Sunday, September 29, 2019

UTEKELEZAJI WA MIRADI KWA WANANCHI NGUZO YA CCM: KIKWETE.

 MBUNGE wa Jimbo la chalinze Ridhiwani Kikwete, akiwa katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo.

 Na Shushu Joel, Chalinze.

MBUNGE wa Jimbo la chalinze Ridhiwani Kikwete amempongeza Diwani wa kata ya Bwilingu na viongozi wa chama cha mapinduzi (CCM) katika kata hiyo, wilayani Bagamoyo mkoani Pwani kwa utekelezaji na usimamizi wa miradi ya maendeleo katika kata ya Bwilingu.


Akizungumza na viongozi hao wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi hiyo, Mh. Kikwete alisema kuwa kwa utekelezaji huu wa miradi ya Maendeleo kwa wananchi ni kielelezo cha ufanisi mzuri wa Serikali ya Chama Cha Mapinduzi hivyo anaamini kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi yapo maneno mengi ya kuwaambia wananchi.


Katika Ziara hiyo Mh. Mbunge amekagua na kujionea miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa maabara ya kisasa katika kituo cha afya cha Bwilingu inayoendelea kujengwa, ujenzi wa zahanati katika Kijiji cha mdaula na Matuli, Ujenzi wa Kituo cha Ushauri Nasaha Majengo, ujenzi wa madarasa mawili, ofisi na vyoo Matuli na Msolwa, ujenzi wa ofisi ya kijiji cha majengo na Miundo mbinu ya kukusanya taka katika Mamlaka ya Mji Mdogo wa Chalinze.


Katika Ziara hiyo Mh. Mbunge ameshauri kuombwa kwa mabadiliko ya matumizi ya fedha zilizopelekwa katika shule ya msingi Matuli kiasi cha milioni 50 kitakachopangwa kutumiwa kujenga madarasa 2 na vyoo shuleni hapo.


Katika kikao hicho Mh. Mbunge ameshauri kuandikwa kwa barua haraka ili fedha hizo zijenge miundo mbinu mingine inayohitajika shuleni.


Pia mbunge huyo amewahakikishia wananchi wa Kata ya Bwilingu kuwa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli imeendelea kutekeleza mahitaji ya wananchi kwa vitendo na kuwaondoa wasiwasi katika kufikia malengo na ndoto zao wananchi wa Kata hiyo.


"Wananchi wenzangu tuzidisheni maombi kwa Rais wetu Dkt Magufuli kwani Jimbo la chalinze amekuwa akilitendea haki kutokana na kila ninachomuomba anatupatia kwa wakati"Alisema hayo Mh.Mbunge wa Chalinze huku akiainisha huduma kama Maji, Afya, Mahitaji ya Wazee, Miundombinu n.k.


Naye Mwenyekiti wa CCM kata ya Bwilingu Mzee Msakamali amemwambia Mbunge kuwa chama kitaendelea kuwa kinara wa usimamizi katika shughuli zote za miradi inayoletwa na chama cha mapinduzi na kumuhakikishia Mh.Mbunge kuwa wamejipanga vizuri kwa ajili ya Uchaguzi huu wa Vitongoji na Vijiji.

Saturday, September 28, 2019

Madini ya Bati mbioni kuanza kuuzwa nje



Tanzania iko mbioni kuandika historia ya kuuza madini ya bati nje ya nchi, ikiwa ni kwa mara ya kwanza kwa nchi kufanya hivyo.

Habari hizo njema zimetangazwa mjini Geita na Waziri wa Nishati, Dotto Biteko wakati wa maonesho ya pili ya teknolojia na uwekezaji katika sekta ya madini yanayoendelea mjini hapa.

Biteko alisema baada ya juhudi kubwa zinazofanywa na serikali katika kuhakikisha nchi inanufaika na utajiri wa madini mbalimbali nchini yakiwemo dhahabu, tanzanite, almasi, shaba, rubi, graphite na mengine, madini ya bati nayo yako mbioni kuingia katika soko la kimataifa.

Alisema katika kuchochea uchumi wa viwanda, Wizara kupitia Tume ya Madini imekwishatoa leseni mbili za usafishaji madini, moja mkoani Dodoma na nyingine Geita, huku leseni nne zikiwa kwa ajili ya uyeyushaji wa madini ya shaba na bati.

Aidha, alisema changamoto kubwa ya usafirishaji wa madini ya bati nje ya nchi inaelekea kupatiwa ufumbuzi kwani Wizara kwa kushirikiana na Jumuiya ya Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu (ICGLR) zipo katika hatua za mwisho kuwezesha upatikanaji wa hati ya kusafirisha madini ya bati.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera aliyehudhuria maonesho ya madini mkoani Geita akiambatana na wachimbaji wadogo kutoka mkoani mwake, Michael Gaguti alisema amekuja kujifunza juu ya mafanikio ya Geita katika soko la dhahabu na pia kujifunza juu ya teknolojia za kisasa, huku akisema anaamini Kagera pia itanufaika kupitia maonesho hayo.

Serikali Yatoa Muda wa Wiki Moja kwa Kiwanda cha kutengeneza saruji cha Dangote kuwasilisha taarifa ya utendaji kazi TIC

NA.MWANDISHI WETU
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji Mhe. Angellah Kairuki ametoa muda wa wiki moja kwa Kiwanda cha kutengeneza saruji cha Dangote kuwasilisha taarifa ya utendaji ambazo kwa zaidi ya miaka miaka mitatu hawajaziwasilisha Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kama sheria na taratibu za nchi zinavyoelekeza.

Waziri Kairuki ambaye aliongozana na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula Katika ziara yake ya kutembelea, kukagua maeneo mbalimbali ya uwekezaji na kuongea na wawekezaji na wafanyabiashara wa Mkoa wa Lindi septemba 27,2019 ameuelekeza uongozi wa kiwanda hicho kuhakikisha kila baada ya miezi sita wanawasilisha taarifa za kiutendaji TIC.

Waziri Kairuki aliwaeleza masikitiko yake viongozi wa kiwanda hicho kwa kutowasilisha taarifa za utekelezaji wao ikiwemo zinazohusu historia ya mradi, mipango ya upanuzi, kodi wanazolipa, faida pamoja na changamoto wanazokabiliana nazo na ushauri wao.

"Nimesikitishwa sana na suala hili la kutopeleka taarifa zenu TIC ambapo inafahamika suala hilo ni la kisheria na lazima litekelezwe kwa wakati,hivyo kuanzia sasa nimewapa wiki moja mhakikishe taarifa hizo zinawasilishwa haraka,"alisisitiza Waziri Kairuki.

Aidha amewapongeza Dangote kwa uwekezaji huo mkubwa pamoja na kuanza ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme wao wenyewe megawati 25 ambao megawati 5 zitaingia kwenye gridi ya taifa.

Amewataka wawekeze na maeneo mengine siyo kwenye saruji tu na kuagiza TIC kupitia mikataba ya utendaji ya wawekezaji wote mahiri kuona ni wapi wanaweza kuwekeza zaidi.

Wakiwa Mkoani Lindi Waziri Kairuki na Mhe. Mabula walitembelea mgodi wa madini ya uno (graphite) uliopo katika Kijiji cha Matambalale Kusini Wilaya ya Ruangwamkoani Lindi na kuona shughuli za awali za mradi huo ambapo Meneja wa kampuni ya Lindi Jumbo inayochimba madini hayo Bw Paul Shauri amesema mgodi utajengwa kwa muda wa miezi tisa na wanatarajia kuwekeza zaidi ya dola za kimarekani milioni 30.

Akiongea mgodini hapo Dkt.Mabula ameziagiza Halmashairi zote vijiji vyenye maeneo ya uwekezaji kufanya zoezi la kuandaa mpango wa matumizi ya ardhi watenge maeneo ya uwekezaji wayahaulishe yawe mali ya kijiji ili mwekezaji akipatikana watimize masharti mengine tu.

"Hakuna sababu ya mwekezaji kuanza kuhangaika na mambo madogo kama hayo ambayo yanampotezea wakati ni lazima halmashauri zijipange ili kumwekea mwekezaji mazingira mazuri avutiwe kuwekeza"alisema Dkt.Mabula

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Hashim Mgandilwa akiwakaribisha Mawaziri hao amesema Serikali ione kuna sababu ya kuharakisha ujenzi wa miundombinu ikiwemo barabara za wilaya hiyo kwani kuna makampuni mengi makubwa yameonesha nia ya kuwekeza.

Amesema wilaya hiyo pia inakabiliwa na changamoto ya mipaka ya asili na kwamba suala hilo tayari linaendelea kutatuliwa kwa viongozi na watendaji kutoa elimu kwa wananchi.

Hali ya utekelezaji wa mapendekezo ya haki za binadamu (UPR) inarizisha: THRDC


Mratibu wa mtandao wa watetezi wa haki za binadamu THRDC Onesmo ole Ngurumo,akizungumza katika mkutano wa mapitio ya mapendekezo ya ripoti ya haki za binadamu kwa Nusu Muhula (UPR-mid term report )

Na Praygod Thadei, Selemani Beta
Asasi za kiraia zaidi ya 100 zimepitia taarifa ya awali ya utekelezaji wa mapendekezo ya haki za binadamu (UPR) kwa Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa katika kipindi cha nusu muhula.
Akizungumza wakati wa mapitio ya ripoti hiyo jana Jijini Dare salaam, Mratibu  wa Taifa wa mtandao wa watetezi wa haki za binadamu Nchini, THRDC Onesmo Ole-ngurumo alisema Mwaka 2016 Tanzania iliridhia mapendekezo 133 kati ya 227.
Alisema kikao hicho kimeangazia namna serikali imetekeleza mapendekezo hayo kabla ya ripoti ya utekelezaji kutumwa Geneva, Uswisi mwaka 2021
Alisema mataifa yote duniani yatawasilisha taarifa zao ifikapo mwaka 2021.
Aidha Mratibu huyo wa kitaifa amegusia changamoto iliyopo katika utekelezaji wa mapendekezo hayo ambayo Tanzania iliyaridhia kuwa ni pamoja na kutokutekelezwa kwa upatikanaji wa katiba mpya.
"Bado kuna miaka miwili ya kusimamia utekelezaji wa mapendekezo hayo kabla ya kufikia mwaka 2021, Tunaomba serikali izifanyie kazi.
"Kati ya mapendekezo yote 67% yamefanyiwa utekelezaji nusu, asilimia 7% utekelezaji wake umekamilika hususani maeneo ya haki za watoto, watu wenye ualbino na kupinga rushwa. 4% hayajatekelezwa mpaka sasa na 12% hayana taarifa kamili kwamba zimefanyiwa nini,"

Alisema tume imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha ripoti hii inakamilika na kuhakikisha mapendekezo hayo yanatekelezwa. Tumekuwa karibu na AZAKI katika mchakato mzima na kufanya mikutano kuhakikisha kuwa tuna taarifa nzuri, na taarifa zote zinazopelekwa



Waziri Jafo Atoa Onyo.....Awataka Wakurugenzi Wawe Makini na Wasimamie matumizi sahihi ya fedha za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

 

Na. Angela Msimbira OR -TAMISEMI
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuhakikisha wanasimamia kwa weledi fedha zilizotengwa kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Ameyasema hayo jana wakati akifungua semina ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakurugenzi  wa Halmashauri na Wasimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa  iliyofanyika katika Ukumbi  wa Auditoriumn, Chuo Kikuu cha Dodoma, Jijini Dodoma.

Mhe. Jafo amesema kuwa hatasita kuwachukulia hatua Wakurugenzi ambao wataenda kinyume na utaratibu wa matumizi ya fedha zilizotengwa kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa kuwa kukuika miongozo iliyotolewa na Serikali katika matumizi sahihi ya fedha hizo.

Mhe. Jafo ameonya matumizi yasiyofaa kwa fedha zilizotengwa kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa na kusisitiza kuwa fedha hizo ni za moto, hivyo matumizi yake yanahitaji kufuata miongozo na taratibu zilizowekwa na Serikali.

Ameendelea kusema kuwa ni marufuku kwa Mkurugenzi kutumia fedha za uchaguzi kinyume na agenda ya uchaguzi na kusisitiza haja ya fedha hizo kutumika kwa wakati.

“Naomba niwape tahadhari, katika matumizi ya fedha ya uchaguzi, fedha hizi za uchaguzi zinazokuja ni kwa ajili ya uchaguzi, naomba mtu asidanganyike wala kurubunika kwa lolote katika mchakato huu wa uchaguzi, katika fedha za moto hizi fedha za moto” Amesisitiza Mhe. Jafo

Mhe. Jafo amesema kuwa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa inasimamia kwa karibu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa hivyo ni matumaini kuwa matumizi ya fedha za uchaguzi zitaenda kama ilivyokusudiwa kwa kufuata miongozo ya matumzi ya fedha hizo.

Amesema kuwa Wakurugenzi wote wa Halmashauri nchini  ndio wenye dhamana ya kusimamia matumizi sahihi ya fedha zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, kinyume na hapo anapaswa kujibu hoja zitakazojitokeza za kushindwa kusimamia fedha hizo vizuri.

Kuhusu wasimamizi wa uchaguzi, Mhe. Jafo amewasihi kutekeleza makujukumu yao kwa weledi na kuhakikisha ratiba ya uchanguzi inafuatwa huku akiwataka kutambua kuwa wasimamizi wamebeba dhamana kubwa katika kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa kuzingatia Demokrasia.

“ Natamani sana mlioteuliwa kuwa wasimamizi wa uchaguzi mwende vizuri mpaka mmalize vizuri kwa mujibu wa kanuni zetu. Mheshimiwa Rais anatamani nchi yake ikatekeleze demokrasia vizuri na ndio maana mnaona ameweza kuwezesha kila eneo kwa lengo kuwa uchaguzi uende ukafanyike vizuri”. Amesema Mhe. Jafo

Amesema Uchaguzi wa Serikali za Mitaa nchini ni muhimu kwa kuwa maisha ya watu yanaanzia katika vitongoji, mitaa na vijiji vyenu, mustakabali wa kuchakata maendeleo lazima uanze katika ngazi husika ambayo uchaguzi huu unaenda kuwapata viongozi na  hawawezi  kupatikana kama wasimamizi wa uchaguzi mtashindwa kufanya kazi yenu vizuri.

Wakati Huohuo, Mhe Jafo amewataka Makatibu Tawala wa Mikoa ambao ndio waratibu wakuu wa uchaguzi kuhakikisha wanafuatilia kwa karibu kila tukio na kuwataka wasikubali kuharibiwa kazi.

 “Makatibu Tawala wa Mikoa wao ni waratibu wakuu wa Uchaguzi katika Halmashauri zao kipindi hiki mna kazi kubwa sana ya kuhakikkisha huko chini mambo yanaenda vizuri na wala msikubali hata kidogo mtu awaahiribie kazi”. Amesisitiza Mhe. Jafo

Awali, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhandisi Joseph Nyamhanga, ameeleza kuwa kikao hicho kinalenga kukumbushana majukumu ya uchaguzi huo na kuna matukio mbalimbali yaliyopo katika tangazo la uchaguzi yanayopaswa kutekelezwa.

Mhandisi Nyamhanga amesema OR-TAMISEMI imeshakamilisha maandalizi yote muhimu ya uchaguzi huo na nyaraka mbalimbali zimeandaliwa na kusambazwa ikiwemo kanuni na muongozo wa uchaguzi huo.

Amesema tayari  imeratibu upatikanaji wa fedha na tayari zimeshatumwa kwenye Sekretarieti za Mikoa yote na anaamini zimeshatumwa kwenye Halmashauri kwa ajili ya maandalizi.

Aidha, Nyamhanga alisema katika uchaguzi wa mwaka huu inakadiriwa kuwa na vituo vya kupigia kura 110,000.

RAMAPHOSA AMTEUA ALIYEKUWA GAVANA WA BENKI KUU TANZANIA PROF. BENNO NDULU KUWA MSHAURI WAKE WA MASUALA YA KIUCHUMI



Rais Cyril Ramaphosa  wa Afrika Kusini amemteua Prof. Benno Ndulu kuwa miongoni mwa watu 18 wanaounda Baraza la kumshauri Rais huyo katika masuala ya uchumi litakaloanza kufanya kazi kuanzia Oktoba 01, 2019.



Baraza hilo lililotangazwa jana na Rais Ramaphosa litakuwa na kazi kubwa ya kuhakikisha uhusiano mzuri na uthabiti katika utekelezaji wa sera ya uchumi na kuhakikisha kuwa Serikali inaweza kujibu mabadiliko ya hali ya uchumi

Baraza linajumuisha viongozi wa ndani na nje ya Afrika Kusini watakaotoa mawazo ya kiuchumi, wakimshauri Rais na Serikali kwa upana zaidi, kuwezesha maendeleo na utekelezaji wa sera za uchumi zinazochochea ukuaji wa umoja

Pamoja na Prof. Benno Ndulu, wengine ni Prof. Mzukisi Qobo, Prof. Dani Rodrik, Prof. Mariana Mazzucato, Mamello Matikinca-Ngwenya, Dkt. Renosi Mokate, Dkt. Kenneth Creamer, Prof. Alan Hirsch, Prof. Tania Ajam, Dkt. Grové Steyn, Wandile Sihlobo, Dkt. Liberty Mncube, Prof. Fiona Tregenna, Prof. Haroon Bhorat, Ayabonga Cawe, Prof. Vusi Gumede, Dkt. Thabi Leoka na Prof. Imraan Valodia


Prof. Benno   Ndulu alikuwa Gavana wa Benki Kuu Tanzania tangu 2008 hadi 2018 baada ya Rais John Magufuli kumteua Profesa Florens Luoga kushika nafasi hiyo.

ASASI ZA KIRAIA ZAJA NA ILANI YA UCHAGUZI


Ilani ya Uchaguzi ya Wanawake ya Uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu wa Tanzania mwaka 2020 imezinduliwa rasmi leo Septemba 27,2019 wakati wa kufunga Tamasha la 14 la Jinsia 2019 katika viwanja vya TGNP Mtandao Mabibo Jijini Dar es salaam.

Ilani hiyo inayojumuisha sauti za wanawake kutoka sauti za wanawake kutoka makundi mbalimbali chini ya Uongozi wa TGNP Mtandao kwa kushirikiana na Taasisi ya Women Fund Tanzania na Mtandao wa Wanawake na Katiba,Uchaguzi na Uongozi imezinduliwa na Mwenyekiti wa TGNP Mtandao Asseny Muro.

Awali akizungumza,Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanawake na Katiba,Ruth Meena alisema ilani hiyo imebeba masuala muhimu yanayohusu wanawake kwenye uchaguzi.

"Ilani hii imebeba ajenda ya mwanamke,turufu ya ushindi 2019/2020 imewalenga wanawake,serikali,vyama vya siasa,wagombea nafasi za uongozi,vyombo vya habari na wapiga kura",alisema Muro.

Alisema ilani hiyo inaendeleza madai ya wanawake watetezi wa haki za ushiriki katika uongozi wa kisiasa tangu taifa lipate uhuru mpaka leo.

"Hii ni ilani ya tano iliyobeba madai ya wanawake tukiwa wadau na washiriki wakuu katika michakato mbalimbali ya uchaguzi.Ilani ya kwanza ilikuwa ya mwaka 2000 ikijulikana kama ilani ya wapiga kura,ilani ya pili ni ya mwaka 2005,ya tatu ni ya mwaka 2015 na ya nne ni ilani ya mwaka 2015",alieleza Muro.

"Sisi wanawake wapiga kura tunatambua ni wadau muhimu kwenye shughuli zote za kisiasa na maendeleo ya jamii.Tunatambua na kudai haki za kushiriki katika uchaguzi kama wapiga kura na wanaowania nafasi za uongozi,walioteuliwa na kugombea hatimaye kushinda nafasi za uongozi kupitia uchaguzi",aliongeza.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao,Lilian Liundi alisema madai yaliyomo kwenye ilani ya uchaguzi ya wanawake yanahusu masuala ya wanawake wote nchini Tanzania.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanawake na Katiba,Ruth Meena akielezea kuhusu Ilani ya Uchaguzi ya Wanawake ya Uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu wa Tanzania mwaka 2020 ambayo imezinduliwa rasmi leo Septemba 27,2019 wakati wa kufunga Tamasha la 14 la Jinsia 2019 katika viwanja vya TGNP Mtandao Mabibo Jijini Dar es salaam.
Kulia ni Mwenyekiti wa TGNP Mtandao Asseny Muro akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Ilani ya Uchaguzi ya Wanawake ya Uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu wa Tanzania mwaka 2020 
Mwenyekiti wa TGNP Mtandao Asseny Muro akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Ilani ya Uchaguzi ya Wanawake ya Uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu wa Tanzania mwaka 2020 
Mwenyekiti wa TGNP Mtandao Asseny Muro akionesha Ilani ya Uchaguzi ya Wanawake ya Uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu wa Tanzania mwaka 2020 
Mwenyekiti wa TGNP Mtandao Asseny Muro akionesha Ilani ya Uchaguzi ya Wanawake ya Uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu wa Tanzania mwaka 2020.
Wafanyakazi wa TGNP Mtandao wakionesha mabango yenye ujumbe wa 'Uongozi sio misuli ni hekima na busara kila mtu anao'.
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao Lilian Liundi akionesha Ilani ya Uchaguzi ya Wanawake ya Uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu wa Tanzania mwaka 2020 .
Mwenyekiti wa TGNP Mtandao Asseny Muro akimkabidhi Ilani ya Uchaguzi ya Wanawake ya Uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu wa Tanzania mwaka 2020,Mkurungezi wa Jinsia Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Julius Mbilinyi.
Uzinduzi wa Ilani ya Uchaguzi ya Wanawake ya Uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu wa Tanzania mwaka 2020 ukiendelea.

Uzinduzi wa Ilani ya Uchaguzi ya Wanawake ya Uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu wa Tanzania mwaka 2020 ukiendelea.
Wanaharakati wakisherehekea wakati wa uzinduzi wa Uzinduzi wa Ilani ya Uchaguzi ya Wanawake ya Uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu wa Tanzania mwaka 2020.

Wanaharakati wakisherehekea wakati wa uzinduzi wa Uzinduzi wa Ilani ya Uchaguzi ya Wanawake ya Uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu wa Tanzania mwaka 2020.
Wanaharakati wakisherehekea wakati wa uzinduzi wa Uzinduzi wa Ilani ya Uchaguzi ya Wanawake ya Uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu wa Tanzania mwaka 2020.
Wanaharakati wakisherehekea wakati wa uzinduzi wa Uzinduzi wa Ilani ya Uchaguzi ya Wanawake ya Uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu wa Tanzania mwaka 2020.

Mkurungezi wa Jinsia Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Julius Mbilinyi akizungumza wakati wa kufunga Tamasha la 14 la Jinsia 2019 katika viwanja vya TGNP Mtandao Mabibo Jijini Dar es salaam.

Mkurungezi wa Jinsia Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Julius Mbilinyi akizungumza wakati wa kufunga Tamasha la 14 la Jinsia 2019 katika viwanja vya TGNP Mtandao Mabibo Jijini Dar es salaam.
Mkurungezi wa Jinsia Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Julius Mbilinyi akizungumza wakati wa kufunga Tamasha la 14 la Jinsia 2019 katika viwanja vya TGNP Mtandao Mabibo Jijini Dar es salaam.

Friday, September 27, 2019

BAGAMOYO WATAKIWA KUJIANDIKISHA

Na Omary Mngindo, Bagamoyo.


WANANCHI Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani, wametakiwa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura, ikiwa ni kuelekea kwenye chaguzi za viongozi wa serikali za vijiji na vitongoji.


Hayo yamebainishwa na Msimamizi wa uchaguzi wilayani hapa Malboard Kapinga, akizungumza na wadau wa zoezi hilo ikiwa ni utekelezaji wa agizo la serikali, lililozitaka halmashauri zote kuitisha vikao na wadau kuzungumzia mchakato huo.


"Halmashauri ya wilaya kwa Mamlaka tuliyopewa chini ya kanuni 9 (1) na (2) ya uchaguzi wa Wenyeviti, tangazo la serikali namba 373 la tarehe 26/4/2019 pamoja na kanuni zake, hapa Bagamoyo tayari zoezi la uandikishwaji limeshaanza," alisema Kapinga.


Aliongeza kwamba uchaguzi wa wenyeviti wa vitongoji katika mamlaka za miji midogo kanuni ya 08 (1) na (2), tangazo la serikali namba 371 la tarehe 26/4/2019, anawatangazia wananchi kuwa Nov 24 mwaka huu kutafanyika uchaguzi wa serikali za mitaa.


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Fatuma Latu amesema kuwa, wameitisha kikao hicho ikiwa ni kutekeleza agizo la serikali linalowataka kuwa na vikao vitakavyohusisha wadau kuelekea kwenye chaguzi zijazo.


"Niwashukuru kwa kujitokeza kwa wingi, kikao chetu kimezingatia maelekezo yaliyotolewa na serikali inayozitaka halmashauri zote nchini kuitisha vikao vitakavyojadili masuala muhimu wakati tunaelekea kwenye chaguzi," alisema Latu.


Wakichangia mada kwenye kikao hicho, Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wilayani humo Mathei Torongey amelalamikia hujuma alizofanyiwa na Mtendaji kijiji cha Mkenge, aliyewavamia wakiwa wanapeana maelekezo kuhusiana na kikao hicho.


"Nimefurahi kuwaona viongozi wa dini mnaounda Kamati ya amani mko hapa, tunawataka mtoe matamko yanayohusiana na kukemea dalili za uvunjifu wa amani, kitendo alichokifanya Mtendaji kinaashiria uvunjifu wa amani," alisema Torongey.


Nae Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mohamed Usinga diwani wa Kata ya Yombo amekumbushia fujo alizofanyiwa na wafuasi wa CHADEMA kwenye chaguzi zilizopita, hatua aliyoielezea imechangiwa na viongozi wao.

MAGAZETI YA LEO SEPTEMBA 27, 2019.