Tuesday, May 9, 2017

WATANO WAFARIKI ARUSHA BAADA YA NYUMBA KUANGUKIWA NA MTI.

nyumba ikiwa imeangukiwa na mti kama inavyoonekana
katika picha
Image result for charles mkumbo
mvua inayonyesha mfululizo Mkoani  Arusha imeleta maafa makubwa katika familia ya mzee Jonathani Kalambiya{55} mkazi wa sokoni II katika kijiji cha kinyeresi wilayani Arumeru Mkoani Arusha baada ya mti
mkubwa uliong’olewa na maji kuangukia nyumba yake na kuua watoto wake wote watano.
Mkasa huo wa usikitisha ulitokea jana majira ya saa 7 usiku baada ya mti huo kung’olewa na maji uliangukia nyumba hiyo iliyokuwa jira na mti huo.

Kamanda wa polisi Mkoani Arusha, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Charles Mkumbo alithibitisha tukio hilo na kuwataja watoto waliokufa katika tukio hilo ni pamoja na watoto wawili wanafunzi wa mzee huyo ambaye ni mlinzi wa hospital ya ya Dr Mohamed ya Jijini Arusha.

Mkumbo aliwataka wanafunzi ambao ni watoto wa mzee Kalambwia ambaye siku ya tukio alikuwa kazini ni pamoja na Miliamu Jonathani(16) mwanafunzi wa kidatu cha pili wa shule ya sekondari ya Inaboishu.

Kamanda alimtaja mwanafunzi mwingine ni ambaye ni mtoto wa mzee huyo ni Grolia Jonathani(11) mwanafunzi wa shule ya msingi Kinyeresi iliyoko wilayani Arumeru Mkoani Arusha.

Amesema watoto wengine wa mzee huyo ni pamoja na mtoto wa kwanza wa mzee huyo aliyetambuliwa kwa jina la Giliad  Jonathani(31),Lazaro Lomnyaki
(26) na Best Jonathani(20).
Kamanda Mkumbo alisema kuwa mti huo uliokuwa katika mlima wa Lake mana uliangukia nyumba hiyo baada ya kung’olewa na mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika Jiji la Arusha na Mkoa kwa ujumla.

Alisema na kuitakia pole sana familia yam zee huyo kwani tukio hilo ni majonzi makubwa sana kwake kwani familia nzima imeondoka na kumtaka kuwa na uvumilivu katika wakati huu mgumu kwake.

Kamanda Mkumbo ametoa wito na ushauri kwa wakazi wa Arusha kuchukuwa tahadhari katika kipindi hiki cha mvua kubwa zinazoendelea kunyesha kwa kukarabati nyumba zao na kuacha kujenga chini ya mti ama kwenye vyanzo vya maji.

Amesema kujenga katika vyanzo vya maji ama chini ya mti ni kujitafutia majanga mengine hivyo ni vema kila mkazi wa Mkoa wa Arusha kuchukuwa tahadhali hiyo.

Aidha kamanda ametoa tahadhari kutokana na habari za uzushizinazoendele kuwa jana kwenye kuaga miili ya wanafunzi kuna mtu alidondoka juu ya mti na kufariki pamoja na mama mmoja mtoto wake mdogo alifariki,amesema habari hizo siyo za kweli wananchi wazipuuze kabisa 


WAANDISHI WA HABARI ZANZIBAR WAPEWA MAFUNZO.

ZAB
Serikali imeshauriwa  kuheshimu uhuru wa vyombo vya habari ili waandishi waweze kupata nafasi ya kufichua matatizo  yanayoikabili jamii na kupatiwa ufumbuzi.

Hayo yamesemwa leo huko Park Hyyat Hotel na mwandishi wa habari kutoka ubalozi wa Marekani nchini Tanzania  Kenneth Cooper wakati alipokuwa akitoa mafunzo kwa wandishi wa habari wa vyombo mbalimbali hapa nchini.

Amesema kuvitisha vyombo vya habari na kuvibinya katika kutekeleza majukumu yake ni kuvipotezea ufanisi na kupelekea kufanya kazi zake kwa woga na kushindwa kufichua maovu.

“Serikali ikubali na iheshimu uwepo vyombo vya habari, kwani kuvibinya nikusababisha matatizo nchini,” alisisitiza Kenneth Cooper.

Alisema vyombo vya habari vina mchango mkubwa kwa jamii kwani vinaweza kuibua matatizo yanayoikabili hivyo kupitia vyombo hivyo yanaweza kufika kwa wahusika.

Akizungumzia njia bora kwa  waandishi kutafuta na kuripoti habari, Cooper alisema mwandishi anatakiwa kuwa makini na mdadisi katika utafutaji wa habari.

Amewaeleza washiriki wa mafunzo kuwa wanapaswa  kujenga uhusiano mzuri na vyanzo vya habari ili  waweze kupata habari kwa urahisi  pamoja na kufuatilia mtiririko wa matukio mbalimbali.

Aidha amewahimiza waandishi kufanya utafiti na kutotosheka na chanzo kimoja cha habari  na kuweka umuhimu wa kutoa nafasi sawa kwa watu watakaohusika katika habari ili kuepuka matatizo.

Hata hivyo amesisitiza waandishi kufanya tathmini  na kujua thamani ya maisha yao ili kuweza kujali usalama wa maisha, kuweka matarajio ya kazi zao pamoja na kuwa na mashirikiano na waandishi wengine katika kutekeleza majukumu yao.

Nae Mwenyekiti wa Jumuiya ya Waandishi wa Habari Zanzibar (ZPC) Abdalla Abdulrahman Mfaume ameushukuru Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania kwa kuwapatia mafunzo hayo jambo ambalo litawajengea uwezo na ameushauri ubalozi huo kuendelea kushirikiana na waandishi wa Zanzibar kwa mafunzo zaidi.

NEC YAANZA KUTOA ELIMU YA MPIGA KURA KWA NJIA YA REDIO.

unnamed
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Kailima Ramadhani akitoa elimu ya mpiga kura kupitia redio A FM ya mkoani Dodoma leo Mei 9 mwaka huu huku akifuatiliwa kwa makini na watangazaji wa redio hiyo.
...................................


Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetoa wito kwa wananchi walioko kwenye halmashauri mbalimbali nchini, kuitumia vyema fursa ya utoaji wa elimu ya mpiga kura kupitia redio za kijamii kwenye halmashauri zao ili kuondoa manung’uniko kwenye chaguzi.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume hiyo Bw. Kailima Ramadhani wakati akizungumzia mpango wa kutoa elimu ya mpiga kura nchi nzima ulioanza kutekelezwa Mei 8 mwaka huu hii katika mikoa kumi nchini.

Alisema kupitia mpango huo wananchi wanaosikiliza redio za kijamii kwenye halmashauri nchini, watapata fursa ya kujifunza elimu ya mpiga kura na kuelewa masuala yote muhimu yanayohusu mfumo mzima wa kupiga kura.

“Tumepanga mpango, Tume itasambaa nchi nzima kuzungumzia elimu ya mpiga kura kwenye redio za kijamii zilizoko kwenye halmashauri zote za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.” alisema Bw. Kailima.

Alisisitiza kwa kutoa wito kwa wananchi walioko maeneo ambayo Tume itakwenda kutoa elimu ya mpiga kura, wasikilize na kuuliza maswali ili waweze kuelewa.

 “Hii ni fursa kwa wananchi ambayo muda mrefu hawajawahi kuipata, hivyo nawaomba wafuatilie ili waweze kuelimika zaidi ili yale manung’uniko ya kura yatakuwa yamekwisha na tutakuwa na uchaguzi mzuri zaidi ya ile ambayo tumeifanya.” Alifafanua Bw. Kailima.

Utekelezaji wa mpango huo umegawanyika katika makundi matatu ambapo kundi la kwanza limeanza kutoa elimu hiyo elimu hiyo kwenye mikoa ya Kagera,Mwanza, Kilimanjaro, Morogoro, Mbeya na Dodoma.

Mikoa mingine itakayojumuishwa kwenye kundi hilo ni Ruvuma, Mara, Pwani na Mtwara ambapo elimu hiyo itatolewa kuanzia tarehe 8 Mei hadi tarehe 20 Mei mwaka 2017.

Kundi la pili linatarajiwa kutoa elimu hiyo kuanzia tarehe 24 Mei hadi tarehe 7 Juni mwaka huu katika mikoa ya Geita, Tanga, Singida, Shinyanga, Lindi, Arusha, Tabora, Kigoma, Iringa, Manyara, Rukwa, Katavi, Songwe, Njombe na Simiyu.

Bw. Kailima alisema kuwa utoaji wa elimu hiyo utajikita kwenye mada kuu ya Elimu ya Mpiga Kura iliyogawanywa kwenye vipindi vitano, itakaytoolewa kwenye redio hizo kulingana mada husika na wananchi kuuliza maswali na kujibiwa na wawasilishaji wa mada hizo kutoka Tume.

“Ni mada ambayo imejumuisha masuala yote muhumu yatakayofanya mpiga kura yeyote au mdau yeyote wa uchaguzi kuisoma au kuisikiliza na akaelewa mfumo mzima wa masuala ya kupiga kura” alisema.

Mbali na kutoa elimu ya mpiga kura kupitia vituo vya redio za kijamii katika halmashauri nchi nzima, Tume pia inatoa elimu hiyo kwa njia ya magazeti na vyombo vingine vya habari  na mitandao ya kijamii, kushiriki kwenye mikutano na maonesho mbalimbali nchini.