Sunday, April 7, 2019

WAZIRI UMMY AAHIDI NEEMA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA DODOMA

 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu (kushoto)akiongea jambo wakati alipofanya ziara ya kukagua jengo la Mama na Mtoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma (General). Kulia ni katibu wa Wizara ya Afya Dkt. Zainab Chaula.
..............................................

Na WAMJW-Dodoma

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ameahidi kutoa Tsh. Milioni 200 kwa ajili ya ujenzi wa jengo jipya la wagonjwa wa nje (OPD) katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.

Waziri Ummy ametoa ahadi hiyo leo wakati alipofanya ziara ya kutembelea jengo jipya la mama na mtoto (Maternity Block) katika Hospitali hiyo ili kujionea hali ya utoaji huduma kwa akina mama wajawazito na watoto.

“Ninaahidi kutoa Milioni 200 kwa ajili ya ujenzi wa jengo jipya la OPD ya kisasa yenye uwezo wa kupokea wagonjwa wengi zaidi tofauti na OPD iliyopo sasa”. Amesema Waziri Ummy.

Waziri Ummy ameutaka uongozi wa Hospitali hiyo kurekebisha na kufanya maboresho katika baadhi ya maeneo yaliyoonekana kuwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuyapa majina majengo yote ya Hospitali hiyo ili kuepusha usumbufu kwa wagonjwa pindi wanapotaka kupata huduma katika majengo tofauti.

Aidha, Waziri Ummy ameutaka uongozi wa Hospitali hiyo kujenga ghorofa ambayo itakua maalum kwa ajili ya matibabu ya watoto pekee yenye uwezo wa kulaza watoto wengi sambamba na chumba cha uangalizi maalum kwa watoto waliozaliwa kabla ya muda (Intensive Neonatal Care Unit) na wale wanaohitaji uangalizi maalum (ICU).

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Zainab Chaula amesema Wizara itaendelea kushirikiana na uongozi wa Hospitali hiyo katika kutatua changamoto mbalimbali zilizoonekana katika Hospitali hiyo ikiwa ni pamoja kuongeza watumishi wa kada mbalimbali ili kukidhi mahitaji.

“Naomba niwaahidi tutaongeza watumishi wa kada mbalimbali ili kuziba mapungufu yanayoonekana, lengo likiwa ni kuboresha huduma katika Hospitali hii inayotegemewa na watu wengi wa Dodoma na kutoka maeneo ya jirani”. Amesema Dkt. Chaula.

Hata hivyo Dkt. Chaula amewataka watumishi wa Hospitali hiyo kushirikiana ili waweze kutoa huduma nzuri kwa wagonjwa wanaokwenda hospitalini hapo.

Katika ziara hiyo iliyoenda sambamba na siku ya Afya Duniani imejumuisha viongozi mbalimbali wa Wizara akiwemo Mkurugenzi wa Sera na Mipango Edward Mbaga wameondoka na azimio la kufanya maboresho katika Hospitali hiyo ikiwa ni pamoja na kujengwa kwa jengo maalum la kupokea wageni mbalimbali wanaokuja Dodoma.
 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akipokea hotuba kutoka kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma Dkt. Ernest Benzi wakati walipofanya ziara ya kukagua jengo la mama na mtoto (Maternity Block). Kulia ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dkt. Zainab Chaula na nyuma viongozi wengine wa Wizara na Hospitali.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiongea na mama aliyejifungua katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma wakati alipofanya ziara ya kutembelea jengo jipya la Mama na Mtoto katika Hospitali hiyo.

Jengo jipya la Mama na Mtoto (Maternity Block) lililopo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma

Friday, April 5, 2019

RAIS MAGUFULI: HATUNA MPANGO WA KUONGEZA MIKOA MPIYA

RAIS Dkt. John Pombe Magufuli amesema Serikali haina mpango wa kuongeza maeneo ya utawala ikiwemo kuanzisha mikoa mipya na badala yake imejipanga kuimarisha huduma na mahitaji ya miundombinu iliyopo ili kuwaletea maendeleo wananchi.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa barabara ya Namtumbo-Kilimasera-Matemanga-Tunduru yenye urefu wa kilometa 193 leo (Ijumaa April 05, 2019), Rais Magufuli alisema Serikali imekusudia kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya barabara, afya, maji, elimu n.k katika maeneo waliopo.

Aliongeza kuwa katika awamu yake yake ya Uongozi, suala la kuongeza maeneo ya utawala halipo na badala yake kuwataka Viongozi wa maeneo hayo wajipange katika kuwaletea maendeleo wananchi badala ya fedha zilizopo kwenda katika kujenga ofisi mpya za Wakuu wa Mikoa mipya na kuwalipa mishahara viongozi hao.

“Tumepanga kuleta maendeleo ya kweli kwa wananchi wetu, tumechelewa kuleta Maendeleo hususani kwa wananchi wetu wa mikoa ya kusini, Serikali ninayoiongoza haina mpango wa kuanzisha mikoa mipya , badala yake pesa hizo tutazielekeza katika ununuzi wa madawa na kuboresha miundombinu ya barabara, elimu na nishati’ alisema Rais Magufuli.

Aidha Rais Magufuli alisema bado yapo baadhi ya maeneo mengi nchini yanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo barabara za lami, hivyo Serikali haitoweza kuleta Maendeleo katika sehemu moja kwa kuwa fedha hizo hazipo na kwamba ina mahitaji makubwa katika kuboresha huduma mbalimbali za kijamii na kiuchumi katika maeneo mbalimbali ya nchi.

Kwa mujibu wa Rais Magufuli alisema malengo ya Serikali ni kuhakikisha kuwa huduma muhimu na za msingi kwa Maendeleo ya wananchi zinapewa kipaumbele ikiwemo ujenzi wa vituo vya afya na Zahanati, kwa kuwa kukamilika kwake kutasaidia kupunguza vifo vya akina mama na watoto ambavyo katika miaka ya nyuma vimekuwa vikisababisha vifo vya makundi hayo ya kijamii.

Akizumgumzia kuhusu Sekta ya Maji, Rais Magufuli alimtaka Waziri wa Maji, Prof. Makame Mbarawa kuwasimamia wakandarasi wa miradi ya maji nchini, kwani Serikali imekuwa ikitenga kiasi kikubwa cha cha fedha katika miradi ya Maendeleo pasipo na kupata matokeo yaliyotarajiwa, na hivyo kuisababishia hasara Serikali.

“Kwa mujibu wa ripoti ya Wizara ya Fedha na Mipango, miradi mingi ya maji imekuwa ikitumia fedha nyingi pasipo na kupata matokeo yoyote na wataalamu wetu hasa wakandarasi wamekuwa wazito kutoa tafsiri za nadharia za utaalamu na kuzileta katika nadharia halisi, na mataifa ya nje yanashangwa tunaposhindwa kuvitumia vyanzo tulivyonazo ili kuweza kuzalisha maji ya kutosha’ alisema Rais Magufuli.

Awali akizungumzia kuhusu ujenzi wa barabara hiyo, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe alisema kujengwa kwa barabara hiyo kutaimarisha mawasiliano katika ukanda wa kusini unaojumuisha Mtwara, Mingoyo, Masasi, Mangaka, Tunduru hadi Mbamba Bay na hivyo kuzidi kufungua fursa za kiuchumi nanchi jirani za Malawi na Msumbiji.

Alisema hadi kukamilika kwake barabara hiyo imegharimu kiasi cha Tsh Bilioni 173, ambapo Shirika la Misaada la Japan limetoa asilima 23.24, Benki ya Maendeleo ya Afrika asilimia63.32 na Serikali ya Tanzania asilimia 13.35 ikiwemo kodi na kulipa fidia kwa wananchi wanaostahili kwa mujibu wa sheria ya barabara ya mwaka 2007.

Naye Balozi wa Japan nchini Tanzania, Shinichi Goto alisema Serikali ya Japan imekuwa mstari wa mbele kuisaidia Tanzania kutekeleza miradi ya maendeleo ikiwemo barabara ya Namtumbo-Kilimasera-Matemanga-Tunduru na itaendelea kusaidia miradi mingine ili kuhakikisha kuwa malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuondoa umaskini kwa wananchi wake yanafikiwa.

RAIS MAGUFULI: HATUNA MPANGO WA KUONGEZA MIKOA MPIYA

RAIS Dkt. John Pombe Magufuli amesema Serikali haina mpango wa kuongeza maeneo ya utawala ikiwemo kuanzisha mikoa mipya na badala yake imejipanga kuimarisha huduma na mahitaji ya miundombinu iliyopo ili kuwaletea maendeleo wananchi.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa barabara ya Namtumbo-Kilimasera-Matemanga-Tunduru yenye urefu wa kilometa 193 leo (Ijumaa April 5, 2019), Rais Magufuli alisema Serikali imekusudia kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya barabara, afya, maji, elimu n.k katika maeneo waliopo.

Aliongeza kuwa katika awamu yake yake ya Uongozi, suala la kuongeza maeneo ya utawala halipo na badala yake kuwataka Viongozi wa maeneo hayo wajipange katika kuwaletea maendeleo wananchi badala ya fedha zilizopo kwenda katika kujenga ofisi mpya za Wakuu wa Mikoa mipya na kuwalipa mishahara viongozi hao.

“Tumepanga kuleta maendeleo ya kweli kwa wananchi wetu, tumechelewa kuleta Maendeleo hususani kwa wananchi wetu wa mikoa ya kusini, Serikali ninayoiongoza haina mpango wa kuanzisha mikoa mipya , badala yake pesa hizo tutazielekeza katika ununuzi wa madawa na kuboresha miundombinu ya barabara, elimu na nishati’ alisema Rais Magufuli.

Aidha Rais Magufuli alisema bado yapo baadhi ya maeneo mengi nchini yanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo barabara za lami, hivyo Serikali haitoweza kuleta Maendeleo katika sehemu moja kwa kuwa fedha hizo hazipo na kwamba ina namahitaji makubwa katika kuboresha huduma mbalimbali za kijamii na kiuchumi katika maeneo mbalimbali ya nchi.

Kwa mujibu wa Rais Magufuli alisema malengo ya Serikali ni kuhakikisha kuwa huduma muhimu na za msingi kwa Maendeleo ya wananchi zinapewa kipaumbele ikiwemo ujenzi wa vituo vya afya na Zahanati, kwa kuwa kukamilika kwake kutasaidia kupunguza vifo vya akina mama na watoto ambavyo katika miaka ya nyuma vimekuwa vikitokea kwa wingi.

Akizumgumzia kuhusu Sekta ya Maji, Rais Magufuli alimtaka Waziri wa Maji, Prof. Makame Mbarawa kuwasimamia wakandarasi wa miradi ya maji nchini, kwani Serikali imekuwa ikitenga kiasi kikubwa cha cha fedha katika miradi ya Maendeleo pasipo na kupata matokeo yaliyotarajiwa, na hivyo kuisababishia hasara Serikali.

“Kwa mujibu wa ripoti ya Wizara ya Fedha na Mipango, miradi mingi ya maji imekuwa ikitumia fedha nyingi pasipo na kupata matokeo yoyote na wataalamu wetu hasa wakandarasi wamekuwa wazito kutoa tafsiri za nadharia za utaalamu na kuzileta katika nadharia halisi, na mataifa ya nje yanashangazwa tunaposhindwa kuvitumia vyanzo tulivyonazo ili kuweza kuzalisha maji ya kutosha’ alisema Rais Magufuli.

Awali akizungumzia kuhusu ujenzi wa barabara hiyo, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe alisema kujengwa kwa barabara hiyo kutaimarisha mawasiliano katika ukanda wa kusini unaojumuisha Mtwara, Mingoyo, Masasi, Mangaka, Tunduru hadi Mbamba Bay na hivyo kuzidi kufungua fursa za kiuchumi na nchi jirani za Malawi na Msumbiji.