Tuesday, April 30, 2019

VULU NA MGALU KUTIMIZA AHADI ZAO MAFIA.


 Pichani Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani Zaynab Vulu akizingumza na viongozi wa Umoja wa Wanawake (UWT) wilaya ya Mafia mkoani Pwani alipokuwa kwenye ziara ya siku moja. Meza Kuu wa mwisho kutoka kushoto Arafa Kisela Mjumbe wa Mkoa, Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Mafia Mtumwa Geo na Mwenyekiti wa CCM Hassani Pango. 

Picha na Omary Mngindo.

 .................................................

Na Omary Mngindo, Mafia.


WABUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani Zaynabu Vulu na Subira Mgalu ambaye ni Naibu Waziri wa Nishati wanataraji kutimiza ahadi walizozitoa wilayani Mafia.


Hayo yamebainishwa na Vulu alipokuwa kwenye ziara ya siku mbili wilayani hapa, iliyolenga kukutana na wana- Jumuia zinazounda Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambapo akiwa Mafia amekabidhi kitanda kimoja kwenye Zahanati ya Maalimbani Kata ya Kiegeani jimboni hapa.

Akizungumza na wana-Jumuia ya Wanawake (UWT) wilayani hapa mbele ya Mwenyekiti Mtuma Ahmad, Katibu Khadija Geo, Mwenyekiti wa CCM Hassani Pango, wa Wazazi Mohamed Fakhi na Katibu Mashaka Milimila, VULU alisema kuwa wakiwa katika ziara wilayani humo kuna ahadi ambazo wameziahidi.

"Wana-Jumuia wenzangu wakati tukiwa kwenye ziara wilayani hapa nikiwa na mbunge mwenzangu Subira Mgalu kuna mazungumzo mengi ambayo yumezungumza ikiwa ahadi ambazo tumezitoa ikiwemo viti 100, tunajipanga wakati wowote tutatimiza ahadi hizo," alisema Vulu.

Aidha mbunge huyo alipokea taarifa za utekelezaji wa ilani ya chama hicho ikiwemo wa ugawaji wa taa za sola kwenye zahanati mbalimbali zinazotolewa na Naibu Waziri Mgalu zinazolenga kuwaboreshea huduma hiyo maeneo hayo.

"Nimepokea shukrani za mbunge mwenzangu Subira Mgalu anbaye ni Naibu Waziri wa Nishati, mmesema amekabidhi taa za sola katika zahanati mbalimbali, nitazifikisha kwake, nasi tupo pamoja katika kuhakikisha tunaisaidia serikali kwenye sekta mbalimbali," alisema Vulu.

Katika ziara hiyo Vulu amekabidhi kitanda kimoja, shuka pamoja na vifaa Tiba katika zahanati ya Malimbani iliyopo Kata ya Kiegeani, huku akiahidi kuchangia pesa taslimu kwenye ujenzi wa jengo la ofisi ya Jumuia hiyo wilayani hapa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa UWT wilayani hapa Mtumwa alisema kuwa Jumuia yao inaendelea na uhamasishaji wa Jumuia pamoja na chama ili kuhakikisha wanaisaidia serikali katika maendeleo ya nyanja zote.

Kwa upande wake Mjumbe wa jumuia hiyo wilayani Mafia Arafa Kisela, amemshukuru Vulu kwa ushirikiano aliowapatia wa gari kwenye uchaguzi wa mwaka 2015, huku akiwataka wana-CCM kuendeleza umoja upendo na mshikamano.

MGOMBEA UDIWANI LINDI (CUF) ALALAMIKIA WASIMAMIZI WA UCHAGUZI.

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) BI Rukia Mbasha akimkabidhi ilani ya chama hicho Diwani mteule wa kata ya Mvuleni Mnuli Saidi Khatibu Baada ya kutangazwa na Msimamizi kuwa Amepita kuwa diwani wa kata hiyo Bila kupingwa

 

Diwani Mteule wa kata ya Mvuleni Mnuli Khatibu (CCM) akionyesha ilani ya Chama hicho baada ya kukabidhiwa

 .................................

Na Hadija Hassan, Lindi.


MGOMBEA Udiwani Kata ya Mvuleni, Halmashauri ya Lindi, Mkoani hapa, Chuma Abdurahamani Saidi (CUF) amesikitishwa na maamuzi yaliyofanywa na wasimamizi wa uchaguzi mdogo Wilayani Hapa kumpitisha mpinzani wake, Mnuli Said Khatibu {CCM} Kuwa Diwani wa kata hiyo kwa madai ya  kushindwa kujibu pingamizi zake.


Chuma ametoa masikitisho hayo wakati alipokuwa akizungumza na Mwandishi wa Habari hiziz, kuhusu kutupiliwa mbali kwa pingamizi lenye vipengele vinne alizokuwa amemuwekea mpinzani wake Mnuli Said Khatibu wa Chama Cha Mapinduzi  {CCM}.


Chuma alivitaja vipengele hivyo kuwa  ni pamoja na mgombea wa {CCM} uhalali wa uraia wake, Kudanganya mwaka aliozaliwa, Majina ya waliomdhamini sio walioweka saini zao kwenye Fomu na tamko la kisheria la mgombea kutosainiwa na Hakimu wa Wilaya, Mkoa, Kamishina au Wakili aliyepata Kibali au kutambuliwa na Serikali.


Kwa upande wa Mnuli mgombea wa {CCM} alimuwekea mpinzani wake Chuma wa {CUF} pingamizi linalohusu kutotoa tamko la kisheria mbele ya Hakimu kama ilivyoelekezwa na kifungu cha 42 {4} {a} cha Sheria ya ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa Namba 4/1979.


Pia, msimamizi msaidizi wa uchaguzi Kata hiyo ya Mvuleni, Ahmed Ally Mpira, amemuwekea pingamizi mgombea wa {CUF} kutowasilisha Picha {4} za rangi za ukubwa na zile zinazotumika kwenye Pasi za kusafiria {Pasport size} zenye muonekano wa rangi nyeupe kwa nyuma kama inavyoelekezwa na Kifungu cha 25 {3} cha kanuni za uchaguzi wa Madiwani {2015}.


Hata hivyo Chuma alisema mpinzani wake Mnuli wa {CCM}, alidai ameshindwa kujibu pingamizi alizomuwekea, ikiwemo kutoonyesha vielelezo kama vile Cheti cha kuzaliwa au cha uraia vinavyomtambulisha ni raia halali wa Tanzania na vitambulisho vya uraia au kupigia kura kwa watu waliomdhamini.


Akitoa taarifa mbele ya waandishi wa Habari, Msimamizi wa uchaguzi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Lindi, Samweli  Gunzar, alimtangaza Mnuli Said Khatibu {CCM} kuwa amepita bila kupingwa,baada ya pingamizi aliyomuwekea Mpinzani wake Chuma Abdurahamani Said wa {CUF} kupita.


Gunza akitumia matakwa ya kifungu cha 45 {2} cha Sheria ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa namba 4 ya mwaka 1979, {sura 292} na kwa Mamlaka aliyopewa na Sheria tajwa hapo juu, “Mimi Samweli Warioba Gunzar msimamizi wa uchaguzi Halmashauri yaWilaya ya Lindi Namtangaza mgombea wa (CCM) Mnuli Said Khatibu kuwa amepita bila kupingwa”Alisema Gunzar.


Akitolea ufafanuzi juu ya namna pingamizi za pande  zote mbili zilivyoshugulikiwa Gunzar alidai kuwa pingamizi zote zilishugulikiwa kwa kuzingatia Sheria na kanuni za uchaguzi wa Madiwani , 2015 ambapo msimamizi wa uchaguzi alifanya maamuzi kwa kuzingatia sheria hizo


Hata hivyo alisema baada ya maamuzi hayo Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi aliwataarifu Wagombea  wote juu ya maamuzi yaliyofikiwa kwa kuzingatia kanuni ya 27 (1) ya kanuni za uchaguzi wa madiwani ya mwaka 2015 ambapo msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi alitoa nafasi kwa wahusika waliotajwa katika kanuni hiyo ambae hakuridhika na maamuzi kukata rufaa kwa Msimamizi wa Uchaguzi


Kwa upande wake Diwani Mteule wa kata hiyo ya Mvuleni Mnuli Khatibu wa Chama cha Mapinfuzi {CCM} alisema amefarijika na kupita kwa Pingamizi alilokuwa amemuwekea mpinzani wake na kwamba anachosubiri ni kuapishwa ili aweze kutekeleza majukumu yake kwa wananchi.


Halmashauri ya Wilaya ya Lindi ni miongoni mwa Halmashauri yenye Uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata ya Mvuleni kufuatia kifo cha aliekuwa Diwani wa kata hiyo kupitia Chama Cha Wananchi (CUF) MHE, IDAROUS YUSUF MANZI


CGF. AFANYA MABADILIKO YA BAADHI YA MAKANDA WA MIKOA.