Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bagamoyo, Shauri Selenda, akizungumza wakati wa kuwatambulisha wajumbe wa Kamati ya Uhamasishaji, Ushirikishaji na Uelimishaji jamii, kuhusu magonjwa ya mlipuko uliofanyika leo Februari 15, 2023. katika Ukumbi wa Chuo cha unesi Bagamoyo.
Afisa Mipango wa huduma za Afya ngazi ya Jamii kutoka Wizara ya afya, Bahati Mwailafu, akizungumza na washiriki wakati wa Mkutano wa kuwatambulisha wajumbe wa Kamati ya Uhamasishaji, Ushirikishaji na Uelimishaji jamii, kuhusu magonjwa ya mlipuko uliofanyika leo Februari 15, 2023. katika Ukumbi wa Chuo cha unesi Bagamoyo.
Washiriki wa Mkutano wa kuwatambulisha wajumbe wa Kamati ya Uhamasishaji, Ushirikishaji na Uelimishaji jamii, kuhusu magonjwa ya mlipuko uliofanyika leo Februari 15, 2023. katika Ukumbi wa Chuo cha unesi Bagamoyo.
Mratibu wa Elimu ya Afya kwa uma wilaya ya Bagamoyo, Jeni Mcharo, akizungumza na waandishi wa habari nje ya ukumbi mara baada ya kumalizika kwa Mkutano wa kuwatambulisha wajumbe wa Kamati ya Uhamasishaji, Ushirikishaji na Uelimishaji jamii, kuhusu magonjwa ya mlipuko uliofanyika leo Februari 15, 2023. katika Ukumbi wa Chuo cha unesi Bagamoyo.
Washiriki wa Mkutano wa kuwatambulisha wajumbe wa Kamati ya Uhamasishaji, Ushirikishaji na Uelimishaji jamii, kuhusu magonjwa ya mlipuko uliofanyika leo Februari 15, 2023. katika Ukumbi wa Chuo cha unesi Bagamoyo.
........................................................................
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bagamoyo, Shauri Selenda, amesema mafanikio ya utekelezaji wa Mipango na mikakati mbalimbali ya serikali inatokana na jamaii kuelewa, kuhamasika na kushirikishwa katika utekelezaji wa mikakati hiyo.
Mkurugenzi huyo wa Halmashauri ya Bagamoyo, ameyasema hayo wakati wa kufunga Mkutano wa kuwatambulisha wajumbe wa Kamati ya Uhamasishaji, Ushirikishaji na Uelimishaji jamii, kuhusu magonjwa ya mlipuko uliofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha unesi Bagamoyo.
Alisema jamii inahitaji kupata elimu juu ya jambo husika ili waweze kushiriki kikamilifu katka mambo mbalimbali yanayoandaliwa na serikali na kwa kutambua hilo serikali imeweza kuandaa namna ya kuwashirikisha, kuwaelimisha na kuwahamasisha kupitia kamati hiyo.
Ameitaka Kamati hiyo itakapopata elimu juu ya kile wanachotakiwa kwenda kukifanya wakafanye kwa utaalamu waa hali ya juu kwa kuwafikia makundi mbalimbaali katika jamii.
Aliwakumbusha kuwa, kazi yao kubwa ni kwenda akutoa elimu, kuhamasisha na kuwashirikisha kuhusu magonjwa ya mlipuko ili kila mmoja awe na uelewa ulio sahihi hali itakayosaidia kwa serikali kutotumia nguvu katika kuhamasisha chanjo zaa magonjwa ya mlipuko.
Kwa upande wake Afisa Mipango wa huduma za Afya ngazi ya Jamii kutoka Wizara ya afya, Bahati Mwailafu, amesema kamati ya Uhamasishaji, Ushirikishaji na Uelimishaji jamii, imeundwa ili kukabiliana na magonjwa ya mlipuko ambapo wananchi wanapaswa kupata elimu sahihi kuhusu magonjwa hayo ili waweze kujilinda na kujitibu.
Alisema lengo la mkutano huo ni kutambulisha kamati ambayo itashiriki katika kutoa elimu, kuhamasisha, na kushirikisha jamii ili waweze kuelewa madhara ya magonjwa ya mlipuko.
Nae Mratibu wa Elimu ya Afya kwa uma wilaya ya Bagamoyo, Jeni Mcharo amesema wanatarajia kupata mafanikio katika Kamati hiyo iliyotambulishwa kwakuwa imeshirikisha makundi mbalimbali ya kijamii.
Alisema mara kadhaa serikali inapotaka jambo la kijamii liwafikie wananchi hutumia makundi mbalimbali ya kijamii ili kurahisisha ufikishaji wa taarifa kutokana na kamati husika kukubalika katika jamii kwani miongoni mwao wapo viongozi wa ngazi mbalimbali wakiwemo wa viongozi wa dini, serikali na asasi za kiraia.
Aliongeza kwa kusema kuwa, mafanikio katika kutoa elimu kuhusu magonjwa ya mlipuko ni jambo kwakuwa tutakuwa tumemsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambae amekuwa akihakikisha wananchi wake wanakuwa salama dhidi ya magonjwa mbalimbali.
Alisema Rais Samia ni mpenda maendeleo hivyo anapenda wananchi wake wawe na afya njema ili waweze kushiriki katika kujiletea maendeleo wenyewe na taifa kwa ujumla.
Aidha, amewashukuru Wizara ya Afya kitengo cha Elimu ya afya kwa uma kwa kuona umuhimu wa jambo hilo na kuchagua mkoa wa Pwani kuwa miongoni mwa mikoa inayostahili kupata kamati hiyo ili kuweza kupambana na magonjwa ya mlipuko.
Mkutano huo
wa kutambulisha wajumbe wa Kamati ya Uhamasishaji, Ushirikishaji na Uelimishaji
jamii, umeandaliwaa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais
TAMISEMI na Shirika la Afya duniani W.H.O.
No comments:
Post a Comment