Sunday, September 18, 2016

WAZIRI NAPE ATOA MILIONI TANO KWA SERENGETI BOYS

ser6

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akimkabidhi Millioni tano Nahodha wa Serengeti Boys Bw. Issa Abdi Makame kama motisha kabla ya kabla ya mechi ya leo dhidi ya Congo-Brazaville iliyofanyika katika Uwanja wa Taifa Septemba 18,2016.
 ser3
Kocha wa Serengeti Boys Bw. Bw.Bakari  Shime akimshukuru Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (Hayupo Pichani) kwa kuwapa motisha wachezaji kabla ya mechi kati ya Serengeti Boys na Congo-Brazaville iliyofanyika katika Uwanja wa Taifa Septemba 18,2016.
 ser1
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza leo Jijini Dar es Salaam na wachezaji wa Serengeti Boys katika hafla fupi ya kuwakabidhi Shilingi Milioni Tano kama motisha kabla ya mechi ya leo dhidi ya Congo-Brazaville iliyofanyika katika Uwanja wa Taifa Septemba 18,2016.
 ser2
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) Bw. Jamali Malinzi akitoa maelezo juu ya maaandalizi ya mechi kati ya Serengeti Boys na Congo-Brazaville iliyofanyika katika Uwanja wa Taifa Septemba 18,2016.
 ser3
Kocha wa Serengeti Boys Bw. Bw.Bakari  Shime akimshukuru Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (Hayupo Pichani) kwa kuwapa motisha wachezaji kabla ya mechi kati ya Serengeti Boys na Congo-Brazaville iliyofanyika katika Uwanja wa Taifa Septemba 18,2016.
 ser4
Nahodha wa Serengeti Boys Bw. Issa Abdi Makame akiahidi kwa Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (Hayupo Pichani) kuibuka na ushindi dhidi ya Congo-Brazaville katika mechi iliyofanyika katika Uwanja wa Taifa Septemba 18,2016.
 ser7
Baadhi ya wachezaji wa Serengeti Boys wakimsikiliza Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (Hayupo Pichani) katika hafla fupi kabla ya mechi yao dhidi ya Congo-Brazaville iliyofanyika katika Uwanja wa Taifa Septemba 18,2016.

MAHUJAJI WA TANZANIA WAKO SALAMA NA WAKO NJIANI WAKIREJEA NYUMBANI TANZANIA

mahu

 Ibada ya hijja imemalizika rasmi katika mji wa Makkah na Madina na mahujaji wa dini ya kiislamu zaidi ya milioni 2 kutoka nchi zipatazo 164 wameanza kurejea makwao walikotoka.

Ibada ya mwaka huu imekuwa ya mafanikio kwa kumalizika salama, hii ni kutokana na Serikali ya Saudi Arabia kuwa na mipango madhubuti kwa kuimarisha miundombinu, usafiri, ulinzi na usalama na kurekebisha dosari zilizojitokeza mwaka jana.

Maeneo ya misikiti yote miwili ya Makkah na Madina yaliimarishwa na yanaendelea kujengwa ikiwa ni pamoja na kupanuliwa ili kuongeza nafasi za kutosha kufanyia ibada.

Mahujaji kutoka Tanzania wapatao 2,000 wako salama na wao ni miongoni mwa walioshiriki katika ibada na sasa wako njiani kurejea Tanzania.

Hatua zilizochukuliwa na mamlaka za ulinzi za Saudi Arabia ni pamoja na kuhakikisha kuwa makundi ya misafara ya mahujaji hayagongani kati ya wanaokwenda na wanaorudi, njia mbalimbali zilikuwa zikifungwa na kufunguliwa ili kuruhusu misafara kwenda uelekeo mmoja bila kukutana. 

Hatua hii ilisaidia kuepusha ajali kama iliyotokea wakati wa ibada ya hijja ya mwaka 2015.

Habari hizi ni kwa mujibu wa Kamati ya Hijja ya Tanzania.

MHALIFU SUGU NA MBAKAJI AUWAWA KIBAHA

rpc-pwani
 Kamanda wa Polisi  mkoa wa Pwani, Kamishna msaidizi wa Polisi ACP-Bonaventura Mushongi wa kwanza kushoto.
.........................................................

 Na Mwamvua Mwinyi,Pwani

MICHAEL William maarufu Michael dada ambae alikuwa akidaiwa ni mhalifu sugu na mbakaji huko wilayani Kibaha ameuwawa na wananchi wenye hasira kali.

Michael ameuwawa huko kwenye pori la shirika la elimu Kibaha-Tumbi,akidaiwa kuwateka watoto wa kike wawili ambao ni wanafunzi kwa lengo la kuwabaka.

Kamanda wa polisi mkoani Pwani,Bonaventura Mushongi akizungumzia tukio hilo,alisema watu hao walimshambulia mtu huyo sehemu mbalimbali za mwili na kumsababishia kifo.

Kwa mujibu wa kamanda huyo wa polisi,alisema tukio lilitokea juzi saa 10 alasiri.

Alisema marehemu huyo alimchukua mwanafunzi mwenye umri wa miaka (11) anaesoma shule ya msingi Kibaha na mwingine mwenye miaka (6) mwanafunzi wa shule ya chekechea ya mama Kawili wote wanaishi Picha ya Ndege.

Watoto hao walikuwa wakicheza rede mtaani kwao karibu na baa ya Lekashingo kata ya Picha ya Ndege ambapo Michael aliwashawishi wamsindikize mtaa wa Lulanzi kwenda kuchukua mzigo wake ambao aliusahau”
“Watoto hao walimkubalia na kuanza kuongozana nae lakini wakiwa njiani ghafla lilitokea gari aina ya toyota noah nyeusi ambayo haikuweza kufahamika namba zake za usajili na kuondoka nao kwenda nao pori la shirika la slimu Kibaha karibu na shule ya sekondari ya Tumbi’
“Wakiwa katika pori hilo mtoto mkubwa alimponyoka wakiwa wamefika kwenye bwawa la maji machafu kisha kuomba msaada ndipo kundi la watu lilipojitokeza na kuanza kumkimbiza na walipomkamata walimpiga hadi kufariki dunia,” alisema kamanda Mushongi.

Kamanda Mushongi ,alisema uchunguzi uliofanywa na jeshi la polisi umebaini marehemu alikuwa mhalifu mzoefu na alikuwa akifanya matukio ya mara kwa mara ikiwemo ya ubakaji na wizi wa mifugo.

Alisema hivi karibuni alikamatwa na kufikishwa mahakama ya wilaya ya Kibaha kwa kosa la kuiba ngombe wanne.

Michael aliachiwa huru yeye na mwenzake Said Mohamed baada ya mlalamikaji kushindwa kufika mahakamani baada ya kuwapata ngombe wake kwa kesi iliyofunguliwa namba KBH/STPU/02/2014.

Jeshi hilo limewakemea wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi badala yake wawafikishe watuhumiwa kwenye vyombo vya sheria kwa hatua zaidi.

MAGAZETI YA TANZANIA LEO TAREHE 18 SEPTEMBA 2016