Posts

MPINZANI WA YANGA CAF KUJULIKANA SAA 8:30 MCHANA LEO.

Image
Yanga SC imeangukia kwenye kapu la kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, ambako watamenyana na moja ya timu zilizofuzu hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo. Hiyo ni baada ya kutolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya sare ya 0-0 na wenyeji, Township Rollers Jumamosi jioni Uwanja wa Taifa mjini Gaborone nchini Botswana. Timu ambazo zimefuzua hatua ya mtoani ambazo Yanga anaweza kukutana nazo ni Fosa Juniors kutoka Madagascar, CARA Brazzaville (Con) , Costa do Sol ya Msumbiji, Akwa United na Enyimba z a Nigeria, Deportivo Niefanga ya Equatorial Guinea, Welayta Dicha ya Ethiopia,, El Masry ya Misri ,Hilal El  Obied ya Sudan, Raja Casablanca na Berkane za Morocco, Djoliba ya Mali, CR Belouizdad , USM Alger za Algeria, La Mancha ya Congo Brazaville na Supersport United ya Afrika Kusini. Timu ambazo zimetolewa Ligi ya Mabingwa na kuangukia Shirikisho ni Yanga ya Tanzania, Aduana Stars ya Ghana,A l-Hilal Omdurman...

AJALI YA GARI YA MKURUGENZI WA TBC, WAWILI WAFARIKI.

Image
Watu wawili wamekufa wilayani Kasulu mkoani Kigoma katika ajali ya gari la Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania TBC Dkt. Ayub Rioba lililokuwa likitokea wilayani Kibondo kwenda Kigoma Mjini. Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma, Kamishna Msaidizi Martin Otieno amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema chanzo cha ajali hiyo ni utelezi uliosababisha gari kuacha njia na kuwagonga waenda kwa miguu watatu. Gari la Mkurugenzi Mkuu wa TBC lililopata ajali lenye namba za usajili  STK 8769 lilikuwa na abiria wawili akiwemo mkurugenzi mkuu wa TBC, Dkt. Ayub Rioba na Mkuu wa kanda ya magharibi TBC Mhandisi Zebron Mafuru ambao  wote wametoka salama na hali zao ni nzuri. Dkt. Rioba yuko katika ziara ya kukagua vituo vipya vya matangazo vilivyojengwa katika maeneo ya mipakani.

RAIS DKT. MAGUFULI AIVUNJA BODI YA NHC.

Image

SERIKALI YATENGA BILIONI TANO KUNUNUA MASHINE YA KUPIMA VIPIMO VYA TB.

Image
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiongea na baadhi ya wadau wa Sekta ya afya hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa dawa ya kutibu kifua kikuu kwa watoto wadogo kueleka maadhimisho ya siku ya Kifua Kikuu tarehe 24 Machi 2019. ................................... NA WAMJW-DAR ES SALAAM. SERIKALI kupitia Wizara ya Afya imetenga shilingi bilioni 5 kwa ajili ya kununua mashine za kupima vipimo vya ugonjwa wa kifua kikuu katika zahanati na vituo vya afya nchini.  Hayo yamezungumzwa jijini Dar es salaam na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi wa dawa za kutibu ugonjwa wa Kifua Kikuu kwa watoto kuanzia umri wa miaka 14 kushuka chini. “Serikali imadhamiria kupambana na ugonjwa wa Kifua Kikuu hivyo tumetenga shilingi bilioni 5 kwa ajili ya kuongeza mashine nyingine za kufanya uchunguzi kwa haraka ugonjwa wa Kifua Kikuu zinazoitwa Genexpert ” alisema Waziri Ummy....

MAGAZETI YA LEO TAREHE 21 MACHI 2018.

Image

MAKAMU WA RAIS ATEMBELEA HOSPITALI YA ABDALLA MZEE PEMBA.

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimjulia hali mtoto Rayna Abdala mwenye umri wa mwaka mmoja aliyelazwa kutokana na kuungua moto katika hospitali ya Abdala Mzee, mkoa wa Kusini Pemba. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimjulia hali mtoto Hafidh Jabir Ali mwenye umri wa miaka 3 aliyelazwa kutokana na kuungua na chai katika hospitali ya Abdala Mzee, mkoa wa Kusini Pemba. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Dkt. Wuxiao Shu juu ya matibabu ya mguu wa mtoto AzarAli mwenye umri wa miaka aliyelazwa  katika hospitali ya Abdala Mzee, mkoa wa Kusini Pemba. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi nje ya majengo ya hospitali ya Abdala Mzee, mkoa wa Kusini Pemba mara baada ya kukagua maendeleo ya hospitali hiyo.  Picha na Ofis...

MSITU WA ZIGUA SASA UMEREJEA KATIKA HALI YAKE YA KAWAIDA.

Image
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mh. Alhaj, Majid Hemedi Mwanga akionyesha sehemu ya makazi ya watu waliokuwa wamevamia msitu wa Zigua hivi karibuni katika Doria maalu ya kukagua msitu huo iliyowashirikisha watendaji kutoka TFS wilaya ya Bagamoyo na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ambapo kwa pamoja wamejiridhisha kwamba hakuna mvamizi aliykuwemo ndani ya msitu huo kwa sasa. ........................................ Hifadhi ya msitu wa zigua imerejea katika hali yake ya kawaida baada ya kuwaondoa wavamizi ndani ya msitu huo. Akizungumza na bagamoyokwanza blog amara bada ya kufanya doria maalum katika msitu huo, Kaimu Meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu nchini (TFS) Halmashauri ya Chalinze David George Ntemi, alisema hali ya msitu huo kwa sasa inaridhisha kutokana na miti kushamiri na baadhi ya wanyama kuonekana kurejea ndani ya msitu huo ambao awali walianza kutoweka. Alisema   hifadhi hiyo ya msitu wa Zigua, ulikuwa umeharibiwa na wananchi ambao walivamia kw...