Thursday, August 15, 2019

WAKAZI KONGO WALILIA DARAJA MTO RUVU

Na Omary Mngindo,  

WAKAZI wa Kitongoji cha Umakondeni Kijiji cha Kongo Kata ya Yombo, wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani, wameomba wapelekewe Mhandisi wa ujenzi kuangalia uwezekano wa kujenga daraja katika mto Ruvu unaopita eneo lao.


Wakazi hao wametoa kilio hicho mbele ya mbunge Dkt. Shukuru Kawambwa, kwenye ziara ya kikazi jimboni humo, ambapo akiwa kijijini hapo wakazi hao walisema kuwa wanaliwa na mamba kutokana na kuvuka ng'ambo ya pili kwa ajili ya kilimo.


Aidha wamelalamikia gharama za kuunganishiwa maji, ambapo walisema kwamba pamoja na kuishi ndani ya eneo la mradi ulioko kijijini hapo, lakini gharama ya huduma hiyo kwa bomba yenye urefu wa mita 50 wanatakiwa walipie shilingi laki mbili.


Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Ally Jasilii alisema kuwa wanalima ng'ambo ya mto Ruvu chini ambapo kila siku wanavuka kwemda na kurudi, hali inayowaweka katika wakati mgumu huku akieleza kwamba kuna wenzao wameliwa au kujeruhiwa na mamba.


"Mheshimiwa Mbunge tunakuomba utuletee Mhandisi aangalie uwezekano wa kujenga daraja katika mto Ruvu chini, sisi tegemeo letu ni kilimo ng'ambo ya mto, wenzetu wameliwa na kujeruhiwa na mamba, tuletee Mhandisi," alisema Jasilii.


Kwa upande wake Ibrahimu Issa alisema kuwa wanakabiliwa na hatari ya mamba kutokana na kutegemea maji ya mto huo, pamoja na wao kuishi ndani ya mradi wa mradi lakini hawana huduma hiyo.


"Tunaambiwa kuunganishiwa bomba yenye urefu wa mita 50 shilingi laki mbili, mimi nina ardhi eka 3 sasa hizo mita zao 50 si zitaishia shamba la jirani yangu, tunakuomba na hili ukalifanyiekazi," alisema mkazi huyo.


Akijibia malalamiko hayo, Dkt. Kawambwa alisema kuwa amepokea malalamiko hayo na kuahidi kuyafanyiakazi, huku akisema kuwa ujenzi wa daraja mto huo unawezekana, huku akisema lakini kazi yake ni kubwa.


"Pamoja na kwamba ujenzi wa daraja mto Ruvu kazi yake ni kubwa, lakini hakuna lisilowezekana, nitakwenda kuzungumza na Wahandisi tutakuja kuangalia uwezekano wake," alisema Dkt. Kawambwa.


Akizungumzia kilio cha gharama ya kuunganishiwa maji, Dkt. Kawawambwa alisema kuwa kimsingi wakazi wanaoishi ndani ya eneo la mradi kungekuwa na unafuu wa bei, na kwamba kwa namna moja au nyingine wanasaidia kulinda miundombinu ya mradi.


"Haya yote nimeyapokea nitakwenda kukutana na viongozi husika kuzungumza nao hatimae kuwapatia mrejesho baada ya mazungumzo yetu, kuhusu mhandisi nitakuja nae kuona namna itakavyowezekana," alimalizia Dkt. Kawambwa.

MWENYEKITI WA BODI TFS AIPONGEZA TFS KWA UTENDAJI ULIOTUKUKA

Image may contain: 2 people, people sitting, table and indoor
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wizara Maliasili na Utalii kwa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania Brigedia Generali Mbaraka Mkeremy amewapongeza waahasibu na watumishi wa TFS kwa kuchagiza TFS kupata Hati Safi za Ukaguzi.


Akizungumza katika kikao na Watumishi wa Kanda ya Nyanda ya Juu Kusini jijini Mbeya jana, Brigedia Generali Mkeremy alisema licha ya TFS kuwa na changamoto nyingi katika utekelezaji wa majukumu yake watendaji wake wameweza kufanya kazi kwa weledi na hata kufanikiwa kupata hati safi kwa mara ya kwanza.


“Najua taasisi hii ina changamoto nyingi lakini niwapongeze kwa namna mlivyojituma na hata kuweza kupata hati safi ya ukaguzi, hati hii ni matokeo ya uwajibikaji katika makusanyo na matumizi.


Nimeelezwa kuwa TFS pia ilivuka malengo ya makusanyo, na imefanikiwa kupunguza malalamiko na kutokuwapo migogoro baina ya watumishi na hayo ni kiashiria cha mafanikio ya taasisi,” Brigedia Generali Mkeremy alisema.


Hii ni mara ya kwanza kwa Brigedia Generali Mkeremy kuzungumza na watumishi wa kada tofauti wa TFS tangu Waziri wa Maliasili na Utalii Dk.Hamisi Kigwangalla aizindue Bodi ya Ushauri ya Wizara kwa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) jijini Mwanza na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali Machi 9,2019.


Brigedia Jenerali Mkeremi alisema kukabiliana na baadhi ya changamoto hususan ujangiri TFS imeamua kuingia kwenye Jeshi Usu ili kuhakikisha uhifadhi endelevu wa misitu nchini.


Kamishna Mhifadhi wa Misitu, Prof. Dos Santos Silayo aliwataka watumishi kuendelea kushirikiana katatika kutatua changamoto za kiutumishi na kiutendaji huku akitanabaisha kuwa mabadiliko ya Jeshi Usu yataenda sambamba na TFS kutoka kwenye Wakala na kuwa Mamlaka kamili.
Image may contain: 4 people, people sitting, suit, table and indoor

MASJiD NOUR WAHITAJI MIL. 366 KUJENGA SHULE

Image may contain: 6 people, shoes, child and outdoor
Na Omary Mngindo, Mlandizi.

TAASISI ya Kiislamu ya Masjid Nour ya Mlandizi Kibaha Vijijini Mkoa wa Pwani, inahitaji kiasi cha sh. Mil. 366 kwa ajili ya kujenga shule ya Kiislamu.

Hatua hiyo inayolenga kuwajengea maadili mema vijana wa kiislamu ili waondokane na mmomonyoko wa maadili, imeandaliwa na taasisi hiyo ambayo tayari imeshapata eneo la kujenga shule hiyo katika Kitongoji cha Vikuruti wilayani hapa.

Katibu wa Bodi ya Wadhamini wa Taasisi hiyo Amin Matambo alisema kuwa, wanataraji kujenga vyumba vinane vya madarasa, nyumba za walimu, ofisi za walimu, msikiti, vyoo na gari ambavyo thmanai yake ni sh. Mil. 366.

Aliongeza kwamba katika baraza la Idd ambalo limefanyika katika msikiti huo, mbali ya Waumini kuhudhuria baraza hilo pia Maimamu kutoka misikiti mbalimbali ndani ya wilaya ya Kibaha wamehudhuria kisha kutoa maazimio na kwenda kufanyiwa kazi.

"Ujenzi wa shule mchakato wake umeshaanza kwa kupata eneo litakalojengwa shule hiyo Kitongoji cha Vikiruti, tumepanga bajeti ya kufanikisha ujenzi huo ambao ni kiasi cha shilingi milioni 366, tutachangishana waumini pamoja na wadau mbalimbali," alisema Sheikh Matambo.

Nae Imamu wa Msikiti wa Mtongani mjini hapa Sheikh,  Juma Ngonyani ameunga mkono maazimio ya ujenzi wa shule hiyo inayolenga kuwajengea watoto wa kiislam maadili mema.

Aidha Ngonyani ameongeza kwamba kuna kila sababu ya Maimamu kujiunga kwa umoja kupambana na baadhi ya walimu wa Madrasa wanaozitumia vibaya dufu katika shughuli za dua za kumswalia (Mtume Muhamad (SAW).

"Haya maazimio yaliyofikiwa kwenye baraza la Idd yamekuja wakati mwafaka, kwani kumekuwepo na baadhi ya walimu wa madrasa wamekuwa na tabia ya kugeuza dua za kumswalia Mtumeu Mhamad (SAW) kama ngoma za kiduku," alimalizia Sheikh Ngonyani.

Wednesday, August 14, 2019

MKOA WA PWANI KUWEKA MAWE YA MSINGI 13 YA VIWANDA.

Image may contain: 4 people, people smiling, people standing
VICTOR  MASANGU, KIBAHA.

KATIKA kuunga  mkono azma ya Rais wa awamu ya tano Dk. John Pombe Magufuli katika kuwa na uchumi wa viwanda serikali Mkoa wa Pwani imejipanga  mwezi huu kuweka mawe ya msingi katika viwanda vipatavyo 13  ambavyo  vitajengwa  katika Wilaya za  Kibaha, Bagamoyo, pamoja na Mkuranga kwa lengo la kuifanya Tanzania kuwa na uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.


Akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake wakiwemo baaadhi ya  wakuu wa idara Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani, Bi Theresia Mmbando amebainisha kuwa zoezi hillo la kuweka mawe ya msingi na kukagua ujenzi wa viwanda hivyo litafanywa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndaikilo ikiwa ni  moja ya utekelezaji wa agizo la Rais Dk. John Pombe Magufuli.


Aidha katika hatua nyingine amekemea vitendo vya baadhi ya wawekezaji kuwanyanyaza wafanyakazi ambao ni wazawa na badala yake kuwataka kuhakikisha wanazingatia sheria na taratibu zote za kazi na kuwapa  vipaumbele zaidi wananchi katika fursa za ajira   ili kutimiza malengo ya serikali katika kukuza uchumi kupitia sekta ya viwanda.


Mkoa wa Pwani katika zoezi hilo litaweka mawe ya msingi katika  baadhi ya viwanda hivyo vikiwemo vya kiwanda cha kutengenezea mikate na biskuti, kiwanda cha kuzalishia nyuzi, kutengenezea nondo, sufuria, mitungi ya gesi, kiwanda cha kuchakata mihogo, kamba za uvuvi pamoja na kingine cha  kuchakata zao la korosho pamona na kinachozalisha chanjo za mifugo.
Image may contain: 6 people, people smiling, people standing

Katibu Mkuu azindua mafunzo ya wakaguzi wa Mifumo ya uzalishaji Dawa na Vifaa tiba (GMP) kwa nchi za SADC

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TMDA Adam Fimbo akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya wakaguzi wa Mifumo ya uzalishaji Dawa na Vifaa tiba (GMP) kwa nchi wanachama wa SADC ambapo Tanzania ndiyo mwenyeji Mafunzo hayo yanafanyika kwenye hoteli ya Habour View jijini Dar es salaam.
Mratibu wa Mradi wa SADC Medicines Reguratory Harmonisation Project (SMRHP) Bi. Sakhile Dube Mwedzi akizungumza katika uzinduzi wa mafunzo hayo.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba TMDA Bi. Gaudensia Simwanza akimkaribisha kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo ili kuzingumza na washiriki wa mafunzo hayo.
Mafunzo hayo yamezinduliwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk Zainab Chaula. Wakufunzi wa mafunzo hayo wanatoka Malmaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA)