Thursday, April 13, 2017

MAJAMBAZI WAPORA MILIONI 18 NA MALI KIWANDANI KISARAWE.

unnamed
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani,kamishna msaidizi mwandamizi,  (SACP) Onesmo Lyanga, akizungumza na waandishi wa Habari.

Na Mwamvua Mwinyi, Pwani.

KUNDI la watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wamevamia kiwanda cha prayose wilayani Kisarawe mkoani Pwani na kupora fedha na mali zenye thamani ya mil. 25.

Kati ya vitu vilivyoporwa ni pamoja na fedha taslimu sh mil. 18,laptop mbili za mil. mbili na simu 14 zenye gharama ya mil. tano. 

Aidha katika tukio hilo watu wanne wenye asili ya kihindi wamejeruhiwa kwa kupigwa na nondo kwenye maeneo mbalimbali ya miili yao. 


Kamanda wa polisi mkoa  wa  Pwani, kamishna msaidizi mwandamizi,  (SACP) Onesmo Lyanga, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo, april 13 majira ya saa 7 usiku  .

Alisema huko maeneo ya kiwanda hicho, kundi la watu zaidi ya sita wakiwa na mapanga na marungu walikivamia na kuwafunga kamba walinzi wawili waliokuwa zamu kisha kuingia ndani ya kiwanda na kujeruhi wahindi wanne. 

Kamanda Lyanga alieleza, licha ya kuwajeruhi watu hao ,waliweza kuwafunga kwa kamba wafanyakazi waliokuwa wakiendelea na uzalishaji kiwandani ambapo  walifanikiwa kupora mali na fedha. 

Alitoa rai kwa wafanyabiashara kuacha kuhifadhi kiwango kikubwa cha fedha ndani na badala yake fedha hizo wakazihifadhi kwenye taasisi za kifedha -bank kwa usalama zaidi. 

“Wafanyabiashara wajitambue kwani kuweka fedha ndani, kwenye kampuni ni risk “ “Kufuatia suala hilo lilivyo tunawashikilia walinzi wa kampuni hiyo kwa uchunguzi zaidi “alisema. 

Kufuatia tukio hilo jeshi la polisi mkoani Pwani, linawashikilia walinzi waliokuwa zamu kwa mahojiano. 

Kamanda Lyanga aliomba ushirikiano kwa jamii kulisaidia jeshi hilo mara watakapobaini watu waliofanya tukio hilo

MAGAZETI YA LEO TAREHE 13 APRILI 2017

BA

Wednesday, April 12, 2017

GOLIKIPA WA MBAO FC ASIMAMISHWA KAZI KWA KUIBEBA SIMBA.

Simba
Uongozi wa klabu ya Mbao FC ya Ilemela jijini Mwanza umemsimamisha mlinda mlango wa timu hiyo Erick Ngwengwe kwa muda usiojulikana kwa tuhuma za upangaji wa matokeo kwa madai kuwa amechukuwa rushwa kwa klabu ya Simba au kuwa na mapenzi binafsi na Simba.

Afisa Habari wa Mbao FC,Christian Malinzi ameuambia mtandao huu kuwa katika kikao kilichoketi siku ya jana uongozi umeamua kumsimamisha kwa muda usiojulikana ili kupisha uchunguzi zaidi juu ya kile kinachoenekana amehusika katika upangaji wa matokeo.

Malinzi alisema kwamba uongozi ulijalibu kutafuta dodosa za tuhuma hizo,umebaini kuwepo kwa viashiria vya upangaji wa matokeo ambavyo vimesababishwa na yeye kwa kuweza kuruhusu magoli ya kizembe.

Alisema kwamba kwa sasa hawawezi kumtuhumu moja kwa moja kuwa ndie aliyehusika na swala hilo ndio maana uongozi umeamua kumuondoa kambini ili kupisha uchunguzi wa kina juu ya yake.

Hata hivyo alisema kwamba ingawa hakuna taarifa ya kuhusika katika swala la kuchukua fedha lakini huenda kukawepo na mapenzi binfsi kwa mchezaji mwenyewe kuipenda timu Pinzani kwani wachezaji wengi wa Tanzania wamegawanyika katika vilabu vya Simba na Yanga.

YANGA KUZINDUA AKAUNTI YA KUCHANGIA MAENDELEO YA KLABU WIKI IJAYO

yanga-vs-tp-mazembe_9kbl2mw1wpk719bcqdrk00u75
Uzinduzi wa akaunti hiyo utafanyika makao makuu ya klabu hiyo yakiongozwa na ofisi ya katibu mkuu wa klabu hiyo , ndugu Charles Boniface Mkwasa .

Akizungumzia uzinduzi huo , katibu mkuu wa klabu hiyo amesema wapo katika hatua za mwisho kukamilisha taratibu za ufunguzi wa akaunti hiyo.

” tupo katika hatua za mwisho kukamilisha hatuza za ufunguzi wa akaunti hiyo. Akaunti itakuwa na uwazi na kila kinachochangiwa kitaonekana na dhumuni la kufungua akaunti hiyo litasimamiwa vyema .

 Ni wazo ambalo wadau , mashabiki na wanachama wamelileta na sisi kama uongozi tumelibariki. Hii ni timu ya wanachama hivyo maamuzi yao chanya tunayeheshimu sana . ” alieleza katibu huyo katika mkutano ambao ulikuwa rasmi kuzungumzia safari ya kuondoka kwa Yanga SC kuelekea Algeria kesho.

HATMA YA UBUNGE WA SOPHIA SIMBA YATOLEWA LEO.

Image result for Sophia Simba images Bungeni
Tume ya Taifa ya Uchaguzi inapenda kuutarifu Umma kuwa; kwa mujibu wa Kifungu cha 37 (3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, Mhe. Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemjulisha Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa; kufuatia Mbunge wa Viti Maalum, SOPHIA MNYAMBI SIMBA kufukuzwa
uanachama wa Chama cha Mapinduzi tarehe 11 Machi, 2017 kiti cha Mbunge huyo wa Viti Maalum Wanawake kwa tiketi ya CCM kiko wazi.
        
Kwa mujibu wa Ibara ya 67 (1) (b) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ili mtu ateuliwe au achaguliwe katika nafasi ya Ubunge ni lazima awe mwanachama aliyependekezwa na Chama  chake husika cha Siasa.

         Kwa kuwa Ndg. SOPHIA MNYAMBI SIMBA amefukuzwa uanachama wa Chama kilichomdhamini, Ibara ya 67 (2) (e) ya Katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inaelekeza kuwa Mbunge huyo amepoteza sifa za kuteuliwa au kugombea Ubunge.
        
Kutokana na kuwepo kwa nafasi wazi ya  Ubunge wa Viti Maalum, taratibu za kujaza nafasi hiyo zinaendelea kwa kuzingatia kifungu cha 86A (8) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343.

Jaji
(R) Semistocles Simon Kaijage
Mwenyekiti
TUME
YA TAIFA YA UCHAGUZI