Friday, March 29, 2019

TPA KANDA YA MTWARA YAKABIDHI MADAWATI YA MILIONI 13 KWA MANISPAA YA LINDI.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya ya Bandari Tanzania (TPA) Deodedth Kakoko kushoto akikabidhi madawati 76 kwa mkuu wa Wilaya ya Lindi Shahibu Ndemanga kulia
........................................


NA HADIJA HASSAN, LINDI

MAMLAKA  ya Bandari Tanzania (TPA) Kanda ya Mtwara imechangia   Madawati 76 yenye thamani  ya sh. Milioni 13 katika Halmashauri ya Manispaa ya Lindi Mkoani humo ikiwa ni namna ya kurejesha  faida  waliyoipata inayotokana na shehena za mizigo na meli

Makabidhiano ya  madawati hayo yamefanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Rahaleo iliyopo katika Halmashauri hiyo yaliyoudhuliwa na Wazazi, Wanafunzi Viongozi wa Serikali ya Wilaya pamoja  na wadau mbali mbali wa Elimu wa halmashauri hiyo

Akizungumza  wakati wa makabidhiano hayo  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Deodedth Kakoko alisema kuwa  Mamlaka hiyo kila mwaka imejiwekea utaratibu wa  kutenga fedha ya  kuchangia katika maeneo waliyoyapa kipaumbele  hasa ya elimu , Afya na Maafa yanapotokea  lengo likiwa kurudisha  faida na kutambulisha Kiasi  kilichopatikana kwa wadau wanaoshirikiana nao

Alisema  kuwa kwa kutambua  jitihada  zinazofanya na Rais Magufuli  ya kutoa elimu bure kwa wanafunzi wameamua kumuunga Mkono kwa kuchangia madawati hayo kwa kuwa elimu ndio msingi wa kila Mtoto hasa  katika karne hii ya sasa

“ Ndugu zangu katika maeneo yanayoweza kuleta  maendeleo ya Binaadamu lakwanza ni Elimu hii ni kwa sababu ukishakuwa na Elimu mengine yote yanafuata, ukiwa na elimu utajua namna ya kufanya matibabu, ukishakuwa na elimu utatafuta ufumbuzi kwa ajili ya Barabara, kwa ajili ya Maji  sasa ni wajibu wetu kama wadau kushirikiana kwa pamoja ili kuweka mazingira wezeshi kwa wanafunzi ili kuweza kusoma vizuri”. Alisema Kakoko

Nae kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa hiyo  Batista kihanza alisema kuwa madawati hayo  yatagawiwa katika shule tatu za  Halmashauri hiyo ambapo  Shule ya msingi Rahaleo itapatiwa madawati 25 , Shule ya msingi Muungano itapatiwa Madawati 25 na Shule ya Mnazi Mmoja itapata Madawati 26

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Lindi Shahibu Ndemanga aliushukuru uwongozi wa Mamlaka ya Bandari (TPA) kwa mchango huo wa Madawati  na kusema kuwa mchango huo umefika katika wakati muafaka ambapo kama Wilaya ilikuwa na uhitaji makubwa ya madawati

“ Tunaupungufu wa Madawati katika baadhi ya Shule na upungufu huu umetokana na Sera ya Elimu bure,  tunaandikisha Wanafunzi wapya na wanaongezeka mwaka hadi mwaka lakini kama hiyo haitoshi tunao mkakati kama Wilaya  wa kuhakikisha tunakomesha utoro na katika juhudi hizi za kupambana na utoro ndio tunajikuta sasa kuwa kumbe tunaingia sasa  katika mpango mwingine wa  kuwarudisha watoto ambao waliacha Shule, kitendo hiki kinaongeza mahitaji ya Viti na Meza  , kinaongeza mahitaji ya Madawati  kwa hivyo kama vile mlijua kama tunao uhitaji katika eneo hili” alieleza Ndemanga

Ndemanga pia alitumia fulsa hiyo kuwahasa wadau wengine kujitoa katika kuchangia  shuguli za kimaendeleo kwani kufanya hivyo kutasaidia kupunguza kero zinazowakabiri wananchi wa maeneo husika na hata kutawasaidia katika kujitangaza kwa wananchi kutambua shughuli wanazozifanya


MAHAKAMA YAKUBALI NASSARI KUVULIWA UBUNGE.

WALIOMALIZA KIDATO CHA NNE 2018 WARUHUSIWA KUBADILI MCHANGANUO WA TAHSUSI NA KOZI MBALIMBALI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dodoma .
......................................

Na.Alex Sonna,Dodoma


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo,amesema kuwa Serikali imetoa fursa ya wiki mbili kwa wanafunzi waliofaulu kujiunga na kidato cha tano kufanya mabadiliko ya machanganuo ya tahasusi na kozi mbalimbali walizochagua kwenye fomu ya F4 Selform.


Hayo yamesemwa  na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo,wakati akiongea na waandishi wa habari leo ofisini kwake amesema kuwa wiki hizo mbili zitaanza mwezi wa Aprili Mosi hadi 14 mwaka huu.


Aidha Jafo amesema kuwa fursa hiyo ni ya kwanza kutolewa mwaka huu na ni mara ya kwanza ambayo itawawezesha wanafunzi kurekebisha mchanganuo huo kulingana na ufaulu walioupata katika matokeo ya kidato cha nne ya mwaka 2018 yaliyotolewa na Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA).


Waziri Jafo amesema kuwa kuanzishwa kwa mfumo huu ni moja ya maboresho yanayofanywa na Serikali ya awamu ya tano katika kuhakikisha sekta ya Elimu inakua kwa kasi na kumpa fursa kila mwanafunzi aliyefaulu kujiunga na kidato cha tano au chuo.


Hata hivyo  amesema kuwa  hali hiyo inatokana na baadhi ya wanafunzi ambao hawakujaza vizuri tahasusi zao kutokana na kutokuwa na uhakika wa ufaulu.


”Ofisi yangu inatoa fursa hii kwa wahitimu kubadili mchanganuo ili kutoa mwanya zaidi kwa wanafunzi kusoma fani au tahasusi itakayomwandaa kuwa na utaalamu fulani kwenye maisha yake ya baadae kwa nafasi yake ambayo anatamani yeye mwenyewe au kwa kushauriwa na wazazi au walezi wake ”amesema Jafo


Hata hivyo amesema Ofisi yake tayari imeshakamilisha zoezi la awali la kuingiza taarifa zilizo kwenye Selform za wanafunzi kwenye kanzidata ya Tamisemi na mabadiliko hayo yatakayofanyika kwa njia ya mtandao yakikamilika kanzidata hiyo itatumika kuwachagua na kuwapangia kidato cha tano na kozi za vyuo.


”Kwa mwanafunzi yeyote atakayekuwa hajabadilisha taarifa zake mpaka muda kuisha Ofisi yake itaamini kuwa wanafunzi huyo ameridhika na machaguo yake ya tahasusi aliyoyafanya hapo awali alipokuwa shuleni” amesisitiza Jafo


Mtandao wanaotakiwa kuutumia ni kuomba ni www.selfom.tamisemi.go.tz  ambao amesema kuwa upo wazi tangu wakati huo.

 

Wednesday, March 27, 2019

FURSA ZA UFADHILI WA MAFUNZO NCHINI THAILAND

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

FURSA ZA UFADHILI WA MASOMO KWA WATANZANIA

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imepokea fursa za ufadhili wa masomo ya muda mrefu katika fani mbalimbali kutoka Serikali ya Thailand.


Kozi hizo zitakazotolewa kwenye Vyuo mbalimbali nchini humo, zitajikita katika fani za Filosofia ya Uchumi Timilifu; Mabadaliko ya Tabianchi, Usalama wa Chakula; Afya ya Jamii na Malengo ya Maendeleo Endelevu.


Wizara inawahimiza Watanzania wenye sifa kuomba nafasi hizo za mafunzo zilizotangazwa na Serikali ya Thailand kwa
mwaka 2019.


Mwisho wa kuomba nafasi hizo ni tarehe 31 Machi 2019. Kwa maelezo zaidi kuhusu kozi hizo na namna ya kuomba,
tafadhali tembelea tovuti  ifuatayo: 



Imetolewa na:
 
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje Na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dar es Salaam
27 Machi 2019