Saturday, February 18, 2023

WAZIRI WA ELIMU AKEMEA WIZI WA MITIHANI.

 No description available.

No description available.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda, akizungumza wakati alipotembelea Chuo cha Wakala wa Maendeleo ya uongozi wa Elimu (ADEM) kilichopo mjini Bagamoyo, february 17, 2023.

................................................................


Na Athumani Shomari.


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda, amesema serikali haitafumbia macho wale wote watakaojihusisha na kuvujisha mitihani kwa namna yoyote ile.

 

Waziri Mkenda aliyasema hayo February 17, 2023 alipotembelea Chuo cha Wakala wa Maendeleo ya uongozi wa Elimu (ADEM) kilichopo mjini Bagamoyo  ambapo alisema kitendo cha kuiba au kuvujisha mitihani ni kitendo cha dhulma dhidi ya wale wanaojituma kufanya mitihani kwa akili zao.

 

Alisema tayari baadhi ya watu walioripotiwa kujihusisha na wizi wa mitihani wameshaanza kuchukuliwa hatua ikiwemo kukamatwa na jeshi la polisi na kuanza kuwahojiwa.

 

Prof. Mkenda amewapongeza polisi nchini kwa kufuatilia matukio ya wizi wa mitihani na wahusika kuwachukulia hatua na kuongeza kwa kusema kuwa, jeshi la polisi nchini linafanya kazi nzuri sana katika kuhakikisha wizi mitihani unakomeshwa.

 

Aliongeza kwa kusema kuwa, walimu wanapaswa kuwa na maadili mema ikiwa ni pamoja na kujizuia kabisa na vitendo vya udanganyifu, wizi au kuvujisha mitihani kwa lengo la kujenga Taifa lenye watu wenye nidhamu, na taaluma iliyopatikana kwa njia sahihi.

 

Waziri Mkenda ameutaka uongozi wa Chuo cha Wakala wa Maendeleo ya uongozi wa Elimu (ADEM) kufundisha maadili pamoja malezi kwa walimu wote watakaosomea uongozi wa elimu ili watakaporudi kwenye shule zao wakasimamie maadili shuleni kwao kwa walimu walio chini yao pamoja na wanafunzi wao.

 

Akizungumza mbele ya Waziri wa elimu, Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Halima Habib alisema kasi ya uandikishaji wa wanafunzi wa darasa la kwanza na ile wanafunzi wa kidato cha kwanza kuripoti shuleni inaendelea vizuri katika wilaya hiyo na kwamba mpaka sasa wanafunzi wote walioripoti ni asilimia 98.

 

Mkuu huyo wa wilaya alitumia nafasi hiyo kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Huluhu Hassan kwa kutoa kipaumbele kwenye elimu hali iliyopelekea wanafunzi wote katika wilaya hiyo kupata vyumba vya madarasa kwaajili ya kusoema.

 

Awali akiwasilisha Taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya ADEM mbele ya waziri, Mtendaji Mkuu wa ADEM, Dkt. Siston Masanja, amesema ADEM ina majukumu mbalimbali ikiwa ni pamoja na Kutoa mafunzo ya muda mrefu na mfupi ya uongozi na usimamizi wa elimu kwa viongozi na watendaji mbalimbali wa elimu katika ngazi zote ikwemo Shule, Kata, Halmashauri, Mkoa, na Wizara.

 

Dkt. Masanja aliongeza kuwa, jukumu linguine ni kufanya tafiti katika maeneo ya uongozi na usimamizi wa elimu ili kubaini na kutafuta ufumbuzi wake lengo likiwa ni kutatua changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika sekta ya elimu.

 

Aidha, Dkt. Masanja alimueleza Waziri wa Elimu, kuwa kozi za muda mrefu zinazotelewa chuoni hapo ni 

 

1.   Astashahada ya Uongozi, Usimamizi na Utawala katika Elimu (Certificate in Education Leadership, Management and Administration- CELMA) ambayo ni kozi mwaka mmoja na ilianzishwa 2014.

 

2.   Stashahada ya Uongozi na Usimamizi wa Elimu (Diploma in Education Management and Administration- DEMA) ambapo kozi hii ni ya miaka miwili, na ilianzishwa mwaka 2014.

 

3.   Stashahada ya Udhibiti Ubora wa Shule (Diploma in School Quality Assurance- DSQA) ambayo hapo awali ilijulikana kama Stashahada ya Ukaguzi wa Shule (Diploma in School Inspection-DSI) iliyoanzishwa mwaka 2014.

 

Alibainisha kuwa, katika kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2018 hadi 2022 jumla ya walimu 4,895 wamehitimu mafunzo ya Stashahada za Uongozi, Usimamizi na Udhibiti Ubora wa Elimu.

 

Dkt. Masanja alisema pamoja na mafanikio yaliyopatikana ADEM inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo.

 

1.   Ufinyu wa bajeti ya kuendeshea mafunzo ya muda mfupi na watendajina viongozi wa Elimu wanaoteuliwa wakiwemo Maafisa Elimu, Maafisa Elimu Kata, Walimu wakuu, Wakuu wa shule na Wadhibiti Ubora wa shule.

 

2.   Baadhi ya Walimu waliochaguliwa kujiunga na masomo yatolewayo na ADEM kukosa ruhusa ya masomo kutoka kwa waajiri wao.

 

Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu-ADEM, ulianzishwa Tarehe 31 Agosti 2001kwa mujibu wa Sheria ya Bunge sura 245. Ambapo kabla ya hapo Chuo hicho kiliitwa Taasisi ya MANTEP (Management Training for Educational Personnel) ambayo ilianzishwa mwaka 1978 na katika kipindi hicho Taasisi ya MANTEP ilijihusisha na utoaji wa Mafunzo ya Uongozi na usimamizi wa Elimu ya muda mfupi na muda mrefu kwa viongozi na watendaji wa sekta ya elimu. 

No description available. 

Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Wakala wa Maendeleo ya uongozi wa Elimu (ADEM) Dkt. Siston Masanja, akisalimiana na Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Halima Habib, katika viwanja vya ADEM.

No description available. 

Mkurugenzi wa Fedha, Mipango na Utawala wa ADEM, Dkt. Emanuel Molel, (kulia) akimkaribisha Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda, alipowasili katika viwanja vya ADEM.

No description available. 

Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Wakala wa Maendeleo ya uongozi wa Elimu (ADEM) Dkt. Siston Masanja, akisalimiana Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda, alipowasili katika viwanja vya ADEM.

No description available.

  No description available. 

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda, akiangalia machaapisho yanayo onesha kazi za ADEM mara baada ya kuwasili katika viwanja vya ADEM, wa kwanza kulia ni Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Wakala wa Maendeleo ya uongozi wa Elimu (ADEM) Dkt. Siston Masanja.

No description available. 

Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Halima Habib, akizungumza katika Ukumbi wa Chuo cha ADEM Wakati Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia alipotembelea chuoni hapo jana February 17, 2023.

No description available. 

Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Wakala wa Maendeleo ya uongozi wa Elimu (ADEM) Dkt. Siston Masanja, akizungumza katika Ukumbi wa Chuo hicho Wakati Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia alipotembelea chuoni hapo jana February 17, 2023.

No description available. 

No description available.

Viongozi wa Elimu Mkoa wa Pwani, Wilaya ya Bagamoyo, Watumishi wa Wakala wa Maendeleo ya uongozi wa Elimu (ADEM) na Kamati ya Ulinzi na Usalama kwa pamoja wakimsikiliza Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda, alipokuwa akizungumza wakati alipotembelea chuo cha ADEM Bagamoyo jana Februry 17, 2023.

No description available. 

Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Wakala wa Maendeleo ya uongozi wa Elimu (ADEM) Dkt. Siston Masanja, akimkabidhi Waziri wa Elimu, Taarifa ya utekelezaji wa Majukumu ya ADEM na machapisho mbalimbali yanayo onesha kazi za ADEM kwa ujumla.

No description available.

Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri- ADEM, Dkt. Naomi Katunzi (kulia) akimkabidhi zawadi ya T-shirt za ADEM, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda, (kushoto)

No description available. 

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda, (kulia) akijaribu zawadi ya T-shirt aliyopewa na uongozi wa ADEM, Kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Wakala wa Maendeleo ya uongozi wa Elimu (ADEM) Dkt. Siston Masanja.

No description available.

No description available.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda, (kulia) akimkabidhi zawadi ya T-shirt, Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Halima Habib, anaeshuhudia (katika) ni Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Wakala wa Maendeleo ya uongozi wa Elimu (ADEM) Dkt. Siston Masanja.

No description available. 

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda, (kulia) akimkabidhi zawadi ya T-shirt, Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Muharami Mkenge, (kushoto).

 

 

TAMASHA LA USIKU WA HABARI DODOMA LAWEKA HISTORIA TUZO MBALIMBALI ZATOLEWA ,WAZINDUA KIKOBA,NAIBU WAZIRI ,RC,WADAU WATIA NENO

 No description available.

NAIBU Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Mhandisi Kundo Mathew,akimkabidhi Tuzo ya Mwandishi Bora wa Mwaka Mkoa wa Dodoma Augusta Njoji kutoka Gazeti la Nipashe kwa taarifa aliyotoa imeonyesha Jitihada binafsi iliyotolewa na Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Dodoma wakati wa  tamasha la usiku wa Habari Dodoma lililoandaliwa na Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Dodoma (CPC) .

Wednesday, February 15, 2023

KAMATI YA UELIMISHAJI JAMII YATAMBULISHWA BAGAMOYO.

 No description available.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bagamoyo, Shauri Selenda, akizungumza wakati wa kuwatambulisha wajumbe wa Kamati ya Uhamasishaji, Ushirikishaji na Uelimishaji jamii, kuhusu magonjwa ya mlipuko uliofanyika leo Februari 15, 2023.  katika Ukumbi wa Chuo cha unesi Bagamoyo.

No description available. 

Afisa Mipango wa huduma za Afya ngazi ya Jamii kutoka Wizara ya afya, Bahati Mwailafu, akizungumza na washiriki wakati wa Mkutano wa kuwatambulisha wajumbe wa Kamati ya Uhamasishaji, Ushirikishaji na Uelimishaji jamii, kuhusu magonjwa ya mlipuko uliofanyika leo Februari 15, 2023. katika Ukumbi wa Chuo cha unesi Bagamoyo.

No description available.  

Washiriki wa Mkutano wa kuwatambulisha wajumbe wa Kamati ya Uhamasishaji, Ushirikishaji na Uelimishaji jamii, kuhusu magonjwa ya mlipuko uliofanyika leo Februari 15, 2023. katika Ukumbi wa Chuo cha unesi Bagamoyo.

No description available. 

Mratibu wa Elimu ya Afya kwa uma wilaya ya Bagamoyo, Jeni Mcharo, akizungumza na waandishi wa habari nje ya ukumbi mara baada ya kumalizika kwa   Mkutano wa kuwatambulisha wajumbe wa Kamati ya Uhamasishaji, Ushirikishaji na Uelimishaji jamii, kuhusu magonjwa ya mlipuko uliofanyika leo Februari 15, 2023. katika Ukumbi wa Chuo cha unesi Bagamoyo.

No description available. 

No description available. 

Washiriki wa Mkutano wa kuwatambulisha wajumbe wa Kamati ya Uhamasishaji, Ushirikishaji na Uelimishaji jamii, kuhusu magonjwa ya mlipuko uliofanyika leo Februari 15, 2023. katika Ukumbi wa Chuo cha unesi Bagamoyo. 

........................................................................

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bagamoyo, Shauri Selenda, amesema mafanikio ya utekelezaji wa Mipango na mikakati mbalimbali ya serikali inatokana na jamaii kuelewa, kuhamasika na kushirikishwa katika utekelezaji wa mikakati hiyo.

Mkurugenzi huyo wa Halmashauri ya Bagamoyo, ameyasema hayo wakati wa kufunga Mkutano wa kuwatambulisha wajumbe wa Kamati ya Uhamasishaji, Ushirikishaji na Uelimishaji jamii, kuhusu magonjwa ya mlipuko uliofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha unesi Bagamoyo.

Alisema jamii inahitaji kupata elimu juu ya jambo husika ili waweze kushiriki kikamilifu katka mambo mbalimbali yanayoandaliwa na serikali na kwa kutambua hilo serikali imeweza kuandaa namna ya kuwashirikisha, kuwaelimisha na kuwahamasisha kupitia kamati hiyo.

Ameitaka Kamati hiyo itakapopata elimu juu ya kile wanachotakiwa kwenda kukifanya wakafanye kwa utaalamu waa hali ya juu kwa kuwafikia makundi mbalimbaali katika jamii.

Aliwakumbusha kuwa, kazi yao kubwa ni kwenda akutoa elimu, kuhamasisha na kuwashirikisha kuhusu magonjwa ya mlipuko ili kila mmoja awe na uelewa ulio sahihi hali itakayosaidia kwa serikali kutotumia nguvu katika kuhamasisha chanjo zaa magonjwa ya mlipuko.

Kwa upande wake Afisa Mipango wa huduma za Afya ngazi ya Jamii kutoka Wizara ya afya, Bahati Mwailafu,  amesema kamati ya Uhamasishaji, Ushirikishaji na Uelimishaji jamii, imeundwa ili kukabiliana na magonjwa ya mlipuko ambapo wananchi wanapaswa kupata elimu sahihi kuhusu magonjwa hayo ili waweze kujilinda na kujitibu.

Alisema lengo la mkutano huo ni kutambulisha kamati ambayo itashiriki katika kutoa elimu, kuhamasisha, na kushirikisha jamii ili waweze kuelewa madhara ya magonjwa ya mlipuko.

Nae Mratibu wa Elimu ya Afya kwa uma wilaya ya Bagamoyo, Jeni Mcharo amesema wanatarajia kupata mafanikio katika Kamati hiyo iliyotambulishwa kwakuwa imeshirikisha makundi mbalimbali ya kijamii.

Alisema mara kadhaa serikali inapotaka jambo la kijamii liwafikie wananchi hutumia makundi mbalimbali ya kijamii ili kurahisisha ufikishaji wa taarifa kutokana na kamati husika kukubalika katika jamii kwani miongoni mwao wapo viongozi wa ngazi mbalimbali wakiwemo wa viongozi wa dini, serikali na asasi za kiraia.

Aliongeza kwa kusema kuwa, mafanikio katika kutoa elimu kuhusu magonjwa ya mlipuko ni jambo kwakuwa tutakuwa tumemsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambae amekuwa akihakikisha wananchi wake wanakuwa salama dhidi ya magonjwa mbalimbali.

Alisema Rais Samia ni mpenda maendeleo hivyo anapenda wananchi wake wawe na afya njema ili waweze kushiriki katika kujiletea maendeleo wenyewe na taifa kwa ujumla.

Aidha, amewashukuru Wizara ya Afya kitengo cha Elimu ya afya kwa uma kwa kuona umuhimu wa jambo hilo na kuchagua mkoa wa Pwani kuwa miongoni mwa mikoa inayostahili kupata kamati hiyo ili kuweza kupambana na magonjwa ya mlipuko.

Mkutano huo wa kutambulisha wajumbe wa Kamati ya Uhamasishaji, Ushirikishaji na Uelimishaji jamii, umeandaliwaa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI na Shirika la Afya duniani W.H.O.