Monday, September 26, 2016

RAIS DKT MAGUFULI ATEMBELEA BANDARI YA DAR ES SALAAM LEO

ban1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitembelea  Bandari ya Dar es salaam leo Septemba 26, 2016 akiwa ameongozana na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, Katibu Mkuu Uchukuzi i Dkt Leonard Chamriho na uongozi wa Bandari.
 ban2

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitoka kuangalia sehemu ya kupakulia mafuta kutoka kwenye meli katika bandari ya Dar es salaam leo Septemba 26, 2016 akiwa ameongozana na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa,  Katibu Mkuu Uchukuzii Dkt Leonard Chamriho na uongozi wa Bandari.
 ban3

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitoka kuangalia sehemu ya kupakulia mafuta kutoka kwenye meli katika bandari ya Dar es salaam leo Septemba 26, 2016 akiwa ameongozana na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa,  Katibu Mkuu Uchukuzi i Dkt Leonard Chamriho na uongozi wa Bandari
 ban4

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitoa maelekezo  kuangalia sehemu ya kupimia kiwango cha mafuta yanayoingia nchini  kutoka kwenye meli (Flow Meter) katika bandari ya Dar es salaam leo Septemba 26, 2016
 ban5

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi Mary Mhayaya kuhusu   chumba cha mitambo ya  uthibiti wa kiwango cha mafuta yanayoingia nchini  kutoka kwenye meli (Oil Flow Meter) katika bandari ya Dar es salaam leo Septemba 26, 2016.
 ban6

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipata maelezo ya chumba cha ukaguzi wa mizigo (scanner) inayoingia nchini  katika bandari ya Dar es salaam leo Septemba 26, 2016.
 ban7

Wafanyakazi wa bandari ya Dar es salaam wakimlaki kwa furaha  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli alipofika kuongea nao baada ya kutembelea bandari ya Dar es salaam leo Septemba 26, 2016 
 ban8

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea na wafanyakazi wa bandari baada ya kutembelea bandari ya Dar es salaam leo Septemba 26, 2016.
 ban9

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea na wafanyakazi wa bandari baada ya kutembelea bandari ya Dar es salaam leo Septemba 26, 2016
 ban10

Mwenyekiti wa Wafanyakazi wa Bandarini Bw. Mashaka Karume, akieleza baadhi ya changamoto wanazokabiliana nazo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli alipotembelea bandari ya Dar es salaam leo Septemba 26, 2016
 ban11

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipata maelezo kutoka kwa   Kampuni ya  Ushushaji Mizigo Bandarini ya Tanzania International Container Terminal (TICTS)  Bw. Donald Talawa  alipotembelea bandari ya Dar es salaam leo Septemba 26, 2016 
 PICHA NA IKULU

Saturday, September 24, 2016

RAIS MAGUFULI AMTEUA DKT. ZAINABU CHAULA KUWA NAIBU KATIBU MKUU TAMISEMI

004
Aliyekuwa Mganga Mfawidhi hospitali ya Rufaa ya Dodoma Dkt. Zainabu Chaula (kushoto) ambaye Rais Magufuli amemteua  kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI ) katika moja ya matukio  hospitali ya rufaa ya Dodoma akionekana kukabidhiwa msaada wa mto wa kulalia na Mkuu wa Vodacom Tanzania Kanda ya Kati,Mruta Hamisi kwa ajili ya wodi ya watoto hospitalini hapo.
.................................
 

SERIKALI KUFANYA ZOEZI LA UTAMBUZI NA USAJILI KWA WATUMISHI WAKE KUANZIA OKTOBA 3

utu1
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angella Kairuki akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, kuhusu zoezi la utambuzi na usajili wa vitambulisho kwa watumishi wa umma litakaloanza tarehe 03 Oktoba. Kulia kwaker ni Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Dkt. Laurian Ndumbaro na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Seerikali Mtandao (EGA), Dkt. Jabir Bakari
 utu2

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulkisho vya Taifa (NIDA), Mohammed Khamis Abdallah akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, kuhusu zoezi la utambuzi na usajili wa vitambulisho kwa watumishi wa umma litakaloanza tarehe 03 Oktoba . Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Seerikali Mtandao (EGA), Dkt. Jabir 
.....................................


SERIKALI inatarajia kufanya zoezi la utambuzi na usajili wa taarifa za watumishi wa umma kuanzia tarehe 3 Oktoba ili kutoa vitambulisho vya Taifa vilivyo na taarifa zote muhimu za mtumishi husika.

Hayo yamebainisha na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki alipokutana na waandishi wa habari ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam.

Kairuki amesema kuwa zoezi hilo la utambuzi na usajili wa wananchi ambalo linaanza na watumishi wa umma ni muhimu na litasaidia kupunguza gharama kwa Serikali na kuondoa usumbufu kwa wananchi kwani taarifa zao zote muhimu zitakuwa sehemu moja hivyo kupunguza kero ya kuulizwa taarifa kila uendapo.

Waziri Kairuki amesema kuwa zoezi hilo litashirikisha Wizara yake pamoja na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia  Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), ambapo taarifa zitakazotumika ni zilizilizopo katika vitambulisho vya mpiga kura.

“Kama mnavyofahamu kuwa Serikali ipo katika maboresho makubwa ya utendaji wake, hivyo ili kuendana na hali hiyo tutaanza zoezi la utambuzi na usajili wa watumishi wa umma kuanzia tarehe 3 Oktoba, zoezi litakalochukua takribani wiki mbili, zoezi hili ni muendelezo wa Serikali kukabiliana na matatizo ya kutokuwa na taarifa sahihi.” Alisema Kairuki.

Aidha Kairuki amewata watumishi wote wa umma kushiriki zaoezi hilo wakiwa na taarifa zote muhimu zinazowatambulisha ambazo ni pamoja na Cheti cha kuzaliwa, vyeti vya elimu, kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha Mzanzibar Mkazi, hati ya malipo ya Mshahara, hati ya kusafiria na kadi ya mpiga kura.

Waziri huyo ametoa wito kwa waajiri kuweka mazingira wezesha ili kufanikisha zoezi hilo ikiwemo kutenga ofisi itakayotumiwa na kwa kazi hiyo pamoja na kusisitiza waajiri wahakikishe watumishi wao wanasajiliwa bila kukusa na taarifa ya zoezi hilo iwasilishe Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawabora ndani ya siku 14 tangu zoezi hilo kukamilika kwake.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt. Laurian Ndumbaro amewataka watumishi wote wa umma kulipa umuhimu mkubwa zaozi hilo na kusisitiza kuwa Serikali haita sita kucghukua hatuia za kinidhamu kwa mujibu wa kanuni za utumishi wa umma kwa mtumishi yeyote atakaye kaidi zoezi hilo.

Awali akijibu swali la mwandishi wa habari kuhusu namna zoezi hilo litakavyotekelezwa nchi znima kwa muda wa wiki mbili tu, Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Mohammed Khamis Abdallah amesema kuwa zoezi hilo litafanikiwa kwani wanao wafanyakazi zaidi ya 460 nchini nzima ambao wapo katika Ofisi za Halmashauri.

Pia aligusia suala la vifaa na kusema kuwa tayari wamewasiliana na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ambayo imewapa mashine za BVR kwa ajili ya kuzitumia katika zoezi hilo la utambuzi na usajili.

Zoezi la utambuzi na usajili wa wananchi hasa watumishi wa uuma kukabiliana na vyanzo vya watumishi hewa kwa kuunganisha mifumo ya utambuzi wa watu na mifumo mingine ikiwemo usimamizi wa rasilimali watu na mishahara katika utumishi wa umma ambapo kuunganishwa kwa mifumo hiyo kutawezesha mifumo hiyo kuwasiliana na kutumia taarifa zilizo kwenye kanzi data ya NIDA suala litakalokuwa limerahisisha upatikanaji wa taarifa.