Tuesday, September 26, 2023

TUNATAKA SIMBA NA YANGA ZIJE KUWEKA KAMBI PWANI WAWEKEZAJI JITOKEZENI KUWEKEZA PWANI KATIKA MICHEZO.

 

KISARAWE PWANI


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe Dkt Selemani Saidi Jafo ametoa wito kwa wawekezaji Tanzania kutumia fursa ya kuwekeza katika miundombinu ya Michezo Pwani,


Akizungumza Wakati wa kikao/Mikutano Mkuu wa Kamati tendaji kilichokutana Kisarawe mkoani Pwani na kutoa wito kwa jamii hasa wawekezaji kuwekeza katika miundombinu ya Michezo katika Maeneo mbalimbali hasa viwanja,


*"Pwani imebarikiwa kuwa na Maeneo mbalimbali mazuri ya kambi za Michezo na viwanja vizuri Ila kutumika ndio shida Sasa nashauri wawekezaji waje kuwekeza huku maana Mazingira ya uwezeshaji na uwekezaji*" alimazia Mhe Dkt Jafo


Aidha Katika kikao/ Mikutano huo umepitisha kwa kauli moja ya kuendelea kwa Kumchagua tena Dkt Jafo kuwa mlezi wa Chama Cha Soka Mkoa wa Pwani Corefa.


*"Napenda kuchukua Nafasi Hii kukupatia taarifa ya kuwa wajumbe Hawa kwa kauli moja wamekuchagua kuwa Mlezi wao kwa Mara nyengine alimalizia Mwwenyekiti wa Chama Cha Soka Mkoa wa Pwani Corefa*" Ndg Robert Munis 

SHULE BORA YATOA MAFUNZO YA MAHIRI YA HISABATI KISARAWE

 

Kisarawe Pwani.


Katika Hatua ya Kuboresha Utendaji,Ufaulu na Ufanisi wa mwanafunzi shuleni Taasisi ya Elimu Tanzania Kwa kushirikiana OR-TAMISEMI Kupitia Program ya shule Bora wamekuja na Uimarishaji Mahiri wa Somo la Hisabati Kisarawe Mkoa wa Pwani ulioanza 26/29-09-2023.


Akizungumza Wakati wa kufungua mafunzo elekezi ya SoMo la Hisabati kwa Wilaya Kisarawe Afisa Mdhibiti Ubora wa Shule wa Wilaya Bi Mbwelu Emanuel Mwankina alifurahishwa na Uwepo wa Mada ya Hisabati katika Mafunzo,


*"Binafsi nimefurahishwa na Uwepo wa Mada ya Somo la Hisabati katika Mafunzo haya maana imekua Changamoto kubwa kwa wanafunzi wengi hasa Kisarawe*" alimazia Bi Mwankina


Aidha kwa upande wake mwakilishi wa Mkuu wa Idara ya Elimu Awali na Msingi Bi Lulu Ndali alisema mafunzo hayo yakawe chachu ya mafanikio kwa Walimu kukaa pamoja kwa wingi na kubadilishana mbinu za Ufaulu na Ufundishaji wa Somo la Hisabati,


Mafunzo haya kwa Walimu kuhusu Uboreshaji wa Ufundishaji na Ujifunzaji wa Umahiri wenye Changamoto katika Somo la Hisabati Mkoa wa Pwani Wilaya Kisarawe kwa ufadhili wa watu wa Uingereza(UK Aid)