Sunday, July 7, 2019

BRELA YATOA MAFUNZO KWA WAFANYABIASHARA PWANI JINSI YA KUJISAJILI KWA NJIA YA MTANDAO

Afisa Mfawidhi kutoka Brela kanda ya kusini ambaye ni mtaalamu wa mfumo wa usajili Francis Mwakalebela aliyesimama akitoa maelekezo kwa  kwa njia ya vitendo washiriki wa mafunzo hayo kuhusina na  namna ya kuweza kusajili makampuni ya na majina ya biashara kwa njia ya mtandao.
...................................

VICTOR MASANGU, PWANI 

BAADHI ya wafanyabiashara  Mkoani Pwani ambao kwa kipindi cha muda mrefu waliokuwa wanakabiliwa na changamoto sugu  ya kufanyiwa vitendo vya utapeli pindi wanapotaka kupatiwa usajili  wa  makampuni yao  pamoja na majina ya  biashara hatimaye wamepata  ufumbuzi baada ya kupatiwa mafunzo maalumu kutoka Wakala wa usajili wa biashara na leseni (BRELA) kwa lengo la kujifunza sheria na taratibu za usajili.


Wakizungumza katika ufunguzi rasmi wa mafunzo maalumu yaliyoandaliwa kwa umma juu ya kujifunza jinsi ya  kutumia mfumo wa usajili wa makampuni na majina ya biashara baadhi ya wafanyabiashara hao akiwemo Abdala Ndauka na Elina Mgonja wamesema kwa miaka mingi wamekuwa wakifanyiwa vitendo vya utapeli hivyo kujikuta wanaingia hasara kubwa katika zoezi zima la upatikanaji wa leseni.


Aidha wafanyabiashara hao wametoa pongezi kwa Brela  kwa kuwapatia mafunzo hayo ambayo yataweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa changamoto mbali mbali ambazo zilikuwa zikiwakabili katika siku za nyuma  katika kutekeleza majukumu yao hususan  kuweza kutumia mfumo wa usajili wa kampuni na majina ya biashara zao.


“Kwa kweli sisi kama wafanyabiashara wa Mkoa wa Pwani tunatoa pongezi zetu za dhati kwa mamlaka husika ya Brela kwa kuona umuhimu ya kutupatia mafunzo hayo ya kujisajili kwa kutumia njia ya mtandao, maana hapo awali tulikuwa tunapata usumbufu mkubwa na wakati mwingine kutapeliwa na baadhi ya watu hivyo kwa sasa tunaweza kutimiza majukumu yetu kwa weledi wa hali ya juu,”walisema wafanyabiashara hao.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa utawala na fedha kutoka Wakala wa usajili wa biashara na leseni (BRELA) Bakari Mketo alibainisha  kwamba lengo la kuandaa mafunzo hayo  kwa wafanyabiashara pamoja na umma kuhusina na kupata huduma za usajili kwa njia ya mtandao ikiwemo kuwajengea uwezo katika suala zima la ulipaji wa madeni kwa wateja wao ili kuondokana na usumbufu  waliokuwa wanaupata.


“Lengo letu kubwa kwa sasa tunazunguka katika mikoa mbali mbali na kwa sasa tumeamua kuwakutanisha wafanyabiashara wa Mkoa wa Pwani ili tuweze kuwapa mafunzo maalumu ambayo yatawawezesha kuweza kujisajili kwa kutumia njia ya mtandao pamoja na kujifunza mambo mbali mbali ambayo yanahusiama na utoaji wa leseni za viwanda,”alisema  Mketo.


Pia alibainisha kwamba  lengo lao kubwa ni kuweka mikakati kabambe ambayo itaweza kuwasaidia wafanyabiashara kuondokana na changamoto mbali mbali ambazo zimekuwa zikiwakabili katika utekelezaji wa majukumu yao, ili waweze kufanya usajili wa makampuni yao pamoja na majina ya biashara zao bila ya kuwepo na usumbufu wowote.


Naye Afisa biashara mkuu kutoka  Wizara ya viwanda na bishara Jane Lyatuu aliwataka  wafanyabishara wote nchini kuhakikisha wanazisajili biashara zao zote pamoja na makampuni, taasisi, na viwanda  kwa lengo la kuweza kuhimili  ushindani uliopo katika soka la bara la afrika kwa kuzingatia ubora wa bidhaa zinazotengezwa nchini.


 KATIKA  mafunzo hayo yaliyokuwa ya  siku mbili yalitolewa  kwa umma juu ya kutumia mfumo wa usajili wa kampuni na majina ya biashra, pamoja na alama za bishara na utoaji wa leseni za viwanda yamewashirikisha wadau mbali mbali wa maendeleo, maafisa biashara, wafanyabiashara wadogo na wakubwa, maafisa maendeleo,  mkaguzi wa ndani pamoja na wanasheria.
  Baadhi ya wafanyabiashara wa Mkoa wa Pwani wakiwa katika zoezi la kujifunza jinsi ya kufanya usajili kwa kutumia mfumo wa mtandao.
Washiriki wa mafunzo hayo kutoka maeneo mbali mbali ya Mkoa wa Pwani wakiwa wanaelekezana jinsi ya kuweza namna na kujisajili  makampuni na majina ya biashra kwa kwa kutumia njia ya mtandao.
Wafanyabishara wa Mkoa wa Pwani wakiwa  katika mafunzo ya kujifunza namna ya kusajili makampuni na majina ya biashara kwa njia ya mtandao.

Afisa maendeleo ya jamii katika halmashauri ya mji Kibaha  Lea Lwanji kushoto akiwa na mshiriki mwenzake wakiwa wanafuatilia  kwa umakini mafunzo ya usajili kwa kutumia mfumo wa njia ya mtandao.

Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa wanaangalia jinsi ya mfumo wa kujisajili kwa njia ya mtandao unavyofanya kazi.

(PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU)
 

BEI YA UFUTA YAONGEZEKA LINDI.

 NA HADIJA HASSAN, LINDI.

Bei ya Ufuta kwenye Mnada wa 5 wa Chama Cha Ushirika cha Lindi Mwambao Kinachojumuisha wakulima wa Wilaya za Lindi, Kilwa na Manispaa ya Lindi Mkoani humo imeendelea kuimarika kutoka Tsh. 2,735 kwa Bei ya juu na Tsh. 2,730 Bei ya chini katika Mnada wa Nne hadi kufikia Tsh. 2,830/= kwa Bei ya juu na Tsh. 2,825/=kwa Bei ya chini.


Akielezea mwenendo wa Bei za Ufuta katika mikoa inayolima zao hilo Mrajisi msaidizi wa vyama vya Ushirika Mkoa wa Lindi Robert Nsunza alisema kuwa ukilinganisha na Mikoa mingine inayolima zao hilo Mkoa wa Lindi umekuwa ukipata Bei nzuri kuliko mikoa mingine.


Alisema katika minada iliyopita Mkoa wa Mtwara uliuza ufuta wao kwa Bei ya Tsh. 2690 kwa kilo Moja, Pwani iliuza kwa Tsh. 2700 Huku Mkoa wa Kondoa ukiuza ufuta wao kwa Bei ya Tsh. 2683.


Nsunza aliongeza kuwa kulingana na soko la zao hilo kwa sasa huenda Bei hizo zikaendelea kuimarika zaidi ambapo Nchini China kwa sasa ufuta unanunuliwa kwa Dola1800 kwa tani.


Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Rashidi Masudi aliwataka wakulima wa zao hilo kuongeza umakini katika kusafisha ufuta wao ili kuendelea kupata Bei nzuri.


Alisema Bei nzuri wanazoendelea kuzipata ni kutokana na wanunuzi kuridhishwa na ubora wa Ufuta wao hivyo ni vyema kuendelea kuzingatia Usafi katika ufuta unaopelekwa kwenye Maghara yao kwa ajili ya kuupeleka kwenye Mnada
 

Mwenyekiti bodi ya VETA atoa maelekezo kwa utawala, ataka wakulima kufikiw


Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), Peter Maduki akizungumza na waandishi wa habari

Na Selemani Magali; Daresalaam

Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), Peter Maduki ameutaka uongozi wa VETA kuhakikisha wanafikisha ubunifu unaonyeshwa katika maonyesho ya sabasaba vijijini.

Maduki amesema faida ya ubunifu huo utaonekana kama wadau watanufaika nao, ubunifu huo ukipelekwa vijijini utawasaidia sana wakulima.

 Amesema wakulima wanachangamoto nyingi ili kufikia malengo yao ikiwemo kukosekana kwa mashine za kuchakata mazao yao, na Veta imekuwa ikionyesha mashine za kujibu changamoto za wakulima sasa ni wakati wa kupeleka huduma hiyo Mikoani.

“Tunataka malighafi ambazo zimeshachakatwa ili kusudi zipate thamani zaid, ukichakata unapata bei ya juu ukilinganisha na mali ghafi, ni vema twende huko tukawasaidie wananchi.

Aidha Mwenyekiti huyo hakusita kuonyesha furaha yake kuona vijana wanaweza kutumia kile walichojifunza darasani, hiyo ni hatua kubwa ambayo inatia moyo kwa mzazi na taifa kwa ujumla.

Pia amefurahishwa baada ya kuona VETA sasa inaweza kutoa mchango katika kuchangia kuimarisha ujenzi wa uchumi wa viwanda hapa Tanznia hasa eneo la usindikaji wa mazao ya Kilimo kwa ajili ya viwanda viwanda vya ndani.

Mwenyekiti anasema tayari serikali imeshawawezesha VETA kubuni miradi mbalimbali sasa ni zamu ya mamlaka kuhakikisha inasaidia wakulima kuongeza thamani ya mazao yao na wanufaike na ubunifu wa VETA.

Aidha amesema VETA wanashirikiana na Shirika la kuendeleza Viwanda vidogo vidogo (SIDO) pamoja na Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) ili kuweza kufikia lengo la uchumi wa viwanda waliojiwekea watanzania kwa kushirikiana na Serikali.

“Kwa sasa VETA inafanya vizuri kwa kushirikiana ba wadau husika wakiwemo taasisi zinazotoa mikopo midogo midogo kwa ajili ya kuwapa mitaji wanafunzi wanaohotimu,kutoa masomo ya ujasiriamali ,tumeingia mkataba na Sido, na taasisi mbalimbali za kifedha,”alisena Maduki.

"Tunataka kuona kuwa wakulima wa mazao yetu hapa Tanzania yanachakatwa na kuwa yanayoweza kutumika, tusingependa kuona mazao yetu yanakwenda nje ya kiwa mali ghafi.

Lakini jambo linguine ambalo limenifurahisha ni kuona vijana wanaweza kutumia kile walichojifunza darasani, hiyo ni hatua kubwa ambayo inatia moyo kwa mzazi na taifa kwa ujumla.


KIKWETE ASIFU MAONESHO YA 43 YA SABABSABA JIJINI DAR.

 


RAIS Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete amezipongeza Wizara ya Viwanda na Biashara na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) kwa maandalizi mazuri ya Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Julius Nyerere.

Akizungumza jana Jumamosi (Julai 6, 2019) mara baada ya kutembelea na kukagua mabanda mbalimbali ya washiriki wa Maonesho hayo, Rais Mstaafu Kikwete alisema hizo ni dalili njema kwa maonesho hayo kwa kuwa yamekuwa bora zaidi ya maonesho yaliyofanyika mwaka jana.



Aidha aliongeza kuwa maonesho ya mwaka huu, yameonesha dhamira ya dhati ya Serikali katika kujenga uchumi wake kupitia viwanda, kwa kuwa katika maonesho ya mwaka huu malighafi nyingi za kilimo zimepewa kipaumbele na wazalishaji wa bidhaa mbalimbali.

“Maonesho ya mwaka huu yamekuwa bora zaidi, kwani tumeshuhudia malighafi nyingi za kilimo zikipewa kipaumbele na hii imekuwa ni dalili njema na point (alama) tunayotakiwa kuifikia kwa sasa” alisema Kikwete.

Awali akitembelea Banda la Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Rais Mstafu Kikwete alilitaka jeshi hilo kuwa wabunifu kwa kuzalisha bidhaa bora zitakazoweza kutumika nje ya Tanzania hususani bidhaa za ngozi ikiwemo viatu vinavyozalishwa na Jeshi hilo.