Thursday, December 19, 2019

RAIS DKT MGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI LA MSIKITI MKUU WA CHATO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Spika wa Bunge la Jamhuri Mhe Job Ndugai, Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma, Rais wa Taasisi ya Al-Hikma Foundation Sheikh Shariff Abdulqadir pamoja na viongozi wengine wa dini wa Mkoa wa Geita akifunua pazia kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Msikiti Mkuu wa wilaya ya Chato wa Al Huda mjini Chato jana Desemba 18, 2019. 

Msikiti huo utakaokuwa na uwezo wa kuchukua waumini 3000 kwa ndani na 6000 kwa nje kwa wakati mmoja, unajengwa kwa ufadhili wa Taasisi ya Al-Hikma Foundation kwa thamani ya Shilingi 1.6bn/-.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Taasisi ya Al-Hikma Foundation Sheikh Shariff Abdulqadir akiangalia mchoro wa utakaavyoonekana Msikiti Mkuu wa wilaya ya Chato wa Al Huda alipowasili kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa msikiti huo utaokuwa na uwezo wa kukaa waumini 3000 kwa ndani na 6000 kwa nje, ukiwa unajengwa kwa ufadhili wa Taasisi ya Al-Hikma Foundation kwa thamani ya Shilingi 1.6bn/-

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea kwenye hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Msikiti Mkuu wa wilaya ya Chato wa Al Huda mjini Chato. 

Msikiti huo utakaokuwa na uwezo wa kuchukua waumini 3000 kwa ndani na 6000 kwa nje kwa wakati mmoja, unajengwa kwa ufadhili wa Taasisi ya Al-Hikma Foundation kwa thamani ya Shilingi 1.6bn/-.
 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma akisalimia wananchi akiwa na Spika wa Bunge la Jamhuri Mhe Job Ndugai wa Taasisi
ya Al-Hikma Foundation Sheikh Shariff Abdulqadir pamoja na viongozi wengine wa dini na serikali wa Mkoa wa Geita kwenye hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Msikiti Mkuu wa wilaya ya Chato wa Al Huda mjini Chato. Msikiti huo utakaokuwa na uwezo wa kuchukua, waumini 3000 kwa ndani na 6000 kwa nje kwa wakati mmoja, unajengwa kwa ufadhili wa Taasisi ya Al-Hikma Foundation kwa thamani ya Shilingi 1.6bn/-.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Spika wa Bunge la Jamhuri Mhe Job Ndugai akisalimia wananchi akiwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma, Rais wa Taasisi ya Al-Hikma Foundation Sheikh Shariff Abdulqadir pamoja na viongozi wengine wa dini na serikali wa Mkoa wa Geita kwenye hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Msikiti Mkuu wa wilaya ya Chato wa Al Huda mjini Chato. 

Msikiti huo utakaokuwa na uwezo wa kuchukua waumini 3000 kwa ndani na 6000 kwa nje kwa wakati mmoja, unajengwa kwa ufadhili wa Taasisi ya Al-Hikma Foundation kwa thamani ya Shilingi 1.6bn/-.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Spika wa Bunge la Jamhuri Mhe Job Ndugai, Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma, Rais wa Taasisi ya Al-Hikma Foundation Sheikh Shariff Abdulqadir pamoja na viongozi wengine wa dini wa Mkoa wa Geita wakipata picha ya kumbukumbu baada ya hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Msikiti Mkuu wa wilaya ya Chato wa Al Huda mjini Chato. 


Msikiti huo utakaokuwa na uwezo wa kuchukua waumini 3000 kwa ndani na 6000 kwa nje kwa wakati mmoja, unajengwa kwa ufadhili wa Taasisi ya Al-Hikma Foundation kwa thamani ya Shilingi 1.6bn/-.

Wednesday, December 18, 2019

UVCCM LINDI YAMSIMAMISHA UONGOZI MWENYEKITI KWA KUGHUSHI UMRI.

NA HADIJA HASSAN 18/12/2019 LINDI

Kamati ya utekelezaji ya umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Lindi imemsimamisha nafasi ya uongozi Rashidi Ally Mbumulile aliyekuwa mwenyekiti wa umoja wa vijana Wilaya ya Nachingwea kwa tuhuma za kugushi umri wake.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Makao makuu ya Chama cha mapinduzi Mkoa wa Lindi Mwenyekiti wa umoja wa vijana UVCCM Majid Luponda jana alisema uamuzi huo umekuja baada ya kamati hiyo kujiridhisha juu ya suala la kughushi umri kwa mwenyekiti huyo kuwa mkubwa unaopata miaka 37.

Luponda alisema kwa mujibu wa kanuni ya umoja wa vijana toleo la mwaka 2017 linamtambua kijana ni Yule ambae amefikisha miaka 14 mpaka 35 “Kutokana na kanuni hii tunashauriwa katika kuchagua ama kugombea katika nafasi yoyote ya uongozi, tunatakiwa kumchagua kiongozi ambaye yuko chini ama miaka 30 ili anapofikia umri wa miaka 35 uwe ndio ukomo wa uongozi wake” alisema Luponda.

“Kwa kutumia kanuni hiyo hiyo inatuelekeza kuwa endapo mtu anapokuwa ametoa taarifa za uwongo hususani za kufoji umri na ikathibitika kuwa umri wake sio umri wa kuwa katika kundi la umoja wa vijana itapelekea kufukuzwa moja kwa moja kwa uongozi wake pamoja na kumuondoa katika kundi la vijana”

Luponda alisema kutokana na hali hiyo kamati ya utekelezaji ya umoja wa vijana ya UVCCM Mkoani humo inamsimamisha nafasi ya uongozi Mohamedi Mbumulile kwa muda usiojulikana mpaka pale vikao vingine vya kitaifa vitakapokaliwa ili kutoa maamuzi.

Pamoja na mambo mengine Luponda pia alitumia fursa hiyo kutangaza ratiba ya mafunzo ya ujasiriamali ambayo yanatarajiwa kufanyika katika Halmashauri zote za Mkoa wa Lindi.


Alisema mafunzo hayo yanatarajiwa kuanza tarehe 20/01/2020 hadi tarehe 31/01/2020 ambayo yataendeshwa na UVCCM kwa kushirikiana na TAEDO

Monday, December 16, 2019

ZIARA YA MAKATIBU WAKUU NGARA MPAKANI MWA TANZANIA NA BURUNDI YAIBUA CHANGAMOTO.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti (wa pili kutoka kulia) pamoja na wajumbe waliotembelea mpaka wakimsikiliza mtaalam kutoka Upimaji na Ramani akiwaeleza historia ya eneo la mafiga matatu (Tanzania, Ruanda na Burundi) katika bonde la Mto Kagera. Nyuma ya Mkuu wa Mkoa ni alama ya mpaka namba (BP 58), ambayo ndiyo alama ya mwisho ya mpaka kati ya Tanzania na Burundi kabla ya mto Kagera. Mpaka mwingine mbali na mto kagera ni mto Mwibu ambao unatoa maji nchi ya Burundi na kuungana na mto Kagera.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Bwana Nicholas Mkapa (aliyevaa miwani) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani Wizara ya Ardhi Bwana Hamdouny Mansour (wa kwanza kulia) kuhusu uwekaji wa alama za mpaka katika bonde la mto Kagera ambalo ni mpaka kati ya Tanzania na nchi za Ruanda na Burundi.  Eneo hilo lina historia ya kupakana nchi tatu (Tanzania, Ruanda na Burundi) na ndiyo maana panaitwa mafiga matatu. Kushoto ni Mthamini Mkuu wa Serikali Bibi Evelyn Mungashwa na Kulia ni Kamishna wa Ardhi Nchini Bibi Mary Makondo.

Mwenyekiti wa msafara uliotembelea mpaka Dkt. Florens Turuka, Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa akiwasili na kupokelewa na viongozi mbalimbali wa Wilaya katika Wilaya ya Bwiigwe Mkoani Kagera kwa ajili ya ukaguzi wa mpaka eneo la Mnanila/Manyovu.

Dkt. Florens Turuka, Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na mwenyekiti wa msafara akijadiliana na kushauriana na wajumbe wa msafara baada ya kuifikia alama ya mpaka (BP 20) iliyopo eneo la Mnanila/Manyovu kwenye mpaka wa kuingia na kutoka nchini Burundi. Eneo hili lina historia kwamba ndiyo chanzo cha mto Malagarasi ambao unatumika kama mpaka kati ya Tanzania na Burundi.

Na Eliafile Solla

Baadhi ya wananchi wanaoishi katika Kata na Vijiji vya mpakani mwa Tanzania na nchi ya Burundi, wamelalamikia sehemu ya ardhi yao kutumiwa kwa shughuli mbalimbali za kibinadamu na raia jirani wa Burundi. Hayo yalijitokeza katika ziara ya Makatibu Wakuu iliyofanyika katika Mikoa ya Kagera na Kigoma kwa lengo la kukagua maeneo yote ya mpaka wa Kimataifa.

Makatibu Wakuu kutoka Ofisi ya Rais- IKULU, TAMISEMI, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi pamoja na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali walifanya ziara Wilayani Ngara, Mkoa wa Kagera, kukagau zoezi la uimarishari wa mpaka uliofanyika mwaka 2014.

Ziara hiyo iliyojumuisha wataalam mbalimbali wanaoshughulikia mpaka wa kimataifa kati ya Tanzania na nchi zinazoizunguka, ilikuwa ya siku nne ambapo wajumbe walitembelea baadhi ya maeneo yaliyopitiwa na zoezi la uimarishaji mpaka lililofanyika mwaka 2014. Katika ziara hiyo pia, wataalam walitembelea maeneo ya mpaka katika Mkoa wa Kagera ambapo walibaini, baadhi ya raia wa Burundi wanafanya shughuli nyingi za kibinadamu katika maeneo ya mpaka kitu ambacho kiusalama siyo sawa.

Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Florens Turuka ambaye ndiye alikuwa mwenyekiti wa wajumbe hao alisema, lengo la kutembelea na kukagua maeneo ya mpaka wa kimataifa uliopitiwa na zoezi la uwekaji wa alama za hifadhi ya mpaka (vigingi) mwaka 2014 ni kukusanya taarifa kutoka kwa wananchi.  Alisisitiza kwamba, taarifa itakayotolewa na wananchi katika maeneo yaliyopitiwa na uimarishaji wa mpaka, itaisaidia Serikali kujua ni mikakati gani iwekwe katika maeneo yanayozunguka mpaka ili kuwalinda wananchi pamoja na mali zao.

Nae mkuu wa Wilaya ya Ngara Luteni Kanali Michael Mtenjele, alisema katika taarifa ya Wilaya kwamba, mpaka kati ya Tanzania na Burundi uko salama na Wilaya imeendelea kuwa na mahusiano na mawasiliano ya karibu na nchi hiyo. Aliongeza kwamba, mara nyingi zinapotokea changamoto mawasiliano ya simu hufanyika na nchi ya Burundi na kuyatatua kitu ambacho kisingewezekana kama mahusiano yangekuwa siyo mazuri.

Taarifa ya Wilaya pia ilibainisha kwamba, zoezi la uimarishaji mpaka lililofanyika mwaka 2014 liliwaathiri baadhi ya wananchi wa Tanzania waliokuwa wanaishi mpakani. Kanali Michael alisema, pamoja na athari ambazo tayari Wilaya ilishabainisha, wajumbe wanaweza kupata taarifa zaidi kuhusu hali ya mpaka kutoka kwa wananchi wanaoishi mpakani watakapokuwa wanatembelea na kukagua maeneo hayo.

Pamoja na wajumbe kutembelea na kukagua baadhi ya maeneo yaliyopitiwa na zoezi la uimarishaji mpaka la mwaka 2014, pia walifanya mikutano ya hadhara na wananchi wa vitongoji na vijiji husika ili kupata taarifa ya hali ya mpaka. Katika mikutano hiyo ya hadhara, baadhi ya wananchi walisema, zoezi la uimarishaji mpaka la mwaka 2014 liliwaathiri wao na mali.

Bibi Jesca Lameck mwenye umri kati ya miaka 75-80 ni mmoja kati ya wananchi waliosema zoezi la uimarishaji wa mpaka la mwaka 2014 lilimuathiri. Bibi Jesca alisema, katika zoezi hilo lililohusisha uwekaji wa alama (vigingi) katika hifadhi ya mpaka, alijikuta sehemu ya shamba lake la miti, kahawa, matunda na makaburi vikiangukia upande wa nchi ya Burundi.

Baada ya kutembelea na kufanya mikutano na wananchi waliopitiwa na zoezi la uimarishaji mpaka la mwaka 2014, mwenyekiti Dkt Florens Turuka, Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi alipokea taarifa kuhusu athari zilizotokana na zoezi hilo, pamoja na changamoto nyingine zinazohusu mpaka tofauti na za uwekaji alama za hifadhi ya mpaka.  Aliushukuru uongozi wa Wilaya ya Ngara kwa jinsi unavyosimamia mahusiano na nchi ya Burundi na kuahidi kuifikisha mbele zaidi taarifa aliyoipata kuhusu changamoto za mpaka wa Tanzania na Burundi.

Saturday, December 14, 2019

MFUMO WA "Online Registration System" WARAHISISHA URASIMISHAJI NA USAJILI WA MAJINA YA MAKAMPUNI NA BIASHARA BRELA


Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu Loy Mhando

Mapema mwaka huu Tanzania kupitia sekta ya viwanda ilibainisha kutenga ekari 127,859 kwa ajili ya viwanda katika mikoa mbalimbali hapa nchini.Aidha jitihada hizo zimepelekea jumla ya viwanda vipya zaidi ya 4,000 vimejengwa katika mikoa hiyo chini ya uongozi wa sarikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli.

Kwa mujibu wa viongozi mbalimba akiwemo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na waziri wa viwanda Mh. Innocent Bashungwa ,serikali imejipanga kuweka mazingira sawa na mifumo ili kuboresha biashara na viwanda kwa kuweka mazingira rahisi na nafuu.

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) inayosimamia urasimishaji wa biashara na majina ya kampuni imeboresha mifumo ya utendaji wake na kurahisisha ili kuwawezesha wafanyabiashara kurasimisha jina la biashara, kusajili majina ya kampuni, alama za biashara na viwanda mahali popote walipo kupitia tovuti ya wakala

Aidha Waziri Mkuu anataja Viwanda vilivyojengwa kuwa ni vya kuzalisha bidhaa za ujenzi (Saruji, Nondo, Vigae, Mabomba, Marumaru, n.k); pamoja na viwanda vya kusindika mazao ya kilimo ikiwemo Nafaka, Matunda, Mafuta ya kupikia na bidhaa za Ngozi.
Mkakati wowote wa kukuza uchumi unawategemea sana wafanyabiashara, Tukiwa kwenye kilele cha miaka 20 tangu Wakala Wa Usajili wa Biashara na Leseni kuanzishwa ni mambo mengi tunajivunia ikiwa ni pamoja na kufanikiwa kupunguza kwa kiasi kikubwa urasimu na rushwa uliokithiri uliokuwa katika taasisi hiyo.

Heko na pongezi nyingi ziende kwa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) kwa kubuni mfumo Madhubuti wa urasimishaji kwa njia ya mtandao Online Registration System (ORS)

Tangu mfumo huo wa (ORS) kuanzishwa yapata mwaka mmoja na miezi kadhaa tu zaidi ya makampuni 7000 yamerasimisha Biashara na kusajili majina ya Biashara na Kampuni. katika mfumo huo hivyo kufanya shughuli za urasimishaji wa biashara na viwanda kwenda kwa haraka zaidi kupitia mfumo huo wa (ORS).

Tathmini iliyotolewa mwezi Juni mwaka huu imeonyesha kwa mwezi BRELA walikuwa wakirasimisha Biashara na kusajili majina ya Biashara na Kampuni. 60 tu lakini sasa kwa mwezi wanarasimisha Biashara na kusajili majina ya makampuni 750 mpaka 800 jambo ambalo linadhihirisha na kuonyesha mafanikio makubwa kwa muda mfupi sana.

Kwa zaidi ya asilimia 50 urasimu na michakato mirefu ya kupata vibali na leseni za biashara pamoja na uwekezaji umepungua kwa kiasi kikubwa.

Kujirasimisha kwa mtandao kunamuwezesha mfanyabiashara kutambulika na hivyo kuingia kwenye mfumo wa ushindani kwenye masoko mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Bodi Tisa Za Mazao Kuunganishwa Ili Kuunda Bodi Tatu Pekee


Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Mtwara
Serikali imedhamiria kuziunganisha Bodi sita za mazao zilizopo chini ya Wizara ya Kilimo na kuwa na Bodi tatu ili kuongeza ufanisi wa kiutendaji

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo jana tarehe 13 Disemba 2019 wakati akizungumza na viongozi wa vyama vya ushirika katika ukumbi wa Wilaya ya Tandahimba akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Mtwara.

Waziri Hasunga amesema kuwa kumekuwa na Bodi nyingi lakini matokeo ya kiutendaji hayaakisi wingi huo hivyo ili kuboresha majukumu yake na kuwa na weledi katika kazi Bodi hizo zitaunganishwa.

Amesema kuwa Bodi saba zitaunganishwa na kuunda Mamlaka moja ya kusimamia mazao ya kimkakati ambayo ni pamoja na Kahawa, Pamba, Mkonge, Tumbaku, Pareto, Korosho, Alizeti na zao la mchikichi.

Waziri Hasunga amesema kuwa mabadiliko hayo yatakayozihusisha Bodi hizo yatapelekea kuundwa kwa idara za kusimamia kila zao.

Bodi nyingine ya pili itasimamia mazao ya nafaka, mboga mboga na matunda (Cereal and Horticulture Authority) pamoja na Bodi ya Sukari itakayosalia kujitegemea.

Amesema, kuwa na Bodi nyingi kumepelekea usimamizi kuwa mgumu kadhalika kuwa na Bodi chache kutaimarisha ufanisi na uwezo wa kuwasimamia watendaji wake.

Sambamba na hayo Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) amesema kuwa Wizara ya Kilimo ipo katika mchakato wa kupitia upya sheria ya Ushirika pamoja na Shirika la ukaguzi wa vyama vya Ushirika-COASCO ili kuimarisha sheria na kuwa na usimamizi madhubuti wa mali za wananchi kwenye Ushirika.

Waziri Hasunga yupo mkoani Mtwara kwa ajili ya ziara ya kikazi ambapo awali alitembelea mkoa wa Pwani na Lindi kwa ajili ya kukagua hali ya uuzaji wa korosho msimu wa 2019/2020, kukagua hatua zilizofikiwa za malipo ya wakulima wa korosho zilizonunuliwa na serikali msimu wa mwaka 2018/2019 na kukagua skimu za umwagiliaji.

Laini Za Simu Zaidi Ya Milioni 19 Zimesajiliwa Hadi Desemba 10 - TCRA

Serikali imesema hadi sasa imefanikiwa kusajili laini milioni 19.681.086 kwa alama za vidole ambayo ni sawa na asilimia 42 zinazomilikiwa na watu mil 7.6 ikiwa zimebaki siku 18 ya zoezi hilo lifikie mwisho.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mhandisi James Kilaba alipokua wakielezea hali ya usajili wa laini za simu za mkononi kwa njia ya alama za vidole kuanzia Mei Mosi mwaka huu hadi Desemba 13 mwaka huu.

Amesema kuwa wananchi wanatakiwa kufuata taratibu za kuweza kupata  vitambulisho vya taifa ili kuweza kusajili laini za simu kwa kutumia alama za vidole.

Kilaba amesema kuwa watu waache kufuata taarifa  ambazo hawana uhakika nazo kwani kuamini taarifa zisizo sahihi ni kutaka kukwamisha zoezi hilo

Amesema pia idadi ya laini ambazo wamiliki wana namba za utambulisho za NIDA (NIN) lakini hawajasajili kwa njia ya alama za vidole ni milioni 5.599.610 ambazo zinamilikiwa na takribani watu milioni tatu.

“Laini za simu zisizosajiliwa kwa alama za vidole ni milioni 21.782 .906 ambazo zinamilikiwa na takribani watu milioni 10.5,” amesema.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dkt. Arnold Kihaule amesisitiza kasi ya uandikishaji NIDA kwani kuna manufaa mengi huku akisema idadi ya watu wasiopata vitambulisho au namba za NIDA na kwamba hawafanyi lolote zaidi ya milioni tatu.

Dkt.Kihaule amesema kuwa na wanamfumo wa kuangalia na kuweza kupata namba ya kitambulisho cha taifa kwa kuweka jina la kwanza na kuweka nyota  jina la  ukoo,nyota, Tarehe yakuzaliwa mwezi na mwaka kwa kuunganisha,nyota  jina la Mama,nyota jina la baba na kutuma kwa namba 15096.

Katika mfano IMA*ALI*25071985*AMINA*SAID na kutuma kwenda namba 15096  hivyo kila mtu alifanya usajili kwa kupiga picha hatua za mwisho.TV
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi James Kilaba akizungumza  na waandishi habari kuhusiana na hali ya usajili wa laini za simu kwa alama za vidole ikiwa zimebaki siku 18 kufungwa laini za simu ambazo hazijasajiliwa na kwa alama za vidole, jijini Dar es Salaam. 
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Dkt. Arnold Kihaule akizungumza  na waandishi wa habari kuhusiana na usajili wa vitambulisho vya Taifa ambao ndio wanatakiwa kusajili laini za simu kwa alama za vidole

KAMATI MAALUM KUTOKA OFISI SABA ZA SERIKALI YATEMBELEA NA KUKAGUA MPAKA WA KIMATAIFA KATI YA TANZANIA NA BURUNDI


Baadhi ya wajumbe wa kamati maalum ya kukagua mipaka ya kimataifa wakipokea taarifa ya kuhusu halisi ya mpaka wa Tanzania na Burundi.

Na: Eliafile Solla


Tanzania ni nchi ambayo iko vizuri na majirani zake kwa maana ya nchi zinazoizunguka na wananchi wake wanashirikiana vyema na majirani zao katika masuala mbalimbali ya kijamii na kimaendeleo kama vile biashara hasa ya kuuziana mazao.

 Haya yalithibitishwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Ngara mkoani Kagera Vedastus Tibaijuka wakati alipokuwa anatoa historia ya mpaka wa Tanzania na nchi jirani ya Burundi kwa kamati maalum iliyojumuisha ofisi saba za Serikali walipofika Wilayani humo kwa lengo la kutembelea na kukagua mpaka wa Kimataifa kati ya Tanzania na Burundi.

Katika kuimarisha mipaka ya kimataifa kati ya Tanzania na nchi jirani zinazo izunguka, Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imeunda kamati maalum kwa ajili ya kuhakikisha wananchi wote wanaoishi kwenye vijiji vya mipakani wanakuwa salama pamoja na mali zao.

 Kamati hiyo maalum inahusisha Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Ofisi ya Rais, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Ofisi ya Rais TAMISEMI. 

Nae mkuu wa Wilaya ya Ngara Lt. Kan. Michael Mtenjele aliieleza kamati hiyo maalum kwamba, Wilaya ya Ngara imegawanyika katika tarafa  4 zenye jumla ya kata 22, vijiji 75 na vitongoji 389. 

Alisisitiza kwamba, Wilaya ya Ngara iko mpakani kabisa mwa Tanzania na Burundi na hivyo siyo ajabu Watanzania kuwa na ndugu, jamaa na marafiki upande wa Burundi au Waburundi kuwa na jamaa Tanzania. Kwa sababu hiyo, wananchi hasa wa vijiji vya mpakani wanaishi vizuri na majirani zao na kushirikiana katika masuala mbalimbali.

Katika taarifa yake kuhusu hali halisi ya mpaka wa kimataifa kati ya Tanzania na Burundi alisema, mpaka huo uko salama na changamoto zinapojitokeza hukutana katika vikao vya ujirani mwema na kuzitatua japo kuna baadhi ya wananchi kutoka Burundi huingia na kuishi upande wa Tanzania bila kufuata sheria na taratibu za uhamiaji.

Mkuu huyo wa Wilaya aliieleza kamati maalum kwamba, kwenye uimarishaji wa mpaka huo uliofanyika mwaka 2014, baadhi ya wanachi wa vijiji vya mpakani walijikuta wakipoteza baadhi ya mali zao kama vile nyumba na mashamba baada ya maeneo hayo kuonekana yako upande wa Burundi na siyo Tanzania. 

Hiyo imekuwa ni changamoto kwa sababu wananchi hao tayari walishakuwa na familia zao katika maeneo hayo na wengine hadi makaburi ya jamaa zao yapo upande wa Burundi na wao wanaishi upande wa Tanzania.

Nae kiongozi wa msafara wa kamati hiyo maalum Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ndugu Ramadhan Kailima, aliipokea taarifa hiyo kuhusu hali halisi ya mpaka wa Tanzania na Burundi na kuahidi kwamba kwa pamoja kama kamati maalum watakaa na kuona ni jinsi gani wanaweza kuwasaidia wananchi walioathirika na uimarishaji mpaka uliofanyika mwaka 2014 kwa maana ya wale ambao baadhi ya maeneo yao yalibaki upande wa nchi jirani ya Burundi.


Saturday, December 7, 2019

WAFANYABIASHARA MBAGALA WAVUTIWA NA HUDUMA ZA TRA KUWAFUATA.

Na Shushu Joel

WANANCHI wa Mbagala jijini Dar es Salaam wamevutiwa na kitendo Cha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuwapelekea huduma ya utoaji Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) zoezi ambalo linaloendeshwa katika mkoa huo.

Wakizungumza mara baada ya kusajiliwa na kuwa walipakodi wafanyabiashara wa maeneo hayo wamekoshwa na huduma ya kufuatwa mahali walipo.

Monira Said ni mmoja wa wateja waliopatiwa huduma za TIN kwa mara ya kwanza alisema kuwa huduma wanazozitoa watu wa TRA ni zenye kiwango cha kipekee.

"Nimefurahia sana kukabidhiwa TIN yangu kwa mara ya kwanza tena bure huku nilikuwa nikijua labda huduma hii ni ya malipo kumbe hapana" Alisema.

Aliongeza kuwa kwa wale ambao hawajachangamkia nafasi hii ni bora wakajitokeza mapema hili waweze kupata huduma za TRA kwani mafanikio makubwa watayaona mara baada ya kuwa katika mfumo wa TRA.


Aidha, alitoa ushauri kwa maofisa wa TRA kuwa mbagala kwa sasa ni moja ya sehemu zinazokuwa kibiashara na moja ya maeneo yenye biashara kubwa hapa jijini Dar es Salaam kama kariakoo.

Naye Haji Khareed ni mwenyekiti wa wafanyabiashara wa nguo katika soko la mbagala alisema kuwa tangu vijana wengi walikuwa wakiwasubili Kwa hamu kubwa watu wa mamlaka ya mapato (TRA) ili wawaelimishe juu ya umuhimu wa kulipa kodi.

Aliongeza kuwa kufuatwa kwa wateja kwenye maeneo yao ya kazi kumewafanya kujiona ni watu wenye thamani sana katika nchi hii.

"Ukilipa kodi unasaidia nchi kutekeleza miradi mikubwa ya kimaendeleo hivyo kila mmoja wetu awajibike katika kulipa kodi na faida lazima aione "Alisema mwenyekiti Khareed.

Naye Afisa mwandamizi wa elimu kwa mlipa kodi Catherine Mwakilagala amewashukuru wafanyabiashara wa mbagala kwa kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kupata huduma toka TRA.

Hivyo amewataka kuendelea kujitokeza pindi wanaposikia watendaji wa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) wamekuja waweze kujitokeza kwa wingi ili kupatiwa huduma. Aidha amewapongeza wakazi wa mbagala kwa kumiminika kujitokeza kupata huduma za elimu.