Saturday, May 9, 2020

MAAFISA TARAFA SIMIYU WAKABIDHIWA PIKIPIKI UTEKELEZAJI AHADI YA RAIS MAGUFULI

 Baadhi ya pikipiki zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa Maafisa Tarafa nchini ambazo zimekabidhiwa rasmi na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini Mei 08, 2020 Mjini Bariadi kwa maafisa tarafa wa mkoa wa Simiyu.
.........................

Na Stella Kalinga, Simiyu RS

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini amewakabidhi pikipiki Maafisa Tarafa 15 wa Mkoa huo ambazo ni utekelezaji wa ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli aliyoitoa mwezi Mei 2019 wakati alipokutana na Maafisa tarafa wote nchini katika kikao kazi jijini Dar es Salaam.


Akiwakabidhi pikipiki hizo Mei 08, 2020 Mjini Bariadi Sagini amemshukuru Mhe. Rais kwa kutoa pikipiki hizo zitakazorahisisha utekelezaji wa majukumu ya Maafisa tarafa huku akiwaagiza kuzitunza na kuzitumia kwa malengo yaliyokusudiwa; ikiwa ni pamoja na kufuatilia mkakati wa elimu wa Mkoa wa kuwawezesha wanafunzi kusoma wakiwa katika likizo ya dharura ya tahadhari ya maambukizi ya Virusi vya Corona.


Tumeandaa mkakati  wa mkoa wa kuwawezesha wanafunzi kusoma kipindi ambacho wako likizo ikiwa ni tahadhari ya maambukizi ya Virusi vya Corona; moja ya majukumu yenu katika kipindi hiki ni kuhakikisha mkakati unatekelezwa kwenye maeneo yenu ya utawala; walimu, maafisa elimu watatimiza wajibu wao nanyi pia mna sehemu yenu,”alisema Sagini.


Aidha, Sagini amewataka maafisa tarafa hao kuzitumia pikipiki hizi kwa kuwafikia wananchi wote wakiwemo wakulima hasa kipindi hiki cha mavuno na lengo kuu likiwa ni kuwaasa kutunza chakula.


Awali akisoma taarifa katibu tawala msaidizi utawalana rasilimaliwatu katika Ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Ekwabi Mujungu amewataka maafisa tarafa hao kuzitumia pikipiki hizo kwa madhumuni yaliyokusudiwa ikiwa ni pamoja na kusukuma shughuli za maendeleo ya jamii ikiwemo  kusimamia miradi ya elimu ,afya kilimo na hifadhi ya mazingira.


Wakati huo huo Mujungu ametoa maelekezo kwa makatibu tawala wa wilaya mkoani Simiyu kutenga fedha kwa ajili ya mafuta na matengenezo ya pikipiki hizo kwa kila tarafa ili pikipiki hizo ziweze kudumu kwa muda mrefu.


Akiongea kwa niaba ya maafisa tarafa mara baada ya kukabidhiwa pikipiki hizo afisa tarafa ya Dutwa ,  Isabela Nyaulingo   amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuwawezesha kupata usafiri huo ambao utarahisisha utendaji kazi wao huku akiahidi kuwa watazitunza na kufuata maelekezo yote waliyopewa na viongozi.


Jumla ya pikipiki 15 zimekabidhiwa kwa maafisa tarafa mkoani hapa zikiwa na thamani ya shilingi milioni 33,285,000/=, ambapo  pikipiki moja inagharimu kiasi cha shilingi milioni 2,219,000.


Tarafa zilizonufaika mkoani  Simiyu ni Dutwa, Nkololo na Muhango(BARIADI), Kivukoni na Busega(BUSEGA), Itilima, Kanadi, Bumela na Kinang’weli (ITILIMA) Mwagala,Sengerema,na Nung’hu( MASWA), Kisesa Nyalanja na Kimali (MEATU).
 Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Utawala na Rasilimali watu katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa,Bw. Ekwabi Mujungu akiwasilisha taarifa ya pikipiki zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa Maafisa Tarafa ambazo zimekabidhiwa Mei 08, 2020 Mjini Bariadi na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini kwa maafisa tarafa wote wa mkoa wa Simiyu.
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini (mwenye suti nyeusi katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Simiyu na Maafisa Tarafa wa mkoa huo mara baada ya kuwakabidhi  maafisa tarafa pikipiki zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa Maafisa Tarafa nchini ambazo alizikabidhi  Mei 08, 2020 Mjini Bariadi kwa maafisa tarafa wote wa mkoa wa Simiyu.
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini (mwenye suti kulia) akizungumza na  Maafisa Tarafa wa mkoa huo kabla ya kuwakabidhi pikipiki zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa Maafisa Tarafa nchini ambazo zimekabidhiwa Mei 08, 2020 Mjini Bariadi na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini kwa maafisa tarafa wote wa mkoa wa Simiyu.

Monday, May 4, 2020

DKT. KAWAMBWA AKABIDHI NDOO ZA MAJI KWA MAKUNDI MBALIMBALI BAGAMOYO.


 Hizi ni baadhi ya ndoo za maji kwaajili ya kunawa mikono, pamoja na sabuni alivyokabidhi Mbunge wa Bagamoyo, Dkt. Shukuru Kawambwa jana Mei 3, 2020 ikiwa ni harakati za kupambana na ugonjwa wa Corona.

 Mbunge wa Bagamoyo, Dkt. Shukuru Kawambwa akizungumza na wananchi wakati wa kukabidhi ndoo za maji kwaajili ya kunawa mikono, pamoja na sabuni katika maeneo mbalimbali jimboni humo.
......................................... 


Na Selestian James.

Mbunge wa jimbo la Bagamoyo mkoani Pwani Dkt. Shukuru Jumanne Kawambwa, amegawa ndoo za maji kwaajili ya kunawa mikono, pamoja na sabuni katika maeneo mbalimbali ya kata ya Dunda, Nianjema na Magomeni ikiwa ni muendelezo wa mapambano dhidi ya maamukizi ya  ugonjwa wa Corona.

Ziara hiyo iliyopitia vijiwe mbalimbali vya pikipiki na maeneo ya masoko, Dkt. Kawambwa amewatahadharisha wafanyabiashara pamoja na watu wanaokuja katika maeneo hayo kupata mahitaji mbalimbali kuwa ugonjwa wa Corona ni hatari sana kwani unaenea kwa kasi mno hivyo hakuna budi kuchukua tahadhari na maradhi hayo.

Aidha, Dkt. Kawambwa amewataka waendesha pikipiki kuhakikisha abiria zao wananawa vizuri mikono yao kwa kutumia maji tiririka na sabuni hizo kabla ya kupanda kwenye usafiri huo, kwani kwa kufanya hivyo kwa kiasi kikubwa watajiepusha na maambukizi hayo.

"Vijana wangu waendesha pikipiki na wafanyabiahara hakikisheni mnachukua tahadhari kwa kiasi kikubwa kuhusu ugonjwa huu ili uweze kujikinga wewe binafsi na familia nyumbani" Alisema Dkt. Kawambwa.

"Tunaona namna ambavyo maambukizi hayo yanavyoendelea siku hadi siku kwa nini nawe usiunge mkono juhudi za muheshimiwa Rais Dkt. Maghufuli na viongozi mbalimbali za kuhakikisha tunabaki salama"? Alimalizia kwa kuhoji.

Alisema ameongea na wahisani waliowahi pia kusaidia katika operesheni ya macho bure ambao ni Bilal eye camp, nao kwa kuona umuhimu wa tahadhari ambapo wamekubali kutoa ndoo za maji na sabuni ili zitumike kunawa mikono.

Dkt. Kawambwa amewatahadharisha juu ya namna ya kukaa kwa nafasi kidogo kutoka mtu mmoja na mwingine ili kujikinga zaidi.

Kwa upande wao madiwani wa viti maalum, Shumina Rashidi na Hafsa Kilingo wamewataka wafanyabiashara hao wa kata hizo kushirikiana na serikali katika kuhakikisha wanashinda vita dhidi ya corona.

Aidha,  madiwani wa kata ya Nianjema Abdul Pyallah na Diwani wa kata Dunda Dickson Makamba wamemshukuru na kumpongeza Mbunge Dkt. Kawambwa, kwa kufanikisha zoezi hilo muhimu.

lakini pia wamewataka wafanyabiashara hao kutosahau umuhimu wa kuvaa barakoa  wakati wote katika shughuli zao za kila siku.

Kwa upande wao waliopokea misaada hiyo ya ndoo za maji na sabuni kwaajili ya kunawa mikoni wamemshukuru Mbunge huyo kwa juhudi zake za kuwajili wananchi wake hasa katika kipindi hiki cha ugonjwa wa homa ya mapafu unaosababishwa na virusi vya Corona.

Wamesema ndoo hizo zimepetaikana katika wakati muafaka ambapo matumizi yake ni muhimu sana katika jamii ili kujikinga na Corona.
 
Diwani wa kata Dunda Dickson Makamba, akinawa mikono mara baada ya kupokea ndoo za maji kutoka kwa Mbunge na yeye kukabidhi kwa wananchi wa kata yake hapo jana Mei 3, 2020.
 
Diwani wa kata ya Nianjema, Abdul Pyallah akikabidhi ndoo za maji kwa wananchi wake baada ya yeye kupokea kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Dkt. Shukuru Kawambwa, Mei 3, 2020.
 
Diwani wa viti maalum, Hafsa Kilingo, akinawa mikono mara baada ya kukabidhi ndoo za maji kwa wananchi.
 
Diwani wa viti maalum, Shumina Rashid, akinawa mikono mara baada ya kukabidhi ndoo za maji kwa wananchi.
Madereva wa Bodaboda wakinawa mikono kwa maji tiririka na sabuni mara baada ya kupokea msaada wa ndoo kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Dkt. Shukuru Kawambwa, Mei 3, 2020. Picha zote Na Selestian James. 

RAIS MHE.DKT.JOHN MAGUFULI AMEMTEUA BRIG.JEN.GABRIEL SAULI MHIDIZE KUWA MKURUGENZI MKUU MSD

BANDARI KAVU YA KWALA YAANZA KAZI.

Image may contain: sky and outdoor
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo, 2 Mei 2020 ameshiriki Mapokezi ya Treni ya Kwanza iliyoleta Makasha 20 kwenye Bandari Kavu ya Kwala iliyopo Ruvu Kibaha.


Akizungumza kwenye Hafla hiyo Mhe. Mhandisi Ndikilo amesema Mkoa wa Pwani umejipanga kikamilifu kutumia Fursa za Kiuchumi na Kijamii zinazotokana na Bandari hiyo.


Amebainisha kuwa Mkoa kupitia Halmshauri ya Wilaya Kibaha upo katika Mchakato wa kuupanga Mji wa Kwala kuwa Mamlaka ya Mji Mdogo ili kwenda sambamba na ukuaji wa Shughuli za Kiuchumi kwenye Eneo hilo.


Aidha ameongeza kuwa Mkoa umeanisha Ekari 4,000 ambazo zinazunguka Bandari kavu ya Kwala na Mji wa Kwala, Ekari hizo zitandaliwa Mpango wa Matumizi mbalimbali ikwemo Viwanda Vikubwa, Vidogo, Maghala, Maegesho ya Magari, Biashara kubwa na Ndogo, Makazi na Makazi Biashara, Matumizi mchanganyiko kama shule, Mahotel, Hospitali, Nyumba za Ibada, na shughuli nyingine za Kijamii.


Mhandisi Ndikilo ameeleza kuwa Mchakato wa kukamilisha matumizi hayo unasimamiwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi


Akitoa rai ya kuharakishwa kwa mchakato huo Ndikilo amesema"Shughuli za Bandari kavu zinaanza Lakini huduma hizi saidizi (Supportive Facilities) Hazijaanza".


Katika hatua nyingine Ndikilo amewakaribisha Wawekezaji wa viwanda kuja Kwala kuchangamkia Fursa zilizopo katika Eneo hilo. amesema eneo hilo lipo karibu na Bandari kavu Kwala, lipo karibu na SGR, lipo karibu na Reli ya TAZARA, lipo karibu na chanzo cha Maji DAWASA.

"Wananchi wa Pwani na Wawekezaji tutumie Fursa za Kiuchumi na Kijamii zinazotokana na Bandari hii"


Nae Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Atashasta Nditiye amesema ujenzi wa Mradi huo ni utekelezaji wa Maagizo ya Mhe. Rais ya kupunguza Msongamano kwenye Bandari ya Dar es Salaam.


Nditiye amewataka Bodi ya Bandari kusimamia kikamilifu na kuhakikisha Mradi huu unakamilika kwa asilimia 100 ifikapo Mwezi Juni 2020.


Pia amekubali Ombi la Mhe Mkuu wa Mkoa wa Pwani la kuwepo kwa Kituo cha Polisi kwenye eneo hilo ili kuimarisha Ulinzi na Usalama hivyo amewataka TPA kuhakisha kunajengwa Kituo hicho cha Polisi.
Image may contain: one or more people, people standing and outdoor