Thursday, October 21, 2021

RAIS SAMIA MGENI RASMI UWT PWANI.

 No description available.

Na Mwamvua Mwinyi, PWANI

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika, mkutano wa kilele Cha wiki ya UWT Taifa na kumuenzi muasisi na mwanamke Shupavu Bibi Titi Mohammed oktoba 23 mwaka huu, huko Ikwiriri Rufiji, viwanja vya Ujamaa.

 

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Pwani, Mwenyekiti wa UWT Taifa ,Gaudensia Kabaka amesema ,pia wanatarajia kutembelea wagonjwa na  kutoa vitu mbalimbali katika vituo vya afya na wanafunzi wa shule ya wasichana Ikwiriri.

 

“Tumeona Mgeni rasmi awe Mwenyekiti wetu wa CCM Taifa ,mwana UWT mwenzetu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani,”Tumeamua kuadhimisha kilele hicho Rufiji kwa sababu ya historia ya mama na mwanamke shupavu aliyemsaidia Baba wa Taifa Mwl.Nyerere kupigania Uhuru Bibi Titi Mohammed.

 

“Wiki ya UWT ilivyoanza ilianzishwa na chama Cha TANU ilikuwa sehemu ya wanawake wa TANU na Mwl.Nyerere alikuwa akisaidiwa na Bibi Titi, ambae alikuwa mhamasishaji mzuri ,muasisi na alikuwa Shupavu “

 

“Mwaka 1977 chama Cha TANU na ASP, umoja ikaanzishwa UWT na mwenyekiti wake akaendelea kuwa Bibi Titi.”

Akielezea wiki hiyo,Kabaka alifafanua maadhimisho hayo yameanza Tarehe 27 septemba hadi Tarehe 04 oktoba kwa kujitangaza na kufanya shughuli mbalimbali ,ambapo kauli mbiu Ni “TUNAHUSISHA KUMKOMBOA MWANAMKE KIUCHUMI ,KIFIKRA NA KISIASA.

 

Alisema mwanamke anapaswa kujikomboa kiuchumi kwa kujishughulisha kusaidiana na baba sambamba na wazazi watambue kuwasomesha watoto wote bila kuwabagua.

 

Hata hivyo Kabaka, aliomba wanawake wajitokeze Rufiji kuadhimisha shughuli hiyo na kumuenzi Bibi Titi Mohammed na kuungana na Rais Samia ambae atakuwa mgeni rasmi.

 

Kuhusu Rais Samia Sina haja ya kueleza ushupavu wake maana ameweza pia kutupatia trilioni 1.3 kwa ajili ya masuala mbalimbali ya kupambana na ugonjwa wa Uviko19 pamoja na ujenzi wa madarasa na vituo vya afya.

 

Nae Mkuu wa mkoa wa Pwani, Abubakari Kunenge alisema licha kuhakikisha sherehe hizo zinafanyika Pwani lakini kumuenzi Bibi Titi Mohammed kwa ukombozi wake.

Alisema hii itasaidia kuutangaza mkoa , kujua historia na kuutangaza kiutalii.

 

Kunenge alieleza, ni dhahiri Rais  Samia anapita katika nyayo za Bibi Titi kwa kuwa Shupavu ambapo katika mkoa wa Pwani ipo miradi ya maji iliyopatiwa fedha kupitia DAWASA ,mradi mkubwa wa bwawa la umeme Stigo-Rufiji tilioni 2.8 zimeshalipwa ,mradi wa Daraja jipya WAMI bilioni 72,Mradi wa reli ya kisasa (SGR) unaogharimu bilioni 37 hivyo wanaPwani wana kila sababu ya kumpenda Rais Samia kwa miradi mikubwa na ya kati inayoendelea .

No description available.

 

WAZIRI MKUU ATAKA MA-RC WASIMAMIE KWA KARIBU MIRADI INAYOANZA KUJENGWA KWA FEDHA ZA UVIKO


No description available.

No description available.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na wenyekiti wa kamati ya kitaifa ya uratibu wa utekelezaji wa mpango  wa maendeleo kwa ustawi wa taifa na mapambano dhudi ya UVIKO 19 akizungumza katika kikao cha kamati hiyo, ofisini kwa Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Oktoba 21, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

..............................................................

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Wakuu wa Mikoa yote nchini wanapaswa kusimamia kwa karibu fedha maalum ya sh. trilioni 1.3 zilitolewa na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) ili kuimarisha huduma za jamii.

“Kule mikoani kutakuwa na kamati maalum na Mkuu wa Mkoa ndiye atakuwa Mwenyekiti wake na Katibu Tawala atakuwa Katibu wao. Pia kutakuwa na mchumi, Mhandisi wa Mkoa, Afisa Manunuzi, Afisa Elimu, Mganga Mkuu wa mkoa, Mwanasheria, Mratibu wa Sekta na tumemuongeza Mhandisi wa TARURA kwani atahitajika japo hayumo kwenye sekretarieti ya mkoa,” amesema.

Waziri Mkuu ametoa wito huo leo (Alhamisi, Oktoba 21, 2021) ofisini kwake Mlimwa jijini Dodoma wakati alipokutana Mawaziri na Makatibu Wakuu ambao ni wajumbe wa Kamati ya Kitaifa inayosimamia miradi ya fedha za kuimarisha huduma za jamii.

Waziri Mkuu ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, amesema Kamati za Ulinzi za Mikoa (KUU) zitakuwa na jukumu la kusimamia kwa karibu utekelezaji wa miradi hiyo na kama kutakuwa suala rushwa wataingia na kuchukua hatua. “Katika kipindi cha miezi tisa, tunatakiwa tuwe tumekamilisha hii miradi,” amesisitiza.

Amesema timu hiyo ndiyo itawajibika kwenda maeneo ya vijijini kuona kama kazi inafanyika kwa viwango vinavyotakiwa kwani kuna baadhi ya miradi utekelezaji wake unapaswa uwe umekamilika ndani ya miezi mitatu.

“Mkoa utaamua ni mfumo gani utumike kusimamia utekelezaji miradi kwenye wilaya zake. Waheshimiwa Mawaziri lazima mwende kukagua miradi hii kulingana sekta zenu na mkifika mkoani ni lazima muambatane na Afisa mhusika kutoka mkoani,” amesema.

Amesema Makatibu Wakuu pia wanapaswa kwenda kuangalia utekelezaji wa miradi hiyo lakini kwa kupeana zamu na Mawaziri wao. “Hii ndiyo Kamati inayosimamia hizi fedha, kwa hiyo tunatakiwa tusimamie miradi yote ya kisekta ili ikamilike ndani ya miezi tisa kama ilivyopangwa. Mheshimiwa Rais ameshasema, sisi kazi yetu ni kuhakikisha kwamba inakamilika. Tusipokwenda hakuna ambaye atawajibika.”

Waziri Mkuu amesema watendaji wa vijiji na kata nao wana wajibu wa kusimamia miradi hiyo huko huko waliko na kusisitiza kuwa wahandisi wahakikishe viwango vya majengo vinaendana na fedha zilizotolewa. Amesema mafundi wanaoajiriwa wapewe mikataba ili wasikimbie kazi.

Kuhusu manunuzi ya vifaa vitakavyotumika kwenye miradi hiyo, Waziri Mkuu amewataka wahakikishe wanatumia ledger. “Manunuzi haya si ya kutoa fedha mfukoni yakaishia hapo. Ni lazima kuwe na ledger. Nimebaini kwenye miradi mingi, BOQ zinaandaliwa lakini kwenye manunuzi, bei inakuwa tofauti na miradi inakwama kukamilika.”

“Kwenye miradi hii, wakinunua vifaa kuwe na daftari la makabidhiano baina ya mnunuzi na Kamati ya Usimamizi. Vifaa vikishanunuliwa ni lazima vikabidhiwe kwa Kamati,” amesisitiza.

Kuhusu posho, Waziri Mkuu ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa amesema: “Hakuna mtu anayepaswa kudai posho katika hii kazi. Tukifanya hivyo, hii miradi haitakamilika. Hata sisi hapa kwenye Kamati hii, Mheshimiwa Rais hajatoa posho, sana sana ametuongezea majukumu,” amesisitiza.  

Mapema, akiwasilisha mchanganuo wa sh. trilioni 1.3 zilitolewa na IMF, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba alisema fedha hizo zimetolewa kulingana na sekta. Sekta hizo ni maji, afya, elimu, utalii, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na hifadhi ya jamii (social protection) ambako kuna TASAF, vijana, wanawake na watu wenye ulemavu.

“Sekta ya maji imepangiwa sh. bilioni 139.4, afya (sh. bilioni 466.9), elimu (sh. bilioni 367.6), utalii (sh. bilioni 90.2), Zanzibar (sh. bilioni 231), TASAF (sh. bilioni 5.5), vijana, wanawake na wenye ulemavu (sh. bilioni 5) na uratibu sh. bilioni 5,” alisema.

Wajumbe wanaounda Kamati hiyo ya Kitaifa ni Waziri wa Nchi, OWM – Sera Bunge na Wenye Ulemavu, Waziri wa Fedha, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Waziri wa Maji, Waziri wa Maliasili na Utalii, Waziri wa Viwanda na Biashara pamoja na Makatibu Wakuu wa wizara hizo.


TAKUKURU LINDI YAJA NA MBINU MPYA KUFUATILIA KERO ZA WANANCHI

 No description available. 

Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Lindi, Mhandis Abnery Mganga, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)

...................................................................

NA HADIJA OMARY- LINDI.

 

TAASISI ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Lindi imeanzisha mpango wa Takukuru inayotembea itakayowawezesha kufahamu na kufanyia kazi kero mbali mbali za wananchi.

 

Akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake na kutoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Taasisi hiyo, kwa kipindi cha julay hadi Septemba 2021, Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Lindi, Mhandis Abnery Mganga, amesema kuwa, kwa kutekeleza Mpango huo maafisa wa Takukuru huambatana na wakuu wa Idara za halmashauri ili kuweza kutatua kero za wananchi .

 

Alieleza kuwa katika Mpango huo wananchi wengi wamejitokeza na kulalamikia Matumizi mabaya ya Madaraka ya viongozi katika maeneo ya kata na vijiji ikiwemo kutopewa taarifa juu ya miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao pamoja na kutosomwa mapato na matumizi ya miradi inayosimamiwa na ngazi ya vijiji na kata.

 

 Aidha alitaja migogoro ya Aridhi isiyoisha, tozo Mbali mbali za Halmashauri, kuchelewa kupata malipo ya mazao yao baada ya kuuzwa na ubadhirifu wa viongozi ni miongoni mwa kero kubwa walizozigundua katika ufuatiliaji huo.

 

Hata hivyo Mganga ameeleza kuwa katika kipindi hiko jumala ya malalamiko shauri 81 yalipokelewa , kati ya hayo 48 yalihusu Rushwa na 33 hayakuhusu Rushwa ambapo alisema kuwa kati ya malalamiko hayo 48 yanayohusu rushwa yalifunguliwa majalada ya uchunguzi ambapo majarada 46 yanaendelea na majalada 2 yamekamilika huku taarifa 33 ambazo hazihusu Rushwa zikihamishiwa katika idara nyingine kwa hatua zaidi.

 

Mganga pia ameeleza namna Taasisi hiyo ilivyojipanga katika kuendelea na kufuatilia miradi mbali mbali ya kimkakati kwenye Mkoa huo katika robo ya pili ya mwaka wa fedha 2021/2022 ikiwemo ya ujenzi wa Barabara vijijini, ujenzi wa Madarasa, Zahanati pamoja na Ujenzi wa Miundombinu ya Maji tandangongoro .