Wednesday, November 13, 2019

TANI 1936 ZA KOROSHO ZAUZWA LINDI.

Na Hadija Hassan, Lindi.

Jumala ya tani 1936 za korosho Ghafi za chama kikuu cha ushirika cha Lindi Mwambao kinachojumuisha Wakulima wa Wilaya ya Lindi (Mtama) Kilwa na Manispaa ya Lindi Mkoani humo zimeuzwa katika Mnada wa kwanza wa chama hicho kwa bei ya juu ya shiringi 2701 na bei ya chini shiringi 2541.

Mnada huo umefanyika katika kata ya Chikonji Manispaa ya Lindi ambapo makampuni 14 yalijitokeza kuomba kununua zao hilo.

Akiwahutubia wananchi pamoja na wanunuzi wa Zao hilo Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi aliwataka wanunuzi kuzingatia Sheria na taratibu zilizowekwa wakati wa kununua zao hilo ikiwa ni pamoja na kulipa fedha kwa wakati.

Zambi, alisema kulingana na utaratibu wa ununuzi wa zao hilo mfanyabiashara anatakiwa kufanya malipo ndani ya siku nne baada ya mnada hivyo ni muhimu kwa wafanya biashara kuzingatia ili wakulima waweze kulipwa fedha zao kwa wakati.

Aidha, pamoja na mambo mengine alitoa msisitizo kwa viongozi wa vyama kufanya maandalizi ya miamala ya wakulima mapema na kuiwasilisha kwenye benk ili mfanya biashara atakapo fanya malipo kwa chama kikuu ziwafikie wakulima kwa haraka.

Nae mkuu wa Wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga aliwataka viongozi wa vyama vya Msingi kutojihusisha na udanganyifu wa aina yoyote unaohusiana na malipo ya Wakulima utakaosababisha upotevu wa fedha kwa wakulima.

Awali akiyataja makampuni yaliyoshinda kununua korosho hizo Mrajisi Msaidizi wa vyama vya ushirika Mkoa wa Lindi, Robert Nsunza alisema kuwa miongoni mwa makampuni yaliyoshinda ni pamoja na Alphonsa company limited kg 100,000 kwa bei ya shiringi 2701, MGM kg 400,000 kwa bei ya shiringi 27000 na kg 200,000 kwa bei ya 2690, Madag kg 51,068 kwa shiringi 2653 katika Ghara la Buco,

Alphonsa kg 100,000 kwa shiringi 2701, MGM kg 400,000 kwa shiringi 2690 na Malangi kg 1003,2846 kwa bei ya 2653 katika ghara la Mtama huku ghara la nangurukuru likianza korosho zake kwa kampuni ya Day2got kg 110 kwa bei ya Shiringi 2267 na bulaya kg 89,795 kwa bei ya Shiringi 2541.

Tuesday, November 12, 2019

Mfumuko wa bei wa Taifa waongezeka kutoka asilimia 3.4 hadi asilimia 3.6


Na Mwandishi Wetu, MAELEZO,Dodoma
MFUMUKO wa bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unaoishia mwezi Oktoba 2019 umeongezeka hadi asilimia 3.6 kutoka asilimia 3.4 mwaka ulioishia mwezi Septemba 2019 ikiwa ni ongezeko la asilimia 0.2. 

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kutangaza takwimu za bei, Kaimu Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii na Sensa ya Watu, Bibi. Ruth Minja amesema kuwa ongezeko hilo limetokana na kasi ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Oktoba, 2019 imeongezeka ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Septemba 2019. 
Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 115.84 mwezi Oktoba, 2019 kutoka 111.83 mwezi Oktoba, 209 
“Ongezeko hili la mfumuko wa bei limetokana na ongezeko la bei za bidhaa za Vyakula na Vinywaji Baridi ambapo mfumuko wa bei kwa mwezi Oktoba, 2019 umeongezeka hadi asilimia 5.1 toka asilimia 4.0 mwezi Septemba, 2019.” Alisema Bibi. Ruth. 
Aidha amesema kuwa mfumuko wa bei kwa bidhaa na huduma zote ambazo hazijumuishi chakula na nishati kwa mwezi Oktoba, 2019 umepungua kidogo hadi asilimia 2.6 kutoka asilimia 2.6 kutoka asilimia 2.7 Septemba, 2019 
Fahirisi za Bei kati ya mwezi Septemba, 2019 na mwezi Oktoba, 2019 zimepungua kwa asilimia 0.1 ambapo badiliko ni sawa na badiliko lilivyokuwa kati ya mwezi Agosti, 2019 na mwezi Septemba 2019 
Alizitaja baadhi ya bidhaa zilizochangia kupungua kwa fahirishi kuwa ni pamoja na mafuta ya taa kwa asilimia 2.5, dieseli kwa asilimia 2.1, petrol kwa asilimia 4.0. vifaa kwa ajili ya uchakataji wa taarifa kama kompyuta kwa asilimia 5.1 na baadhi ya huduma binafsi. 
Tanzania kupitia Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ambayo ndiyo mamlaka ya kutangaza takwimu pamoja na nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki imekuwa na utaratibu wa kutangaza matokeo ya mfumuko wa bei kila mwezi ambapo ambapo mfumuko wa bei katika nchi hizo utangazwa.

Wanaharakati washauri vyama vya siasa kuacha kujitoa...wadai huko ni kusiginwa kwa demokrasia nchini



Mwanaharakati huru Mackdeo Shilinde akizungumza jijini Dar es Salaam leo kuhusu kuwaomba vyama vilivyojitoa katika mchakato wa uchaguzi kurudi kuendelea na uchaguzi huo


Baadhi ya Waandishi wa habari.
Mwandishi wetu, Dar es Salaam

WANAHARAKATI wamewaomba vyama vya upinzani kurudi katika ulingo wa uchaguzi mdogo wa serikali za mitaa wakisema kitendo chao cha kujitoa wanawakosesha haki wananchi kuchagua kiongozi wanayemtaka.

Hatua hiyo imekuja kufuatia vyama vikuu vya upinzani Tanzania kujitoa kwa madai ya wagombea wao kuondolewa na serikali pasipo na kuwa na sababu ya msingi.

Akizungumza na Bagamoyokwanza blog, Mwanaharakati wa Mambo ya kijamii, Mackdeo Shilinde, amesema vyama vya siasa vinapaswa kuwa mfano wa kuheshimu mamlaka lakini pia kuwapa haki viongozi wa chini yao ya kuendelea kuwani nafasi za uongozi.

Amesema sababu ambazo zimetajwa na vyama vya upinzani kuwa watu wao wameondolewa katika nafasi za kugombea kwa sababu nyepesi hazina mashiko kwa sababu tayari viongozi hao walishakata rufani zao na maamuzi juu ya hatma yao yalikuwa bado hayajatoka, kitendo cha kuwakataza ni kusigina siasa.

“Unajua vyama vya siasa vinatakiwa kuheshimu taratibu na sharia, kwa mujibu  wa kanuni za uchaguzi, wale wote ambao walionekana kuwa na dosari katika fomu zao walitakiwa kukata rufaa, na baadae wapewe hatma ya rufaa zao, na wagombea wengi walifanya hivyo lakini kabla ya rufaa hizo kusikilizwa vyama vimekimbilia kujitoa na kuhatarisha nafasi za watu kugombea huu ni unyama” alisema.



Amewashauri Viongozi wa vyama vya upinzani kurudi tena wakatafakari na wagombea wao, wakawashirikishe waseme je ni kweli wagombea wao hawataki kushiriki kwenye uchaguzi wa serikali za mtaa? lakini vilevile vyama vya upinzani wakafate taratibu wa katiba yao




Hata hivyo Mwanaharakati wa mambo ya kijamii kutoka taasisi isiyo ya kiserikali ya Alliance for Development (ADO), Ally Mwinyi amesema kuwa wagombea wa vyama vya upinzani wanaojiondoa kugombea katika uchaguzi wa serikali za mtaa wanadhoofisha afya ya demokrasia nchini na kuwanyima wananchi demokrasia ya kuchagua kiongozi wanaye mtaka.




"Jambo hili la kujitoa kwenye uchaguzi wa serikali za mtaa si jambo zuri kwa afya ya Demokrasia na ni kuwanyima wananchi demokrasia ndani ya demokrasia"




Mwinyi amesema kuwa demokrasia ni kuwa tayari kufata zile hatua zote za uchaguzi kwa sababu zisipofatwa ni kuharibu kanuni na taratibu zilizowekwa kwaajili ya afya ya Demokrasia.




Hata hivyo Mwinyi amesema kuwa kitendo cha baadhi ya vyama vya siasa kutoa tamko kabla  ya majibu ya rufaa zao hayajatoka hii si picha nzuri kwani vyama hivyo kwani vinasigina demokrasia.




"Sisi kama wanaharakati tunachopenda kutoa rai yetu kwa vyama viheshimu demokrasia, vionyeshe kuwa wao ndio wa kwanza wa kuonyesha afya ya demokrasia".




Mwinyi amesema kuwa watanzania wanahitaji watu kwaajili ya kuwatetea pamoja na kuwaongoza na hakuna njia nyingine isipokuwa ni kufanya uchaguzi kwa kufata taratiu zilizowekwa.


Friday, November 8, 2019

DIWANI WA TENGELEA AGAWA BAISKEL NA VIFAA VYA MICHEZO

Na Shushu Joel

DIWANI wa kata ya Tengelea, wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani Shabani Manda amegawa baiskeli 11 kwa makatibu tawi wa chama cha mapinduzi (CCM) kwenye kata hiyo kwa lengo la kuwasaidia ili wapate wepesi wa usafiri kwenye utekelezaji wa majukumu yao.

Akizungumza na viongozi wa chama hicho diwani Manda alisema kuwa viongozi wa chama wamekuwa wakipata changamoto kubwa ya kuwafikia wanachama kutokana na kukosekana kwa usafiri wa haraka hivyo baiskeli hizi zitasaidia sana.

"Baiskeli hizi naamini zitakuwa suluhisho la viongozi wa ccm kuhangaika kuwafikia wanachama wake na hivyo kazi zao zitakuwa nyepesi"Alisema.

Aliongeza kuwa kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa sidhani kama Kuna wapinzani watakao jitokeza kugombea maana utekelezaji wa ilani ya ccm umefanyika kwa 100%.

Pia diwani huyo amegawa vifaa vya michezo vya mpira wa miguu kwa timu 20 kutoka kila kitongoji.

Aidha aliongeza kuwa vifaa hivyo ni juhudi zake za kuwapenda wananchi wake kwa kuhakikisha wanapata mahitaji yao.

Kwa upande wake captain wa timu ya Bungizi fc Mpame Mpame amempongeza diwani huyo kwa kugawa vifaa vya michezo kwenye vitongoji vyote ili kuinua vipaji vya vijana katika kata yake.

Naye katibu wa ccm kata Tengelea Twahili Koki amempongeza diwani huyo kwa kutoa usafiri kwa viongozi wa matawi wote 11 na hivyo kupelekea kutokomeza kabisa adha ya usafiri kwa watendaji hao wa chama cha mapinduzi.

Hivyo aliongeza kuwa vifaa hivyo vitasomeka ni mali ya ccm na si diwani tena kutokana na jinsi diwani mwenyewe alivyoamua kwa viongozi hao.

Aidha amewataka makatibu tawi wote 11 waliopata baiskeli hizo kuzitunza ili kuhakikisha zinasaidia kazi za chama kama ilivyokusudiwa kufanyika.

WANA CCM MATULI WAMLILIA MAGUFULI

Na Omary Mngindo

WANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kijiji cha Diguzi Kata ya Matuli Morogoro vijijini mkoa wa Morogoro, wamemuomba Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa Dkt. John Magufuli kufuatilia kura za maoni kijijini hapo.

Wakizungumza na Waandishi wa Habari, Wakazi Maulid Lwambo, Ramadhani Makwangu, Amini Jonathani na Aisha Mohamed wamesikitishwa na hatua ya kukatwa kwa mgombea ambaye ameshinda kura za maoni Nassoro Ramadhani.

"Diwani Luca Lumomo anatusumbua sana, huyu ni jamii ya mfugaji, hivyo anataka kutumia nafasi yake kutaka kukiteka kijiji chetu kukifanya kiwe cha wafugaji, kwa kuwa yeye ni mfugaji hivyo anatumia nafasi hiyo kutaka Mwenyekiti wa kijiji chetu nae awe mfugaji," alisema Lwambo.

Amemuomba Rais John Magufulo ambaye ni Mwenyekiti wa chama hicho Taifa aangalie figisu hizo wanazofanyiwa kwani diwani wao amekuwa tatizo kubwa kwa maendeleo ya kiniji chao.

Nae Ramadhani anayetetea kiti hicho amesema kuwa anafanyiwa figisu hizo na uongozi wa CCM wilaya wakishinikizwa na diwani wao Lumomo ambaye anatumia nafasi yake ya udiwani kushinikiza ili mgombea wake Daud Ndukuye apite.

Amina alisema kuwa figisu hizo zinazofanyika kwa mgombea ambaye ni chaguo lao linatokana na shinikizo wanalompandikizia Ramadhani kwamba ameiingizia serikali hasara kutokana na kukataa kwa mradi wa mpango wa urasimishaji ardhi kijijini hapo.

Kwa upande wake Lumomo amekanusha kujihusisha na figisu zinazotajwa, huku akisena kuwa kulikuwa na ongezeko la wana-CCM siku moja kabla ya kufanyika kwa kura za maoni, hatua iliyomlazimu mgombea was nafasi hiyo kupinga.

Katibu Mwenezi wa chama hicho Mkoa wa Morogoro Anthony Mhando alisema kuwa taarifa hizo anazisikia juu juu tu lakini hazijamfikia rasmi katika ofisi yake

Thursday, November 7, 2019

WAANDISHI WAJIFUNZA HABARI ZA GESI ASILIA

NA HADIJA HASSAN, Dar es salaam.

SHIRIKA la Maendeleo ya Mafuta na Gesi Tanzania (ThPDC) limetoa mafunzo ya namna ya uandishi wa habari za gesi Asilia kwa Waandishi wa habari 20 wa Mikoa ya Lindi na Mtwara Mafunzo hayo ya siku moja yalianza na ziara ya kutembelea vituo viwili Vya kupokelea gesi kutoka Madimba Mkoani Mtwara na songosongo Wilayani kilwa, kituo cha Somanga Wilayani Kilwa Mkoani Lindi na Kinyerezi Jijini Dar es salaam ambapo wanahabari walipata fursa ya kufahamu shughuli mbali mbali zinazofanywa katika vituo hivyo.

Akizungumza na Bagamoyo kwanza blog Meneja Mawasiliano wa Shirika la Maendeleo ya Gesi na Mafuta TPDC Marie Mselemu alisema kuwa lengo kubwa la mafuzo hayo kwa wanahabri ni kuwajengea uwezo wanahabari ili waweze kuandika vizuri habari zinazohusu masuala ya Gesi asilia.

"Kwa kuwa tasnia ya Ges ni Tasnia mpya Shirika litaendelea kutoa mafunzo ya ujuzi na uweledi kwa Wanahabari kila tunapopata fursa ili muweze kuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kuielezea Sekta hii lakini pia kuelimisha Umma Kwa ukaribu na ufasaha zaidi" alisema Mselemu.

Kwa upande wake Jongo Sudy mwandishi wa habari wa kituo cha Clouds TV alisema kuwa pamoja na mambo mengine mafunzo hayo yamemsaidia kufahamu namna ambavyo gesi inasafirishwa kutoka kituo cha kuchimba gesi cha Songosongo Wilayani kilwa na Madimba Mkoani Mtwara kuelekea Somanga na kwenda kinyerezi.

"Kilichonifurahisha zaidi japo sio kitu cha kawaida Wakati tuko katika kituo cha Somanga tujiandae na safari ya kuelekea Dar es salaam ni pale ambapo kituo cha jirani cha Songas kilipo anza kutoa mlipuko na gesi kuvuja ndipo wanahabari tulipo taka kufahamu na kujifunza kwa vitendo zaidi Juu kile kinachoendelea " alieleza Sofia Nyarusi mwandishi wa habari wa gazeti la Uhuru.