Friday, March 3, 2017

RAIS DKT. JOHN MAGUFULI ATOA MIEZI MINNE MRADI WA MAJI NG'APA MKOANI LINDI KUKAMILIKA.

lin2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Ng’apa mara baada ya kutembelea mradi wa Maji wa eneo hilo ambao unasuasua kukamilika. Rais Dkt. Magufuli ametoa miezi minne kwa Mkandarasi kampuni ya Overseas Infrastructure Alliance Private Limited ya India kuhakikisha kuwa inakamilisha ujenzi wa mradi huo na sio kuleta visingizio.
lin1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa Waziri wa Maji Mhandisi Gerson Lwenge kuhakikisha kuwa Mradi wa Maji wa Ng’apa uliopo mkoani Lindi unakamilika ndani ya miezi mine na si vinginevyo.
lin13
Sehemu ya Mradi wa Maji wa Ng’apa mkoani Lindi ambao Rais Dkt. Magufuli ametoa miezi minne kwa mkandarasi anayejenga mradi huo ili uweze kukamilika haraka. PICHA NA IKULU
LIND1LIND2

HATIMAE GODBLES LEMA NJE KWA DHAMANA YA MILIONI MOJA.

lema
Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, imemuachia huru Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini, Godbles Lema (CHADEMA) kwa dhamana ya shilingi milioni moja pamoja na wadhamini wawili wenye vitambulisho vinavyotambulika na serikali.

Mbunge Lema alikaa mahabusu kwa takribani miezi minne akikabiliwa na kesi ya uchochezi, katika Gereza Kuu la Arusha lililopo Kisongo, na kwamba amefanikiwa kupata dhamani na kupokewa na washabiki wake waliomtandikia kanga ili apite wakati akitoka mahakamani hapo.

Hukumu hiyo ndogo imesomwa na jaji aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo, Fatuma Magimbi  katika mahakama kuu Arusha.

Akizungumza nje ya mahakama hiyo, Lema alisema kuwa amejifunza mengi alipokuwa mahabusu kwa kipindi chote hicho na kwamba ameandaa waraka wa kumwandikia Raisi kuelezea yale aliyoyaona alipokuwa mahabusu.

Nae mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe alisema kuwa wanamkaribisha tena Lema bungeni na kwamba kamati ya chama imemaliza vikao vyake mjini hapa na kuwashukuru wabunge wa mikoa mbali mbali waliofika kutetea dhamana ya lema.

16 WASHIKILIWA NA POLISI PWANI KWA TUHUMA ZA UJAMBAZI / MAUAJI.


 Kamanda wa  Polisi  Mkoa wa  Pwani,  Kamishna Msaidizi wa  Polisi  (ACP)  Boniventure Mushongi.

 JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

Makachero wa Jeshi  la  Polisi  Mkoa wa  Pwani wakishirikiana na  wale kutoka  Makao Makuu ya Polisi, tunamshikilia  Khalid Mohamed (29) ambae ni fundi ujenzi na mkazi wa kwa Mathias Wilaya ya  Kibaha akiwa na Silaha aina ya SMG na risasi 14.

Mtuhumiwa huyo, tulimkamata huko eneo la Misugusugu Kata ya Misugusugu na Tarafa na Wilaya ya  Kibaha akiwa na Silaha hiyo aina ya SMG ambayo namba zake zimefutwa pamoja na risasi 14  jana Tarehe 02/03/2017 majira ya 17:15  HRS.

Mtuhumiwa huyo,  mb ali na  kukutwa na Silaha hiyo, pia alikutwana  risasi  4 za Shotgun, Mlipuko mmoja, Sime  moja, maski moja na koti moja vyote vikiwa vimehifadhiwa kwenye mfuko wa Rambo chini ya Ardhi kwenye Shamba la mtu  aliyejulikana kwa jina  moja  la Swai.

Uchunguzi  wa Awali umeweza kubaini kuwa, mtuhumiwahuyo na wenzake wengine 15 ambao tunawashikilia wamekiri kujihusisha na matukio ya uporaji kwenye maeneo mbalimbali ya Mkoa wa  Pwani,  likiwemo  tukio  la mauaji ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya  Liwale mwaka 2012-2016,  Ephraim  Mfingi  Mbaga (54) aliyuwawa  akiwa nyum bani kwake baada ya kupigwa risasi  kwenye  paja lamguu  wa  kushoto na kujeruhiwa kwa  kitu chenye ncha  kali ambapo alipoteza maisha akiwa njiani akipelekwa Hospitali ya Rufaa ya Tumbi.

Imetolewa na:-
Kamanda wa Polisi Mkoa wa  Pwani
Boniventure Mushongi (ACP)
03 March 2017.      

MAGAZETI YA TANZANIA LEO 03 MARCH 2017.