Monday, August 22, 2016

UVCCM KUFANYA MAADAMANO YA KUMPONGEZA RAIS MAGUFULI AGOSTI 31/ 2016

Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Shaka Hamdu Shaka akiwaonesha Waandishi wa habari barua walioiandikia Jeshi la Polisi kuomba kibali na Ulinzi cha kufanya Maandamano hayo ya amani,wanayotarajia kufanya Agosti 31,kwa lengo la kumpongeza na kueleza Wananchi utendaji kazi wa Rais Dkt John Pombe Magufuli.
 OTH_8200

Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Shaka Hamdu Shaka akitoa ufafanuzi kwa baadho ya maswali mbalimbali yaliyokuwa yakiulizwa na Waandishi wa habari kuhusiana na Maandamano hayo ya amani yanayotarajiwa kufanyika Agosti 31,kwa minajili ya kumpongeza na kueleza Wananchi utendaji kazi wa Rais Dkt John Pombe Magufuli.
 

Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Shaka Hamdu Shaka akizungumza na Waandishi wa habari Makao makuu ya Ofisi hizo mapema leo jijini Dar kuhusiana na kufanya maandamano ya amani Agosti 31,kwa minajili ya kumpongeza na kueleza Wananchi utendaji kazi wa Rais Dkt John Pombe Magufuli.
.................................................................................................................


Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) wanatarajia kufanya maandamano ya Amani Agosti 31 kwa ajili ya kueleza utendaji kazi wa Rais Dk.John Pombe Magufuli kwa Watanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja huo, Shaka Hamdu Shaka amesema kuwa maandamano hayo wameshamwandikia barua mkuu wa jeshi la Polisi kwa ajili ya kupata ulinzi siku hiyo’

Amesema kuwa wasipopata ulinzi watafanya kwa kujilinda wenyewe ikiwa ni lengo la kufikisha ujumbe kwa wananchi juu ya utendaji kazi wa Rais Dk. John Pombe Magufuli.Shaka amesema kuwa Rais Dk.John Pombe Magufuli amefanya watendaji kuwa na utii pamoja na maadili katika utoaji wa huduma kwa wananchi.

Aidha amesema kuwa maandamano hayo wanaawalika na vijana wa vyama vingine kushiriki kwa lengo moja tuu,la kuunga mkono utendaji wa Rais Dkt.John Pombe Magufuli.



TAARIFA YA TANESCO BAGAMOYO KWA WATEJA WAKE

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) linaendelea kuwatangazia wateja wake wote wa Wilaya ya Bagamoyo kuwa, kutokana na kukatika kwa waya wa mawasiliano, (Optic Fiber) kati ya Dar es Salaam na Bagamoyo, Ofisi ya Shirika hilo wilayani Bagamoyo bado inashindwa kutoa huduma za kupokea malipo na kuuza LUKU kwa muda mpaka hapo waya huo utakapoungwa.

Kwa mujibu wa taarifa ya Ofisi ya Uhusiano MakaoMakuu yaTANESCO, Kwa sasa Shirika linawaomba wateja wake wanaotaka kununua umeme au kulipia huduma zingine za umeme kutumia njia mbadala ya mitandao ya Simu na makampuni mengine yenye mikataba na TANESCO.

Jitihada zinaendelea ili kuhakikisha mkongo huo wa mawasiliano unaungwa mapema iwezekanavyo. Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza.

JESHI LA POLISI LAWATOA HOFU WANANCHI.

Msemaji-wa-Jeshi-la-Polisi-Advera-John-Bulimba-akielezea-juu-ya-kukamatwa-kwa-watu-16-waliojihusisha-na-mlipuko-wa-mabomu-Arusha-na-kumwagia-Mashekh-Tindi-kali
Katika siku za hivi karibuni, kumekuwepo na mitazamo tofauti miongoni mwa jamii kufuatia kuonekana kwa askari polisi wakifanya mazoezi katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Kufuatia hali hiyo, jeshi la polisi nchini, linatumia fursa hii kuwatoa hofu wananchi kwamba mazoezi hayo ni ya kawaida kwa askari wa jeshi la polisi
Aidha, jeshi la polisi linawataka wananchi kuendelea na shughuli zao za kawaida kwa sababu mazoezi hayo hayalengi kuzuia shughuli zozote halali zinazofanywa na wananchi.

Imetolewa na:

Advera John Bulimba – Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP)
Msemaji wa Jeshi la Polisi,

Makao Makuu ya Polisi.

MAGAZETI YA TANZANIA LEO TAREHE 22-08-2016.

kach

Sunday, August 21, 2016

TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI MWANZA

index
TAREHE 21.08.2016 MAJIRA YA 10:00 USIKU KATIKA ENEO LA CLUB YA VILLA PARK RESORT KATA YA KIRUMBA WILAYA YA ILEMELA MKOA WA MWANZA, ASKARI NAMBA G.5092 PC JOHN NYANGE WA OFISI YA MKUU WA UPELELEZI NA MAKOSA YA JINAI MKOA WA MWANZA (RCO), ALIUAWA KWA KUCHOMWA NA KITU CHENYE NCHA KALI ENEO LA SHINGONI NA MTU ALIYEKUWA ANAUGOMVI NAE.

INADAIWA KUWA MAREHEMU ALIKUA NA UGOMVI WA MUDA MREFU NA MTU ALIYEJULIKANA KWA JINA MAGINA HUSSEIN MIAKA [27] FUNDI COMPUTER MSUKUMA NA MKAZI WA MTAA WA KIGOTO, AMBAPO MAREHEMU ALIKUWA AKIMDAI BWANA MAGINA HUSSEIN COMPUTER AINA YA LAPTOP.  

NDIPO USIKU WA LEO MAJIRA TAJWA HAPO JUU WALIKUTANA ENEO LA CLUB YA VILLA PARK HUKU MTUHUMIWA WA MAUAJI HAYO IKISEMEKANA KUWA ALIKUWA NA WENZAKE WATANO NDIPO WALIMVAMIA NA KUMCHOMA NA KITU CHENYE NCHA KALI SHINGONI NA KUFARIKI DUNIA NJIANI WAKATI AKIPELEKWA HOSPITALI.

MAREHEMU KWA SASA ALIKUWA NI MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA STEFANO MOSHI MEMORIAL UNIVERSITY COLLEGE CHA MJINI MOSHI, ALIKUWA ANASOMEA SHAHADA YA SAYANSI YA HABARI NA MAWASILIANO MWAKA WA PILI, AIDHA ALIREJEA MWANZA BAADA YA KUPATA LIKIZO KUJA KUIANGALIA FAMILIA YAKE NDIPO UMAUTI UKAMKUTA.

WATUHUMIWA SITA AKIWEPO MAGINA SELEMANI AMBAYE ALIKUWA NA UGOMVI NA MAREHEMU PAMOJA NA WENZAKE WATANO WAMEKAMATWA, WAPO KATIKA MAHOJIANO NA JESHI LA POLISI HUKU UCHUNGUZI KUHUSIANA NA KIFO HICHO UKIWA BADO UNAENDELEA,  PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA WATUHUMIWA WOTE WATAFIKISHWA MAHAKAMANI, MWILI WA MAREHEMU  UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA YA BUGANDO KWA UCHUNGUZI.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WANANCHI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA, KWAMBA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LIMESIKITISHWA NA KIFO CHA ASKARI HUYU KWANI LIMEMPOTEZA ASKARI KIJANA AMBAYE BADO JESHI LILIKUWA LINAMTEGEMEA. 

LAKINI PIA ANAWATAKA WATU WENYE TABIA ZA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWA KUWAPIGA WENGINE HADI KUFIKIA KUPOTEZA MAISHA KUWA WANAFANYA KOSA LA JINAI, NA KAMA WATU WANADAIANA WAFUATE TARATIBU ZA KISHERIA ZILIZOWEKWA ILI KUEPUSHA VIFO VINAVYOWEZA KUEPUKIKA, HIVYO JESHI LA POLISI LINAWATAKA KUACHA TABIA HIYO MARA MOJA KWANI HATUA KALI ZA KISHERIA ZITACHUKULIWA DHIDI YAO.

IMETOLEWA NA:
DCP: AHMED MSANGI
KAMANDA WAPOLISI (M) MWANZA