa vyombo vya habari katika kusaidia taasisi zinazotoa msaada wa sheria kwa jamii.
Wakili Harold Sungusia akisisitiza jambo alipokuwa akiwasilisha mada kwa baadhi ya wahariri na wanahabari waandamizi katika semina kwa wanahabari iliyoandaliwa na LSF.
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakifuatilia mada anuai.
Ofisa Uhusiano wa Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF), Robart Zephania (mbele aliyesimama) akizungumza katika semina hiyo.

CCM YAITAKA SERIKALI KUCHUKUA HATUA MAUAJI YA PWANI.

POLEP
Chama Cha Mapinduzi kimeitaka Serikali kuchukua hatua za haraka kuhusu matukio ya Mauaji yanayoendelea katika Wilaya za Kibiti, Mkutanga na Rufiji Mkoani Pwani ili kuepusha mauaji hayo kuendelea kutokea.

          Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, HUMPHEY POLEPOLE, amesema hayo Jijini Dar es salaam   leo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mauaji yanayoendelea katika Wilaya hizo.

          POLEPOLE pia amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha vinaelekeza akili, nguvu zao katika Wilaya hizo kwa kuwa maujia hayo yanasababisha kuzorota kwa shughuli za maendeleo.

          Amesema chama kwa muda mrefu kimekaa kimya kikiamini hatua zitachukuliwa kwa kuwa wanachama wake na watendaji wameendelea kupoteza maisha ambapo amesema kwa sasa imetosha.

Kuhusu suala la uchaguzi ambao unaendelea ndani ya Chama hicho amesema mauaji hayo yanakiweka Chama katika mazingira magumu ya kufanya chaguzi zake hivyo ni vema hatua zikachukuliwa sasa.

          Katika hatua nyingine, POLEPOLE amesema Chama kimeipongeza Kamati Maalum ya kuchunguza Mchanga wa Madini kwa kazi nzuri iliyofanywa sanjari na kuwaomba wananchi kumuunga mkono Rais JOHN MAGUFULI kwa hatua alizozichukua kwa watendaji kutokana na Ripoti ya Mchanga wa Madini.

KIBAHA YAZINDUA JUKWAA LA UWEZESHAJI WANAWAKE KIUCHUMI

MSHAMA
Mkuu wa wilaya ya Kibaha ,Assumpter Mshama na mbunge wa viti maalum mkoani Pwani Subira Mgalu mwenye kiremba cha blue wakitembelea mabanda mbalimbali ya bidhaa za wajasiriamali wa Mji wa Kibaha ,baada ya kuzindua jukwaa la wanawake la kuwawezesha kiuchumi mjini hapo .(picha na Mwamvua Mwinyi )
....................


WILAYA ya Kibaha imezindua jukwaa la uwezeshaji wanawake kiuchumi na kuchagua viongozi wake watakaoongoza katika kipindi cha miaka mitano.

Jukwaa hilo limempitisha Betty Msimbe kuwa mwenyekiti huku Sada Duda akichaguliwa katibu kipindi hicho .

Afisa maendeleo ya jamii halmashauri ya Mji wa Kibaha ,Leah Lwanji aliwataja viongozi hao ambao wamechaguliwa na akina mama wajasiriamali mbalimbali .

Alieleza kuwa kuundwa kwa jukwaa hilo kutasaidia kuwezeshwa vikundi vya akinamama wajasiriamali kirahisi .

Leah alisema wanawake waungane waache kujiweka binafsi ili kupiga hatua kimaendeleo na kiuchumi .

Hata hivyo alisema ,katika kipindi cha mwezi april hadi may mwaka huu halmashauri ya Mji huo imechangia sh .mil 56 kwa kukopesha vikundi 34 vya wanawake ,kwenye kata 14 zilizopo mjini humo .

Leah alielezea kwamba ,July hadi desemba mwaka 2016 ,walitoa mil .16 kwa vikundi Tisa na Jan – march mwaka 2017 wametoa mil.70 kwa vikundi 46 .

Alisema kwa upande wa fungu la vijana afisa maendeleo huyo ya jamii ,wametoa asilimia kumi katika mapato ya ndani kwa kutoa sh.mil 32 zilizopelekwa saccos ya vijana .

“Tunamkabidhi mkuu wa wilaya ya Kibaha hundi ya sh.mil 56 kutoka NMB itakayogawiwa katika vikundi 34″ alisema Leah .

Nae diwani wa viti maalum Mji wa Kibaha ambae pia ni katibu wa jukwaa la uwezeshaji mkoani Pwani ,Elina Mgonja alisema ,umoja wao utawawezesha kuwa na sauti kupigania fursa za kiujasiriamali .

Alisema wamejipanga kuthubutu kuanzisha miradi mbalimbali na kushikana mkono ili kujikwamua kimaisha .

Elina alitoa rai kwa wanawake kujitambua na kujithamini .

Nae mkuu wa wilaya ya Kibaha ,Assumpter Mshama ,aliwataka wanawake wathubutu kuanzisha viwanda vidogo na vikubwa kwenda na sera ya uchumi wa viwanda .

Aliwaomba wajenge tabia ya kugombea nafasi za uongozi bila kuwaachia wanaume .

Assumpter alisema kinamama waamke waache kulala kwani sio wakati wa kuzorota na kusemana majungu na kukatishana tamaa .